Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 28 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina Kuna msemo wa kiswahili usemao tahadhari kabla ya hatari na hivyo ndivyo ilivyo kwa ugonjwa wa Homa ya Ini ambapo kama mtu ataenda kufanya uchunguzi mapema anaweza kupata chanjo au matibabu, lakini kama atachelewa basi anaweza kupata hata ugonjwa wa saratani. 

    Ikiwa leo ni siku ya Kimataifa ya kuelimisha kuhusu ugonjwa huo Leah Mushi wa Idhaa hii amezungumza na Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Mfumo wa Chakula na ini kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, nchini Tanzania Dkt. Swaleh Kitabu Pazi, mazungumzo yaliyofanikishwa na Evarist Mapesa Afisa Uhusiano kutoka Hospitali hiyo ya Muhimbili.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Leo katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Homa ya Ini, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limetoa wito wa kuongeza kwa kiwango kikubwa upimaji na matibabu ya ugonjwa huo unaosababishwa na virusi, likionya kuwa ugonjwa huo unaofahamika kwa lugha ya kiingereza na kitabibu kama Hepatitis unaweza kuua watu wengi zaidi kuliko malaria, kifua kikuu na Virusi Vya Ukimwi kwa pamoja kufikia mwaka 2040 ikiwa mwenendo wa sasa wa maambukizi utaendelea..
    2. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametoa wito kwa nchi zote wanachama kuhuisha dhamira yao ya kutekeleza Mkataba wa Wakimbizi wa mwaka 1951, akisema haki ya watu wanaokimbia mateso kutafuta hifadhi inazidi kutiliwa shaka, kuwekewa vikwazo au kunyimwa.
    3. Na baada ya jana ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na dawa za kulevya na uhalifu UNODC kuonesha jinsi biashara ya utapeli mtandaoni inavyozidi kukua duniani, leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, IOM, limefafanua zaidi kuwa nyuma ya biashara hiyo kuna maelfu ya waathirika wa biashara haramu ya binadamu wanaolazimishwa kufanya uhalifu kwa vitisho na ukatili.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    10 min
  • 27 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kusikiliza simulizi za wananchi kuhusu uhamazishaji wa kudhibiti Ebola. Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC, imeonya kuhusu ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu unaofanyika kupitia matangazo bandia ya mitadaoni ya fursa za ajira. Zaidi ya watu 300,000 wanakadiriwa kushikiliwa katika vituo vya ulaghai Kusini-Mashariki mwa bara la Asia, ambako hunyang’anywa hati za kusafiria na kulazimishwa kufanya utapeli mtandaoni.
    2. Kamanda wa Kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, MONUSCO, Luteni Jenerali Ulisses De Mesquita Gomes, amethibitisha dhamira ya ujumbe huo ya kuimarisha usalama wa vituo vya afya katika eneo la Mongbwalu, jimboni Ituri, ambalo ni kitovu cha mlipuko wa Ebola. Amesema mashambulizi ya makundi yenye silaha na watu kuyakimbia makazi yao vinaweza kuvuruga ufuatiliaji wa wagonjwa na upatikanaji wa matibabu.  Walinda amani wa Nepal wanaendelea kulinda raia na miundombinu ya afya, kwa kushirikiana na jeshi la Congo na mamlaka za eneo hilo.
    3. Na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa za Kulevya na Uhalifu, UNODC, imeonya kuhusu ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu unaofanyika kupitia matangazo bandia ya ajira mtandaoni. Zaidi ya watu 300,000 wanakadiriwa kushikiliwa katika vituo vya ulaghai Kusini-Mashariki mwa barani Asia, ambako hunyang’anywa pasipoti na kulazimishwa kufanya utapeli mtandaoni.  UNODC inasema uhalifu huo sasa unasambaa hadi Afrika na maeneo mengine duniani, na kuwataka wanaotafuta ajira nje ya nchi kuthibitisha kampuni, mikataba na mawakala kabla ya kusafiri.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    11 min
  • 24 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania kupitia mradi wake wa Dumisha Amani kwa Maendeleo Endelevu awamu ya pili, unaotekelezwa kwa kushirikiana na serikali ya nchi hiyo kupitia Ofisi ya Rais inayohusika na Maendeleo ya Vijana, limeendelea kutumia mafunzo ya ufundi stadi kama njia ya kudumisha amani na kuwajengea uwezo vijana kiuchumi. 

    Hii ni katika kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu, SDGs likiwemo namba moja la kuondokana na umaskini na namba 16 linalolenga pamoja na mambo mengine kujenga amani kwenye jamii.Rashid Malekela, balozi kijana wa UNDP Tanzania alihudhuria mafunzo hayo na kutuandalia mada hii kwa kina.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Wanawake, UN Women, limeonya kuwa wanawake na wasichana katika mji wa El Obeid nchini Sudan sasa wanakabiliwa na hatari mbili wanapokwenda kuchota maji ambayo ni mashambulizi ya droni mchana yanawalazimu kusubiri hadi usiku, ambako hukumbana na ubakaji na ukatili mwingine wa kingono.
    2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limesema kuwa msaada wa chakula kwa zaidi ya wakimbizi 130,000 nchini Burundi, wengi wao wakitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRc unaweza kusitishwa kuanzia mwezi Oktoba mwaka huu endapo halitapata ufadhili wa haraka.
    3. Na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa la kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC MONUSCO, umefanikiwa kurejesha utulivu katika eneo la Nyakunde jimboni Ituri, hatua iliyowezesha kurejea kwa harakati dhidi ya ugonjwa wa Ebola.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    10 min
  • 23 JULAI 2026

    Mada kwa kina hii inakupeleka Pwani ya Kenya katika Kaunti ya Kilifi ambako mradi wa ‘Tushauriane Tuimarishe Kilimo Biashara’ unaotekelezwa kwa msaada wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, umewezesha wakulima wa eneo hilo kubadili mtazamo na kufanya kazi kwa pamoja. Ingawa changamoto za kijinsia zimekuwepo kwa muda mrefu, sasa mradi huo umefungua njia inayoleta nuru katika uhusiano wa kijinsia, mienendo ya kaya na matokeo ya kilimo biashara. Je nini kinafanyika? Feissal Kirwa kupitia video iliyoandaliwa na FAO anakusimulia zaidi.

    10 min
  • 22 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Huko DRC madini ya kimkakati mashariki mwa nchi yamekuwa kichocheo cha mizozo. Mgeni wetu leo pamoja na mambo mengine anaangazia jinsi vita imezuia wao kuendelea na uchimbaji madini. 

    Yeye anaishi Goma, lakini Salama Machaano, wa redio washirika wetu, Adventista World Radio, Tumaini Mkuu iliyoko Bukavu, jimboni Kivu Kusini alifnga safari hadi Goma kuzungumza naye.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo limekuwa na mjadala wa wazi wa ngazi ya juu kuhusu “Utawala wa rasilimali za asili: Msingi wa amani, usalama na ustawi” chini ya kipengele cha ajenda ya “Kudumisha amani na usalama wa kimataifa.” Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akihutubia kikao hicho ameeleza vipaumbele vinne kuwa ni kuhakikisha manufaa ya haki yanapatikana kutokana na rasilimali za asili, kuimarisha uwazi na ushirikiano ili kukabiliana na biashara haramu, kukuza utatuzi wa amani wa migogoro inayohusiana na rasilimali, na kuzingatia masuala ya mabadiliko ya tabianchi katika kuzuia migogoro na kujenga amani.
    2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limetoa wito wa kulindwa kwa raia na kuruhusiwa kwa misaada ya kibinadamu kuwafikia wenye uhitaji nchini Sudan baada ya shambulio lililotekelezwa juzi tarehe 20 Julai kwa kutumia ndege zisizo na rubani likilenga soko la Ar Rahad katika jimbo la Kordofan Kaskazini na kusababisha vifo vya watoto wawili na kuwajeruhi wengine sita.
    3. Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) limeeleza kusikitishwa sana na taarifa kwamba makumi ya wahamiaji wamefariki dunia au hawajulikani walipo kufuatia kuzama kwa meli katika pwani ya Mauritania, ambapo tarehe 18 Julai manusura 38 waliokolewa na Walinzi wa Pwani wa Mauritania karibu na mji wa Nouadhibou walipokuwa wakijaribu bahati yao kuelekea nchini Hispania. IOM kupitia Mkurugenzi wake wa Kanda ya Afrika Magharibi na Kati, Sylvia Ekra, imesema watu wanaendelea kuhatarisha maisha yao kwa sababu zinazowasukuma kuondoka katika nchi zao bado zipo.
    4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, na mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi,  kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “MAJI HAYAPOZI MOYO ILA YAKIWA BARIDI.”

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

    10 min
  • 21 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Jana katika moja ya viunga vya jiji la Nairobi, wadau mbalimbali wakiwemo wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na raia wa Afrika Kusini na Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Kenya, ili kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela walikitembelea Kituo cha Kulelea Watoto ya Yatima kinachofahamika kwa jina Serah’s Vision Children’s Home na walikaa kituoni hapo kwa dakika 67.

    Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

    1. Ikiwa ni miezi tisa tangu kusitishwa kwa mapigano kati ya Jeshi la Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas, hali ya usalama kwa raia wa Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel inaendelea kuzorota. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imesema hii leo kuwa hakuna eneo linaloweza kuchukuliwa kuwa salama kwa Wapalestina, huku Wizara ya Afya ya Palestina ikiripoti kuwa zaidi ya watu 1,100 wameuawa katika mashambulizi ya jeshi la Israel tangu Oktoba mwaka 2025.
    2. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, limeonya kuhusu hatari ya safari za baharini kuelekea barani Ulaya kupitia bahari ya Atlantiki baada ya watu 144 kuripotiwa kufariki au kutoweka katika pwani ya Mauritania wiki iliyopita. Katika tukio la hivi karibuni watu 387 waliokolewa katika operesheni za uokoaji.
    3. Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO linasema licha ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola wa virusi aina ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kuendelea kuenea kwa kasi, baadhi ya maeneo yanaanza kuonesha dalili za hali kutengamaa kutokana na hatua za haraka za kudhibiti ugonjwa huo.

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

    12 min
  • 20 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa (SDGs) yanatambua kuwa kuwawezesha vijana, kulinda mazingira na kuimarisha uhakika wa kupata chakula ni miongoni mwa nguzo muhimu za kujenga jamii zenye ustahimilivu na maendeleo endelevu. 

    Kupitia malengo kama vile la Kutokomeza umaskini, kutokomeza njaa na hatua dhidi ya mabadiliko ya tabianchi , jamii zinahimizwa kuwekeza katika suluhisho zinazowawezesha wananchi kujitegemea huku zikihifadhi mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Hatua hizo zinatekelezwa katika enoe la Kajiado Kaskazini, katika kaunti ya Kajiado, kusini mwa Kenya kama anavyosimulia Kelvin Keitany wa radio washirika, Domus Radio.

    1. Hii leo Umoja wa Mataifa umekuwa na matukio mbalimbali ya kuadhimisha siku ya Mandela, Rais wa kwanza mweusi wa taifa la Afrika Kusini kwa mchango wake wa utetezi wa haki. Miongoni mwa kulikofanyika maadhimisho hayo ni Nairobi, Kenya ambako Stella Vuzo wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa alikuwa shuhuda wetu. 
    2. Licha ya idadi ya magari duniani kuongezeka kwa zaidi ya bilioni moja, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO limesema vifo vinavyotokana na ajali za barabarani vimepungua kwa asilimia 21 kati ya mwaka 2011 na 2025. Hata hivyo, ajali hizo bado zilisababisha vifo vya zaidi ya watu milioni 1 mwaka jana na zinaendelea kuwa chanzo kikuu cha vifo kwa watoto na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 29
    3. Na, Je, msikilizaji wangu, uliwahi kujiuliza kwa nini binadamu bado wanarudi kuchunguza Mwezi ulioko anga za juu , zaidi ya miaka 50 baada ya kutua huko kwa mara ya kwanza? Leo Julai 20, dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya mwezi. Umoja wa Mataifa uliitenga siku hii kuenzi tukio la kihistoria la mwaka 1969, wakati wanaanga wa safari ya Apollo 11 walipoweka nyayo za kwanza za binadamu mwezini. Lakini maadhimisho haya hayaishii kwenye historia tu bali yanasisitiza pia umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa katika utafiti wa anga za juu na kuhakikisha uchunguzi wa mwezi unafanyika kwa amani na kwa manufaa ya watu wote duniani.".

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    10 min
  • 17 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunamsikia Pauline Farini Kibuya wa shirika la Congo Notre Avenir yaani Congo Mustakabali Wetu kutoka DRC akizungumza na Idhaa hii kuhusu jinsi wanavyosongesha amani kwa taifa la DRC Congo. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.

    1. Katibu Mkuu António Guterres aliyeko ziarani nchini China amehutubia mdahalo kuhusu Tahadhari za Mapema kwa Wote katika Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi unaofanyika kwenye jukwaa la kimataifa la Akili Mnemba na Tabianchi jijini Shanghai na kutoa wito wa kuharakisha maendeleo ya mifumo ya tahadhari za mapema inayotumia akili mnemba ili kuzuia majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Hata hivyo amesema "tahadhari lazima zifikie kila mtu aliyeko hatarini kwa lugha wanazoelewa na mifumo ya mawasiliano wanayoweza kuiamini."
    2. Kesho Julai 18 ikiwa ni siku ya kimataifa ya Nelson Mandela, Rais wa Kwanza Mweusi wa Afrika Kusini, huko Geneva, Uswisi hii leo mashindano ya 18 ya Nelson Mandela ya Mahakama ya Kimataifa ya Kuigiza yamefikia kilele kwa timu ya Chuo Kikuu cha Midlands State kutoka Zimbabwe kuibuka mshindi ilihali Chuo Kikuu cha Strathmore kutoka Kenya kimeshika nafasi ya pili.
    3. Hii leo hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa, nchi wanachama na marafiki wa mpira wa miguu au kabumbu, wamezindua kampeni ya mwaka mmoja ya  Dunia Moja, Mchezo Mmoja, Lengo Moja kwa lengo la kutumia mpira wa miguu kama kichochea cha kuimarisha afya ya akili kwa vijana, tukio linalofanyika siku mbili kabla ya fainali ya mashindano ya Kombe la Dunia kwa wanaume. Akizungumza mapema kabla ya tukio hilo Sahira Al Nahari, ambaye ni Kiongozi kijana mchechemuzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs amesema, "kwa hiyo, mpira wa miguu una mengi ya kutufundisha. Tunapokabiliwa na janga la kimataifa, hebu tuzielekeze fikra zetu kwenye viwanja vya mpira wa miguu. Tunapotazama kinachotokea viwanjani, tunajifunza nidhamu, ustahimilivu, na jinsi ya kuinuka tena baada ya kupoteza jambo muhimu sana."
    4. Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "CHOPOCHOPO."

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners