Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 27 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini DRC yanosababishwa na kundi la waasi la M23 mjini Goma. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kukumbuka waathiriwa wa mauaji ya halaiki tutasikia ujumbe wa Umoja wa Mataifa.Hali ya usalama kwenye mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ikiendelea kuwa tete, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, nchini humo, MONUSCO pamoja na SAMIDRC ambao ni ujumbe wa kulinda amani kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC wanadhibiti uwanja wa ndege wa Goma.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO kwa kushirikiana na polisi wa kitaifa wa nchi hiyo  PNC wameongeza doria katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bushagara jimboni Kivu Kaskazini kufuatia ongezeko la vitisho na mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa M23.Katika makala Anold Kayanda anatupeleka nchini Tanzania ambako katika kuhamasisha elimu iliyo salama inayolenga kumlea na kumfundisha mtoto kwa njia chanya zisizoumiza, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, (UNICEF) linamuangazia Mwalimu Magesa Stanslaus ambaye ambaye amebadilika kutoka katika matumizi ya viboko na sasa anatumia motisha tofauti kuwarekebisha wanafunzi wake.Na mashinani fursa ni yake Miguel Ángel Moratinos, Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Muungano wa Ustaarabu Umoja wa Mataifa UNAOC akitoa ujumbe kuhusu mauaji ya halaiki na sheria za kimataifa za haki za binadamu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    10 min
  • Hali tete ikiendelea Goma DRC, MONUSCO/SAMIDRC wadhibiti uwanja wa ndege
    Hali ya usalama kwenye mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini, Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, ikiendelea kuwa tete, ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, nchini humo, MONUSCO pamoja na SAMIDRC ambao ni ujumbe wa kulinda amani kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika, SADC wanadhibiti uwanja wa ndege wa Goma. Ripoti ya Selina Jerobon inafafanua zaidi.
    3 min
  • Akili Mnemba haikwepeki, tuiwezeshe ili ituwezeshe kwa manufaa ya walimu na wanafunzi - Walimu
    Akili Mnemba au AI inakuja kwa kasi kubwa sana na kubadilisha mwenendo wa walimu na wanafunzi darasani. Inaleta fursa za kipekee kama kufundisha kwa njia ya kibinafsi na upangaji wa masomo wenye ufanisi zaidi. Lakini pamoja na zana hizi, changamoto zimeibuka: kutegemea sana teknolojia hii, masuala ya kimaadili, na kupungua kwa ujuzi wa kusoma kwa kina. Walimu wanajifunza jinsi ya kuendesha mabadiliko haya, wakiwaonesha wanafunzi jinsi ya kutumia AI kama mshirika wa kufikiri badala ya njia ya mkato ya kuuliza na kunakili. Ubunifu na kufikiri kwa kina vinabaki kuwa ujuzi muhimu zaidi, ambao hakuna teknolojia inayoweza kuchukua nafasi yake. Je, walimu wana mawazo gani? Assumpta Massoi anakupeleka Paris, Ufaransa kusikia mazungumzo ya walimu wawili wakijadili mustakabali wa Akili Mnemba kwenye ufundishaji. 
    4 min
  • Safari yangu Kyrgyzstan ilikuwa ya matumaini na elimu: Suhaila
    Katika siku ya Elimu duniani kutana na Suhaila msichana mkimbizi kutoka Afghanistan ambaye kupitia mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi  UNHCR wa kuwahamishia wakimbizi katika nchi ya tatu aliwasili Jamhuri ya Kyrgyzstan ambako sio tu alipata maskani ya kudumu na wazazi wake bali pia matumaini na elimu iliyompa ari ya kurejesha matunda yake nyumbani alikotoka. Flora Nducha na taarifa zaidi.
    3 min
  • 24 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini DRC, na katika elimu tunamsikia msichana wa Afghanistan ambaye ni mnufaika wa ufadhili wa Umoja wa Mataifa. Makala inatupeleka nchini Oaris kumulika matumizi ya AI katika elimu na mashinani tunakwenda nchini Sudan.Mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo yameonya kwamba kuongezeka kwa uhasama kwenye viunga vya mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kunakohusisha kundi lisilo la kiserikali linalojihami kwa silaha, M23 kumesababisha watu wengi zaidi kuhama katika eneo hilo lenye utajiri wa madini, huku kukiwa na hofu kwamba mji mkuu wa eneo hilo Goma unaweza kuangukia mikononi mwa wapiganaji hao.Tukiwa bado katika siku ya Elimu duniani kutana na Suhaila msichana mkimbizi kutoka Afghanistan ambaye kupitia mpango wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wa kuwahamishia wakimbizi katika nchi ya tatu aliwasili Jamhuri ya Kyrgyzstan ambako sio tu alipata maskani ya kudumu na wazazi wake bali pia matumaini na elimu iliyompa ari ya kurejesha matunda yake nyumbani alikotoka.Makala leo ikiwa ni siku ya elimu duniani Assumpta Massoi anakukutanisha na walimu wawili huko Paris nchini Ufaransa wakijadili mustakabali wa Akili Mnemba au AI kwenye ufundishaji darasani. Mahojiano hayo yameandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na UTamaduni, UNESCO.Na katika mashinani Nour Abdallah, Mkimbizi wa ndani katika eneo la Zamzam nchini Sudan kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP, anasema janga la njaa limelazimisha jamii kula chakula cha mifugo huku wakiwa na matumaini kwani chakula cha msaada kinaendelea kuwasilishwa kwenye maeneo yaliyoathiriwa na vita.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    12 min
  • Kuna hofu mji mkuu wa eneo la Goma unaweza kuanguka katika mikono ya M23
    Mashirika ya Umoja wa Mataifa hii leo yameonya kwamba kuongezeka kwa uhasama kwenye viunga vya mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kunakohusisha kundi lisilo la kiserikali linalojihami kwa silaha, M23 kumesababisha watu wengi zaidi kuhama katika eneo hilo lenye utajiri wa madini, huku kukiwa na hofu kwamba mji mkuu wa eneo hilo Goma unaweza kuangukia mikononi mwa wapiganaji hao. Selina Jerobon anaeleza zaidi.
    3 min
  • 23 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC kumulika mausala ya AI kwenye elimu tukielekea siku ya kimataifa ya elimu inayoangazia matumizi ya AI na changamoto zake. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa methali.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO, umethibitisha kuwa waasi wa M23 wametwaa baadhi ya maeneo jimboni Kivu Kusini, miongoni mwao ikiwa mji wa Minova, ukisema hali hiyo inatia wasiwasi mkubwa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema watoto na familia zao wanaorejea kaskazini mwa Gaza baada ya kuanza utekelezaji wa usitishaji mapigano wanakutana na uharibifu mkubwa na kuporomoka kwa miundombinu.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP leo limesema limefanikiwa kuhamisha msaada wa kwanza wa chakula kuingia Sudan kwa ajili ya kulisha watu 80,000 kwa mwezi mmoja kupitia mto Nile.Na katikakujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya msemo “HIVI KWELI KISAUNI KUTOTA MVINDE?”Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min
  • Mradi wa FAO umenikomboa mimi na familia yangu: Mkulima Noor Ahmed
    Katika jimbo la Kandahar nchini Afghanistan Noor Ahmen mkulima wa ngano amenufaika na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO unaotoa mafunzo ya kilimo, kugawa  mbegu na pembejeo kwa wakulima. Mradi huu ambao unafadhiliwa pia na Benk ya Dunia umezisaidia familia nyingi za wakulima sio tu kuinua kipato bali pia kuboresha lishe na kukabili changamoto ya kutokuwa na uhakika wa chakula. Bosco Cosmas anafafanua zaidi katika Makala hii
    4 min
  • Asante IFAD kwa kutuwezesha watu wenye ulemavu Liberia
    Nchini Liberia, mradi unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD umejengea uwezo watu wenye ulemavu wa kuona na kuwawezesha kuongeza vipato na vile vile uhakika wa kupata chakula. Simulizi ya Sabrina Moshi wa redio washirika SAUT FM mkoani Mwanza nchini Tanzania, inaelezea zaidi.Tuko kaunti ya Lofa, kaskazini kabisa mwa Liberia, magharibi mwa Afrika, tunakutana na Hawa Kamara, yeye ni mlemavu wa kutoona. Yeye pamoja na wenzake wa chama cha watu wenye ulemavu wa kutoona hapa Lofa, wanathibitisha kuwa unapoamua kufanya kitu, hakuna kinachokuzuia.Kupitia mradi wa Mabadiliko ya kilimo kwa wakulima wadogo na uchechemuzi wa kilimo biashara au STAR-P, mavuno ya mpunga kwenye shamba la kikundi hicho, yameongezeka kwa asilimia 300.Hawa anasema, “Mwanzoni hatukuwa na kitu kabisa. Tulihangaika sana kulima mpunga. Lakini baada ya IFAD kutufikia katika maisha yetu na kutusaidia, mambo yalianza kubadilika. Walitupatia pembejeo na mbegu za ubora wa juu kuanzisha mashamba. Tulitumia mbegu hizo kupanda kwenye mashamba yetu Bakadu.”Awali walilima ekari 1.2 tu, lakini baada ya kupatiwa vifaa vya kisasa vya kilimo wameweza kulima hadi ekari 4.3.Mavuno ya mpunga yameongezeka. Wanasagisha mashine, kiasi cham chele wanauza na ziada ni kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.Hawa akiwa kwenye shamba lake la mpunga anasema,“Kabla ya STAR-P nilijihisi nimepotea na mpweke. Lakini sasa ninaweza kulima mwenyewe shambani, na ninaweza kujihudumia mimi na pia familia yangu. Zamani niliacha shule. Lakini baada ya kuanza mradi huu, nimerejea shuleni na ninataka kuwa mhasibu mkubwa duniani.”
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners