Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 30 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya elimu kwa watoto mashariki mwa DRC na Mkutano wa pili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT unaofunga pazia leo jijini Nairobi Kenya. Makala inaturejesha nchini DRC na mashinani inatupeleka katika bonde la Ziwa Victoria, kulikoni?Wakati ghasia zinazoendelea huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC zinaripotiwa kusababisha zaidi ya watoto milioni 1.8 kutokuweko shuleni, shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF nchini humo linajitahidi kwa udi na uvumba kuhakikisha watoto wanapata elimu kwani ni haki yao ya msingi.Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau mbalimbali wa amendeleo ya miji.Makala inakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan jimboni Kivu Kaskazini katika kitongoji cha Mavivi kuwasikia walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania,kikosi cha 11, TANZBATT11, wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO wakielezea sio tu majukumu yao, bali pia wanajivunia kile wanachofanya kwa kuzingatia Mei 29 imeadhimishwa siku ya kimataifa ya walinda amani.Na katika fursa ni yake Mhandisi Coletha Ruhamya, Naibu Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria, Mradi unaofanikishwa na Benki ya Dunia ambao unakabiliana na masuala ya usafi wa mazingira katika ziwa hilo. Anaeleza umuhimu wa usimamizi endelevu wa bonde hilo kote nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • Malawi inachukua hatua madhubuti kukabiliana na changamoto za makazi - Mercy Bety Dube
    Mkutano wa pili wa siku mbili wa Baraza Kuu la Makazi la shirika la Umoja wa Mataifa la Makazi Duniani UNHABITAT leo unafunga pazia jijini Nairobi Kenya. Baraza hilo linalofanyika kila baada ya miaka minne ni chombo cha juu kabisa duniani cha kufanya maamuzi kuhusu maendeleo ya miji endelevu na limewaleta pamoja wawakilishi kutoka nchi zote 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa pamoja na wadau mbalimbali wa amendeleo ya miji. Flora Nducha na taarifa zaidi.
    3 min
  • 29 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia Walinda Amani wa Umoja wa Mataifa ikitupeleka nchini DRC, Sierra Leone na Ghana. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na maana ya neno "MISHEMISHE.”Leo ni Siku ya Kimataifa ya Walinda Amani ambayo mwaka huu inajikita na maudhui ya “mustakabali wa ulinzi wa amani.”Katika ujumbe wake wa siku hii Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema walinda amani wa Umoja wa Matafa wako katika changamoto kubwa “Leo hii, walinda amani wanakabiliwa na hali zinazozidi kuwa ngumu katika dunia inayozidi kuwa na changamoto, ikiwemo uugawanyika na kutofautiana kwa mitazamo duniani kunazidi kuongezeka, operesheni za ulinzi wa amani zinakabiliwa, hatari zaidi kutokana na wingi wa vitisho kama vile ugaidi na walinda amani kulengwa kwa makusudi kupitia taarifa potofu zenye madhara makubwa na changamoto zinazovuka mipaka kuanzia janga la mabadiliko ya tabianchi hadi uhalifu wa kimataifa.Kikosi cha 11 cha Tanzania kinachohudumu chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo MONUSCO kimeungana na walinda amani wengine kuadhimisha Siku ya Walinda Amani Duniani. Maadhimisho hayo yamefanyika Mavivi, yakiongozwa na Brigedia Jenerali Diamond Meshack Madie, Mnadhimu Mkuu wa Vikosi vya MONUSCO.Shirika la Umja wa Mataifa la Mazingira UNEP limezindua mpango mpya wa dola milioni 15 kusaidia uwekezaji endelevu katika Bonde la Kongo – moja ya mifumo muhimu zaidi ya ikolojia duniani. Mpango huu unalenga kufungua fursa za biashara rafiki kwa mazingira kwa wajasiriamali wadogo na wa kati katika sekta za kijani. Msitu wa mvua wa Bonde la Kongo ni moja ya vyanzo vikubwa vya kaboni duniani na ni makazi ya watu zaidi ya milioni 75, wakiwemo jamii za asili.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili mtaalam wetu leo ni Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi  Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno "MISHEMISHE.”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Walinda amani wa UN kutoka Mongolia waokoa wakazi wa Abiemnhom nchini Sudan Kusini
    Kuelekea siku ya walinda amani Mei 29, tunakwenda nchini Sudan Kusini kumulika walinda amani na ulinzi wa raia. Katika taifa hilo changa zaidi duniani  walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Mongolia wanaohudumu kwenye Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (UNMISS) walikuwa msaada mkubwa wakati kijiji cha Abiemnhom kaskazini mwa Sudan Kusini kilipovamiwa. Walinda amani hao walifika haraka  kutoka kituo chao cha karibu na kutoa msaada wa kuokoa manusura na miili ya waliouawa. Je nini kilifanyika zaidi Sharon Jebichii anasimulia kwenye makala hii iliyotokana na video ya UNMISS.
    3 min
  • 28 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia haki za binadamu nchini Ukraine na upatikanaji wa elimu nchini Kenya. Makala tunakupeleka nchini Sudan Kusini, na amashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Uchunguzi kuhusu Ukraine imehitimisha kwamba vikosi vya kijeshi vya Urusi vimetenda uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, hasa mauaji, kupitia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani (drones) yaliyoelekezwa dhidi ya raia.Mradi wa "operesheni rejea shuleni" unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na wizara ya elimu ya Kenya, shirika liliso la kiserikali la Hapag Lloyd na wadau wengine kwa kuzipa fedha familia zisizojiweza kuendesha shughuli za kiuchumi, umerejesha mautumaini ya elimu kwa mamia ya watoto katika Kaunti ya Kwale Pwani ya Kenya  ambao waliacha shule sababu ya umasikini.  Katika makala ikielekea siku ya walinda amani kesho Mei 29, tunamulika harakati za walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini SUdan Kusini za kulinda raia na mwenyeji wako katika makala hii iliyoandaliwa kupitia video ya ujumbe wa  Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani Sudan Kusini, UNMISS ni Sharon Jebichii.Na katika mashinani huku machafuko yakiendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, wafanyakazi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wako mashinani mjini Goma na maeneo mengine yaliyoathirika ili kutoa msaada muhimu, ikiwa ni pamoja na kufanikisha nia ya wakimbizi wanaorejea nchini mwao Rwanda. Raab na Ruusi ni baadhi yao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • Alice Kamau: Asante UNICEF na wadau ndoto ya mwanangu ya elimu imerejea
    Mradi wa "operesheni rejea shuleni" unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na wizara ya elimu ya Kenya, shirika liliso la kiserikali la Hapag Lloyd na wadau wengine kwa kuzipa fedha familia zisizojiweza kuendesha shughuli za kiuchumi, umerejesha mautumaini ya elimu kwa mamia ya watoto katika Kaunti ya Kwale Pwani ya Kenya  ambao waliacha shule sababu ya umasikini. Flora Nducha na maelezo zaidi.
    3 min
  • 27 MEI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kuangazia siku ya familia iliyokutanisha wadau wakimulika pamoja na mambo mengine nafasi ya vyombo vya habari katika kuimarisha malezi na makuzi ya mtoto.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura OCHA hii leo imesema wakati mpango tata wa Israeli wa kugawa misaada kwenye eneo la Palestina la Gaza linalokaliwa kimabavu na Israeli ukiendelea, Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena umesihi mamlaka za Israeli kuruhusu ongezeko la kiwango cha misaada ya kufikia walengwa kwenye eneo hilo lililozingirwa ili kuepusha uhaba wa chakula..Kadiri nchi zinavyokumbwa zaidi na majanga ya asili, gharama halisi za majanga ni mara 10 zaidi ya ilivyodhaniwa hapo awali, zikiwa na athari mbaya zaidi katika sekta za afya, makazi, elimu na ajira, imesema Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kupunguza hatari za majanga katika ripoti iliyochapishwa Jumanne.Nchini Namibia, makazi yaliyojengwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA kwa ajili ya wajawazito wanaoishi maeneo ya mbali kusubiria ili kujifungua kwa usalama, yamesaidia kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga.Na katika mashinani, kupitia video iliyoandaliwa na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Sudan Kusini UNMISS, tunakutana na Mary Aban Akon, mkazi wa kijiji cha Hai Matar huko Sudan Kusini. Yeye ni miongoni mwa wakimbizi waliorejea nyumbani baada ya kupatiwa makazi mapya yaliyojengwa kwa msaada wa mashirika ya kibinadamu chini ya mradi uliofadhiliwa na Umoja wa Mataifa na wadau wake.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Vijana Kenya watumia mpira wa miguu kutokomeza umasikini na kuishi maisha bora - Peter Omondi
    Katika kuelekea siku ya kandanda, kabumbu au mpira wa miguu duniani itakayoadhimishwa Jumapili wiki hii Mei 25 ikibeba maudhui nguvu ya kdandanda katika kuleta mabadiliko tuabisha hodi Nairobi Kenya ambapo leo Peter Omondi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Global Youth Forum linalounganisha vijana Kenya kwa lengo la kutokomeza umasikini na kuishi maisha bora kupitia michezo mbalimbali ikiwemo kandanda akizungumza na Idhaa hii ya Kiswahili anaeleza umuhimu wa kandanda katika ajenda ya Umoja wa Mataifa ya maendeleo endelevu. Anaanza kwa kujitambusha.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners