Hii leo jaridani tunaangazia mlipuko wa ugonjwa wa marburg nchini Tanzania, na mfumo wa faya nchini humo. Makala inatupeleka nchini Geneva, Uswisi na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, linachunguza sampuli za watu wawili kati ya wanane waliofariki dunia mkoani Kagera nchini Tanzania kubaini iwapo wamekufa kwa ugonjwa wa homa ya Marburg ambayo inashukiwa kulipuka kwenye wilaya mbili za mkoa huo ulioko kaskazini-magharibi mwa Tanzania.Mfumo wa kidijitali unafadhiliwa na serikali ya Canada kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto (UNICEF) nchini Tanzania umeanza kuonesha mafanikio katika kurahisisha huduma kama vile usajili wa wagonjwa, usimamizi wa maduka ya dawa na bima na kuwezesha wahudumu wa afya kujikita zaidi katika huduma.Makala inatupeleka Geneva, Uswisi ambako kwa uratibu wa Pascal Sim wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, tunakuletea mwandishi wa habari kutoka Tanzania ambaye ni mnufaika wa ziara ya mafunzo kuhusu utendaji wa Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu.Na mashinani fursa ni yake Mwanaisha Halua kutoka Kenya ambaye ni mnufaika wa mafunzo ya ukulima wa mazao rafiki wa mabadiliko ya tabianchi yanayotolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula, WFP akisema mojawapo ni viazi vitamu vya rangi ya chungwa ambavyo vina lishe bora na ni virutubisho vingi.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!