Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 13 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kumulika siku ya redio duniani, maudhui yakiwa Radio na Tabianchi, na ni kwa vipi chombo kinachodaiwa kutwamishwa na maendeleo ya teknolojia kinaendelea kusaidia kuelimisha umma kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabianchi, Teonas Aswile wa TBC Taifa nchini Tanzania anaeleza.Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC ambapo hali inazidi kuwa tete na leo Mkurugenzi Mtendaji wa shirkika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, Catherine Russell, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa ghasia mashariki mwa mwa  nchi hiyo katika majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, ambapo watoto na familia wanakabiliwa na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.Naibu mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masiala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA nchini Sudan Edmore Tondhlana akizungumza na UN News amesema hali nchini Sudan inaendelea kuwa janga la kibinadamu wakati vita ikishika kasi na watu wakiendelea kufurushwa makwao. Amesema "Tunashuhudia hali ambapo Sudan ina mahitaji ya kibinadamu yaliyo miongoni mwa makubwa zaidi duniani. Takriban watu milioni 30 wanahitaji msaada wa kibinadamu. Hili ni ongezeko la takriban watu milioni tano zaidi ikilinganishwa na mwaka uliopita, pia, Sudan ina idadi kubwa zaidi ya watu waliopoteza makazi yao.Na leo ni siku ya Redio Duniani mwaka huu ikibeba maudhui Redio na mabadiliko ya tabianchi. Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO lengo la maudhui haya ni kudhihirisha jukumu la redio katika kusambaza ujumbe na kuelimisha kuhusu changamoto za mabadiliko ya tabianchi, kutanabaisha kuhusu hatua endelevu na kuwapa sauti wanaharakati wa mabadiliko ya tabianchi.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa      nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno “MSUMBI”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    12 min
  • Akibomoa kibanda chake Goma DRC, mkimbizi asema ana hofu kurejea Saké
    Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo.Miongoni mwao ni Kibira Bakulu, baba wa watoto 5, aliyekimbia mapigano eneo la Saké, mwezi Februari mwaka jana, takriban kilomita 10 kutoka Goma.Akiwa katika harakati za kubomoa kibanda chake katika kambi ya nane ya CEPAC Mugunga huko Goma, Bwana Bakulu anasema walishangaa, bila kuwa tayari, kuambiwa warudi walikotoka."Tumepatiwa saa 72 tuwe tumeondoka na kurejea Saké, kwani vita vimeisha. Sisi hatua uhakika kamili kwa sababu tuliondoka Saké kutokana na vita. Kama inabidi kusukumwa tuondoke, hatuna la kuchagua,” amesema Bwana Bakulu.Ana hofu ya kurejea Saké, akisema, “kule tulikuwa tunaishi Sake na tukirejea tutaishi vipi? Tunaomba viongozi wajitahidi watusaidie ili watuhakikishia usalama.Alipoeleza hali halisi amesema, “ hii siku ya leo hapa unaniona, watu wamepita hapa wakifanya vurugu, wananyang’anya kila kitu ulichonacho, iwe simu wanabeba. Sasa tunashindwa kufahamu amani iko katika kiwango gani?”Kwa mujibu wa Bwana Bakulu, walishaamua kuwa hawataweza kurudi na kama ni kufa basi watafia Goma, lakini sasa wamelazimishwa kurejea Saké.
    2 min
  • Wakimbizi Goma waanza kufungasha virago huku wakiwa na hofu
    Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea. Miongoni mwao ni Kibira Bakulu, baba wa watoto 5, aliyekimbia mapigano eneo la Saké, mwezi Februari mwaka jana, takriban kilomita 10 kutoka Goma.
    2 min
  • 12 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia matokeo ya maandamani nchini Bangladesh, na machafuko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Makala inatupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na ofisi ya haki za binadamu (OHCHR) imefichua kuwa viongozi wa juu wa serikali ya Bangladesh walihusika moja kwa moja katika ukandamizaji wa maandamano makubwa yaliyoitikisa nchi hiyo mwaka 2024 na kusababisha vifo vingi.Baada ya waasi wa M23 jimboni Kivu Kaskazini, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupatia wakimbizi waliokuwa wamesaka hifadhi kambini mjini Goma, wawe wamerejea makwao ndani ya saa 72 kuanzia juzi jumatatu, mamia wameanza kutii amri hiyo licha ya hofu inayowakabili ya kule wanakotakiwa kurejea.Makala inatupeleka jijini Nairobi, Kenya ambako ambako Kevin Keitany wa redio washirika wetu Domus FM kwa kuzingatia kuwa kesho Februari 13 ni Siku ya Kimataifa ya Redio, ametutumia maoni ya vijana wawili wanaozungumzia namna redio imewasaidia kusambaza ujumbe wao kuhusu hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Mashinani fursa ni yake Tupokigwe Simon, msichana      mwenye  umri wa miaka 16, ambaye ni mwanaharakati wa  Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na hisabati , STEM, wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, akieleza umuhimu wa  msichana katika sayansi na kuwahimiza wasichana wenzake kusoma  sayansi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    10 min
  • 11 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Uganda kumulika ni kwa nini Uganda imekivalia njuga Kiswahili akieleza mwandishi wetu wa Uganda John Kibego ambaye amezungumza na mwandaaji mwenza wa kongamano hilo Dkt. Kisembo Ronex Tendo, Mkurugenzi wa shirika la Afrika Mashariki Fest.Umoja wa Mataifa na wadau wanasalia na wasiwasi mkubwa kufuatia amri iliyotolewa Jumatatu na waasi wa M23 huko jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ya kupatia wakimbizi wa ndani saa 72 wameondoka kwenye kambi mjini Goma na viunga vyake, na kurejea vijijini mwao.Katika Ukanda wa Gaza ambako Rolando Gomez, Mkuu wa Mawasiliano kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Geneva Uswisi, amezungumza na waandishi wa habari akimnukuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akisema lazima kuepusha gharama zozote zinazoweza kuibuka iwapo uhasama utaanza upya Gaza kwani italeta janga kubwa.Na akihutubia viongozi huko Paris Ufaransa kwenye mkutano wa Kuchukua Hatua kwa Akili Mnemba ili inufaishe wote, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesisitiza udharura kwa dunia kuwa tayari kukabiliana na changamoto zitokanazo na teknolojia hiyo iliyo mikononi mwa wachache licha ya kuleta mapinduzi kwenye sekta lukuki kama vile elimu, afya, na kilimo.Mashinani mashinani fursa ni yake Tiphaine Lucas, mwanamke Mratibu wa Mpango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo, FAO kuhusu kutegua mabomu na Ukarabati wa Ardhi nchini Ukraine, akitumia sayansi na teknolojia kukagua sampuli za udongo katika ardhi ya Kiukreni ya kilimo iliyoathiriwa na mabaki ya vita na silaha zilizolipuka, sehemu kuu ya kazi yake hatarishi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    11 min
  • Kakuma - Je, unafahamu kwamba nyenje ni chanzo cha protini?
    Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, kutokana na ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kundi la vijana wanajishughulisha na ufugaji wa wadudu nyenje (Crickets) ili kukabiliana na changamoto ya utapiamlo miongoni mwa watoto wachanga. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners