Babananiii

Babananiii

By Fabian C. MwakabanjeArtsBooks
Download on the App Store

Babananiii episodes

  • Unapochagua Kazi Zingatia
    CHAGUA KAZI UNAYOIPENDA:
    Jambo la kwanza na lililo muhimu kushinda mengine yote kuhusu kazi ni kuhakikisha kwamba unaipenda kwa dhati na kufurahia kuifanya. Ziko kazi za aina mbalimbali - k.m. kilimo; ufugaji; biashara; kutoa huduma mbalimbali kama vile ualimu; udaktari; ukarani; n.k. Kazi hizo zinaweza kufanywa mahali mbalimbali - k.m. kijijini; mjini; nyumbani; ofisini; kiwandani; n.k. Vile vile kazi hizo zinaweza kufanywa kwa njia mbalimbali - k.m. Kiujamaa; kiushirika; kwa kuajiriwa; kwa kujiajiri mwenyewe peke yako; n.k. Mambo yote haya, pamoja na hadhi ya kazi yenyewe katika jamii unamoishi huenda pia yakaongezea kukufanya upende kazi moja kuliko nyingine.
    Kwa vyovyote swali la kwanza la kujiuliza mwenyewe ni hili; *"Kama kazi zote hizo zingeweza kuniletea kipato kilicho sawa, na kama uwezo wa kujipatia kazi zote hizo ungekuwa ni sawa; je, moyoni ningependelea na kufurahia zaidi kufanya kazi zipi?"*
    Tayarisha orodha ya kazi zote zile ambazo unazipenda moyoni, ukianzia na kazi zile ambazo unazipenda zaidi kushinda nyingine.
    *"Unapotayarisha orodha hii jitahidi sana usiingiwe na mawazo yoyote yanayohusu mshahara au kipato cha aina yoyote."*
    CHAGUA KAZI UNAYOIWEZA:
    Hatua ya pili katika kufanya uchaguzi wa kazi inayokufaa ni kuchunguza kwa makini orodha yako uliyoitayarisha ya kazi unazozipenda ili uone kwamba ni kazi gani miongoni mwake ambazo utaweza kuzimudu. "Haina maana kufanya kazi usiyoiweza eti kwa kuwa unaipenda.* Kuna mambo mbalimbali ambayo lazima uyatupie macho wakati wa kuamua jambo hili la uwezo wako kuhusu kazi fulani fulani. Kila inapowezekana yafaa uombe ushauri kutoka kwa watu unaowaamini na wanaokufahamu vizuri (k.m. waalimu wako, wazazi, rafiki n.k.) Hawa wataweza kukuambia udhaifu wako na uwezo wako kuhusu kazi unazozipenda.
    Baadhi ya mambo muhimu ambayo lazima uyapime mwenyewe au uyaombee ushauri ni haya yafuatayo:-
    *1. Maarifa:*
    Je, unao ujuzi, au elimu, au kipaji au mazoea, au wepesi wa kujifunza kufanya kazi hiyo unayoipenda?
    *2. Afya:*
    Je, afya yako itakuruhusu kufanya kazi hiyo bila matatizo yoyote?
    *3. Tabia:*
    Je, tabia yako inaoana na kazi hiyo? Kwa mfano kama kazi hiyo inahitaji uvumilivu na wewe ni kijana asiye mvumilivu, basi kazi hiyo haikufai ijapokuwa unaipenda.
    *Kama wewe ni mtu unayetamani kudokoa dokoa, usilogwe ukachagua kazi ya kutunza fedha, kwani hiyo hatimaye itakupeleka jela.* Vijana wengi waliokimbilia kushika kazi wanazozipenda bila ya kujipima vizuri kiuwezo, wameandamwa na majuto. Ni juu yako uchunguze kwa makini ile orodha yako uliyoitayarisha na kuondoa au kufuta zile kazi ambazo una mashaka kwamba hutazimudu vizuri kielimu, kiafya, kitabia n.k.
    *Baada ya kufanya hivyo panga upya kazi zilizosalia katika orodha hiyo ukianzia na kazi zile ambazo una hakika nazo zaidi kwamba utaziweza kuzimudu bila wasiwasi.*
    AHSANTENI SANA..... Tutaendelea sehemu nyingine kesho!!! Muwe na usiku mwema!!
    7 min
  • KIJANA NA KAZI/FAIDA YA KAZI PT. 3
    *FAIDA ZA KAZI* inaendelea.....
    4. KAZI ITAIMARISHA AFYA YAKO
    Katika sehemu nyingi mbalimbali duniani imeanza kuonekana kwamba akina mama huwa na maisha marefu zaidi kuliko akina baba. Kuna sababu mbalimbali ambazo huleta tofauti hiyo, na mojawapo ambayo wataalam wengi wanakubaliana nayo ni ile inayohusu kazi. Wanasema kwamba kwa vile kina mama wanafanya kazi zaidi kuliko kina baba (yaani hawastaafu kufanya kazi ya kupika au ya kutunza usafi wa nyumba) miili yao inapata nafasi kubwa ya kufanya mazoezi na kuimarika. Ni dhahiri kwamba kazi mbalimbali hutoa nafasi ya kutosha kwa mazoezi ya viungo mbalimbali vya mwili. Ukikaa bila kazi za kutosha mwili huchakaa upesi zaidi. Hata hivyo yafaa ukumbuke kwamba kazi ni lazima ziwe za kiasi. Zikizidi mno au zikiwa nzito mno mwili utashindwa kuzimudu, na matokeo yake yatakuwa ni afya mbaya na maisha mafupi. Vile vile usisahau kwamba kuna chache fulani fulani ambazo huweza kudhuru afya endapo tahadhari maalum hazitachukuliwa wakati wa kuzifanya k.m. uchimbaji wa baadhi ya madini fulani fulani, au ufanyaji kazi katika mazingira yasiyofaa, n.k.
    *** Mwisho wa Faida za Kazi ***
    KWA NINI NI LAZIMA TUFANYE KAZI
    Katika maelezo yaliyotangulia tumeona faida unazoweza kupata kutokana na kufanya kazi. Pamoja na faida hizi kuna sababu nyingine
    *'muhimu'* ambazo zinakulazimisha ufanye kazi ukipenda usipende. *Wazazi wako na jamaa wengine wanakutazamia ufanye kazi ili uwape nafasi ya kupumua.* Hawawezi kuendelea kukutumikia wakati wote. Kuna kikomo cha utumishi wao kwako. *"Hata kama huoni aibu kuendelea kusaidiwa saidiwa nao, yafaa ukumbuke kwamba utafika wakati ambao uwezo wao utapungua, nawe mwenyewe itabidi uchukue jukumu la kuwasaidia.*
    Zaidi sana wazazi na jamaa zako wanakutazamia ufanye kazi ile uweze kujipatia maendeleo yako mwenyewe katika jamii. Kwa mfano wanakutazamia uoe au uolewe, na ujipatie nyumba na watoto wako mwenyewe. Hayo yatatoka wapi bila kazi? *Si haki, wala si vizuri wazazi na jamaa zako wakushughulikie katika mambo kama hayo.* Unapaswa ujilishe wewe mwenyewe na watoto wako kwa jasho lako bila kutegemea msaada toka kwa wengine.
    Jamii na taifa, nao kwa upande wao wanakutazamia ufanye kazi ili usiwe mzigo kwao. Watu wanaozurura ovyo bila kazi mara nyingi huonekana wanapendelea kuwa wahalifu wa sheria, au walalamikaji, au wenye kutaka kuleta *mapinduzi* yasiyo na msingi wa maana katika maendeleo ya nchi.
    Hivyo licha ya kupunguza mzigo na wasiwasi kwa jamii na taifa lako, wewe mwenyewe unaweza kusaidia pia kuongeza uchumi wa nchi yako kama utaamua kufanya kazi badala ya kuzurura ovyo. Taifa na jamii wanakutazamia ukuze uchumi na maendeleo ya nchi, sio tu kwa faida ya wengine, bali kwa faida yako mwenyewe. Je, ukiugua utatibiwa? Unadhani hizo dawa zitatoka wapi? Je, ukisafiri hutatumia vyombo vya usafiri? Unadhani vyombo hivyo vinaingia bure nchini? Huna budi ufanye kazi ikiwa unataka utoe mchango wako kwa huduma mbalimbali unazozipata katika jamii na taifa.
    *Pengine mojawapo ya sababu muhimu sana ambayo inakulazimisha ufanye kazi ni ile ya kutumia kipawa chako kwa faida ya wengine.* Kwa mfano katika jamii na taifa mara kwa mara hutokea upungufu wa waalimu, madaktari, viongozi wa vijiji, viongozi wa dini, n.k. je, kama wewe una kipawa au uwezo wa kumudu kazi kama hizo, huoni ni lazima uitikie mwito wa kutumikia jamii na taifa lako ikiwa utaombwa kufanya hivyo? Kama utakataa, na wengine nao watakataa, taifa litakuwa wapi? Jambo hili tutalifikiria zaidi katika maelezo mengine hapo baadaye.
    6 min
  • FAIDA YA KAZI PT. 2
    *FAIDA YA KAZI* Inaendelea....
    *2. KAZI ITAKUONGEZEA FURAHA*
    Licha ya uchumi kazi inaweza kuwa jambo la kufurahisha sana. Mtu hufurahia anapofanya kazi yenyewe, na hufurahia pia, anapoona matokeo ya kazi yake, hasa iwapo kazi hiyo iwe ni ile inayohusiana na kuleta mabadiliko mapya mbalimbali.
    Isitoshe, shughuli za kazi zinasaidia sana kupitisha wakati na kumwondolea mtu mawazo yasiyofaa. Vile vile kazi huweza kuwa njia nzuri sana ya kumwezesha mtu akutane na watu wengi mbalimbali ambao humchangamsha kwa njia nyingi; na mara nyingi kazi imekuwa ndio njia muhimu ya kujipatia marafiki wa aina mbalimbali. Watu wengi waliokwishastaafu huanza kulalamika kwamba wanakosa kitu cha kuwashughulisha vya kutosha, na zaidi sana wanasumbuliwa na *upweke* unaowaandama kutokana na kuwakosa wale ambao walikuwa na mazoea ya kukutana kutana nao katika kazi.
    *"Kweli mtu akikunyima kazi amekuondolea furaha katika maisha."*
    *3. KAZI ITAKUFANYA MAISHA YAWE NA THAMANI*
    Hatupo hapa duniani ili tule, tunywe tustarehe, na tuishi kwa kujifikiria nafasi zetu sisi wenyewe tu, bali maisha yetu yana lengo; *nalo ni kutumika kwa Utukufu wa Aliyetuumba.*
    Watu ambao hawana lengo kama hilo mara nyingi maisha yao hujaa wasiwasi, tupu (vanity) na kutotosheka. Baadhi yao huwa ni wale ambao unawaona wakihangaika mchana na usiku kuwinda shibe na starehe. Baadhi ya wengine ni wale ambao unasikia kwamba wameamua kujiua wenyewe kwa vile hawaoni faida ya kuendelea kuishi.
    Lakini ukiishi maisha yenye lengo la utumishi utatambua jinsi ulivyo na thamani kubwa kwa wengine, na hutathubutu kuzurura ovyo bila kazi yoyote japo uwe tajiri kiasi gani. Pia hutathubutu kukomesha maisha yako mwenyewe kwa vile utajiona kwamba wewe sio mali yako mwenyewe, bali upo kwa kutimiza lengo fulani. *"Watu wengi wanaotosheka katika maisha huwa ni wale ambao wakitazama nyuma wanaridhika kuona kwamba wametoa mchango wao katika kuleta maendeleo na ustawi wao na wa wenzao; na wakitazama mbele wanaona kwamba bado wanayo nafasi kubwa ya kuendelea kutimiza lengo kama hilo."*
    Itaendelea kesho.........
    Ahsanteni
    6 min
  • KIJANA NA KAZI (The Youth Got To Work)
    Kijana na kazi, ni mfululizo wa mafunzo yaliyomo katika kitabu kiitwacho kijana na kazi kilichochapishwa mwaka 1983 na EMAU (Elimu ya Malezi ya Ujana). My name is Fabian C. Mwakabanje, a Tanzanian educator, I coordinate young adults literacy program in public schools. In these episodes i seek to empower the written words through the voice for those many in my community who can't read nor write or they just don't have that reading habit.
    5 min

About Babananiii

From the publisher's feed

A literate African empowering the community through literacy programs.