Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 13 MACHI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo Idhaa hii imezungumza na Lucy Gidamis, Wakili ambaye kwa sasa anafanya kazi na shirika la Msichana Initiative nchini Tanzania akijikita katika kutetea na kutekeleza haki za wanawake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno Wakfu.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC hii leo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO umekabidhi magari sita kwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini ili kuwezesha shughuli za polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Afya duniani WHO na la kuhudumia watoto UNICEF yametangaza kuwepo kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa surua barani ulaya, jumla ya wagonjwa 127,350 waliripotiwa kati yao watoto wakiwa zaidi ya asilimia 40.Na hii leo ikiwa ni chungu cha 10 cha Ramadhan, ikikamilisha fungu la kwanza kati ya mafungu matatu ambapo ni siku 30 za mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameanza ziara yake ya siku nne nchini Bangladesh ikiwa ni utaratibu wake wa kila mwaka wa kushiriki Ramadhan na jamii za waislamu walio kwenye changamoto mbalimbali.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua neno Wakfu.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    11 min
  • Haki Elimu - Ujumbe wetu mkuu kwenye CSW69 ni elimu kwa mtoto wa kike
    Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu hii leo Machi 12 katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijinoi New York, Marekani. Mkutano huu wa mwaka huu unafanyika katika hali ya kihistoria kwa kuzingatia kuwa ni miaka 30 tangu Mkutano wa wanawake ulipofanyika jijini Beijing - China  mwaka 1995 na kuweka maazimio muhimu kuhusu masuala mazito ya kumkomboa mwanamke dhidi ya ukandamizaji kote duniani. Maelfu ya wanawake na wadau wengine wanakutana kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York. Miongoni mwao ni Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.
    4 min
  • 12 MACHI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80, na yaliyojiri katika mkutano wa CSW69. Makala na mashinani tunasalia hapa hapa makao makuu, kulikoni?Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amezindua Mpango mpya wa UN80, unaolenga kuimarisha kazi na ufanisi wa chombo hicho ambacho mwaka huu kinatimiza miaka 80 tangu kuanzishwa kwake huku akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kimataifa..Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome.Makala tukisalia hapa hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa Jijini New York, Marekani ambako Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, (CSW69) umeingia siku ya tatu, nimezungumza na Nuria Mshare ambaye amewakilisha taasisi ya Haki Elimu ya nchini Tanzania.Na Katika mashinani fursa ni yake Janet Zebedayo Mbene kutoka Tanzania aliyehududhuria mkutano huu hapa makao makuu, kama mwenyekiti wa shirika lisilo la kiserikali la mtandao wa uwezeshaji wa wanawake Tanzania na angependa kuwashauri wanawake na wasichana wanaopitia changamoto wajikite katika fursa mbalimbali. Kila kitu kina changamoto. Wajitie moyo na waondoe uoga, na kwa kile kidogo walicho nacho wanaweza kujiinua na kuinua jamii kwa ujumla.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!  
    12 min
  • Jumuiya ya kimataifa ishikeni mkono Sudan Kusini kwa maslahi ya wananchi - Micklina Kenyi
    Wakati mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW69 ukiendelea hapa New York Marekani nchini Sudan Kusini wanawake na wasichana wanaendelea kuonja shubiri ya vita, wakibakwa, kuuawa, kukosa elimu na kupitia changamoto nyingine lukuki sababu ya vita. Mmoja wa washiriki wa mkutano wa CSW69 kutoka Sudan Kusini akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii ya Kiswahili amesema sasa imetosha amekuja na ujumbe mmoja tu, anataka jinamizi la vita lazima likome. 
    3 min
  • 11 MACHI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa kina inayomulika mkutano wa CSW69 ulioanza Jana Jumatatu hapa New York, Marekani, ikiwa ni miaka 30 tangu mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake uliofanyika Beijing mwaka 1995, ukiweka msingi wa mabadiliko yanayoshuhudiwa sasa ya usawa wa kijinsia. Pia tunakuletea muhtasari na sauti za vijana kutoka mashinani.Katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa asubuhi hii kwa saa za New York, Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, amekutana na wawakilishi wa Asasi za Kiraia wanaoshiriki Mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake CSW69. Bwana Guterres amezitaka Asasi za Kiraia kuendelea kuzisukuma nchi kuweka mazingira bora kwa ajili ya usawa wa wanawake na wasichana na pia  akakumbushia kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kuwaunga mkono katika kulitimiza lengo hilo.Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk kupitia Msemaji wake, ameripoti ukatili unaoendelea katika pwani ya Syria tangu Machi 6, ambapo anasema takriban raia 111 wameuawa, wengi wao kwa misingi ya kiimani. Hospitali pia zimeshambuliwa na Umoja wa Mataifa unatoa wito wa uchunguzi huru na uwajibikaji kwa wahusika.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) nchini Malawi limeongeza wigo wa mpango wake wa Mlo Shuleni unaopatikana kwa kununua vyakula vinavyolimwa na wananchi wa karibu katika maeneo hayo. Mradi huo unaotekelezwa wilayani Nkhotakota, unanufaisha wanafunzi 10,000 na kusaidia wakulima wadogo 1,200, hivyo kuimarisha upatikanaji wa chakula na uchumi wa ndani.Na Katika mashinani huku mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 ukiendelea hapa makao makuu, tutakwenda Kajiado nchini Kenya kusikia ujumbe wa vijana kuhusu usawa wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!  
    12 min
  • 10 MACHI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69 na wakimbizi wanaokimbia machafuko nchini DRC kwenda Burundi. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka nchini Lebanon, kulikoni?Hii leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani unaanza mkutano wa 69 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW69, kusanyiko kubwa zaidi la kila mwaka la Umoja wa Mataifa linalomulika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake mwaka huu washiriki wakiwa zaidi ya 25,000.Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi.Makala leo tunamwangazia Fatuma Mfumia, dereva pekee wa kike katika shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhuduia Watoto, UNICEF Tanzania.Na mashinani mashinani fursa ni yake Ghada Dawiche’s ambaye licha ya machungu yaliyomkumba baada ya kupoteza bintiye aliyekuwa mfanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR nchini Lebanon, pamoja na mjukuu wake wa kiume wakati kombora la Israeli lilipopiga nyumba yao nchini  Lebanon, anasema Umoja, nguvu na tumaini ndio ujumbe mkuu anaowapa wanawake wote waliopoteza wapendwa wao vitani na katika kupigania haki za wanawake.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners