Serikali ya Kenya ni zuzu. Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amewaandalia wanariadha wa nchi yake makaribisho ya kifahari; wametembezwa mijini kwa magari ya kifahari kuwapungia mikono wananchi, wakapewa kitita cha fedha na zawadi ya magari. Hapa Kenya, serikali imenyamaza kama maji mtungini bila kujivunia nafasi ya kwanza ambayo Kenya ilipata barani Afrika katika mashindano ya Olimpiki ya Tokyo Japan, 2020.