Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 19 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Syria, ambako viongozi wa ngazi mbalimbali za Umoja wa Mataifa wamendelea kusisitiza hitaji la kutanguliza ulinzi wa manusura na uhifadhi wa ushahidi wa uhalifu. Pia tunapata ufafanuzi wa neno na muhtasari wa habari.Karla Quintana kutoka Mexico ameteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres hii leo kuongoza Taasisi Huru ya kuchunguza watu waliotoweshwa nchini Syria, taasisi ambayo imeundwa na Baraza la Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Juni mwaka jana 2023. Guterres amewaambia waandishi wa habari hii leo kwamba yeye na timu yake lazima waruhusiwe kutekeleza kwa kina jukumu lao, na vile vile mifumo yote ya kimataifa ya kusongesha ulinzi wa haki za binadamu nchini Syria na uwajibikaji wa uhalifu uliotendwa lazima wawe na wanachohitaji ili kutekeleza majukumu yao muhimu.Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekuwa na kikao cha ngazi ya mawaziri kuhusu Akili Mnemba, au AI ambapo Katibu Mkuu António Guterres amesema pamoja faida kubwa ya teknolojia hiyo bado kuna changamoto iwapo haitasimamiwa vema na binadamu. Hivyo amependekeza kuundwa mwa mfumo wa kimataifa wa kuendeleza Akili Mnemba kwa uwiano na usawa, ukijikita kusaidia nchi zinazoendelea kuzuia kuibuka kwa pengo la teknolojia hiyo kati ya walio nayo na wasio nayo.Na huko Bunia, jimboni Ituri mashariki mwa Jamhuri ya Kidemorkrasia ya Congo, DRC vijana 24 wakiwemo wanawake 6 wamenufaika na mafunzo ya siku tano ya mbinu za kisasa za kilimo kutoka walinda amani wa Bangladeshi wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUSCO. Lengo ni kuwezesha kilimo kuwa chanzo cha kipato kwa wakazi na kuimarisha uchumi wa eneo hilo.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya neno “AKRABA.” Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!  
    10 min
  • FAO Tanzania yatoa mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa wenyeji Tanzania kupitia Mradi wa ACP MEAs 3
    Mradi wa ACP MEAs 3 unaoendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO, na kufadhiliwa na Muungano wa Ulaya, EU umetoa mafunzo ya ufugaji nyuki kwa wakulima nchini Tanzania. Mradi huu unawapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu, na hivyo kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kwa kuunga mkono jamii za wenyeji, Mradi huu unalenga kukuza ukuaji wa uchumi na kuwawezesha wakulima kulinda wachavushaji, ambao ni muhimu kwa uzalishaji katika kilimo na afya ya mfumo ikolojia. Tupate simulizi zaidi katika makala hii iliyoandaliwa na Flora Nducha kupitia video ya FAO Tanzania.
    3 min
  • Guterres: Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji tujikumbushe changamoto wanazokumbana nazo
    Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya Uhamiaji, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
    2 min
  • 18 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia siku ya wahamiaji duniani ikimulika mchango wa wakimbizi na wahamiaji katika ukuaji wa kiuchumi na kukuza jamii zao n aza wenyeji. Tutasikia kutoka mkuu wa IOM, Katibu Mkuu wa UN na wahamiaji Burundi na Chad. Pia tunaangazia ufugaji nyuki Tanzania.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kupitia ujumbe wake mahususi kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji ametoa wito kwa ulimwengu kuitumia siku hii kujikumbusha kwamba pamoja na kwamba tunasherehekea michango ambayo mamilioni ya wahamiaji hutoa kwa jamii leo pia ni siku ya kujikumbusha changamoto ambazo wahamiaji wanaweza kukumbana nazo.Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM.Makala inatupeleka nchini Tanzania kufuatilia Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO uitwao ACP MEAs 3 ambao umwewapa wakulima zana na ujuzi muhimu katika ufugaji nyuki endelevu kwa lengo la kuboresha maisha yao huku wakikuza bayoanuwai na uhifadhi wa mazingira. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO Tanzania Selina Jerobon amefuatilia mafanikio ya mradi huu na kituandalia makala hii.Na mashinani katika siku hii ya kimataifa ya wahamajia Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linasisitiza umuhimu wa kuwawezesha wanawake na wasichana walio ukimbizini na kuongeza mikakati ya kifedha inayozingatia jinsia. Bi Banti Ahmat ni mmoja wa wakimbizi na anelezea jinsi ambavyo mradi wa IOM wa bustani za jamii unavyoleta matokeo chanya kwa wahamiaji na jamii za wenyeji nchini Chad.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min
  • Mafunzo ya IOM kwa msichana mhamiaji mwenye ulemavu, yaleta furaha kwa mama yake
    Nimefurahi sana kwani binti yangu mwenye ulemavu ambaye tulihamia naye makazi ya muda kufuatia kuongezeka kina cha maji ya Ziwa Tanganyika, hapa Burundi sasa amepatiwa stadi za kumwezesha kujikwamua kiuchumi. Ni kauli ya Odette Niyonkuru, raia mhamiaji wa ndani nchini Burundi akizungumzia mustakabali wa binti yake huyo kwenye video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM. Odette anaenelea kueleza manufaa ya uwezeshaji huu kwa bintiye kama anavyofuatilia Assumpta Massoi.
    3 min
  • 17 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika mafanikio katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU na juhudi za vijana wakimbizi nchini Uganda kuhakikisha hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka Gaza.Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili  ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Ethiopia kumulika mwelekeo wa usajili wa watoto wanapozaliwa na faida zake.  Na mashinani Maram, mama kutoka Deir al-Balah Gaza, ambako familia zinahaha kuokoa mali zao na kukarabati mahema yao yaliyoharibiwa na upepo mkali na maji ya mvua wakati huu wa msimu wa baridi, na kuleta athari kwa watoto wao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    11 min
  • Harakati za wazazi kuona watoto wao wanasajiliwa nchini mwao baada ya kuzaliwa
    Tarehe 11 mwezi huu wa Desemba, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF lilitoa ripoti yake kuhusu usajili wa vizazi duniani ikionesha maendeleo makubwa katika idadi ya watoto wanaosajiliwa na kupatiwa vyeti vya kuzaliwa. Maeneo mengine kama nchi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara ongezeko ni dogo ikilinganishwa na kwingineko. Ingawa hivyo licha ya changamoto zilizoko kwa nchi za Afrika zilizo Kusini mwa jangwa la Sahara katika kutoa huduma hiyo, mafanikio yanaanza kuonekana kama inavyosimulia makala hii iliyoandaliwa na Assumpta Massoi kupitia video ya UNICEF.
    5 min
  • Mjumbe wa UN aendelea na ziara ya kukutana na wadau nchini Syria
    Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili  ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi. Ikiwa ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Mataifa kuhakikisha mabadiliko ya utawala nchini Syria yanafanyika kwa amani na kuisaidia Syria kutokuingia kwenye mgogoro zaidi, Bwana Pederson aliyewasili jana Damascus  hadi sasa ameshakutana na Kamanda wa Utawala Mpya Ahmed al-Sharaa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Muda Mohammed al-Bashir.Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi yake inasema Pederson ameeleza muhtasari wa matokeo ya Mkutano wa Kimataifa wa Aqaba kuhusu Syria uliofanyika tarehe 14 ya mwezi huu wa Desemba akisisitiza haja ya kuwepo kwa mpito wa kisiasa unaoaminika na unaoongozwa na kumilikiwa na Wasyria wenyewe kama kanuni za azimio 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (2015) zilivyopendekeza. Aidha Mjumbe huyo maalum amesisitiza azma ya Umoja wa Mataifa ya kutoa usaidizi wa kina kwa watu wa Syria.Taarifa imedokeza kuwa Bwana Pedersen ana shughuli nyingi zilizopangwa siku zijazo katika harakati za kusaka suluhu ya amani nchini Syria.
    2 min
  • 16 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia serikali ya mpito nchini Syria na wakimbizi na wahamiaji wanaosaka hifadhi nchini Uganda. Makala tunakupeleka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Syria Geir O. Pedersen bado yuko nchini Syria alikowasili jana Jumapili  ikiwa ni wiki moja baada ya wapiganaji wa Hayʼat Tahrir al-Sham (HTS) walioko kwenye orodha ya vikundi vya kigaidi kutwaa mji mkuu Damascus na kusababisha Rais Bashar Al-Assad kukimbia nchi.Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, sirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR nchini Uganda limetoa rai kwa jumiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewamwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na Ethiopia kumulika mwelekeo wa usajili wa watoto wanapozaliwa na faida zake.  Na mashinani fursa ni yake Mkombola Melio, mhudumu wa afya ambaye pia ni mnufaika wa mradi wa maji na usafi uitwao RUWASA au Rural Water and Sanitation project inaofadhiliwa na Benki ya Dunia Afrika nchini Tanzania akisema mradi huo umezisaidia jamii kuondokana na maambukizi yanayosababisha magonjwa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners