
Sign up to save your podcasts
Or


Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka mjini Caracas nchini Venezuela, mshikamano na raia wa nchi hiyo wadhihirika wakati huu wakiwa kwenye majonzi baada ya matetemeko ya ardhi kukumba wananchi. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.
Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, tunasalia huko huko Nairobi Kenya kwani leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Lengelenge lako si jipu langu”.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayokupeleka jijini Nairobi nchini Kenya ambako kunafanyika Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Usimamizi wa Matumizi ya Intaneti, IGF, mahususi kwa bara la Afrika pekee, AfIGF. Stella Vuzo, Afisa Habari wa UNIS Nairobi, Kenya amezungumza na mmoja wa vijana washiriki na kukuletea maoni yake.
Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
Katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambako miongo ya vita imeacha maelfu ya watoto bila familia, elimu au usalama, Lydie Mbusa Mwenge ameweka maisha yake katika mstari wa mbele wa kupigania haki za wasichana walioathiriwa na vita. Mwenge ni mwanzilishi na mratibu wa shirika la Action Intervention des Femmes Entrepreneurs pour le Développement, linalojikita katika kulinda na kuwawezesha wasichana walio chini ya umri wa miaka 18, hususan wale manusura wa ubakaji, kupoteza familia zao au kulazimika kuishi mitaani. Bi. Lydie Mwenge amezungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii, ungana nao.
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, leo tunaelekea nchini DRC, kwa Lydie Mwenge, Mwanaharakati wa kupigania haki hususan za wasichana walio na umri wa chini ya miaka 18 walioathirika na vita inayoendelea nchini humo ukiwemo ukatili wa kingono.
Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
From the publisher's feed

14 Listeners

43 Listeners

5 Listeners

95 Listeners

25 Listeners

9 Listeners

18 Listeners

4 Listeners

7 Listeners

15 Listeners

8 Listeners

9 Listeners

4 Listeners

4 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners