Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNHCR: Chonde chonde jumuiya ya Kimataifa tuishike mkono Uganda kwa faida ya waomba hifadhi na wakimbizi
    Mwaka 2024 ukielekea ukingoni, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR  nchini Uganda limetoa rai kwa jumuiya ya kimataifa kutolisahau taifa hilo la Afrika Mashariki ambalo ni maskani ya idadi kubwa zaidi ya waomba hifadhi na wakimbizi barani Afrika. Rai hiyo iliyotolewa mwishoni mwa wiki inataka ufadhili wa fedha uongezwe ili liweze kuendelea kukirimu watu hao ambao wengi wanakimbia machafuko. Huyo ni Moulid Hujale afisa wa UNHCR nchini Uganda akitoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kushikamana na Uganda akiwa  kwenye makazi makubwa ya wakimbizi ya Kiryandongo Magharibi mwa nchi hiyo. Anasema kuna mambo matatu muhimu ambayo dunia inapaswa kufahamu kuhusu Uganda na wakimbizi.“Mosi Uganda inahifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi na waomba hifadhi Afrika ikiwa na zaidi ya watu milioni 1.7 wengi wao wakitoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC na Sudan Kusini.”Zaidi ya hapo ukarimu wa Uganda anasema hauna kipimo“Pili, Uganda ina sera ya kufugua mlango kwa wakimbizi na pia kwa miongo mingi imekuwa ikiwakaribisha watu wanaokimbia machafuko bila kujali utaifa wao. Kitu ambacho ni kikubwa na cha kipekee kuhusu nchi hii ni kwamba wakati wakimbizi wanapowasili hapa hupewa ardhi, mahali pa kuishi na hata kulima mazao kwa ajili ya kujikimu. Wana uhuru wa kutembea na haki ya kuajiriwa. Hawajatengwa lakini wanaishi  ndani ya jamii inayowahifadhi. Sera hii ya Uganda inawaruhusu wakimbizi kujumuishwa katika huduma za kitaifa ambapo wanafaidika na elimu na huduma za afya.”Lakini Kutokana na changamoto za fedha Moulid anasema ukarimu huo sasa uko njia panda"Tatu: Ukarimu wa Uganda uko hatarini kwani wakimbizi zaidi wanaingia kutoka nchi jirani. UNHCR, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, liko mashinani kufanya kazi na Serikali ya Uganda kusaidia kutoa msaada wa kuokoa maisha kwa watu hawa. Hata hivyo, rasilimali ni chanche. Tunahitaji msaada wenu ili Uganda iendelee kuwa mfano wa kuigwa kwa dunia nzima.”Kwa nyjibu wa UNHCR licha ya idadi kubwa ya watu na rasilimali kidogo, sera za Uganda zinammanisha kwamba wakimbizi ni sehemu ya maisha ya kijamii na kiuchumi na ongezeko la rasilimali litakidhi haja za waliopo sasa na watakaokuja.
    3 min
  • Sasa tunalima mboga shuleni na nyumbani - Wanafunzi Buhigwe Tanzania
    Kupitia mradi wa Pamoja wa Kigoma, KJP,  awamu ya Pili, Shule ya Msingi Buhigwe, iliyoko wilayani Buhigwe, mkoa wa Kigoma, ilipatiwa mafunzo kupitia Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), likishirikiana na asasi isiyo ya kiserikali RECODA. Mafunzo haya yalilenga mbinu bora za kilimo ambapo wanafunzi waliweza kuanzisha bustani za mboga kupitia somo la Elimu ya Kujitegemea. Mradi umeanza kutekelezwa na matunda yanaanza kuonekana kama asimuliavyo Assumpta Massoi kwenye makala hii.
    4 min
  • 13 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia hali nchini Syria, na msaada wa kibinadamu kw awakimbizi nchini Chad. Makala inatupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC, kulikoni?Ofisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa.Kutokana na idadi kubwa ya wakimbizi wanaoingia Chad wakitoka Sudan kuwa ni wanawake na watoto, Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi,  UNFPA limeimarisha huduma za afya ya wanawake na watoto.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Tanzania kusikia jinsi wanafunzi wananufaika na mradi wa Umoja wa Mataifa shuleni na majumbani.Na mashinani fursa ni yake Aline kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC ambaye ni mnufaika wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP wa kuwezesha wanawake na wasichana kusoma na kuandika ili waweze kujimudu kimaisha na kuondokana na unyanyasaji wa kijinsia, akisema JHARDEE anamaanisha bustani, na LEGYUME ni maharage.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min
  • UN: Lazima kuhakikisha Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao
    Ofisi ya mjumbe Maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syria (OSE) imesema wakati huu ikifuatilia kwa karibu hali na maendeleo nchini Syria ni muhimu kuhakikisha kwamba Wasyria wanashika usukani wa mustakbali wao na kwamba kuna ujumbe wa pamoja na mshikamono kuhusu hilo kutoka kwenye jumuiya ya kimataifa. Flora Nducha na taarifa zaidi.
    2 min
  • 12 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa ikiangazia wanawake na wasichana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambapo ukatili wa kingono ni jinamizi linalowakumba kila uchao kutokana na mapigano yanayoendelea kwenye eneo hilo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno MIDABWADA.Leo si siku ya kimataifa ya huduma za afya kwa wote mwaka huu ikibeba mudhui “Huduma za afya kwa wote ni jukumu la serikali” yakisisitiza kwamba Uwekezaji katika huduma za afya kwa wote UHC, unaimarisha usawa na uwiano wa kijamii na pia unanufaisha uchumi wa taifa kwa kuboresha afya na ustawi, kuongeza ushiriki wa wafanyikazi na tija, na kujenga mnepo kwa watu, familia na jamii.Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Syri Geir O. Pedersen leo amesema “Picha kutoka kwenye magereza ya Sednaya na vituo vingine vya kizuizini nchini Syria vinadhihirisha unyama na ukatili usiofikirika ambao Wasyria wamevumilia na umekuwa ukiripotiwa kwa miaka mingi.”Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres yuko ziarani Lesotho ambako akihutubia Bunge la nchi hiyo amesema bara la Afrika lina utajiri mkubwa wa vyanzo vya nishati endelevu kuanzia sola, upepo hadi maji lakini bado haijatumika ipasavyo kwani waafrika milioni 600 hawana umeme.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MIDABWADA”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    10 min
  • Baada ya kunusuriwa na programu ya IOM, mhamiaji kutoka nchini Ethiopia asema katu hatorudi Yemen
    Janga la kibinadamu likizidi kushika kasi nchini Yemen, shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM linaongeza kasi ya mpango wake wa kurejesha wahamiaji nyumbani kwa hiari, VHR. Mradi huu hupatia wahamiaji waliokwama njia salama ya kurejea nyumbani kwao. Kupanuliwa kwa mradi huu kunafuatia idadi ya wahamiaji nchini Yemen kuongezeka na kufikia 6,300 mwezi Oktoba mwaka huu, kwa mujibu wa mfuko wa IOM wa  Ufuatiliaji wa wahamiaji.Mwaka huu wa 2024, IOM imeshafanya safari 30 za ndege kupitia mradi huo wa VHR ikiwemo ya tarehe 5 mwezi huu waDesemba ambapo wahamiaji 175 wa Ethiopia walirejeshwa Yemen kutoka uwanja wa ndege wa Aden. Makala hii inafuatilia miongoni mwa wahamiaji hao yaliyowasibu hadi kukubali kurejea nyumbani kwa hiari. Msimulizi wako ni Assumpta Massoi.
    5 min
  • 11 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya WHO inayohusu malaria, na juhudi za UNICEF na wadau wake nchini Rwanda za kusaidia watoto waliozaliwa na ulemavu kuweza kutembea. Makala tunakupeleka nchini Yemen na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Takwimu mpya zilizotolewa leo na ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO, zinaonyesha kuwa ingawa takriban wagonjwa bilioni 2.2 wa malaria na vifo milioni 12.7 vya ugonjwa huo vimeepukwa tangu mwaka 2000 bado ugonjwa huo unaendelea kuwa tishio kubwa la kimataifa la afya hususan katika Kanda ya Afrika ya WHO na hivyo juhudi zaidi zahitajika kuutokomeza.Nchini Rwanda Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa msaada wa UNICEF Uswisi na Liechtenstein wamesaidia tiba kwa njia ya mazoezi kuponya watoto wenye ulemavu wa viungo. Selina Jerobon anasimulia akiangazia mtoto mmoja, Joshua.Katika makala Assumpta Massoi anakupeleka Yemen kusikia yaliyojiri baada ya ndoto za vijana kuelekea Saudi Arabia kuishia Yemen.Na mashinani mashinani hivi majuzi dunia iliadhimisha siku ya watu wenye ulemavu duniani ikiangazia uthabiti, ujumuishaji na fursa sawa kwa wote. Kutana na Dorice Mkiva, Mtaalamu wa usimamizi wa maarifa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Tanzania ambaye alipoteza uwezo wake wa kutembea akiwa na umri mdogo na sasa anatumia sauti yake kutetea haki za watoto.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners