Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 24 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina nayomulika mabaharia wanawake, ambapo tunamsikia mmoja wao, Mary Jane Siy Chuan, Fundi wa Umeme melini,  akisema, “ninapoingia melini, wafanyakazi wengine wanahoji kama vile, kwa nini kuna mwanamke baharini.”Kukiwa na dalili za kuwa sitisho la mapigano kati ya Iran na Israel linaanza kushika mizizi, mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki, IAEA Rafael Grossi. ametoa wito kwa Iran kuanza tena ushirikiano na jumuiya ya kimataifa ili kupunguza mvutano unaoendelea kuhusu mpango wake wa nyuklia. Grossi amesema amempa Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ombi la kukutana na kushirikiana, “akitilia mkazo kuwa hatua hii inaweza kufungua njia ya suluhisho la kidiplomasia kwa mgogoro wa muda mrefu” kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.Msemaji wa Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) Thameen Al-Kheetan ameripoti leo kwamba hadi kufikia sasa takribani Wapalestina 410 wameuawa na jeshi la Israeli wakati wakijaribu kupata msaada kutoka kwa vituo vipya vya misaada vilivyokumbwa na utata huko Gaza.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, limeripoti leo kuwa linakadiria kuwa wakimbizi milioni 2.5 duniani kote watahitaji kuhamishiwa Kwenda katika nchi nyingine mwaka ujao.Na mashianani fursa ni yake Zahra Nader, raia wa Afghanistan ambaye ni mwandishi wa habari na mwanaharakati wa haki za wanawake, anayeishi uhamishoni kutokana na zahma nchini mwake. Akizungumza kutoka Geneva, USwisi anasimulia hali halisi ya wanawake nchini Afghanistan, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia haki zao..Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    10 min
  • TANLAP Tanzania tunahamasisha wanawake wengi kushiriki kwenye uchaguzi ili washiriki kuamua mambo yanayowahusu - Christina Kamili Ruhinda
    Katika mahojiano haya, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda alipozungumza na Anold Kayanda wa Idhaa hii kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya hali ya wanawake duniani CSW69 uliofanyika mapema mwaka huu hapa New York, Marekani, anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake  wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.
    4 min
  • Muziki waunganisha jamii zilizogawanyika Malakal nchini Sudan Kusini
    Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambalo kwa miezi ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha machafuko. Sharon Jebichii anatupasha zaidi
    3 min
  • 23 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, na juhudi za kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro Sudan Kusini.  Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani nchini Kenya.Hali ya taharuki yaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Grossi, leo ametoa wito wa dharura wa shirika hilo kuruhusiwa kufika kwenye maeneo hayo yaliyoharibiwa, ili kutathmini kiwango halisi cha uharibifu.Katika juhudi za kuimarisha mshikamano na kurejesha matumaini miongoni mwa jamii zilizotengana kwa migogoro, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kwa kushirikiana na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, hivi karibuni waliandaa tamasha maalum la muziki katika mji wa Malakal, jimbo la Upper Nile – eneo ambalo kwa miezi ya hivi karibuni limekuwa kitovu cha machafuko.Katika makala Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Mashirika yanayotoa huduma ya msaada wa kisheria nchini Tanzania, TANLAP, Christina Kamili Ruhinda anaeleza wanavyotekeleza mpango wao wa kuhakikisha wanawake  wanapata nafasi zaidi kwenye meza za uamuzi nchini Tanzania.Na mashianani fursa ni yake Priscillah Lesurkukwa, Mwanamke mkulima kutoka kaunti kame ya Samburu nchini Kenya ambaye ni mnufaika wa mradi wa Shrika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP, ambao umewapatia wakulima mafunzo ya kutengeneza makinga maji na kuchimba mashimo yenye umbo la nusu mwezi ili kuvuna na kuhifadhi maji kwenye mashamba yao, na sasa mbinu hizo zimebadilisha mazingira kuwa na malisho ya kijani kibichi na miti inayostawi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    11 min
  • Baada ya Marekani kushambulia vito vya nyuklia vya Iran, IAEA yataka fursa kutathimini uharibifu
    Hali ya taharuki yaendelea kushuhudiwa Mashariki ya Kati kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwishoni mwa wiki. Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki IAEA, Rafael Grossi, leo ametoa wito wa dharura wa shirika hilo kuruhusiwa kufika kwenye maeneo hayo yaliyoharibiwa, ili kutathmini kiwango halisi cha uharibifu. Flora Nducha na tarifa zaidi
    2 min
  • Burundi yamwezesha mkimbizi fundi seremala kutoka DRC kuendeleza stadi yake na kujipatia kipato
    Burundi inaonesha kwa vitendo mshikamano na wakimbizi kwa kuwapa fursa ya kupata elimu, huduma za afya, ajira na huduma nyingine za kitaifa, na hivyo kuwasaidia kuchangia katika jamii wanamoishi. Miongoni mwa wakimbizi hao ni Amani Lukoo Elie kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akiambana na mke wake na watoto 5 wamesaka hifadhi kusini-magharibi baada ya kukimbia mapigano jimboni Kivu Kaskazini. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Assumpta Massoi amefuatilia kile wanachofanya sasa ili kuweza kujikimu.
    4 min
  • 20 JUNI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi”, tukisikia ujumbe wa Umoja wa Mataifa na kazi wanazozifanya kuinua Maisha ya wakimbizi, na pia tunakuletea sauti za wakimbizi kutoka DRC, Burundi, Ethiopia na Sudan Kusini.Leo ni Siku ya Wakimbizi Duniani, mwaka huu ikibeba maudhui “Mshinamano na wakimbizi” na Umoja wa Mataifa umetaka mshikamano huo kwa vitendo wakati idadi ya watu wanaolazimika kufungasha virago na kukimbia makayo yao ikifikia kiwango cha kihistoria.Tukisalia na siku ya wakimbizi duniani tunaelekea  eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia  mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao.Katika makala Assumpta Massoi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR anakupeleka Kusini-Magharibi mwa Burundi kwenye kituo cha wakimbizi cha Musenyi kumsikia mkimbizi kutoka DRC ambaye ananufaika na kauli mbiu ya siku ya wakimbizi mwaka huu ya Mshikamano na Wakimbizi.Na mashianani tukisalia na siku ya wakimbizi duniani, tutakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kumsikia mtoto mkimbizi ambaye alitumikishwa katika vita na waasi wenye silaha.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapatiwa msaada na WFP mpakani mwa Ethiopia
    Katika eneo la Mata, karibu na mpaka wa Ethiopia na Sudan Kusini, ambakomaelfu ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini wanapokea msaada wa dharura kupitia juhudi za Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP. unaolenga kuwalinda baada ya kukimbia  mapigano makali nchini mwao. Nyibol Chueny Puok, mama wa watoto 4 ni miongoni mwao. Sharon Jebichi anatupasha zaidi...
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners