Sign up to save your podcastsEmail addressPasswordRegisterOrContinue with GoogleAlready have an account? Log in here.
Ni jukwaa la kila wiki la kuzungumzia mapenzi miongoni mwa vijana; mahusiano, kuchumbiana na mengi yaliyowakaa mioyoni.... more
FAQs about Vijana na Mapenzi:How many episodes does Vijana na Mapenzi have?The podcast currently has 41 episodes available.
June 25, 2021VIJANA NA MAPENZI PODCAST: Kijana alalamikia kuchezewa shere na mpenzi waliyepatana FacebookSiku hizi, mitandao ya kijamii imekuwa ikitumiwa na wengi kujitafutia wachumba, wengine wamefaulu na wengine wakikosa. Kijana mmoja amewasilisha malalamiko yake kupitia podcast hii akisema hamwamini tena mpenziwe wanayechumbiana mtandaoni akihisi kwamba anamchezea shere. Je, aendelee na uhusiano huo na mwanadada ambaye hajawahi kukutana naye ana kwa ana ama aukatize?...more12minPlay
June 19, 2021VIJANA NA MAPENZI PODCAST: Jamaa abaki njia-panda baada ya kuachwa na mkePodcast hii inamwangazia jamaa mwenye umri wa miaka 30 ambaye hajui la kufanya baada ya mkewe kumtoroka. Kijana huyo anayefanya kazi katika Kaunti ya Isiolo anasema kwamba siku moja mkewe alimwomba ruhusa ya kwenda kuwaona wazazi wake na hadi sasa hajarejea. Mwanamke huyo aliondoka pamoja na mtoto wao wa umri wa miaka 3 na anapopigiwa simu na mumewe anasema kwamba aliolewa kwingine. Kijana huyu yuko katika njia-panda asijue la kufanya. Mshauri wa masuala ya kijamii, Rachel Mahungu anampa ushauri katika podcast hii....more11minPlay
June 11, 2021VIJANA NA MAPENZI PODCAST: Mchumba wako afaa kujua kiwango cha mshahara wako?Suala la fedha katika mahusiano ya kimapenzi, bila shaka limechangia kuvunjika kwa mahusiano mengi kutokana na ukosefu wa uwazi. Mada hii inalenga kuangazia namna ya kulijadili mnapochumbiana. Washauri wa masuala ya kijamii, Alex Munyere na Rachel Mahungu wanalichanganua katika podcast hii....more15minPlay
June 03, 2021VIJANA NA MAPENZI PODCAST: Ni sawa kuchumbiana mitandaoni?Mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook, WhatsApp, Twitter, Instagram na kadhalika imerahisisha pakubwa njia za mawasiliano katika karne hii. Ni hali ambayo imechangia kubadilika kwa mbinu za watu kuchumbiana ambapo wengine hutumia mitandao kuwatafuta wachumba. Lakini je, hili linafaa? Tumehusisha kauli za wananchi kuhusu mapenzi ya mitandaoni vilevile kushiriki mazungumzo na vijana na washauri wa masuala ya kijamii kuihusu mada hii....more18minPlay
May 27, 2021VIJANA NA MAPENZI PODCAST: Dalili za mapenzi kuanza kwenda mramaKatika awamu hii ya pili ya kipindi cha Vijana na Mapenzi, tunaangazia ishara mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia kutambua iwapo uhusiano wa kimapenzi hauendi popote na ni wakati wa kutengana. Wananchi wametoa kauli zao kuihusu mada hii huku washauri, Alex Munyere na Rachael Mahungu Mboya wakitoa ushauri kuhusu mada hii. Mtayarishi ni Beatrice Maganga....more13minPlay
May 19, 2021Vijana na Mapenzi Podcast; Mambo ya Kuzungumzia wakati wa 'dating' yaani miadiAwamu ya kwanza ya Vijana na Mapenzi inaangazia suala la miadi yaani dating, Je ni kipi ambacho huzungumziwa wakati wa date? Tumewashirikisha vijana kujadili suala hili, vilevile kupata kauli za washauri wa masuala ya mahusiano....more9minPlay
May 16, 2021VIJANA NA MAPENZI PODCAST; Wanaume wa Nigeria wanajua kupenda; Wetu ni 'mali-ngumu'Wasichana wa Kenya wanaeleza sababu za kuwapenda wanaume wa Nigeria au Wazungu; kwamba wanajua mapenzi, kutumia pesa, kuvinjari na kuwapa raha za peponi. Kwamba wanaume wa Kenya hawajui kupenda, wana mikono birika. Ni gumegume tu...si wanaume kamili. Nao wanaume wa Kenya wanahofia ushindani na kusalimu amri; wanasema kwamba ni sawa tu...acha wapendane....more16minPlay
February 11, 2021Vijana na Mapenzi. ValentinesNi msimu wa mapenzi, Je ni lazima mpenziwe akupe zawadi siku ya Valentines, na asipo kupa ina maana kwamba hakupendi? Wakenya wanalizungumzia suala hili vilevile washauri wa masuala ya mahusiano ambayo wana mtazamo wao kulihusu....more15minPlay
February 03, 2021Episode 3: Vijana na Mapenzi Online DatingKatika awamu hii tunaangazia utumiaji wa mitandao katika kuchumbiana. Je, inafaa ama haifai? Vijana wamelizungumzia suala hili katika kipindi hiki vilevile kuna ushauri wa mjuzi wa masuala ya mahusianio, Rachel Mahungu....more18minPlay
January 22, 2021Episode 2: The red flags during datingEpisode 2 is about the red flags during dating...more13minPlay
FAQs about Vijana na Mapenzi:How many episodes does Vijana na Mapenzi have?The podcast currently has 41 episodes available.