Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 10 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya wahamiaji na wakimbizi nchini Libya, na wakimbizi wajasiriamali katika makazi ya wakimbizi ya Kakuma nchini Kenya. Makala inatupeleka Jerusalemu Mashariki, na mashinani nchini Chad, kulikoni?Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limeeleza mshtuko mkubwa na wasiwasi wake kufuatia kugunduliwa kwa makaburi mawili nchini Libya walimozikwa wahamiaji kadhaa, baadhi yao wakiwa na majeraha ya risasi.Katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, kutokana na ufadhili wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kundi la vijana wanajishughulisha na ufugaji wa wadudu nyenje (Crickets) ili kukabiliana na changamoto ya utapiamlo miongoni mwa watoto wachanga.Katika makala Sharon Jebichii anakupeleka Mashariki ya Kati kumulika ziara aliyofanya Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Dharura, OCHA huko Ukingo wa Magharibi na Gaza ili kujionea hali halisi ya raia.Na mashinani kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, nampisha  Daralssalam, kutoka Sudan ambaye alikuwa Mhadhiri Chuo Kikuu lakini sasa mkimbizi nchini  Chad akieleza changamoto alizopitia na kuomba jamii ya kimataifa isaidie wanawake wa Sudan.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!  
    10 min
  • Juhudi za mahakama Tanzania kutekeleza Lengo namba 16 ya SDG
    Leo katika makala Hamad Rashid wa Redio washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro Tanzania aanaangazia kuhusu namna Tanzania inaendelea kufanikisha Lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linatilia mkazo upatikanaji wa amani, haki na taasisi imara kwa kupunguza mrundikano wa mashauri au kesi mahakamani, kuwezesha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu katika jamii.
    4 min
  • 07 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunaangazia hali ya haki za binadamu nchini Jamhuri ya kidemokasia ya Congo DRC, Na masuala ya afya nchini Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville. Makala inatupeleka nchini Tanzania, na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, leo akizungumza katika Kikao Maalum cha Baraza la Haki za Binadamu kinachofanyika jijini Geneva, Uswisi, ameonya kuwa ghasia zinazoendelea mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zinaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa hazitashughulikiwa.Wananchi wa Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville, ni mashuhuda wa jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limewasaidia kukabiliana na ugonjwa wa macho na ngozi unaosababishwa na nzi mweusi wanaozaliana kwenye mito na vijito, ugonjwa ambao uliathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi kutokana na muwasho wa kila mara na upofu.Katika makala Hamad Rashid wa Redio washirika KidsTime FM ya mkoani Morogoro Tanzania anaangazia kuhusu namna Tanzania inaendelea kufanikisha Lengo Namba 16 la Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa linalotilia mkazo upatikanaji wa amani, haki na taasisi imara kwa kupunguza mrundikano wa mashauri au kesi mahakamani, kuwezesha upatikanaji wa haki kwa makundi maalumu katika jamii.Na mashinani fursa ni yake Ahmed kutoka kaunti ya Laikipia nchini Kenya, ambaye kupitia video iliyoandalia na Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji, IOM anaeleza jinsi ambavyo ukame wa mara kwa mara unavyoathiri mifugo ya.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    11 min
  • Congo-Brazaville yaelekea kutokomeza ugonjwa wa ngozi na macho
    Wananchi wa Jamhuri ya Congo, au Congo-Brazaville, ni mashuhuda wa jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO limewasaidia kukabiliana na ugonjwa wa macho na ngozi unaosababishwa na nzi mweusi wanaozaliana kwenye mito na vijito, ugonjwa ambao uliathiri shughuli zao za kijamii na kiuchumi kutokana na muwasho wa kila mara na upofu. Assumpta Massoi na taarifa kamili.
    2 min
  • 06 FEBRUARI 2025
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwakina inayotupeleka Havan Cuba ambapo mmoja wa walumbi wa lugha ya Kiswahili Jorum Nkumbi, ambaye pia ni mwandishi wa vitabu anayetumia sanaa ya uandishi wa vitabu kuitangaza lugha mama yake ya Kiswahili amezindua kitabu kipya hivi karibuni wakati wa kongamano la kimataifa la Kiswahili. Mengine tuliyokuandalia ni kama yafuatayo.Yerusalem Mashariki eneo la wapalestina linalokaliwa na Israeli ambako Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA, Tom Fletcher yuko ziarani na amepata shuhuda halisi za wanaokabiliwa na kufurushwa makwao. Mmoja wao ni Um Nasser ar Rajabi ambaye amemweleza kuwa Nimekuwa kwenye ndoa katika nyumba hii kwa miaka 50.Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wamelezea wasiwasi wao mkubwa kuhusu mahitaji ya dharura ya ulinzi na mazingira magumu yanayokabili raia kwenye eneo la Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC lenye utajiri mkubwa wa madini, wakati huu uhasama ulioshika kasi tangu mwezi uliopita kati ya jeshi la serikali na waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda umesababisha vifo vya watu 900, majeruhi zaidi ya 2000 na kufurusha watu 700,000 mjini Goma. Wametaka pande kinzani zizingatie sheria ya kimatiafa ya kibinadamu na zilinde raia wote.Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Hakimiliki, WIPO hii leo limetoa ripoti mpya kuhusu mustakabali wa usafirishaji wa watu na bidhaa duniani ikimulika teksi za angani, magari yasiyokuwa na dereva pamoja na maroketi yanayoweza kutumika ten ana tena tofauti na sasa, likisema ndio majawabu ambayo wabunifu na wagunduzi wanahaha duniani kote ili kupunguza usafirishaji unaochafua mazingira.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, mchambuzi wetu Dkt. Josephat Gitonga, kutoka Kenya ambaye ni mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi kwenye kitivo cha tafsiri na ukalimani anatufafanulia maana ya methali “MTI WENYE MATUNDA NDIO HURUSHIWA MAWE”.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!  
    12 min
  • Tumetembea wiki mbili kufika kambini Bushagara lakini bado hapa si nyumbani - Mwamini
    Kutana na Mwamini Sebororo mmoja wa mamilioni ya raia wa Jamhuri ya Kidemkrasia ya Congo DRC waliopoteza makazi yao na kila kitu katika jimbo la Kivu Kaskazini mashariki ya taifa hilo huku mgogoro ukiendelea kufurusha watu zaidi. Kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu imekuwa mtihani mkubwa kwa wakimbizi wa ndani na jamii zinazowahifadhi. Kupitia video ya shirika la umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Flora Nducha anafafanua zaidi katika Makala hii.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners