Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 05 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama Goma DRC, na masuala ya haki za binadamu. Makala na mashinani inaturejesha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kufuatilia simulizi za wakimbizi wa ndani.Maisha yanarejea katika hali ya kawaida huko Goma baada ya siku kadhaa za mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (FARDC) na waasi wa M23 mashariki mwa. Mwandishi wetu wa habari jimboni Kivu Kaskazini amesema kwamba shughuli zinaanza tena katika mji wa ziwa la Kivu, Goma, wakati M23 imechukua wilaya nyingi za mji mkuu wa Jimbo hili.Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa (OHCHR) imesisitiza haja ya kusonga mbele kuelekea awamu inayofuata ya usitishaji mapigano huko Gaza, kuachiliwa kwa mateka na wafungwa wote waliokamatwa kiholela, kukomesha vita na kujenga upya Gaza, kwa kuheshimu kikamilifu sheria ya kimataifa ya kibinadamu na sheria za kimataifa za haki za binadamu.Makala leo inakukutanisha na Mwamini Sebororo mmoja wa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC waliopoteza makazi yao na kila kitu katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki ya taifa hilo huku mgogoro ukiendelea kufurusha watu zaidi, akiwa kambini Bushagara anasimulia kilichomsibuNa katika mashinani tutarejea nchini Jamhuri wa Kidemokrasia ya Congo DRC kusikia ujumbe wa mkimbizi wa ndani ambaye ni mwathirika wa vita Goma.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min
  • M23 wasitisha mapigano
    Maisha yanarejea katika hali ya kawaida huko Goma baada ya siku kadhaa za mapigano kati ya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (FARDC) na waasi wa M23 mashariki mwa. Mwandishi wetu wa habari jimboni Kivu Kaskazini amesema kwamba shughuli zinaanza tena katika mji wa ziwa la Kivu, Goma, wakati M23 imechukua wilaya nyingi za mji mkuu wa Jimbo hili. Alikutana na Muhindo Kibwana muendesha pikipiki akiwa kwenye maegesho yake ya kazi, jina lake limebadilishwa kwa usalama wake.
    2 min
  • 04 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kushuhudia sintofahamu na maombi ya wakazi wa Goma baada ya waasi wa M23 kutwaa mji huo. Mashinani tunakwenda Somalia na pia tunakuletea muhutasari wa habari.Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Bruno Lemarquis, ametoa wito wa kufunguliwa haraka kwa Uwanja wa Ndege wa Goma. Amesema uwanja huu uliofungwa kutokana na mapigano kati ya vikosi vya jeshi la DRC na waasi wa M23 ni muhimu kwa usafirishaji wa misaada ya kibinadamu. Hospitali zimejaa na maelfu ya raia hawana msaada wa dharura.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la idadi ya watu na afya ya uzazi, (UNFPA), na la misaada ya kibinadamu na dharura (OCHA) leo yamesisitiza kuwa kusitishwa kwa ufadhili wa Marekani kunawaacha mamilioni 'hatarini'. Hayo yakijiri tayari imefahamika kuwa Rais Donald Trump anaiondoa Marekani katika Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu na pia kuacha kulifadhili shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina.Na ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Saratani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limeeleza kiasi takwimu kuhusu ugonjwa huo kwamba mathalani  kwa mwaka 2020 saratani ilisababisha vifo karibu milioni 10 sawa na kifo kimoja kati ya sita duniani. Aidha WHO imebainisha kuwa saratani zinazojitokeza zaidi ni saratani ya matiti, mapafu na utumbo mpana.Na katika mashinani  fursa ni yake Safiya Jeylaani, mkazi wa Barawe katika Jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia ambye baada ya kuhudhuria hafla ya kujadili umuhimu wa upatikanaji wa huduma za afya kwa Wasomali wote katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu iliyoandaliwa na Umoja wa Mataifa anasema jamii wanapaswa kuelimishwa kuhusu afya kutumia lugha mama.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!  
    10 min
  • UNFPA - Wakimbizi zaidi ya 18,000 wa Sudan sasa wanaishi katika kambi ya Korsi CAR
    Vita inayoendelea Sudan kwa zaidi ya miezi 18 sasa inaongeza wimbi la wakimbizi ndani na nje ya nchi kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA. Shirika hilo linasema takriban wakimbizi 18,000 waliokimbia vita Sudan hivi sasa wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Korsi katika eneo la Birao, jimbo la Vakaga Katikati Mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR ambako UNFFPA inawapatia huduma muhimu zikiwemo za aya ya uzazi. Flora Nducha anatujuza zaidi katika makala hii
    1 min
  • Maandamano huko Goma DRC, wakimbizi waomba UN iwafikishie misaada
    Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi
    4 min
  • Tutafute majadiliano badala ya kugawanyika - Guterres
    Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
    2 min
  • 03 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC, na ujumbe wa Katibu Mkuu wa UN kuhusu Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu. Makala inatupeleka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na mashinani tunarejea DRC, kulikoni?Ikiwa ni wiki moja sasa tangu waasi wa M23 watangaze kutwaa Goma, jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, na kisha serikali kutangaza Beni kuwa mji mkuu wa sasa wa jimbo hilo, hii leo Jumatatu Februari 3, maandamano makubwa ya amani yamefanyika mjini Beni, yakiongozwa na mashirika ya kiraia na wananchi.Ikiwa kesho Februari 4 ni Siku ya Kimataifa ya Udugu wa Kibinadamu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres,kupitia ujumbe mahususi kwa ajili ya siku hii ametoa wito wa kuimarisha umoja, usawa, na kuheshimiana katika kipindi hiki cha ongezeko la ubaguzi na kutovumiliana duniani.Makala inatupeleka Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, kwenye kambi ya wakimbizi ya Korsi inayohifadhi zaidi ya wakimbizi 18,000 kutoka Sudan wengi wakiwa ni wanawake na watoto na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA linawasaidia.Na katika mashinani  Lodja Salizre, Mkimbizi wa ndani katika kambi ya Loda jimboni Ituri kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemocrasia ya Congo DRC akileleza ni kwa jinsi gani vita inayoendelea vimeameathiri yeye na familia yake na jinsi ambavyo uwepo wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo inavyosaidia maisha ya kila siku ya wakazi wake.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    10 min
  • Hali ni tete mashariki mwa DRC, msaada wa kibinadamu haufikii wahitaji - Mashirika
    Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kutoa wito wa kurejeshwa kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kwani hali inazidi kuwa tete na kuuzidi uwezo wa mashirika hayo kusaidia. Selina Jerobon amefuatilia matamko ya mashirika hayo na kutuandalia taarifa ifuatayo. Janga la haki za binadamu katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) linaendelea kuzidi kuwa baya kutokana na ripoti zinazonyesha kuwa kundi la wapiganaji la M23 limeendelea kusonga kusini kuelekea Bukavu, imeeleza Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa (OHCHR) leo Januari 31 mjini Geneva, Uswisi.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) katika taarifa iliyotolewa katika mji Mkuu wa DRC, Kinshasa, limesema licha ya juhudi hizo zinazoendelea ili kusaidia watu, kuongezeka kwa ghasia kumelazimisha IOM na mashirika mengine ya kibinadamu kusitisha operesheni katika maeneo yaliyoathirika zaidi, na hivyo kusitisha msaada wa kuokoa maisha kwa maelfu ya watu.Kwa upande wake Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeeleza wasiwasi wake kuhusu ugumu wa ufikiaji wa wanaohitaji msaada mashariki mwa DRC.Msemaji wa WFP DRC, Shelley Thakral leo Januari 31 akiwa jijini Kinshasa DRC anasema, "kwa kweli watu wanakosa chakula, maji safi, vifaa tiba na huo ni wasiwasi mkubwa kwa hivyo mnyororo wa usambazaji umenyongwa kwa sasa ikiwa unafikiria kuhusu ufikiaji kwa njia ya ardhi, anga, wakati kila kitu kimefungwa. Kwa hivyo kipaumbele chetu cha kwanza ni wazi ni usalama wa wafanyakazi. Tunataka kurejea kwenye shughuli zetu mara tu usalama utakapoturuhusu.”
    2 min
  • Umeme wa uhakika wanufaisha wanafunzi na jamii nchini Senegal
    Senegal, taifa lenye watu zaidi ya milioni 18.5 liko kwenye mwelekeo wa kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya umeme. Benki ya Dunia inasema kiwango cha kupata umeme kwenye taifa hilo sasa ni asilimia 84. Wakati huu ambapo asilimia zaidi ya 30 ya jamii za vijijini hazina huduma hiyo, serikali kwa kushirikiana na wadau kama vile Benki ya Dunia na sekta binafsi imechukua hatua na mabadiliko yameanza kuonekana. Je ni yapi? Assumpta Massoi anaelezea kwenye makala hii.
    4 min
  • 31 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya usalama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na tutakuletea simulizi ya wakimbizi wa ndani nchini humo. Makala inatupeleka nchini Senegal na mashinani nchini Afghanistan, kulikoni?Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameendelea kutoa wito wa kurejeshwa kwa amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo (DRC) kwani hali inazidi kuwa tete na kuuzidi uwezo wa mashirika hayo kusaidia..Kutana na mkimbizi Masimango Mango kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ambaye kwa sasa anaishi kwenye makazi ya wakimbizi wa ndani ya Lushagara Goma jimboni Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC, anasema kwa hakika vita imemchosha na anacholilia ni amani ili arejee nyumbani na familiia yake.Makala tunakwenda Senegal, magharibi mwa AFrika ambako nishati ya umeme imeleta mabadiliko makubwa kwenye kijiji ambacho awali kiligubikwa na kiza nyakati za usiku.Na katika Zulaikha kutoka Afghanistan ambaye ana matumaini katika msimu huu wa baridi kutokana na msaada wa fedha kutoka Shirika la Marekani la Misaada ya kimaendeleo USAID na lile la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda karibu!  
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners