Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Msichana Bangladesh: Sikufahamu ufundi bomba ni nini, sasa ILO imeniwezesha
    Nchini Bangladesh, mradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana kuvunja mwiko na kuingia kwenye tasnia ambazo zimezoeleka kuwa ni za wanaume, mathalani ufundi bomba. Mradi huo unaolenga wanufaika 24,000 wenye umri kati ya miaka 18 na 35 unatekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kwa kushirikiana na serikali ya Bangladesh.Video ya ILO hapa Cox’s Bazaar inamleta kwako mmoja wa wanufaika hao ambaye hata hivyo jina lake halikutajwa, akiwa ameshikilia vifaa vya ufundi bomba anasema, awali sikufahamu kuhusu hii kozi hadi nilipofahamu kupitia Idara ya Maendeleo ya Vijana. Hii ni mara ya kwanza fursa hii imetufikia katika shule ya sekondari ya juu ya Moheshkhali. Tunajifunza stadi badala ya kupoteza muda nyumbani itanisaidia maisha yangu ya baadaye.Nikihitimu masomo naungana na kaka kwenye duka lakeAnakiri kuwa kabla ya kushiriki mafunzo haya hakuwa anafahamu kabisa ufundi bomba ni kitu gani. Lakini sasa amejifunza kuhusu vifaa mbalimbali ikiwemo msumeno wa mabomba, spana na kadhalika.ILOMradi wa kuimarisha stadi na kufungua fursa za kiuchumi, ISEC miongoni mwa wanawake na vijana, umewezesha wasichana Cox’s Bazaar nchini Bangladesh.Na ndoto yake ni kwamba nikihitimu masomo nitakwenda kuungana na kaka yangu kwenye duka lake linalounza vifaa vya ujenzi. Nataka niwe mjasiriamali kama yeye, nijitegemee na nisaidie familia yangu. Siku hizi kwenye nyingi zilizoendelea na hata hapa Bangladesh wasichana wanafanya aina zote za kazi.Wanaweza kufanya kazi ngumu kama wanaume, nami nataka kuwa hivyo.Video ya ILO inamalizika mnufaika huyu amekamilisha kufunga bomba na sasa maji yanatoka, na mkufunzi anatumia maji hayo kunawa mikono.Malengo namba 4, 5, na 8 ya SDGs yanatekelezwaMradi huu ulizinduliwa mwezi Septemba mwaka 2023 ukifadhiliwa na…
    2 min
  • Gaza: Zaidi ya watoto 70 wameuawa tangu Januari 1 huku gharama za maisha zikizidi kupanda
    Hali ya maisha kwa raia wa Gaza inaendelea kuwa mbaya msimu huu wa baridi kali kutokana na vikwazo vya kufikisha misaada, kupanda kwa gharama za maisha na mashambuizi yanayoendelea kukatili maisha ya raia wakiwemo watoto 74 waliouawa tangu Januri Mosi mwaka huu  yamesema mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF ambalo linasema kuuawa kwa watoto hao 74 katika siku saba za kwanza za mwezi huu ni dhihirisho la jinamizi linaloendelea kuighubika Gaza na mashambulizi ya Israel hayaonyeshi dalili yoyote ya kukoma ikiwemo ya jana usiku katika mji wa Gaza, Khan Younis na kwenye makazi ya Pwani ya wakimbizi wa ndani ya Al Mawasi ambayo Israel yenyewe iliyatenga hapo awali kama maeneo salama. Kwa mujibu wa UNICEF jana Jumanne pekee watoto 5 wameripotiwa kuuawa Al Mawasi. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEFF Catherine Russell amesema "Kwa watoto wa Gaza, mwaka mpya umeleta vifo zaidi na mateso kutokana na mashambulizi, kunyimwa huduma, na kuongezeka kwa hali ya baridi. Usitishaji wa mapigano umechelewa kwa muda mrefu na watoto wengi sana wameuawa au kupoteza wapendwa wao katika mwanzo mbaya wa mwaka mpya.”© UNRWA/Fadi ThabetMwanaume na mwanae wakiwa wameketi wakiota moto Nuseirat katikati mwa GazaGharama za chakula zinaendelea kupanda GazaKwa upande wake shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula Duniani WFP limesema kana kwamba mashambulizi hayatoshi sasa kupanda kwa gharama za chakula ni mtihani mwingine kwa watu wa Gaza kwani kilo 25 za unga zinauzwa hadi dola za Marekani 150 gharama ambayo watu wengi hawawezi kumudu  na watoto ni wahanga wakubwa wakilzimika kulala njaa. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X limesema linapokuja suala la mashambulizi Gaza “Hakuna tofauti, wahudumu wa kibinadamu, hata wawe ni nani nao wamekuwa wakilengwa mara kwa mara. Kupuuzwa huku kwa wazi kwa sheria za kimataifa za kibinadamu hakuwezi kuachwa kuwa ndio kawaida mpya.” Pia limesema Gaza hospitali zimekuwa mitego ya vifo, familia zimesambaratika, watoto wanakufa kwa baridi na njaa inakatisha maisha  ya watu wengi 
    2 min
  • 08 JANUARI 2025
    Zaidi ya watoto 70 wameuawa Gaza tangu Januari 1 huku gharama za maisha zikizidi kupanda.Mafunzo ya ufundi bomba kuniwezesha kutunza familia yangu – Msichana Bangladesh.Mradi wa UNICEF wa kuunganisha taarifa na kusajili watoto wanufaisha jamii Burundi.Mashinani nchini Tanzania kuhusu haki za watoto
    10 min
  • 07 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini DRC katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Bulengo kushuhudia jinsi Umoja wa Mataifa unavyowasaidia wanawake waathrika wa ukatili wa kingoni kuweza kujitegemea na kumudu mahitaji ya familia zao.Kwa mujibu wa takwimu zilizothibitishwa na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, takriban watu 5,601 waliuawa nchini Haiti mwaka 2024 kutokana na ghasia za magenge, likiwa ni ongezeko la zaidi ya mauaji 1,000 ya mwaka 2023. Katika moja ya matukio mabaya zaidi na ya kushtua mwaka jana, takriban watu 207 waliuawa mapema Desemba kwenye mauaji yaliyoratibiwa na kiongozi wa genge lenye nguvu la Wharf Jérémie katika eneo la Cité Soleil huko Port-au-Prince. Wengi wa waliouawa walikuwa wazee walioshutumiwa kusababisha kifo cha mtoto wa kiongozi huyo kwa njia ya uchawi.Leo, Umoja wa Mataifa na Serikali ya Lebanon wametoa ombi la nyongeza ya dola milioni 371.4 za kimarekani, zikilenga kutoa msaada wa kuokoa maisha ya walioathiriwa na mzozo wa hivi karibuni na janga la kibinadamu linaloendelea nchini humo.Na Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk leo ameeleza kusikitishwa sana na ongezeko kubwa la watu walionyongwa nchini Iran mwaka jana. Takriban watu 901 wameripotiwa kunyongwa katika mwaka 2024, arobaini wakiwa wamenyongwa katika wiki moja tu ya mwezi Desemba.Mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi, UNFPA tunamsikia Zubaida AbouBaker, mama mkimbizi wa ndani katika kambi ya Tawila iliyoko Darfur Kaskazini nchini Sudan akisimulia machungu yaliyomkumba kufuatia migogoro inayoendelea nchini humo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    10 min
  • Raia wa Mali walioko ughaibuni waonesha mfano bora wa kuwekeza nyumbani
    Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo, IFAD kwa kushirikiana na wadau na kupitia msaada wa Muungano wa Ulaya unasaidia raia wa Mali wanaoishi ughaibuni kuwekeza kwa ufanisi nyumbani Mali.Wamefanya hivyo kwa kuwasaidia kuanzisha Ciwara Capital, kampuni ya uwekezaji inayomilikiwa na raia wa Mali na sasa wanasaidia wakulima wa mpunga nchini Mali kuimarisha na kuongeza uzalishaji wa mpunga, ikiwemo eneo la Mopti ambalo limekuwa likikabiliwa na ukosefu wa usalama na hivyo wakulima kugubikwa na umaskini.Mfumo huu unadhihirisha kuwa badala ya waafrika kutuma dola bilioni 55 kila mwaka nyumbani kusaidia familia, fedha hizo zinaweza kuwekezwa kwenye miradi endelevu. Je ni kwa vipi, Assumpta Massoi anafafanua kwenye makala hii iliyoandaliwa na IFAD.
    4 min
  • Kupata taarifa sahihi kutoka kwa wataalamu wa afya ni muhimu kama ilivyo kujiandaa - Ugonjwa wa HMPV
    Huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus (HMPV) wakati huu wa msimu wa baridi nchini China na kuleta hofu ulimwenguni kuhusu uwezekano wa kutokea kwa janga jingine la ugonjwa kama ilivyokuwa Covid-19, mamlaka ya afya nchini humo inasema kiwango na nguvu za ugonjwa huo viko chini ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana, ameeleza Hans Kluge, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni kanda ya Ulaya akisisitiza ulimwengu kupata taarifa sahihi. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
    3 min
  • 06 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus, na watoto waathirika wa vita Gaza. Makala inatupeleka nchini Mali na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Huku kukiwa na ripoti za kuongezeka kwa maambukizi ya magonjwa ya mfumo wa kupumua vikiwemo virusi vya metapneumovirus (HMPV) wakati huu wa msimu wa baridi nchini China na kuleta hofu ulimwenguni kuhusu uwezekano wa kutokea kwa janga jingine la ugonjwa kama ilivyokuwa Covid-19, mamlaka ya afya nchini humo inasema kiwango na nguvu za ugonjwa huo viko chini ikilinganishwa na wakati kama huu mwaka jana, ameeleza Hans Kluge, Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni kanda ya Ulaya akisisitiza ulimwengu kupata taarifa sahihi.Baada ya miezi 14 ya vita Gaza maelfu ya watu wakiwemo watoto wamesalia na ulemavu wa maisha kwa kulazimika kukatwa viungo kutokana na kujeruhiwa katika vita inayoendelea kwa miezi 15 akiwemo mtoto wa umri wa miaka 7 Mahmmoud ambaye sasa amepooza baada ya kupigwa risasi mgongoni na anahitaji huduma za haraka za afya ili akatibiwe limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Magharibi mwa Afrika kusikia jinsi raia wa taifa la Mali walioko ughaibuni wanavyoleta nuru kwa wakulima wa mpunga nchini mwao.Mashinani fursa ni yake Hilda, Mama mwenye umri wa miaka 31 ambaye ni mkimbizi kutoka Burundi anayeishi katika makazi ya wakimbizi nchini Tanzania, anashukuru mfuko wa msaada wa marekani wa kitengo cha Idadi ya watu, wakimbizi na uhamiaji, PRM (Population, Refugees, and Migration Bureau, PRM) kwa huduma za afya ya watoto na kinamama wajawazitito kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa ya kughudumia wakimbizi UNHCR.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!  
    10 min
  • Mzazi wa Mahmooud: Mwanangu amepata kilema cha maisha sababu ya vita isiyokoma Gaza
    Baada ya miezi 14 ya vita Gaza maelfu ya watu wakiwemo watoto wamesalia na ulemavu wa maisha kwa kulazimika kukatwa viungo kutokana na kujeruhiwa katika vita inayoendelea kwa miezi 15 akiwemo mtoto wa umri wa miaka 7 Mahmmoud ambaye sasa amepooza baada ya kupigwa risasi mgongoni na anahitaji huduma za haraka za afya ili akatibiwe limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA. Taarifa ya Thelma Mwadzaya inafafanua zaidi
    2 min
  • Faida ya magari ya umeme inaweza isionekane kwa sasa lakini si muda mrefu yatakuwa na manufaa kwa mazingira na uchumi
    Kijana Mtanzania Gibson Kawago hivi karibuni kupitia kampuni yake ya WAGA inayoshughulika na uvumbuzi wa teknolojia zinazolenga kupambana na uchafuzi wa mazingira ya ulimwengu, ametangaza kuanzisha vifaa vinavyotumika kuchaji magari ya umeme lengo likiwa ni kuwasaidia watu wa eneo lake, Afrika Mashariki kupata huduma ya kuchaji magari yao ili wahame kutoka katika matumizi ya mafuta ya kisukuku kama petroli na dizeli. Lakini je ana majibu gani kwa wale ambao bado hawaoni faida ya ya magari ya umeme kwa mazingira ikiwa bado vyanzo vya umeme ni chafuzi? Katika mazungumzo haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii, Gibson anafafanua.
    4 min
  • UN: Vifo vitokanavyo na baridi Gaza vinazuilika, usitishaji mapigano na misaada ndio jawabu
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM leo limeonya juu ya vifo vitokanavyo na msimu wa baridi kali Gaza likisema limesikitishwa sana na athari mbaya za mvua za msimu wa baridi na baridi kali kwa Wapalestina waliokimbia makazi yao na kuishi katika mazingira magumu huko Gaza, kwani hilo ni janga la kibinadamu lisilo na kifani. Kupitia taarifa iliyotolewaleo mjini Geneva Uswisi Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope  amesema "Watu walio katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na takriban watoto wachanga saba, wamekufa kutokana na baridi kali au hypothermia, na vifo hivi vya kusikitisha vinasisitiza haja ya haraka ya makazi na msaada mwingine wa kibinadamu kuwafikia watu wa Gaza mara moja," Ameongeza kuwa hali hii inachochea janga zaidi la kibinadamu ambalo tayari linawakumba watu waUkanda wa Gaza. Mvua kubwa na mafuriko yameyakumba makazi ya wakimbizi wa ndani yaliyojengwa kwa mahema na kulazimisha familia kuachwa katika maeneo ya wazi kwenye hali mbaya ya baridi, zikijitahidi kutengeneza mahema yaliyoharibika kutokana na matumizi ya miezi kadhaa. © UNRWAChakula kinagawiwa kwa watu waliokimbia makazi yao huko Jabalia, kaskazini mwa Gaza.Vikwazo vya Israel ni changamoto kwa misaadaPia IOM imesema vikwazo vya utaratibu wa kufikia wenye uhitaji, kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, vimezuia kwa kiasi kikubwa utoaji wa misaada, huku watu 285,000 pekee wakipokea msaada wa makazi tangu Septemba 2024. Kwa mujibu wa IOM hadi kufikia Katikati ya Desemba mwaka jana inakadiriwa kuwa watu wapatao 945,000 bado wanahitaji msaada wa haraka wa kukabiliana na msimu wa baridi ikiwemo nguo za kuongeza joto, mablanketi na tepu za kuima mahema dhidi ya mvua na baridi. Tangu Katikati ya Novemba mwaka jana IOM imewasilisha karibu vifaa 180,000 vya makazi ya dharura kwa washirika ndani ya Gaza na ina zaidi ya vifaa milioni 1.5 vya msimu wa baridi ikiwemo mahema, vifaa vya kuziba  na vitanda ambavyo viko tayari kwenye maghala na sehemu zavivuko, lakini vikwazo vikali vya ufikiaji vinawazuia kufikia wenye uhitaji. © UNICEF/Abed ZaqoutWavulana wawili wakibeba chupa za maji katika kambi ya wakimbizi inayofadhiliwa na UNWRA huko Khan Younis kusini mwa Gaza.Usitihsaji mapigano ndio suluhuIOM imesisitiza wito wake wa dharura wa kusitisha mapigano ili kuwezesha utoaji salama na wa haraka wa msaada wa kuokoa maisha kwa wale wanaouhitaji sana. Pia inasisitiza wito wake kwa pande zote kuzingatia sheria za kimataifa za kibinadamu, kuhakikisha ulinzi wa raia, kuachiliwa kwa mateka wote na kuruhusu ufikiaji salama, wa haraka, usiozuiliwa na endelevu wa wenye uhitaji. Watu wa Gaza wanastahili usalama, makazi na utu. IOM iko tayari kuhamasisha misaada na kusaidia jamii zilizofurushwa, lakini fursa ya ufikiaji wa kibinadamu lazima itolewe ili kuwezesha hili amesisitiza mkuu wa IOM. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema Licha ya hali ngumu, timu za UNRWA zinaendesha makao yote ya Umoja wa Mataifa, na kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watu wanaohitaji. Limeongeza kuwa Vita vilipoanza karibu miezi 15 iliyopita, UNRWA iligeuza shule zake, vituo vya afya, na maghala kuwa makazi na kuna wakati ambapo vita ikiendelea UNRWA ilipokea watu milioni 1 waliokimbia makazi yao 
    2 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners