Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 16 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Ukanda wa Gaza ambako sitisho la mapigano kati ya Israeli na Palestina lililotiwa Saini tarehe 10 mwezi Oktoba mwaka jana wa 2025 limewezesha wakulima wa eneo hilo kurejea mashambani. Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.

    1. Mashirika mawili ya Umoja Umoja wa Mataifa lile la Uhamiaji, IOM na la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR kupitia taarifa waliyoitoa kwa pamoja jijini Gneva Uswusi na BangKok Thailand, wameeleza wasiwasi mkubwa kufuatia taarifa kwamba boti mbili zilizokuwa zimebeba zaidi ya watu 500 huenda zimezama katika pwani ya Myanmar katika siku za hivi karibuni. Kwa mujibu wa taarifa za awali, boti hizo mbili ziliondoka mwishoni mwa mwezi Juni kutoka Jimbo la Rakhine nchini Myanmar zikiwa zimewabeba zaidi ya abiria wa jamii ya Rohingya, wakiwemo baadhi waliokuwa wametoka katika kambi za wakimbizi za Cox's Bazar nchini Bangladesh.
    2. Zaidi ya watoto milioni 23 wengine zaidi ya wale ambao wako tayari kwenye umaskini duniani wanaweza kutumbukia katika umaskini wa kipato ifikapo mwisho wa mwaka huu wa 2025 kutokana na kuendelea kwa mzozo wa Mashariki ya Kati na athari zake kwa biashara ya kimataifa, kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) jijini New York, Marekani.
    3. Na Uganda leo imeanza rasmi kuhesabu siku 42 kuelekea kutangazwa kumalizika kwa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola baada ya mgonjwa wa mwisho aliyethibitishwa kuwa na maambukizi kupimwa mara ya pili na kubainika hana virusi hivyo, kisha kuruhusiwa kutoka hospitalini. Hatua hiyo ni mafanikio muhimu katika juhudi za nchi hiyo kudhibiti mlipuko, imesema taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Ulimwenguni, WHO ofisi ya Uganda.

    Mwenyeji wako ni Feissal, karibu!

    10 min
  • 15 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya stadi kwa vijana tunamulika jinsi gani vijana waliojiendeleza katika stadi ya akili mnemba au wengine wanaita akili unde, kwa kiingereza Artificial Intelligence au AI, wanarahisisha maisha ya jamii. 

    Na tunamuangazia kijana Kalebu Gwalugano kutoka Tanzania, Muasisi na Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Neurotech iliyoanzishwa mwaka 2022. Kijana huyu ni Mhandisi wa AI na akiwa Dar Es Salaam, mji mkuu wa kibiashara wa taifa hilo la Afrika Mashariki, amezungumza na mwenzetu Japhael Jambo. 

    Pia tunakuletea Muhtasariw a habari.

    1. Ikiwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Stadi za Vijana, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres amesema kuwezesha vijana kufikia uwezo wao kamili kunahitaji uwekezaji mkubwa katika elimu na mafunzo jumuishi yenye ubora. Ametambua mchango wa vijana kote duniani kwamba wanaendelea kutoa mchango mkubwa kama wabunifu, viongozi na mawakala wa mabadiliko katika kujenga jamii zenye usawa, ustahimilivu na maendeleo endelevu hata hivyo mabadiliko ambayo dunia inapitia sasa yakichochewa na maendeleo ya teknolojia za kidijitali, athari za mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuongezeka kwa hali ya kutokuwa na uhakika wa kiuchumi na pengo la usawa yanahitaji vijana kuwa na ujuzi mpya unaowawezesha kushindana na kunufaika na fursa zinazojitokeza.
    2. Ingawa mwaka 2025 duniani kiwango cha chanjo kwa watoto kiliongezeka kwa asilimia moja ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, kiwango cha chanjo bado kiko asilimia moja chini ya kiwango cha mwaka 2019, kikiwa kimeendelea kubaki ndani ya kiwango finyu tangu mwaka 2009. Hayo ni kwa mujibu wa makadirio ya kila mwaka ya mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa lile la afya duniani, WHO na la kuhudumia watoto, UNICEF kuhusu viwango vya kitaifa vya chanjo.
    3. Na ripoti mpya ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR inazitaka pande zinazohusika katika vita nchini Sudan, pamoja na serikali na kampuni zinazofanya biashara ya Gum Arabic, gundi inayotokana na aina fulani ya miti ya Acacia kuhakikisha shughuli zao zinaendana na sheria za kimataifa na hazichangii kuendeleza mzozo.

    Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

    10 min
  • 14 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika mkutano wa HLPF hapa makao makuu ya UN kumsikia Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye amewakiwakilisha Chuo Kikuu cha Mount Kenya cha nchini Kenya chenye matawi mbalimbali katika Afrika Mashariki katika mkutano wa United Nations Academic Impact (UNAI), Mpango unaosisitiza nafasi muhimu ya taasisi za elimu ya juu katika kuhimiza maendeleo endelevu na kuunga mkono utekelezaji wake. 

    1. Baada ya ziara yake mjini Bunia, jimboni Ituri nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo, Mkurugenzi Mtendaji wa WHO anayehusika na Programu ya Dharura za Afya, Dkt. Chikwe Ihekweazu, amewambia waandishi wa habari Geneva, Uswisi kwamba mlipuko wa sasa ni moto ambao kinachouchochea kiko katikati, huku ukiendelea kusambaa.
    2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Bahari (IMO) limesema lina wasiwasi mkubwa kufuatia mashambulizi ya jana usiku yaliyolenga meli kwenye mlango wa bahari wa Hormuz na viunga vyake na kusababisha vifo vya takribani mabaharia wawili na wengine kadhaa wamejeruhiwa. Kupitia taarifa yake iliyotolewa London, Uingereza, IMO imesema inafanya kazi kwa haraka na mamlaka husika ili kubaini mazingira halisi ya tukio hilo.
    3. Na uungwaji mkono wa umma kwa wakimbizi unaendelea kuwa imara licha ya kuwepo kwa changamoto na kutokuweko kwa uhakika wa mustakabali duniani, hii ni kwa mujibu wa utafiti wa pamoja uliofanywa na kampuni ya IPSOS na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR, Utafiti umebaini kuwa asilimia 66 ya washiriki katika nchi 29 wanakubaliana kwamba watu wanaokimbia vita au mateso wanapaswa kuruhusiwa kusaka hifadhi katika nchi nyingine, ikiwa ni punguzo la asilimia moja tu ikilinganishwa na mwaka 2025.Utafiti huu umefanywa ikiwa ni miaka 75 tangu kupitishwa kwa Mkatab awa Kimataifa wa kulinda wakimbizi.

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

    10 min
  • Uhaba wa maji watishia mafanikio ya SDGs – Guterres

    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba dunia ipo nyuma katika kutekeleza ahadi zake kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama na huduma za kujisafi. Hivyo basi amezitaka serikali, sekta binafsi na jamii kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhaba unaoongezeka wa maji, uchafuzi wa mazingira na shinikizo linalotokana na mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

    4 min
  • 13 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunaangazia malengo ya maendeleo endelevu, uhuru wa usafiri katika maji, na shughuli za Redio Miraya za kutumia redio kujenga amani na kutoa tahadhari za mapema za hali ya hewa nchini Sudan Kusini. 

    1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameonya kwamba dunia ipo nyuma katika kutekeleza ahadi zake kuhusu upatikanaji wa maji safi na salama na huduma za kujisafi. Hivyo basi amezitaka serikali, sekta binafsi na jamii kuchukua hatua za haraka kukabiliana na uhaba unaoongezeka wa maji, uchafuzi wa mazingira na shinikizo linalotokana na mabadiliko ya tabianchi.
    2. Taarifa iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Usafiri wa Baharini (IMO) imeeleza kuwa Baraza la shirika hilo lililohitimisha kikao chake cha 137 linasisitiza tena umuhimu wa kulinda haki na uhuru wa usafiri katika maji kwa mujibu wa sheria za kimataifa. 
    3. Nchini Sudan Kusini, Redio ndiyo chanzo kikuu cha taarifa kwa takribani asilimia 60 ya wananchi wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. Ndiyo maana kuendelea kwa matangazo ya Radio Miraya ambayo yamedumu kwa miaka ishiriki katika redio hii inayomilikiwa na UNMISS yaani Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani Sudan Kusini ni kipaumbele cha juu katika juhudi zake za kuzuia migogoro na kujenga amani.

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

    10 min
  • Miaka 20 tangu kuanzishwa kwake Redio Miraya bado ni muhimu nchini Sudan Kusini

    Nchini Sudan Kusini, Redio ndiyo chanzo kikuu cha taarifa kwa takribani asilimia 60 ya wananchi wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. Ndiyo maana kuendelea kwa matangazo ya Radio Miraya ambayo yamedumu kwa miaka ishiriki katika redio hii inayomilikiwa na UNMISS yaani Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani Sudan Kusini ni kipaumbele cha juu katika juhudi zake za kuzuia migogoro na kujenga amani.

    3 min
  • 10 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina na leo tunakwenda Afrika Mashariki hususan nchini Tanzania katika visiwa vya Zanzibar. Tunamulika jinsi serikali ya Zanzibar kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo nchini humo, UNDP wanaboresha huduma za utalii kwa kutumia Akili Mnemba au AI. 

    1. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa kupunguzwa kwa misaada rasmi ya maendeleo tangu Januari 2025 kumesababisha takribani wanawake na wasichana milioni moja duniani kupoteza huduma muhimu katika nchi zilizoathiriwa na migogoro. Ikitolewa leo Geneva, Uswisi na New York, Marekani na shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya wanawake, UN Women, ripoti hiyo iliyopatiwa jina ‘Zaidi ya Kiwango cha Kuvumilika’ miongoni mwa changamoto ilizozitaja ni pamoja na kuwa asilimia 84 ya mashirika ya wanawake yameripoti kuongezeka kwa mahitaji ya huduma, lakini takribani asilimia 90 ya mahitaji hayawezi tena kuyakidhi na kwamba mashirika mawili kati ya matano yanatarajia kufungwa ndani ya mwaka mmoja kutokana na ukosefu wa fedha.
    2. Huko Sudan, nchi inayoumia kwa vita kwa miaka minne sasa, kumetangazwa mlipuko mpya wa ugonjwa wa kipindupindu hali inayozidisha wasiwasi kuhusu usalama wa jamii zilizo hatarini, hususan katika mji wa El-Obeid uliozingirwa, ambako mashambulizi ya kila siku ya ndege zisizo na rubani yanaendelea kuzuia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu. Dkt. Shible Sahbani, Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) nchini Sudan akizungumza kwa njia ya video na waandishi wa habari leo mjini Geneva, uswisi amesema, “tumerekodi zaidi ya wagonjwa 1,330 wa kipindupindu, huku watu 114 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Hii inaonesha kiwango cha vifo miongoni mwa wagonjwa wa kipindupindu cha asilimia 13.7, ambacho ni cha juu sana. Na bila shaka, msimu wa mvua unaotarajiwa utaifanya hali kuwa mbaya zaidi.”
    3. Na utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuhusu Ufuatiliaji wa Elimu Duniani, umeonesha kuwa misaada ya kimataifa kwa sekta ya elimu imeendelea kupungua na nchi 113 duniani zinatumia fedha nyingi kulipa madeni kuliko pesa wanazoziwekeza kwenye elimu. Matokeo ya utafiti huo yamewekwa wazi leo mbele ya viongozi kutoka nchi mbalimbali wanaohudhuria Mkutano wa Mageuzi ya Elimu TES+4 unaofanyika Paris, Ufaransa ili kufuatilia utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa kwanza wa Mageuzi ya Elimu uliofanyika mwaka 2022 na pia ili kusongesha zaidi ufikiaji wa Lengo namba 4 la Maendeleo Endelevu linalohusu Elimu Bora.

    Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!

    10 min
  • Ushirikiano kati ya wahudumu wa afya na wanajamii unavyosaidia kupambana na Ebola DR Congo

    Wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo ukiendelea kuenea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatua zimepigwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Uwezo wa kutoa matibabu umeongezeka, linasema Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO na kuwaruhusu ndugu kuwaona jamaa zao kumeongeza utayari wa wagonjwa kujitokeza. Anold Kayanda na maelezo zaidi. 

    4 min
  • 09 JULAI 2026

    Hii leo jaridani tunaangazia washindi wa Tuzo ya UNFPA, harakati za kutokomeza Ebola nchini DRC, na watoto wenye ulemavu nchini Kenya. 

    1. Profesa Serigne Gueye, daktari bingwa wa mfumo wa njia ya haja ndogo  kutoka Senegal na mmoja wa wataalamu mashuhuri duniani wa matibabu ya fistula ya uzazi, amesema kutokomeza tatizo hilo kunategemea kuimarishwa kwa mifumo ya huduma za afya ya uzazi na kuhakikisha kila mwanamke anapata huduma za dharura za uzazi kwa wakati.
    2. Wakati mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo ukiendelea kuenea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, hatua zimepigwa katika kuimarisha mapambano dhidi ya ugonjwa huo. Uwezo wa kutoa matibabu umeongezeka, linasema Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO na kuwaruhusu ndugu kuwaona jamaa zao kumeongeza utayari wa wagonjwa kujitokeza.
    3. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa juzi Julai 7 imeeleza kuwa ingawa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yameboresha maisha ya mabilioni ya watu duniani, kasi ya maendeleo bado haitoshi kufikia malengo yaliyowekwa ili kufikia mwaka 2030 yawe yametimizwa. Na ingawa Umoja wa Mataifa unaendelea kuhamasisha kuwa hakuna anayepaswa kuachwa nyuma katika maendeleo lakini kundi la watu wenye ulemavu bado ​ linakumbana na changamoto nyingi. Kevin Keitany wa Radio washirika wetu Radio Domus ya nchini Kenya ametembelea moja ya mashirika yanayosaidia watu wenye ulemavu nchini humo ili kuangazia harakati zao za kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.

    Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners