Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Ukraine: Miaka 3 ya kumbukumbu mbaya, juhudi zifanyike mzozo uishe - Guterres
    Mkutano wa 58 wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu umeanza leo jijini Geneva, Uswisi ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezungumzia kiza kilichotanda duniani hivi sasa kutokana na mapigano  yanayoendelea sehemu mbalimbali kuanzia Ukraine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC  hadi Ukanda wa Gaza, yakiambatana na ukiukwaji mkubwa wa haki, akitaka kila juhudi zichukuliwe kusaka amani ya kudumu. Selina Jerobon na taarifa kamili..
    3 min
  • Maelfu wavuka mto Rusizi kwa mtumbwi kutoka DRC na kuingia Burundi ili kuokoa maisha yao
    Maelfu ya watu wanawasili nchini Burundi, wakikimbia mapigano yanayozidi kushamiri huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hususan katika majimbo ya Kivu Kusini na Kivu Kaskazini. Waasi wa M23 wanaendelea kupanua wigo wa maeneo wanayomiliki, hali inayotumbukiza raia kwenye changamoto za usalama, na kulazimu wale wanaoweza kukimbia. Wengine wameuawa, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, na majeruhi wako hospitalini ambako huduma nazo zimedorora kwani M23 wamefunga barabara katika maeneo yote wanayodhibiti. Lakini wale wanaokimbilia Burundi hali yao iko vipi? Evarist Mapesa anakusimulia zaidi kupitia video iliyoandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.
    6 min
  • 21 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia mahitaji ya wakimbizi wanaokimbia machafuko DRC wakielekea nchini Burundi, na hali ya wakimbizi wa ndani Gaza wakati huu wa msimu wa baridi. Makala tunakurejesha nchini DRC na mashinani tunakwenda nchini Tanzania.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR limetoa ombi la dola milioni 40.4 ili kujiandaa na kutoa huduma za kuokoa maisha na usaidizi kwa wakimbizi wa ndani na waliokimbilia nchi jirani baada ya wakati huu ambapo mashambulizi ya waasi wa M23 yanazidi kufurusha raia kutoka Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Congo, DRC.Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, familia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya.Katika makala Evarist Mapesa anakupeleka eneo la mpakani mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, na Burundi kufuatilia mmiminiko wa wakimbizi kutoka DR Congo.Na mashinani fursa ni yake Regnihadah Mpete kutoka Tanzania ambaye anatumia kiswahili, lugha ya taifa nchini Tanzania kufundisha vikundi vya wanawake wilayani Biharamulo, mkoani Kagera jinsi ya kujikinga na magonjwa. Mafunzo serikali  kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) kupitia TIP ambao ni Mtandao wa Madhehebu ya Dini mbalimbaliMwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    12 min
  • Watoto watota kwa mvua katika ukanda Gaza, huku baridi kali ikitishia afya zao
    Huko Gaza Kaskazini, kwenye eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli, wanafamilia zilizofurushwa makwao kutokana na vita kati ya Israeli na wanamgambo wa Hamas wanavumilia msimu wa baridi kali katika makazi ya muda ya mahema yanayopigwa na upepo na mvua usiku na mchana, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF. Nyumba zao zimeharibika na kuacha watoto kuishi katika mazingira mabaya. Ni sauti ya watoto wakitembea katikati ya mahema ya muda kwenye vichochoro vilivvyojubikwa na matope, hapa Gaza Kaskazini, huku wakijaribu kukwepa madimbwi ya maji yaliyosababishwa na mvua kubwa.Kupitia video iliyoandaliwa na UNICEF, Shahd Omar, msichana mwenye umri wa miaka kumi na saba, anaonekana amembeba nduguye, wengine wanaonekana wamekujikunyata kutokana na baridi. Shahd sasa akiwa amesimama nje hema lao anaelezea jinsi nyumba zao zilivyoharibiwa.“Tunavumilia hali ngumu sana,mvua kubwa, baridi, na upepo mkali, maisha ni magumu sana. Nyumba yetu ilivyoshambuliwa na kubomoka tulijitoa kwenye vifusi. Nyumba yetu imeharibika, hatuna samani, hakuna vituo vya kujikinga, wala mahali pa kukaa ili kupata joto. Maisha ni magumu. Hema letu lilikuwa karibu kupeperuka kwa sababu ya upepo mkali.”Kwingineko hapa, watoto wanaonekana wakicheza kwenye matope nje ya mahema zao huku maji yakitiririka kama mto. Layla Abu Asi ni mama wa watoto watatu, mwenye umri wa miaka 27 anasema,“Baridi hii ni kali mno, haiwezi kuvumilika ,upepo huu mkali umeleta madhara makubwa kwenye hema letu. Tangu asubuhi, maji ya mvua yamejaa kwenye hema letu, kila kitu kilichomo ndani kikilowa na kujaa maji. Watoto wangu wametota kwa maji ya mvua. Hii ni hali mbaya zaidi ambayo tumewahi kukumbana nayo.”UNICEF na wadau wanafanya kila wawezalo kuwasaidia wakazi wa Gaza.
    3 min
  • 20 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani mada kwa kina ikimulika harakati za uhamasishaji kabla na baada ya maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani iliyoadhimishwa hivi karibuni na mchango wa redio katika juhudi za uhifadhi wa mazingira na kuchagiza maendeleo ya jamii huko Ramogi nchini DRC. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa maneno.Idadi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC walioingia Burundi kufuatia mashambulizi yanayofanywa na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, mashariki mwa DRC sasa imeongezeka na kufikia 20,000.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani, WFP kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter, limechapicha picha zikionesha wakimbizi walio njiani wakipikiwa chakula, wakati huu ambapo M23 wametwaa miji ya Goma jimboni  Kivu Kaskazini, na Bukavu na Kamanyola jimboni Kivu Kusini.Na katika hatua nyingine ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ikipatiwa jina UNJHRO imeripoti jinsi kutoroka kwa wafungwa kwenye gereza la Goma jimboni Kivu Kaskazini kulivyoleta hofu na mashaka kwenye jamii.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili Mlumbi wa Lugha Joramu Nkumbi kutoka Tanzania anafafanua upatanisho wa kisarufi wa baadhi ya maneno.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    11 min
  • Tanzania yataja mambo ya kuzingatiwa ili ulinzi wa amani uwe na tija
    Historia ya ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa ulianza miaka mitatu tu baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa wenyewe. Na kutokana na umuhimu wa ulinzi wa amani kote duniani, shughuli hiyo imedumu kwa miaka yote hiyo 77 hadi sasa na bado ni muhimu lakini inaendelea kukumbwa na changamoto kama anavyofafanua Brigedia George Mwita Itang’are wa Tanzania, moja ya nchi 10 duniani zinazochangia zaidi vikosi vya ulinzi wa amani.
    4 min
  • OCHA yasihi kufunguliwa kwa viwanja vya ndege Goma na Kavumu - DRC
    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
    2 min
  • 19 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia msaada wa kibinadamu nchini DRC, na simulizi y amkimbizi wa DRC aliyekimbilia nchini Uganda. Makala inatupeleka nchini Tanzania, namashinani nchini Kenya, kulikoni?Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa likifanya kikao cha dharura jijini New York, Marekani kujadili hali ya usalama inayozidi kuzorota kila uchao huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya kibinadamu nchini humo, Bruno Lermaquis amesema kupanuka kwa mzozo huo kumezidi kugharimu maisha na mustakabali wa raia.Sina mpango tena wa kurejea nyumbani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ni kauli yake Twagirayesu Gato, mwanafunzi huyu raia wa DRC aliyekimbia  nchini mwake mwaka jana na kuingia Uganda ambako sasa anapata hifadhi. Amesema hayo kwenye video ya shirika la Umoja wa MAtaifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR iliyochapishwa katika ukurasa wa YouTube wa shirika hilo.Makala inatupeleka nchini Tanzania ambako tunamsikiliza Brigedia Jenerali George Mwita Itang’are, Mkuu wa Kituo cha Mafunzo ya Ulinzi wa Amani cha Tanzania (TPTC) akitoa wito kwa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa kuendelea kuunga mkono ulinzi wa amani duniani kwa kuzikabili changamoto wanazokutana nazo walinda amani. Anold Kayanda anasimulia.Na mashinani ikiwa hivi majuzi Dunia iliadhimisha siku ya redio duniani fursa ni yake Irene munyua kutoka Kenya akieleza washirika wetu Radio Domus kuhusu umuhimu wa radio kwa jamii katika maisha ya kila siku.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners