Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 13 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti mpya kuhusu hali ya usalama na afya ya watoto kote duniani, na amnai na usalama nchini Syria. Makala inatupeleka nchini Uganda na mashinani nchini DRC, kulikoni?Ripoti mpya ya kila mwaka kuhusu mustakabali wa watoto ambayo imetolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF, imeonya kwamba dunia inaingia katika zama mpya za majanga kwa watoto.Wasyria wana matarajio makubwa kwa nchi yao, na hamu kubwa ya watu kutoka katika kila nyanja ya jamii kuja pamoja na kuunda katiba mpya, ambayo lazima ianze na mazungumzo ya kitaifa yaliyo jumuishi. Hayo ni kwa mujibu wa Najat Rochdi, Naibu Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, ambaye amekuwa Damascus kukutana na wajumbe kadhaa wa mamlaka ya mpito ili kuhakikisha Wasyria wote wana uwezo wa kushiriki katika mustakbali wa nchi hiyo.Makala inatupeleka nchini Uganda ambako shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa muda sasa limekuwa likifanya jukumu muhimu katika kuwezesha usajili wa watoto.Na mashinani fursa ni yake Antoinette Nzale, mkimbizi wa ndani katika kijiji cha Fataki iliyoko Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo, DRC akishuhudia jinsi ambavyo juhudi za pamoja za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO na wanajeshi wa serikali FARDC zinavyowawezesha wakimbizi wa ndani kuanza kurejea katika mazingira yao ya awali taratibu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    10 min
  • Najat Rochidi: Syria ina fursa kubwa ya kutoka gizani na kuingia kwenye nuru
    Wasyria wana matarajio makubwa kwa nchi yao, na hamu kubwa ya watu kutoka katika kila nyanja ya jamii kuja pamoja na kuunda katiba mpya, ambayo lazima ianze na mazungumzo ya kitaifa yaliyo jumuishi. Hayo ni kwa mujibu wa Najat Rochdi, Naibu Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria, ambaye amekuwa Damascus kukutana na wajumbe kadhaa wa mamlaka ya mpito ili kuhakikisha Wasyria wote wana uwezo wa kushiriki katika mustakbali wa nchi hiyo. 
    3 min
  • WMO: Moto Marekani umeonesha umuhimu wa tahadhari za mapema
    Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani (WMO) leo hii likiwa limeutangaza mwaka jana 2024 kuwa mwaka uliokuwa na joto zaidi kuwahi kurekodiwa, leo pia WMO imeendelea kusisitiza umuhimu wa tahadhari za mapema kuhusu majanga ya tabianchi ili kuokoa maisha ya watu. WMO imeeleza kwamba tahadhari za mapema zilizotolewa na Idara ya Hali ya Hewa ya Taifa la Marekani  zimesaidia kwa kiasi fulani kuokoa maisha ya watu katika moto wa nyika uliosambaa na kuteketeza maeneo makubwa mji wa Los Angels katika jimbo la California. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
    3 min
  • Serikali patieni vijana taarifa sahihi na stahiki ili watekeleze wajibu wao
    Umoja wa Mataifa unaeleza kwamba duniani kote kuna vijana bilioni 1.2 wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24. Idadi hii ni saw ana asilimia 16 ya wakazi wote wa dunia. Kama hiyo haitoshi, idadi hiyo ya vijana inatarajiwa kufikia bilioni 1.3 ifikapo mwaka 2030, yaani miaka mitano ijayo. Lakini changamoto ni kwamba bado serikali nyingi hazijaweza kutumia wingi wa idadi hii kusongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs. Kwa hali hiyo baadhi ya vijana wameamua kutumia fursa na kujiongeza ili vijana wenzao waweze kufahamu wanachopaswa kufanya ili SDGs zifanikiwe ifikapo 2030. Miongoni mwao ni Paul Siniga, kijana kutoka Tanzania ambaye mwezi Oktoba mwaka huu alikuweko kwenye makao makuu ya UN jijini New York, Marekani kushiriki vikao vya ngazi ya juu. Assumpta Massoi alitaka kufahamu kwa kina ni hatua zipi alichukua hadi kufika aliko sasa.
    4 min
  • 10 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia moto wa nyika mjini California Marekani, na waathirika wa kimbunga Chido nchini Msumbiji. Makala tunasikia kijana Paul Siniga kutoka Tanzania na mashinani tunakupeleka nchini Kenya, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa duniani (WMO) leo hii likiwa limeutangaza mwaka jana 2024 kuwa mwaka uliokuwa na joto zaidi kuwahi kurekodiwa, leo pia WMO imeendelea kusisitiza umuhimu wa tahadhari za mapema kuhusu majanga ya tabianchi ili kuokoa maisha ya watu. WMO imeeleza kwamba tahadhari za mapema zilizotolewa na Idara ya Hali ya Hewa ya Taifa la Marekani  zimesaidia kwa kiasi fulani kuokoa maisha ya watu katika moto wa nyika uliosambaa na kuteketeza maeneo makubwa mji wa Los Angels katika jimbo la California.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linaendelea kusambaza msaada wa kibinadamu ili kurejesha matumaini ya waathirika wa kimbunga Chido kilichotokea tarehe 15 Desemba mwaka jana nchini Msumbiji na kuziacha taabani jamii za majimbo ya Cabo Delgado, Nampula na Niassa.Katika makala Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa anazungumza na kijana Paul Siniga kutoka Tanzania ili kufahamu safari yake hadi kuweza kufika makao makuu ya Umoja wa MAtaifa, New York, Marekani.Na mashinani Nur Bashir kutoka jamii ya wfugaji katika kaunti ya Turkana nchini Kenya ambaye kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji anaeleza jinsi jamii zake zinavyoathiriwa na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min
  • Nosizi Ndube: Kukosa utaifa haikukwamisha ndoto yangu ya elimu, asante UNHCR na wadau mbalimbali
    Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefanikiwa kumnyanyua msichana Nosizi Dube na kutimiza ndoto yake ya kuepuka ndoa ya utotoni na kupata shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Msichana huyo mwenye umri wa miaka 24 ni wa kwanza katika jamii ya Washona wanaoishi mjini Nairobi Kenya kupata elimu katika ngazi hiyo. Mpango wa UNHCR wa kupambana na kutokuwa na utaifa kwa ushirikiano na serikali ya Kenya umekuwa chachu ya mafanikio ya msichana huyo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya alimtembelea Nosizi nyumbani kwake ili kupata undani wa safari yake..
    6 min
  • 09 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa Kina inayotupeleka Kenya ambapo Shirika la Umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limefanikiwa kumnyanyua msichana Nosizi Dube na kutimiza ndoto yake ya kuepuka ndoa ya utotoni na kupata shahada ya kwanza ya chuo kikuu. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchaambizi wa neno KWEGO.Mwezi mmoja tangu kuanguka kwa utawala wa Bashar Al-Assad, zaidi ya wakimbizi 125,000 wamerejea Syria "wakiwa na matumaini baada ya miaka mingi ya kuishi uhamishoni", lakini wamejikuta wakikabiliwa na hali mbaya nchini mwao, wameeleza leo wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa. Likiwa linaongoza wito kwa jumuiya ya kimataifa "kutoka kwenye maneno hadi vitendo" ili kuwasaidia watu walio waliorejea ambao sasa wako katika mazingira magumu, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limesema familia nyingi zina uhaba wa makazi na njia kidogo za kiuchumi.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeongeza ombi lake la fedha kufikia dola milioni 73.2 kwa ajili ya kusaidia zaidi ya watu milioni 1.1 kote nchini Syria katika kipindi cha miezi sita ijayo, wakati nchi hiyo ikiingia katika kipindi cha mpito kufuatia kuanguka kwa serikali ya Bashar Al-Assad. Ombi hili ni nyongeza katika ombi la awali la dola milioni 30 lililotolewa mwezi Desemba mwaka jana 2024 likilenga mahitaji yanayoongezeka ya majira ya baridi Kaskazini Magharibi mwa Syria.Miezi 15 baada ya vita huko Gaza, mamia kwa maelfu wanaendelea kuishi katika shule za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipalestina (UNRWA) zenye msongamano ambazo zimegeuzwa kuwa makazi. UNRWA imeeleza kuwa hata viwanja vya michezo kwa watoto sasa ni nyumba kwa waliofurushwa. Shirika hilo limesisitiza kuwa misaada zaidi ya kibinadamu lazima iingie Gaza na kusitishwa kwa mapigano ni muhimu zaidi kuliko hapo awali.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo fursa ni yake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “KWEGO”.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • UNICEF Burundi: Mradi wa UNICEF wa kuunganisha taarifa na kusajili watoto wanufaisha jamii
    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linaisaidia serikali ya Burundi katika kuunganisha taarifa za watu katika mifumo inayosomana ya kiraia na ya huduma ya afya. Euphrasie Butoyi mama akiwa amembeba mtoto wake mchanga, amekuja katika ofisi za msajili za eneo la Busoni jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, anasema,“kabla ilikuwa vigumu kumwandikisha mtoto. Umbali ulikuwa mrefu. Tulikuwa tunalazimika kulipia tiketi ya safari kwa ajili yetu na mashahidi. Tulikuwa tunaweza kwenda kule hata mara mbili bila kupata cheti cha kuzaliwa.” Damien Ndayisenga ni msajili wa kijamii anathibitisha hilo kwa kusema, “ukweli kabla ya hatua hii, ofisi ya usajili wa raia ya Busoni ilikuwa imezidiwa na idadi kubwa ya watu wanaokuja kusajili watoto wao ili kupata vyeti vya kuzaliwa. Lakini huduma hii imerahisisha.” Hakika mradi huu umekuwa mkombozi kama anavyoendelea kueleza Euphrasie Butoyi. Anaposema faranga elfu 10 fedha ya Burundi hiyo ni takribani dola nne za kimarekani, “leo tofauti ni kuwa kituo cha afya kiko karibu na sisi kwa hiyo si lazima tena kulipa nauli kwa ajili ya mashahidi. Sasa ni rahisi kwetu kusajili watoto wetu baada tu ya kuzaliwa. Hata mume wangu hajui kama niko naandikisha hapa wakati huu. Anadhani nitapata tu chanjo ya mtoto lakini nitakapomuonesha cheti cha kuzaliwa cha mtoto wetu, atafurahi sana. Hatalazimika tena kwenye ofisi za serikali na kulipa faranga za Burundi 10,000 kwa ajili ya usafiri. Ni faida kwetu.” UNICEF pia inasaidia katika kuandikisha watoto ambao walichelewa kusajiliwa katika umri mdogo na hiyo imesaidia sana watoto walio katika mazingira magumu kupata huduma za msingi za kijamii ambazo hapo awali walikuwa nazikosa kwa kuwa hawana utambulisho wowote unaotambuliwa kiserikali. Katika mkoa wa Bugabira jimboni Kirundo kaskazini mwa Burundi, tunakutana na Jean Baptiste Mutaniyonka baba wa mtoto mwanafunzi Karerwa Olivier anaeleza changamoto walizokuwa wanakumbana nazo hapo awali kabla ya huduma ya usajili kuletwa karibu. “Mara ya kwanza nilipoenda kwenye ofisi za mkoa kusajili ilikuwa imefungwa kwa sababu ya sikukuu. Mara ya pili, mashahidi walitutaka kuwapatia faranga za Burundi elfu kumi nila mmoja. Sikuwa na fedha hiyo kwa hiyo ilibidi tuahirishe hiyo miadi ili tutafute pesa.” Mzazi huyu ili kuonesha namna cheti cha kuzaliwa kilivyo na umuhimu mkubwa katika maisha ya mtoto nchini Burundi anasema, “bila cheti cha kuzaliwa mtoto hana haki ya kupata kupata huduma ya bure katika hospitali. Tulikuwa tunaondoka bila bila kupata matibabu. Na katika hali kama hiyo tuligeukia katika tiba za asili au katika maduka ya dawa. Ilikuwa hivyo hivyo katika shule. Watoto wangu walikuwa wanarejeshwa nyumbani kwa kukosa cheti cha kuzaliwa.” Huyo ni Olivier Karerwa mwenyewe, mtoto wa Jean Mutaniyonka. Olivier amesajiliwa kupitia mradi huu wa UNICEF na anasema anataka kuwa mwalimu atakapohitimu masomo yake. Anne Rwasa ni bibi anazungumzia ilivyo rahisi sasa kumuhudumia mjukuu wake akisema, lakini leo mtoto  awe na homa au kuumwa tumbo tunakimbia katika kituo cha afya ambako anapata huduma ya bure ya afya.” Mradi huu wa UNICEF Burundi wa kuunganisha taarifa za watoto za serikali ili ziweze kusomeka pia katika taasisi nyingine kama vile vituo vya afya umepata  pia usaidizi kutoka kwa kamati ya UNICEF ya Uingereza.  
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners