Kwenye kikao cha 58 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kinachoendellea mjini Geneva Uswisi, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa M ataifa, Volker Türk , amezungumzia hali ya kuzorota na kutoeleweka inayohusu haki za binadamu duniani kote akielezea wasiwasi mkubwa kuhusu kudhoofika kwa makubaliano ya kimataifa kuhusu haki za binadamu,na kuonya kwamba ushawishi wa viongozi wa kiimla, matajiri wakubwa, na viongozi wa kimabavu unatishia kuvuruga maendeleo ya miongo kadhaa. Anold Kakayanda na taarifa kamili.Asante Flora katika taarifa yake Türk amesisitiza umuhimu wa kuhifadhi haki za binadamu na utawala wa sheria ili kuzuia kurudiwa kwa ukatili wa zamani.Moja ya masuala ya dharura yaliyotiliwa mkazo na Türk ni mgogoro wa kibinadamu unhaoendelea huko Gaza. Amelaani uharibifu uliosababishwa na hatua za kijeshi za Israeli dhidi ya mashambulizi ya Oktoba 7, 2023 yaliyofanywa na Hamas na makundi mengine ya wapiganaji wa Kipalestina.Türk amesisitiza haja ya kudumisha usitishaji mapiganona kutoa wito wa mchakato wa amani unaozingatia haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na haki ya kujitawala na uwajibikaji. Ametaka kuachiliwa kwa mateka, kukomeshwa kwa vizuizi vya kiholela, na kuanza tena kwa msaada wa kibinadamu mara moja ndani ya Gaza.Kuhujsu mgogoro unaoendelea nchini Ukraine amersema bado ni suala la kutia wasiwasi, huku raia wakiishi kwa hofu ya mara kwa mara kutokana na mashambulizi yasiyokoma.Türk amekemea vikali vikwazo vya Shirikisho la Urusi juu ya haki za msingi katika maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na kuelezea masikitiko yake kuhusu ripoti za mauaji ya kiholela na mateso ya kimfumo ya wafungwa wa vita wa Kiukraine.Almeihimiza jumuiya ya kimataifa kufanya kazi kuelekea amani endelevu inayoheshimu haki na matarajio ya watu wa Ukraine.Türk pia ameelekeza mawazo kwenye maeneo mengine yenye migogoro, ikiwa ni pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Myanmar, Haiti, na Sudan.Alielezea jinsi watawala wa kiimla, wanasiasa wahubiri wa chuki, na walanguzi wanavyotumia machafuko kwa faida zao binafsi.Amesema Athari za migogoro huenea zaidi ya mstari wa mbele, zikiathiri minyororo ya usambazaji duniani na nafasi za kidijitali.Ametoa wito kwa watu binafsi kutambua jukumu lao la pamoja kwa kufanya maamuzi ya kimaadili ya ununuzi, kushiriki kisiasa, na kuunga mkono uwajibikaji kwa ukiukwaji wa haki za binadamu.Hata hivyo amesema demokrasia zilizoimarika haziko salama dhidi ya kudorora kwa haki za binadamu. Türk ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mwelekeo nchini Marekani, ambako maendeleo kuhusu usawa wa kijinsia na sera za kupinga ubaguzi yanarudi nyuma.Pia amekosoa Shirikisho la Urusi kwa ukandamizaji wake wa jamii za kiraia na vyombo vya habari huru, ambapo wapinzani wanakabiliwa na unyanyasaji, kukamatwa, au kufurushwa.Kudhoofika kwa haki za binadamu katika mataifa yenye nguvu, Türk alionya kwamba kunaweka mfano hatari kwa ulimwengu mzima, akisisitiza hitaji la dharura la mshikamano wa kimataifa na uwajibikaji kuhusu ha\ki za binadamu.