Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNFPA: Elimu ndio ufunguo wa kutokomeza FGM Kenya
    Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu tunaelekea Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa  ya idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA kutokomeza janga hilo. Mwandishi wetu wa Nairobi Thelma Mwadzaya amefuatilia kuhusu suala hilo na kwa undani zaidi ungana naye ..
    6 min
  • 10 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na tunaelekea nchini Kenya kuangazia moja ya ukiukwaji Mkubwa wa haki za binadamu dhidi ya wanawake, jinamizi la ukeketaji na jitihada zinazochukuliwa na UNFPA na wadau mbalimbali. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na mashinani inayotupeleka nchini Namibia.Baada ya serikali ya Bashar Al-Assad kupinduliwa na kuibuka kwa taarifa za baadhi ya nchi duniani kuanza kusitisha mchakato wa kushughulikia maombi ya Wasyria waliokuwa wameomba hifadhi kuokoa usalama wa maisha yao pindi hali ilipokuwa tete nchini mwao, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) linaendelea kutoa wito kwa mataifa yote kufungua milango, kuwapa hifadhi na ulinzi raia wa Syria wanaotafuta usalama. UNHCR imeahidi pia mara tu hali ya Syria itakapokuwa wazi zaidi, itatoa mwongozo kuhusu mahitaji ya ulinzi kwa Wasyria walioko hatarini.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limekaribisha mchango wa dola za Marekani milioni 22 kutoka shirika la Korea Kusini la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa (KOICA) ili kuimarisha mnepo kwa tabianchi na uhakika wa chakula kwa wakulima wadogo, wafugaji na makundi yaliyoko pembezoni nchini Kenya, Somalia na Sudan Kusini. Vituo vya utabiri wa hali ya hewa vinatabiri hali ya La Niña mashariki mwa Pembe ya Afrika na uwezekano wa kupunguza mvua katika kipindi hikiNa walinda amani wa kikosi cha 11 cha Tanzania -TANZBATT-11 kinachohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, MONUSCO jimboni Kivu Kaskazini wametunukiwa nishani ya umoja wa mataifa ikiwa ni alama ya kufanya kazi  kwa utii,uhodari na uaminifu. Miongoni mwao ni Private Selina Kisemvule.Katika mashinani ikiwa ni siku ya mwisho ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, fursa ni yake Rais Nangolo Mbumba wa Namibia ambaye kupitia ukurasa wa X wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA anawahimiza wananchi na dunia nzima kwa jumla kusimama kidete ili  kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • WHO na UNICEF wafikisha chanjo ya polio kwenye maeneo yasiyofikika ya West Pokot Kenya
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya  hivi karibuni wamezindua kampeni ya  chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa. Flora Nducha amefuatilia kampeni hiyo na kutuandalia taarifa ifuatayo..
    3 min
  • UN yaahidi kusaidia Wasyria kuiboresha nchi yao
    Kufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria. Taarifa iliyoandaliwa na Anold Kayanda inaeleza zaidi.
    2 min
  • Simfahamu baba yangu, natamani nimfahamu kwani nakosa upendo wake
    Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanazuiwa kutumia chakula, fedha au vitu vingine kwa ajili ya kushawishi ngono kutoka kwa mtu mwingine. Operesheni za ulinzi wa amani za Umoja wa Mataifa zinachukua hatua zaidi kuepusha ukosefu huo wa maadili , lakini bado visa hivyo vinaendelea kutokea. Katika baadhi ya matukio, watoto waliozaliwa kupitia uhusiano wa aiana hiyo wanasalia nyuma kwenye mazingira ya mizozo ambako baada ya baba zao kumaliza kuhudimia, huondoka na kubaki bila baba. Makala hii ya leo inamulika kisa kimoja cha mama na mtoto ambao wamesalia baada ya mlinda amani aliyempatia ujauzito mama husika kuondoka na kurejea nchini mwake. Msimulizi wako ni George Musubao
    4 min
  • 09 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Syria, na kampeni ya chanjo ya polio huko Pokot nchini Kenya. Makala tunasalia huko huko DRC na mashinani tnakwenda nchini Msumbiji, kulikoni?Kufuatia jana Wananchi wa Syria kutwaa madaraka kutoka kwa uongozi uliowatawala kwa mabavu kwa zaidi ya miongo mitano, viongozi wa Umoja wa Mataifa wameendelea kutoa wito wa kuhakikisha mabadiliko haya yanakuwa fursa ya mustakabali bora kwa kuzingatia haki za binadamu, uhuru na haki kisheria.Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa ushirikiano na serikali ya kenya na wadau wengine wa afya  hivi karibuni wamezindua kampeni ya  chanjo ya polio katika jamii ya wafugaji na wakulima ya kaunti ya West Pokot Mashariki mwa Kenya ambako mara nyingi ni vigumu kufikiwa.Makala tunakwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza mama ambaye alipatiwa ujauzito na mlinda amani wa Umoja wa Mataifa na kisha kujifungua mtoto ambaye anasimulia kadhia ya kutomfahamu baba na wito wake kwa mama yake mzazi. Msimulizi wako ni George Musubao mwandishi wa Idhaa ya Umoja wa MAtaifa nchini DRC.Katika mashinani wakati huu ambapo Dunia inaendelea kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, fursa ni yake Benilde Nhalivilo. Mkurugenzi mtendaji wa jukwaa la kitaifa la haki za watoto nchini Msumbiji ambaye kupitia video ya Benki ya dunia barani Africa anasisitiza utekelezaji wa sheria kuhakikisha mustakabali usio na ukatili wa kijinsia katika elimu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    10 min
  • Asante WFP kwa kusambaza dawa za kuua magugu mmebadii maisha yangu: Mkulima Catherine Wanjala
    Mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP wa kusambaza dawa ya bioherbicide ya kuuwa magugu kwenye mashamba ya mtama na mahindi kwa wakulima wa Kakamega magharibi mwa Kenya umekuwa mkombozi mkubwa kwa wakulima kama Catherine Wanjala ambaye  magugu hayo yalimuharibia mazao na hata kuilazimisha familia yale  kulala njaa wakati  mwingine kwa kukosa chakula. Kwaa ufafanuzi zaidi ungana na Flora Nducha katika makala hii.
    4 min
  • Miaka 15 ya Mkataba wa Kampala kuhusu wakimbizi wa ndani au IDPs, wito watolewa kwa nchi kuidhinisha na kutekeleza
    Katika kuadhimisha miaka 15 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika chini Muungano wa Afrika, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Ruven Menikdiwela na Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za Wakimbizi wa ndani Paula Gaviria Betancur wametoa kauli ya pamoja ya kupongeza Muungano wa Afrika kwa maono haya ya mbali na pia kuzisihi nchi zote barani Afrika kuutekeleza mkataba huo muhimu. Selina Jerobon na maelezo zaidi.
    3 min
  • 06 DESEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika, na siku ya kimataifa ya kujitolea inayotupeleka nchini DRC. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Zambia, kulikoni?Katika kuadhimisha miaka 15 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Kampala wa Ulinzi na Usaidizi wa Wakimbizi wa Ndani barani Afrika chini Muungano wa Afrika, Kamishna Mkuu Msaidizi wa Ulinzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, Ruven Menikdiwela NA Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za Wakimbizi wa ndani Paula Gaviria Betancur wametoa kauli ya pamoja ya kupongeza Muungano wa Afrika kwa maono haya ya mbali na pia kuzisihi nchi zote barani Afrika kuutekeleza mkataba huo muhimu.Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya kimataifa ya kujitolea kwa ajili ya amani na maendeleo, tunakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako mmoja wa wafanyakazi wa kujiolea wa Umoja wa Mataifa anaelezea uzoefu wake na ni kwa nini anajivunia kufanya kazi hiyo.Makala leo inatupeleka Kakamega Magharibi mwa Kenya kwa mkulima mdogo wa mahindi Catherine Wanjala aiyeathirika vibaya na magugu yajulikanayo kama Kichawi au Witchweed, na hata kuilamisha familia yake kulaa njaa wakati mwingine kwa kukosa mavuno, lakini ahuweni ilimwijiia pale mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP wa kusambaza dawa za kupambana na magugu hayo ulipomfikia.Katika mashinani wakati huu ambao Dunia inaadhimisha siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia, fursa ni yake Mheshimiwa Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, ambaye kupitia mtandao wa X wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA anasisitiza mchango wa wanaume kwa kutokomeza unyanyasaji wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners