Katika episode hii ya Nukta the Podcast, tunajadili kwa kina namna teknolojia ya akili bandia (Artificial Intelligence – AI) inavyozidi kutumika katika vyuo vikuu nchini Tanzania na mjadala unaoibuka kuhusu athari zake kwa elimu ya juu.
Kupitia mahojiano na wahadhiri, wanafunzi, wataalamu wa saikolojia na teknolojia, mjadala huu unaangazia pande zote mbili za AI kama nyenzo ya kurahisisha ujifunzaji na kama changamoto inayoweza kudidimiza fikra huru, ubunifu, na maadili ya kitaaluma, hasa katika taaluma nyeti kama udaktari na uhandisi.
Episode hii inachambua maswali muhimu:
• Je, AI inawasaidia wanafunzi au inawafanya wategemezi kupita kiasi?
• Vyuo vikuu vina sera na miongozo ya kudhibiti matumizi ya AI?
• Serikali na wadau wa elimu wana nafasi gani katika kulinda ubora wa wahitimu?
Hii ni sauti ya mjadala mpana unaoendelea duniani, ukiangalia kwa jicho la Tanzania. Sikiliza ujipatie ufahamu, hoja, na mitazamo tofauti kuhusu mustakabali wa elimu ya juu katika zama za AI.
🎧 Nukta the Podcast – Mahali ambapo hoja nzito hukutana na uhalisia.