Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UN: Vifo vitokanavyo na baridi Gaza vinazuilika, usitishaji mapigano na misaada ndio jawabu
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM leo limeonya juu ya vifo vitokanavyo na msimu wa baridi kali Gaza likisema limesikitishwa sana na athari mbaya za mvua za msimu wa baridi na baridi kali kwa Wapalestina waliokimbia makazi yao na kuishi katika mazingira magumu huko Gaza, kwani hilo ni janga la kibinadamu lisilo na kifani. Kupitia taarifa iliyotolewaleo mjini Geneva Uswisi Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope  amesema "Watu walio katika mazingira magumu, ikiwa ni pamoja na takriban watoto wachanga saba, wamekufa kutokana na baridi kali au hypothermia, na vifo hivi vya kusikitisha vinasisitiza haja ya haraka ya makazi na msaada mwingine wa kibinadamu kuwafikia watu wa Gaza mara moja," Ameongeza kuwa hali hii inachochea janga zaidi la kibinadamu ambalo tayari linawakumba watu waUkanda wa Gaza. Mvua kubwa na mafuriko yameyakumba makazi ya wakimbizi wa ndani yaliyojengwa kwa mahema na kulazimisha familia kuachwa katika maeneo ya wazi kwenye hali mbaya ya baridi, zikijitahidi kutengeneza mahema yaliyoharibika kutokana na matumizi ya miezi kadhaa. © UNRWAChakula kinagawiwa kwa watu waliokimbia makazi yao huko Jabalia, kaskazini mwa Gaza.Vikwazo vya Israel ni changamoto kwa misaadaPia IOM imesema vikwazo vya utaratibu wa kufikia wenye uhitaji, kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA, vimezuia kwa kiasi kikubwa utoaji wa misaada, huku watu 285,000 pekee wakipokea msaada wa makazi tangu Septemba 2024. Kwa mujibu wa IOM hadi kufikia Katikati ya Desemba mwaka jana inakadiriwa kuwa watu wapatao 945,000 bado wanahitaji msaada wa haraka wa kukabiliana na msimu wa baridi ikiwemo nguo za kuongeza joto, mablanketi na tepu za kuima mahema dhidi ya mvua na baridi. Tangu Katikati ya Novemba mwaka jana IOM imewasilisha karibu vifaa 180,000 vya makazi ya dharura kwa washirika ndani ya Gaza na ina zaidi ya vifaa milioni 1.5 vya msimu wa baridi ikiwemo mahema, vifaa vya kuziba  na vitanda ambavyo viko tayari kwenye maghala na sehemu zavivuko, lakini vikwazo vikali vya ufikiaji vinawazuia kufikia wenye uhitaji. © UNICEF/Abed ZaqoutWavulana wawili wakibeba chupa za maji katika kambi ya wakimbizi inayofadhiliwa na UNWRA huko Khan Younis kusini mwa Gaza.Usitihsaji mapigano ndio suluhuIOM imesisitiza wito wake wa dharura wa kusitisha mapigano ili kuwezesha utoaji salama na wa haraka wa msaada wa kuokoa maisha kwa wale wanaouhitaji sana. Pia inasisitiza wito wake kwa pande zote kuzingatia sheria za kimataifa za kibinadamu, kuhakikisha ulinzi wa raia, kuachiliwa kwa mateka wote na kuruhusu ufikiaji salama, wa haraka, usiozuiliwa na endelevu wa wenye uhitaji. Watu wa Gaza wanastahili usalama, makazi na utu. IOM iko tayari kuhamasisha misaada na kusaidia jamii zilizofurushwa, lakini fursa ya ufikiaji wa kibinadamu lazima itolewe ili kuwezesha hili amesisitiza mkuu wa IOM. Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limesema Licha ya hali ngumu, timu za UNRWA zinaendesha makao yote ya Umoja wa Mataifa, na kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watu wanaohitaji. Limeongeza kuwa Vita vilipoanza karibu miezi 15 iliyopita, UNRWA iligeuza shule zake, vituo vya afya, na maghala kuwa makazi na kuna wakati ambapo vita ikiendelea UNRWA ilipokea watu milioni 1 waliokimbia makazi yao 
    2 min
  • Papua New Guinea: Tuhuma za uchawi dhidi ya wanawake zapatiwa  ‘muarobaini’
    Kila mwaka, mamia ya wanawake nchini Papua New Guinea, taifa la visiwani katika bahari ya Pasifiki, hushutumiwa kimakosa kuwa ni wachawi. Matokeo yake hukumbwa na ukatili miongoni mwa wanajamii. Hata hivyo Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Maendeleo duniani, UNDP nchini humo, limechukua hatua.Kiongozi mkubwa wa Kijiji chetu alifariki dunia, na tulipoenda kwenye maziko, ambapo kila mtu alisema sisi ni wachawi na tulikula moyo wake. Ni kauli ya Annabele, jina lake halisi limehifadhiwa kwa ajili ya usalama wake akielezea tuhuma zilizowakabili kwenye jamii yao ya jimbo la Enga nchini Papua New Guinea, hadi kushambuliwa kwa nondo za moto na nyumba zao kuteketezwa kwa moto. Video ya UNDP inamnukuu akisema kuwa walikuwa 9, ambapo wanne walifariki dunia na watano akiwemo Annabele, walinusurika, “kesho yake asubuhi Askofu na wenzake walifika, halikadhalika jeshi na polisi, na ndio walituokoa.” Askofu huyo Justine Soongie Dayosisi ya Wabag jimboni Enga anasema walipowachukua waliambiwa wahakikishe hawarudi kijijini, “sababu kubwa ya mtu kutuhumiwa ni jamii kukosa uelewa kuhusu chanzo cha kifo. Watu wengi hawafahamu kuwa mtu anaweza kufa kutokana na kiharusi. Watu wetu wa Enga watauliza ni nani amesababisha?” Annabelle baada ya kuokolewa alipelekwa hospitali na kupatiwa matibabu ambayo hata hivyo bado ana kovu na maumivu. Kisha walipelekwa nyumba salama zinazoendeshwa na Kanisa Katoliki kwa ufadhili wa UNDP, ambako waliishi kwa miezi takribani mitano wakipatiwa mavazi, malazi na chakula. Askofu Justine Soongie anasema,“baada ya miezi kadhaa hospitalini, tunarudi kwa familia na jamii na kuzungumza nao mara kadhaa. Tunawaelimisha kuwa ni kosa kumtuhumu mtu uchawi, kuna sheria, na hana pahala pengine pa kwenda, hivyo atarudi.” Jamii ilieleweshwa na Annabelle kwenye video anaonekana tayari yuko kijijini na sasa analima shamba na hata anasema hata mazao anayolima akivuna, anapika na wanajamii wanakula pamoja naye. 
    3 min
  • 03 JANUARI 2025
    Vifo vitokanavyo na baridi Gaza vinazuilika, usitishaji mapigano na misaada ndio jawabu: UN.Tuhuma za uchawi dhidi ya wanawake Papua New Guinea zapatiwa  ‘muarobaini’ na UNDP.Makala ni kuhusu Gibson Kawago, mwanzilishi wa kampuni ya WAGA akizungumzia kuanzisha vifaa vya kuchaji magari ya umeme Tanzania.Mashinani ni IFAD Zimbabwe. 
    10 min
  • 31 DESEMBA 2024
    Kipindi maalumu wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wenyeji wao wanaeleza namna walivyonufaika na misaada ya Umoja wa Mataifa na mashirika yake na pia wanaeleza matumaini yao kwa mwaka ujao wa 2025. 
    12 min
  • 30 DESEMBA 2024
    Leo jaridani: Mwaka 2024 ulighubikwa na machungu lakini kuna matumaini 2025 asema Guterres.UNMAS yaondolea hofu wakulima Beni, DRC kwa kutegua masalia ya mabomu.Makala inatupeleka Uganda kusikiliza msichana mkimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Ashiimwe Baganiza mwenye ndoto ya kuwa wakili ili kuwatetea wanawake.Mashinani ni mradi wa Siku 1000 wa UNICEF Zambia. 
    11 min
  • Nilikuwa miongoni mwa Wacuba wa kwanza kujifunza Kiswahili: Profesa Jacomino
    Ujumuishwasji wa lugha mbalimbali katika dunia iliyoshikamana katika Nyanja mbalimbali ni moja ya malengu ya Umoja wa Mataifa kuanzia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa hadi kwenye nchi wanachama unalichagiza hilo. Hamasa hiyo imezichagiza nchi nyingi kuanza kukumbatia lugha ambazo kwa asili hazizungumzwi kama alivyobaini Flora Nducha wa Idhaa hii ambaye hivi karibuni alikuwa Cuba kwenye Kongamano la Kimataifa la Kiswahili na kukutana na Profesa Juan Jacomino ambaye ni mhadhiri katika chuo kikuu cha Havana na ni miongoni mwa watu wa mwanzo waliokwenda Tanzania kujifunza Kiswahili na sasa anakifundisha nchini mwake Cuba. Anafafanua kuhusu safari yake ya kujua Kiswahili katika makala hii..
    6 min
  • 27 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia sherehe za krismasi katika ukanda wa Gaza lich ya migogoro inayoendelea, na magonjwa ya mlipuko. Makala inatupeleka Havana Cuba na mashinani nchini Uganda, kulikoni?Katika kuandhimisha Siku ya Kimataifa ya Kujitayarisha dhidi ya Magonjwa ya Mlipuko, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi kote ulimwenguni kuzingatia masomo yaliyopatikana katika dharura za kiafya zilizopita ili kusaidia kujiandaa kwa dharura zijayo.Tukiwa bado katika msimu wa sikukuu ya krismasi, tunakwenda mji wa Gaza, huko Ukanda wa Gaza, Mashariki ya Kati kusikia jinsi sikukuu hii ilivyoadhimishwa na hisia mchanganyiko kwenye kanisa katoliki la Familia Takatifu kwenye viunga vya zamani kwenye mji huo.Makala inatupeleka Havana Cuba kuangazia umuhimu wa utekelezaji wa moja ya ajenda za Umoja wa Mataifa ya kukumbatia lugha mbalimbali duniani ambapo Flora Nducha wa Idhaa hii akiwa Cuba hivi karibuni kwenye kongamano la Kimataifa la Kiswalihi alikutana na raia wa nchi ambaye ni mwalimu wa Kiswahili.Mashinani fursa ni yake Ange Rukenura, msichana alieyekimbia makazi yake pamoja na ndugu zake sita kufuatia mashambulizi ya waasi waliojihami nchini  Jamhuri ya Kidemocrasi ya Congo, DRC akisema licha ya rasilimali ndogo anashukuru ukarimu wa Uganda na msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR kwa kuwapatia matumaini.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners