Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNHCR: Zaidi ya wakimbizi 63,000 wa DRC wamewasili Burundi wengi wanaishi kwenye uwanja wa Rugombo
    Zaidi ya watu 63,000 sasa wamewasili Burundi wakikimbia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wengi wao wanaishi katika hali ngumu ndani ya uwanja wa michezo wa Rugombo jimboni Cibitoke (CHIBITOKE) huku wakisubiri kuhamishiwa kwenye kambi rasmi za wakimbizi. Flora Nducha amefuatilia safari ya mmoja wa wakimbizi hao, kwako Flora.
    3 min
  • Wanawake wajengewa uwezo wa tofauti ya matumizi ya lazima ni muhimu ili kujikwamua kiuchumi
    Mwaka 1995 huko Beijing, China kwenye mkutano wa nne wa kimataifa wa wanawake lilipitishwa Azimio la Beijing na Mpango wa Utekelezaji, ambalo pamoja na mambo mengine lililenga kusongesha haki za wanawake. Mwaka huu wa 2025 ikiwa ni miaka 30 baadaye, tathmini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, inaonesha kuwa nchi zimesonga mbele katika usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake, kuanzia kuharamaisha ubaguzi kwenye ajira hadi mipango ya kuhimili tabianchi inayozingatia jinsia. Lakini bado kuna vikwazo vya kijamii, kiuchumi na kisiasa na ndio maana wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake mwaka huu wa 2025 kipaumbele ni kusongesha uwezeshaji, haki na usawa. Ni katika kumulika harakati hizo, Assumpta Massoi anakupeleka Singida nchini Tanzania kwenye maadhimisho yaliyoambatana na ujengeaji uwezo. 
    5 min
  • UN: Sasa ni wakati wa kutimiza ahadi ya usawa wa kijinsia
    Katika kuelekea siku ya kimataifa ya wanawake ambayo huadhimishwa kila mwaka Machi 8 leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kunafanyika hafla maalum ya kuadhimisha siku hiyo ambayo mwaka huu imebeba maudhui “Kwa wanawake na wasichana wote: haki, usawa, uwezeshaji.” Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women Sima Bahous amesema ni wakati wa kutekeleza kwa vitendo ndoto ya azimio la Beijing miaka 30 iliyopita la kufanya usawa wa kijinsi kuwa hali halisiKwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres pamoja na kupongeza mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kusongesha usawa wa kijinsia duniani amesemaNatts….“Hata hivyo, mafanikio haya yaliyopatikana kwa jitihada kubwa bado ni dhaifu na hayatoshi kabisa.Mateso ya muda mrefu, ukatili, ubaguzi na ukosefu wa usawa wa kiuchumi bado vinaathiri jamii zetu.Kila baada ya dakika kumi, mwanamke huuawa na mwenzi wake au mwanafamilia.”Ameongeza kuwa wanawake na wasichana milioni 612 wanaishi chini ya kivuli cha migogoro ya silaha ambapo haki zao mara nyingi huchukuliwa kama zisizo na thamani.Akitaja takwimu amesema chini ya theluthi mbili ya wanawake duniani wanashiriki katika soko la ajira na wale wanaoshiriki hulipwa mishahara ya chini kuliko wanaume.Hivyo ameonya kwamba“Kwa kasi hii, itachukua miaka 130 kutokomeza umasikini uliokithiri kwa wanawake na wasichana.Amemesema badala ya kuingiza usawa wa haki kama jambo la kawaida, dunia inashuhudia kuenea kwa ubabe na chuki dhidi ya wanawake.Kwa muktadha huo amesistiza kwamba “Hatuwezi kukaa kimya wakati maendeleo yanaporudishwa nyuma. Lazima tupambane.”Akizungumzia sauti za vijana kushiriki katika harakati za usawa na haki za wanawake, kwenye hafla iliyofanyika mjini Geneva Uswisi kuadhimisha siku ya wanawake mwanafunzi kutoka Kenya James Mumo Nyumu amesisitiza kuwa hakuna nchi yoyote iliyotekeleza ahadi yao ya dunia isiyo na ukatili dhidi ya wanawake.Amesema “Maono ya Beijing yalikuwa ramani ya siku zijazo ambazo bado hatujazifikia kikamilifu,” alisema akiongeza kuwa “Nguvu kwa wanawake si tishio ni zawadi kwa jamii.”Hivyo amesisitiza kwamba“Kizazi changu kinadai hatua zaidi,” akitoa wito wa kuchukua hatua zaidi ya Beijing kwani“Kazi yetu haijakamilika.”
    4 min
  • 07 MACHI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wanawake, na hali ya wanawake wajawaito nchini Ukraine. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni?Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo ikiangazia haki za wanawake miaka 30 baada ya Azimio la Beijing inaonesha uwepo wa maendeleo katika usawa wa kijinsia, kama vile sheria dhidi ya ubaguzi na sera jumuishi za kijinsia. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza uwepo bado wa ubaguzi wa kijinsia uliojikita katika jamii, ukiendelea kuwazuia wanawake na wasichana kupata fursa.Zikiwa zimesalia siku mbili ya leo na kesho kufika tarehe 8 Machi Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tunaendelea kuangazia hali ya wanawake duniani. Sharon Jebiichi anatupeleka Ukraine kutukutanisha na Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini humo ambaye anaangazia madhila wanayokutana nayo wanawake wajawazito wa Ukraine.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake kwenye mkoa mmoja ulioko katikati mwa Tanzania.Na mashinani kesho Dunia ikiadhimisa siku ya kimataifa ya wanawake duniani tunakwenda nchini Kenya kusikia ujumbe wa mwanaharakati wa wanawake kuhusu uswa wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    12 min
  • Ukraine: Mwakilishi wa UNFPA Ukraine Uller Muller na hali ya wanawake wajawazito nchini humo
    Zikiwa zimesalia siku mbili ya leo na kesho kufika tarehe 8 Machi Siku ya Kimataifa ya Wanawake, tunaendelea kuangazia hali ya wanawake duniani. Sharon Jebiichi anatupeleka Ukraine kutukutanisha na Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini humo ambaye anaangazia madhila wanayokutana nayo wanawake wajawazito wa Ukraine.Ni Ulla Muller, Mwakilishi wa muda wa Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu UNFPA nchini Ukraine, akieleza kuhusu changamoto zinazowakumba wanawake wajawazito wa Ukraine.Anasema, “ninaweza kukuambia hadithi nyingi ambazo zimebaki nami kwa sababu nakutana na wanawake hawa kila mara, na mapenzi yangu kwao hayana mipaka.”Uller Muller anasimulia kisa cha mwanamke mmoja akisema,"Kuna mwanamke anayeitwa Ira ana umri wa miaka 31, na tayari anamlea mtoto mvulana wa umri wa miaka sita. Hivi karibuni aligundua kuwa ni mjamzito tena na anatarajia mapacha watatu. Ni hali ya kutisha na kuchanganya."Bi. Muller anaendelea kueleza kuwa mwanamke huyo alikuwa njiapanda asijue abaki alee ujauzito katika hali hiyo ya mabomu kila mahali au andoke? Hatimaye aliamua kubaki na kwa usaidizi wa UNFPA akafanikiwa kujifungua lakini kabla ya wakati. Uller Muller, anaitathimini hali hiyo akisema,"Faraja yake ya kuweza kujifungua salama iliakisi uthabiti wa akina mama wengi wa Kiukraine ambao wanaamua kutoondoka. Wanaamua kuwa bado wanapaswa kujenga mustakabali wa maisha yao. Bado wanapaswa kuishi maisha yaliyo karibu na hali ya kawaida kadri wawezavyo. Na hilo linajumuisha kuleta uhai katika hali ya vita."
    2 min
  • 06 MACHI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo Umoja wa Mataifa kupitia miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP nchini Tanzania, unaolenga kuhakikisha wanawake na wasichana wanajumuishwa kwenye mipango ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kwa kuwajengea uwezo.Kuelekea Siku ya Kimataifa ya Wanawake Machi 8, tathmini mpya ya Umoja wa Mataifa iliyowekwa wazi leo ikiangazia haki za wanawake miaka 30 baada ya Azimio la Beijing inaonesha uwepo wa maendeleo katika usawa wa kijinsia, kama vile sheria dhidi ya ubaguzi na sera jumuishi za kijinsia. Hata hivyo, ripoti hiyo inaeleza uwepo bado wa ubaguzi wa kijinsia uliojikita katika jamii, ukiendelea kuwazuia wanawake na wasichana kupata fursa.Ripoti nyingine ya Umoja wa Mataifa iliyochapishwa leo ikiangazia Sudan imefichua vitendo vya watu kukamatwa kiholela, mateso, na unyanyasaji huko Khartoum vinavyotekelezwa na Vikosi vya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) na pia Jeshi la Serikali ya Sudan (SAF). Ripoti hiyo imearifu pia kuwa makumi ya maelfu ya watu wamewekwa katika mazingira duni tangu Aprili 2023.Kutokana na kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu duniani, Umoja wa Mataifa leo jijini Geneva, Uswisi kutenga dola milioni 110 ili kusaidia majanga yaliyopuuzwa katika nchi 10 barani Afrika, Asia, na Amerika Kusini, zikiwemo Niger, Somalia, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Zambia.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “MCHAWI AKIFICHUA MIRIMO YA WACHAWI HU UAWA”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    11 min
  • Hali ya usalama ikidorora DRC, hofu sasa ni mustakabali wa watetezi wa haki za binadamu
    Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi. (Taarifa ya Anold Kayanda)Mary Lawlor akizungumza leo jijini Geneva-Uswisi amesema, "watetezi wa haki za binadamu mashariki mwa DRC wako hatarini sana kulengwa na kulipiziwa kisasi kwa kazi yao ya kutetea haki za binadamu. Wanahitaji msaada sasa, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa kuhamishwa kwa muda pamoja na familia zao.”Kundi la waasi la M23, limeendelea kusonga mbele katika eneo hilo la mashariki mwa DRC tangu lilipoanza mashambulizi yake mapema mwaka huu, na wale waliorekodi na kufichua ukiukwaji wa haki zao wamekuwa wakilengwa moja kwa moja, amesisitiza Bi. Lawlor."Katika wiki za hivi karibuni nimepokea taarifa nyingi za tahadhari zinazohitaji msaada na nimezungumza moja kwa moja na watetezi walioko mashinani," amesema Lawlor na kuongeza kuwa watu hao wanaishi kwa hofu na hatari ni halisi na kwama hivi karibuni, mtetezi mmoja alimpa taarifa kuwa waasi wa M23 wameandaa orodha ya watetezi wa haki za binadamu watakaokamatwa katika maeneo waliyoyadhibiti.Mtaalamu huyo  amesema amepokea ripoti za kuaminika za watetezi wa haki za binadamu kushikiliwa bila mawasiliano, kutoweshwa kwa nguvu, na kuteswa huko Rutshuru na Masisi, Kivu Kaskazini, huku takribani watetezi sita wa haki za binadamu wakiripotiwa kutoweka baada ya kujaribu kutoroka Goma baada ya jiji hilo kuchukuliwa na M23."Baadhi ya watetezi wa haki za binadamu hawakuwa na chaguo jingine ila kukimbia makazi yao. Wale wanaofanikisha kufika katika miji mingine wanakosa rasilimali za kupata malazi au kukidhi mahitaji yao ya kila siku," amesema na kwamba, "wengine wamebaki katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi lakini wana hofu kubwa kuhusu usalama wao. Mtetezi mmoja alimuuliza jinsi wanavyoweza kuendelea kujificha huku M23 ikianza kufanya ukaguzi huko Goma.Tangu magereza yalipovunjwa  huko Goma, Kalehe, Bukavu, na Uvira, maelfu ya wafungwa, wakiwemo wahalifu wakatili na viongozi wa makundi yenye silaha waliohukumiwa kwa ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaofikia uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, walitoroka na kuingia mitaani. Baadhi yao wanawatishia watetezi wa haki za binadamu waliotoa msaada wa matibabu, kisaikolojia na msaada wa kisheria kwa waathiriwa na mashahidi waliotoa ushahidi wakati wa kesi hizo. Na wakati huo huo watetezi wa haki za binadamu wakikabiliwa na vitisho na hofu ya kulipiziwa kisasi, waathiriwa hawana wa kuwategemea, ameeleza mtaalamu huyo.Katika mazingira ambayo tayari ni magumu kwa watetezi wa haki za binadamu, Mtaalamu huyo maalumu wa Umoja wa Mataifa anasisitiza hatari kubwa ya ukatili wa kingono inayowakabili watetezi wa haki wa kike."Tunajua kuwa ukatili wa kingono unaohusiana na migogoro mashariki mwa DRC ni wa kiwango cha juu, na kwamba wanawake wanaopinga ukiukwaji wa haki za binadamu katika muktadha huu, na wanaojitokeza kwa kazi yao, mara nyingi ndio wanaoathirika zaidi," Lawlor amesema akiongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kufikiria kwamba miaka 25 tangu kupitishwa kwa azimio la kihistoria la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake, amani na usalama, matukio haya yanatokea mbele ya ulimwengu unaoonekana kutokuwa na msimamo thabiti.Mtaalamu huyo pia ameelekeza umakini kwa hatari wanazokabiliana nazo watetezi wa haki za binadamu katika maeneo ya vijijini na yaliyojitenga, ikiwa ni pamoja na mauaji, kutoweshwa kwa nguvu, na utekaji nyara, na akaangazia athari za kisaikolojia zinazowakumba wale walioko mashinani."Watetezi tayari walikuwa wakikabiliwa na vitisho katika eneo hilo – kutoka kwa serikali na makundi yenye silaha  lakini kama alivyonieleza mtetezi mmoja wa haki za binadamu wa…
    2 min
  • Miaka 30 baada ya Azimio la Beijing kuhusu haki za wanawake, safari bado ni ndefu
    Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa  shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawake hazipaswi tu kukumbukwa bali zinahitaji kutekelezwa kikamilifu. Flora Nducha anafafanua zaidiAkizungumza wiki hii mjini Geneva Uswisi katika majadiliano ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 30 ya Azimio la Beijing (#Beijing30), Bi. Bahous amebainisha umuhimu wa kuharakisha maendeleo ya usawa wa kijinsia akiwataka viongozi wa dunia kuchukua hatua thabiti ili kuhakikisha haki za wanawake zinapewa kipaumbele wakati wa changamoto zinazoendelea duniani.Amesema “Miaka 30 iliyopita dunia iliweka ahadi ya kusongesha fursa na utu wa wanawake na wasichana wote. Ahadi hiyo haikuwa maneno matupu kwenye karatasi, ilikuwa ramani ya njia na wito wa mshikamano . Na kwa miongo mitatu imechochea hatua, wasichana wengi sasa wako shule, wanawake wengi wako bungeni , kuna sheria nyingi zaidi zinawalinda wanawake dhidi ya ukatili, na mataifa mengi zaidi yanatambua usawa wa kijinsia ni lazima.”Licha ya mafanikio hayo yote Bi, Bahous amesema ndio kwanza mkoko unaalika maua kwani safari bado ni ndefu“Hebu tuwe wakweli hatujafika tunapopaswa kuwa. Haki za wanawake na wasichana zinashambuliwa, fursa za wanawake kupaza sauti zinazidi kupungua na endapo tutaendelea na kasi hii msichana aliyezaliwa leo atakuwa na umri wa miaka 39 kabla wanawake hawaja na viti vingi bungeni kama wanaume, atakuwa na umri wa miaka 68 kabla ndoa za utotoni hazijakomeshwa, na atakuwa na umri wa miaka 137 kabla umasikini uliokithiri kwa wanawake na wasicha haujatokomezwa. Hatuwezi kulikubali hili.”Mkuu huyo wa UN Women ameyahimiza mataifa yote kuchukua hatua sasa ili kuhakikisha ndoto za azimio la Beijing hazisalii kuwa ndoto bali maisha halisi.
    3 min
  • 05 MACHI 2025
    Hii leo jarida linamulika wasiwasi kuhusu hali ya watetezi wa haki za binadamu nchini DRC, wakati huu hali ya usalama si shwari mashariki mwa nchi; kuelekea siku ya wanawake duniani, Mkuu wa UN Women arejelea Azimio la Beijing; vilabu vya Dimitra  nchini DRC vinavyosaidia wanawake na wanaume kuketi pamoja na kutatua changamoto zinazowakabilia; mashinani ni Ramadhani huko Gaza.Hali ya kibinadamu ikiendelea kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mtaalamu Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na hali ya watetezi wa haki za binadamu, Mary Lawlor leo ametoa wito wa msaada wa dharura na wa vitendo kwa watetezi wa haki za binadamu katika eneo hilo. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Kuelekea siku ya wanawake duniani itakayoadhimishwa mwishoni mwa wiki hii ambayo ni tarehe 8 mwezi Machi, Mkurugenzi Mtendaji wa  shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women, Sima Bahous, amesisitiza kwamba ahadi zilizowekwa kwenye Azimio la Beijing miaka 30 iliyopita kuhusu haki za wanawake hazipaswi tu kukumbukwa bali zinahitaji kutekelezwa kikamilifu. Flora Nducha anafafanua zaidiMakala inakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambako mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) ulioanzishwa kati ya mwaka 2008 hadi 2023 umeleta mabadiliko chanya ukiimarisha usawa wa kijinsia. Mwenyeji wako ni Sharon Jebichii.Ibrahim Al-Ghandour, mpalestina huyu akiwa eneo la Gaza mbele ya nyumba yake iliyogeuzwa kifusi kutokana na mashambulizi ya Israeli akielezea maoni yake ya mfungo unaoendelea wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners