Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Huu ni wakati wa kuchukua hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi na AI-Guterres
    Viongozi wa kimataifa wa masuala ya kisiasa na biashara wanaokutana Davos Uswisi kwa ajili ya jukwaa la kiuchumi duniani WEF, leo wamekabiliwa na ukweli mchungu kutoka kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, akilaani ukosefu wa ushirikiano wa kimataifa katika dunia inayokosa mwelekeo, ikikabiliwa na hatari mbili kubwa ambazo ni mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiyodhibitiwa. Flora Nducha na taarifa zaidiAkizungumza katika Jukwaa hilo la kila mwaka la Kiuchumi Duniani Katibu Mkuu amewaonya viongozi wa dunia na wakuu wa biashara kuhusu vitisho viwili vinavyoongezeka kwa ubinadamu mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba au AI isiodhibitiwa amesema “Kunapokuja suala la tishio la kimataifa nyuklia sio tishio pekee. Leo hii tunakabiliwa na matishio mawili makubwa ambayo yanahitaji kupewa uziti Mkubwa wa kimataifa na hatua kwa sababu yanatishia kubadili kabisa maisha tunayoyajua, janga la mabadiliko ya tabianchi na upanuzi wa kasi wa wigo wa akili mnemba.”Akikosoa ukosefu wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto hizi kubwa, Guterres ametoa wito wa kuchukua hatua za pamoja haraka ili kushughulikia dunia aliyoiita  dunia inayokosa mwelekeo “Hebu tukabili ukweli , leo hii watu wengi wanapoitazama dunia hawaoni ushirikiano mkubwa wala maarifa ya kutosha . Licha yah atua zilizopigwa uwekezaji katika nishati jadidifu , teknolojia na masuala ya  kiafya ni dunia na matatizo yetu mengi yanazidi kuwa mbaya”Kuhusu mabadiliko ya tabianchi, Guterres amelinganisha uraibu wa dunia kwa nishati ya mafuta na mnyama wa Frankenstein, akisisitiza madhara yake makubwa.Amebainisha kuwa baadhi ya bandari kuu za mafuta duniani ziko hatarini kutokana na viwango vya bahari kuongezeka, jambo linalosababishwa na uchomaji wa makaa ya mawe, mafuta, na gesi asilia.Katibu Mkuu amekemea viwanda na taasisi za kifedha zinazosuasua kwenye ahadi zao za tabianchi, akisema hii ni kukosa maono na usaliti wa sayansi na watumiaji wanaotafuta uendelevu.Akizungumzia hatari na fursa za AI, Guterres ameelezea kama upanga wa makali mawili. Ingawa inatoa matumaini katika kubadilisha sekta za afya, kilimo, na elimu, ameonya kuhusu hatari kubwa ikiwa haitadhibitiwa.Amesema AI isiyodhibitiwa inaweza kuvuruga uchumi, kudhoofisha imani kwa taasisi, na kuongeza ukosefu wa usawa.Guterres amehitimisha kwa kutoa wito wa mshikamano wa kimataifa katika kukabiliana na changamoto hizi muhimu akisema “kubadili mwelekeo wa taasisi kunahitaji kubadili fikra kwa sababu tunakabiliwa na changamoto kubwa zinazoweza kuiangamiza dunia na sishawishiki kwamba viongozi wanalielewa hili.”Amesisitiza umuhimu wa kurekebisha mifumo ya utawala wa kimataifa ili kukabiliana ipasavyo na migogoro ya kisasa, akionya kuwa utashi wa kisiasa ni muhimu lakini bado haupo katika kiwango cha kutosha.Ujumbe wake ni bayana kwamba sasa ni wakati wa kuchukua hatua za pamoja na za haraka.
    4 min
  • 22 JANUARI 2025
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea-Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo ameliambia jukwaa la kiuchumi duniani WEF huko Davos Uswisi kwamba ukosefu wa ushirikiano wa kimataifa unaiweka rehani dunia kwa majanga ya mabadiliko ya tabianchi na AI-Mradi wa mfuko wa kimataifa wa ufadhili wa maendeleo ya kilimo IFAD waimarisha kiuchumi watu wenye ulemavu wa kuona Liberia-Makala inatupeleka jimboni Kandahar Afghanistan kukukutanisha na mkulima wa ngano aliyenufaika na mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO unaotoa mafunzo ya kilimo, kugawa mbegu na pembejeo kwa wakulima-Na mashinani tunabisha hodi Kenya kumsikia mkimbizi mfanyabiashara ndogo ndogo,
    12 min
  • 21 JANUARI 2025
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea -Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres asikitishwa na hatua ya serikali ya Marekani kutangaza kujitoa kwenye mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi wa Paris na kuitaka kufikiria upya uamuzi huo-Rais Donald Trump wa Marekani ametia saini amri ya kiutendaji ya kuondoa uanachama wa Marekani kwenye shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO-Gaza kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa malori ya misaada yanaendelea kuingia Gaza baada ya kuanza utekelezaji wa usitishaji uhasama-Mada kwa kina leo inatupeleka Bahrain Asia Magharibi kumulika uzamiaji na uvunaji wa kito cha thamani cha lulu-Na mashinani tunabisha hodi Kajiado Kenya kuangazia juhudu endelevu za utunzaji wa misitu 
    12 min
  • Asante sana walinda amani wa UNIFIL kwa ujasiri wenu, katu hatutasahau huduma yenu bora mnayotoa - Guterres
    Nchini Lebanon tarehe 17 mwezi huu wa Januari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa ziarani Lebanon alitembelea walinda amani wa Umoja wanaohudumu chini ya ujumbe wa Mpito wa UN nchini Lebanon, UNIFIL, ambao walikumbwa na zahma wakati jeshi la Israeli liliposhambulia kituo chake kinyume na azimio namba 1701 la mwaka 2006, linalozuia mashambulizi kwenye eneo tenganishi kati ya Israeli na Lebanon. Walinda amani hawa walijeruhiwa wakati kituo chao kiliposhambuliwa na jeshi la Israeli, kinyume na makubaliano ya kutoweko kwa jeshi eneo la mstari wa buluu, au tenganisha kati ya Lebanon na Syria, kama anavyoeleza Thelma Mwadaya katika makala hii.
    4 min
  • Elimu haina umri wala kuchelewa, wala mwisho: Philip Long'olea
    Migogoro, vita na mabadiliko ya tabianchi mara nyingi vimekuwa vikiwapora watoto fursa ya elimu na hata kusambaratisha mustakbali wao na wengi wanajikuta wakiishia kwenye makambi ya wakimbizi linasema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Kwa kulitambua hilo shirika hilo linaendesha miradi mbalimbali ya kuhakikisha watoto waliokosa elimu hata kama wana umri mkubwa wanapewa fursa ya pili kusoma kama ilivyokuwa kwa mkimbizi Philip Lon’golea kutoka Sudan aliyekimbilia Uganda kwanza lakini sasa yuko kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Cicely Kariuki anatujuza zaidi
    3 min
  • 20 JANUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia juhudi za kukabiliana na mlipuko wa homa ya marburg Tanzania, na elimu kwa wakimbizi katika makazi ya Kakuma nchini Kenya.  Makala inatupeleka nchini Lebanon na mashinani inaturejesha Gaza.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, WHO, Dkt. Tedros Ghebreyesus amesema wanashirikiana na serikali ya Tanzania kudhibiti mlipuko wa homa ya Marbug iliyoripotiwa mkoani Kagera, kaskazini magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki.Migogoro, vita na mabadiliko ya tabianchi mara nyingi vimekuwa vikiwapora watoto fursa ya elimu na hata kusambaratisha mustakbali wao na wengi wanajikuta wakiishia kwenye makambi ya wakimbizi linasema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Kwa kulitambua hilo shirika hilo linaendesha miradi mbalimbali ya kuhakikisha watoto waliokosa elimu hata kama wana umri mkubwa wanapewa fursa ya pili kusoma kama ilivyokuwa kwa mkimbizi Philip Lon’golea kutoka Sudan aliyekimbilia Uganda kwanza lakini sasa yuko kwenye kambi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya.Katika makala Thelma Mwadzaya anatupeleka Lebanon ambako tarehe 17 mwezi huu wa Januari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa ziarani Lebanon alitembelea walinda amani wa Umoja wanaohudumu chini ya ujumbe wa Mpito wa UN nchini Lebanon, UNIFIL, ambao walikumbwa na zahma wakati jeshi la Israeli liliposhambulia kituo chake kinyume na azimio namba 1701 la mwaka 2006, linalozuia mashambulizi kwenye eneo tenganishi kati ya Israeli na Lebanon.Na mashinani tutaelekea Gaza kusikia kauli kutoka kwa mkimbizi wa ndani baada ya kuanza kutekelezwa usitishaji uhasama na kuachiliwa kwa mateka na wafungwa.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Angela Tabiri, mbobevu wa hisabati anayehaha kuona wasichana Afrika wanapenda STEM
     Ikiwa Umoja wa Mataifa unaunga mkono masomo ya Sayansi, Teknolojia na Hisabati, au STEM, Angela Tabiri ni mwanahisabati bora duniani, Mtafiti na Mhadhiri kutoka Chuo cha African Institute for Mathematical Sciences (AIMS) kilichoko Accra nchini Ghana Magharibi mwa bara la Afrika, amekuwa akitoa mchango katika kuhakikisha wasichana nchini humo wanapata elimu ya hisabati kupitia taasisi yake ya FemAfricMaths. Kwa kufanya hivyo anatimiza lengo namba 4 ya Malengo endelevu ya Umoja Mataifa(SDGs) linalohimiza elimu bora kwa wote na lile namba 5 linalozungumzia usawa wa kijinsia. Kutoka mjini Mwanza kaskazini magharibi mwa Tanzania, Sabrina Moshi wa redio washirika Saut Fm amefanya mahojiano na mtaalamu huyo. Angela anaanza kwa kueleza namna alivyokuwa na ndoto hadi kuanzisha FemAfricMaths ili kuwasaidia wasichana barani Afrika.
    5 min
  • Antonio Guterres atembelea kikosi cha UNIFIL na kukipongeza kwa kazi nzuri
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amepongeza na kutoa shukrani kubwa kwa uvumilivu na kujitolea kunakofanywa na walinda amani wa Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL, wakati wa ziara yake hii leo katika makao makuu kikosi hicho mjini Naqoura. Flora Nducha na taarifa zaidi Asante Assumpta Guterres ambaye yuko Lebanon tangu jana kwenye ziara ya mshikamano akizungumza na uongozi wa kikosi hicho cha UNIFIL na wafanyakazi, amewapongeza kwa ujasiri na juhudi zao katika mazingira magumu zaidi ya kazi ya kulinda amani duniani.Amesema “Hampo tu kwenye mstari wa Bluu wa Lebanon, mpo kwenye mstari wa mbele wa amani,”akitambua jukumu lao muhimu katika kudumisha utulivu licha ya mashambulizi na vitisho vya kiusalama.Katibu Mkuu ameelezea kuhusu mchango muhimu wa kikosi hicho katika kuzuia vurugu, kupunguza mvutano, kuruhusu upatikanaji wa misaada ya kibinadamu, na kuwalinda raia amesema “Kazi yenu imekuwa muhimu na ya kipekee katika kurejesha utulivu kusini mwa Lebanon na katika mstari wa Bluu.”Audio fileAmesisitiza umuhimu wa kufuata Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa namba 1701, akitoa wito kwa pande zote kuheshimu usalama wa maeneo ya Umoja wa Mataifa na kuhakikisha usalama wa walinda amani ikiwemo msitari wa Bluu amba oni eneo tenganishi baina ya Israel na Lebanon.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa ameonya kwamba “Mashambulizi dhidi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa  hayakubaliki kabisa, yanakiuka sheria za kimataifa, na yanaweza kuwa uhalifu wa kivita.”Pia alilaani uwepo wa vikundi vyenye silaha na ukiukwaji unaofanywa na vikosi vya ulinzi vya Israeli ndani ya eneo la kazi la UNIFIL.Akiangazia siku zijazo, Guterres ameelezea matumaini ya kipindi endelevu cha utulivu na maendeleo katika kutekeleza Azimio namba 1701, linalolenga kuimarisha amani na utulivu wa kudumu kati ya Lebanon na Israeli.Amehitimisha taarifa yake kwa kusema“Kwa pamoja, tunaweza kufanikisha fursa hii ya kipekee,” na kuahidi kuendelea kuunga mkono kikosi hicho na kushirikiana kwa karibu na nchi zinazochangia wanajeshi wa UNIFIL ili kuboresha uwezo wa kiutendaji na kuhakikisha usalama wa walinda amani.
    3 min
  • Hisia mchanganyiko Gaza baada ya tangazo la sitisho la uhasama
    Leo ni siku ya tatu tangu kutolewa tangazo la muafaka wa usitishaji uhasama Ukanda wa Gaza kati ya Israel na kundi la Palestina la Hamas, muafaka utakaoanza kutekelezwa mwishoni mwa wiki. Je raia wa Gaza wanahisi vipi baada ya miezi 15 ya jinamizi la vita? Selina Jerobon anatupasha zaidi katika taarifa iliyoandaliwa na mwandishi wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa kutoka Gaza.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners