Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 17 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia uhakika wa chakula barani Afrika, utumikishaji wa watoto jeshini Sudan Kusini, na ujumbe wa mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana kutoka asasi ya kiraia nchini Zimbabwe.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Chakula na Kilimo, FAO, pamoja na Mpango wa Chakula Duniani, WFP, yametoa onyo kali kuwa hali ya ukosefu wa uhakika wa chakula inatarajiwa kuwa mbaya zaidi kwa mamilioni ya watu katika nchi 13 zilizotajwa kuwa maeneo hatari ya njaa kati ya mwezi Juni na Novemba mwaka huu wa 2026.Watoto tisa waliokuwa wakihusishwa na vikosi vya ulinzi katika Jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wameanza safari mpya ya maisha baada ya kutambuliwa, kuachiliwa na kukabidhiwa kwa ajili ya kurejeshwa katika familia na jamii zao.Leo tunakupeleka Zimbabwe kwa mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana kutoka asasi ya kiraia ya “Unlimited Hope Alliance”. Kandoni mwa moja ya mikutano ya Zama Zijazo ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani alipata fursa ya kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii akipaza sauti kwa viongozi wa dunia kuhakikisha wanawake na wasichana wa vijijini hawapewi kisogo katika ajenda za maendeleo, elimu na teknolojia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • Hata kama ulipata mimba ukiwa na umri wa miaka 14 huo sio mwisho wa maisha yako - Mary Chigumira
    Leo tunakupeleka Zimbabwe kwa mwanaharakati wa haki za wanawake na wasichana kutoka asasi ya kiraia ya “Unlimited Hope Alliance”. Kandoni mwa moja ya mikutano ya Zama Zijazo ya Umoja wa Mataifa hapa New York Marekani alipata fursa ya kuzungumza na Flora Nducha wa Idhaa hii akipaza sauti kwa viongozi wa dunia kuhakikisha wanawake na wasichana wa vijijini hawapewi kisogo katika ajenda za maendeleo, elimu na teknolojia. Flora Nducha anafafanua zaidi alichomueleza katika taarifa hii
    3 min
  • 16 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturejesha hapa Makao Makuu ya UN kusikia mahojiano maalum na ya kina baina ya Flora Nducha wa Idhaa hii na Mkuu mpya wa ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Dawa na Uhalifu UNODC. Pia tunakuletea Muhtasari wa habari.Kumekuwepo na imani kwamba ugonjwa wa Ebola si halisi, hali iliyowafanya baadhi ya wananchi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kuzika wapendwa wao waliokufa kwa Ebola bila kufuata hatua za kujikinga dhidi ya maambukizi. Kutafuta suluhu ya changamoto hiyo, Shirika la Afya Duniani WHO kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la chama cha Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu, IFRC, wamesikiliza maoni ya jamii kuhusu taratibu za mazishi.Takriban nusu ya watoto wote duniani au watoto bilioni 1.1 sasa wanakabiliwa na angalau hatari tatu za mabadiliko ya tabianchi zinazolingana, zikihatarisha afya zao, elimu, na maisha yao, imesema ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF.Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, yuko nchini Haiti kwa ziara maalum ya mshikamano ili kujionea hali halisi ya wananchi walioathiriwa na ghasia na ukosefu wa usalama. Akiwa huko, Guterres anakutana na wananchi, kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Haiti, na kutathmini juhudi za serikali, Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa za kurejesha utulivu nchini humo.Mwenyeji wako ni Feissal Kirwa, karibu!
    12 min
  • 15 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kufuatilia ziara ya kihistoria ya Rais wa Baraza Kuu la UN, Annalena Baerbock, kwenye kituo cha kukusanya, kuchakata  na kurejeleza taka cha Korogocho (Korogocho Material Recovery Facility - MRF) kujionea namna vijana wanavyogeuza taka kuwa fursa ya kiuchumi na silaha ya kutokomeza umasikini na uhalifu mitaani.Kufuatia makubaliano ya sitisho la mapigano la kudumu baina ya Marekani na Iran yaliyotangazwa jana jumapili Juni 14, viongozi wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa wampongeza kufikiwa kwa makubaliano hayo huku wakihimiza yaheshimiwe na pia kufunguliwe upenyo maalum wa kupitisha misaada ya kibinadamu katika mlango bahari wa Hormuz huko nchini Iran.Kutoka Mashariki ya Kati twende Afrika, ambako mapigano nchini Sudan yanaelezwa kutoonesha dalili yoyote ya kupungua, huku pande zinazohasimiana zikituhumiwa kutumia mbinu za kukamatwa kiholela, mateso na kutoweshwa kwa raia kwa nguvu. Taarifa iliyotolewa leo na Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Kuchunguza Ukweli kuhusu Sudan imesema vitendo hivyo vinaweza kuhesabiwa kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.Na leo ni Siku ya siku ya Uelimishaji Kuhusu Ukatili dhidi ya Wazee Duniani ambapo Umoja wa Mataifa umesema hatua zaidi zinahitajika kuwalinda wazee dhidi ya ukatili, huku ukionya kuwa uelimishaji pekee hautoshi na kwamba dunia inapaswa kuimarisha sheria, huduma za afya na mifumo ya kuripoti matukio ya unyanyasaji.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • 12 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umehitimishwa jana katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali wa Serikali na Mashirika yasiyo ya Serikali walikusanyika kutoka kila pembe ya dunia kujadili hatua zilizopigwa katika kipindi cha miaka 20 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Watu Wenye Ulemavu, CRPD. Mmoja wa waliohudhuria ni Bwana Kibaya Laibuta ambaye licha ya kupoteza uwezo wa kuona akiwa na umri wa miaka 24 alipokuwa mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Nairobi bado alifanikiwa kusonga mbele akamaliza masomo yake ya sheria na masomo mengine ya ngazi za juu na sasa miaka mingi baadaye ni Jaji katika Mahakama ya Rufaa ya Kenya. Siri yake ya mafaniko ndio hasa anaihamasisha kote duniani na anaiweka wazi katika mazungumzo yafuatayo na Anold Kayanda wa Idhaa hii ya Umoja wa Mataifa ili watu wengine wenye ulemavu wafanikiwe kama yeye. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za hatua za kupambana na UKIMWI, maambukizi ya ugonjwa wa Ebola hasa kwa watoto DRC, na ujumbe katika siku ya kimataifa ya kupinga utumikishaji wa watoto.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela.
    10 min
  • 11 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umetamatishwa leo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Idhaa hii imepata fursa ya kuzungumza na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya mkutano huu muhimu, Mtanzania Zuleikha Tambwe. Pia tunakuletea jifunze Kiswahili na muhtasari wa habari kama zifuatazo..Hatari ya Ebola wakati wa Kombe la Dunia la Soka 2026 ni ndogo na hakuna sababu ya mashabiki kubadili mipango yao ya safari kuelekea Canada, Mexico na Marekani, limesema Shirika la Afya Duniani WHO kombe hilo liking’oa nanga leo. Mkurugenzi wa WHO Kanda ya Ulaya, Hans Henri P. Kluge, amesema hakuna wagonjwa wa Ebola katika nchi hizo wala Ulaya na amesisitiza, “Safirini kama kawaida na furahieni mashindano hayo.” WHO imefafanua kuwa Ebola haisambai kwa njia ya hewa na visa vingi vipo katika maeneo ya mbali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Annalena Baerbock, amehitimisha ziara  ya siku mbili jijini Nairobi nchini Kenya, ambapo amesisitiza nafasi muhimu ya Umoja wa Mataifa katika kuendeleza maendeleo, amani na ushirikiano barani Afrika. "Kila siku Umoja wa Mataifa na washirika wake huokoa maisha. Bila UN, mamilioni ya watoto wasingepata elimu kupitia UNICEF wala chanjo muhimu kupitia WHOna tusingekuwa na ushirikiano kama huu."Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, uliokuwa unafanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani umefikia tamati leo. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.” Kibaya Laibuta, Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini Kenya, ambaye pia ni mlemavu aliyeoona au  kipofu, ameshiriki na anaeleza alivyouona mkutano huu.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Lililo lujani ni la lusu”.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    11 min
  • 10 JUNI 2026
    Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina maalum ambayo kama nilivyokujuza hapo awali inaangazia mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, unaofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa chini ya kauli mbiu “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.”Washiriki wanajadili namna ya kutokomeza ukandamizaji, ukatili na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu, kuimarisha mifumo ya huduma na msaada, pamoja na kuongeza ushiriki na uwakilishi wao katika maisha ya kisiasa na umma. Miongoni mwa wanaohudhuria mkutano huo ni Nassriya Nassir Ali mbunge wa watu wenye ulemavu kutoka nchini Tanzania, yeye anaulemavu wa kusikia au kiziwi. Leah Mushi amefanya mahojiano naye na hapa mkalimani wake wa lugha ya Alama Tusajigwe Ernest anajibu kwa sauti. Pia tunakuletea mhtasari wa habari tukimulika haki za elimu kwa watoto nchini Sudan, usalama wa mabaharia na judhibiti wa kusambaa kwa virusi vya Ebola hasa wakati huu wa michezo ya kimataifa ya kuwania kombe la dunia. Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    11 min
  • 09 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Kesho kutwa Alhamisi ya Juni 11, macho na masikio yanaelekezwa Mexico, Canada na hapa Marekani kwa ajili ya fainali za kombe la dunia kwa mpira wa miguu, au soka al maarufu kabumbu. Ingawa hivyo zama za sasa za mchezo huo maarufu zaidi duniani zinakumbwa na madhara ya  athari za mabadiliko ya tabianchi. Ongezeko la joto kali linavuruga mechi na kuzua wasiwasi kuhusu mustakabali wa mchezo huo. Ni kwa kuzingatia hilo, Sekretarieti ya Mkataba wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, UNFCCC inamulika suala hilo na kutoa mapendekezo ya nini kifanyike kwani hivi sasa madhara ya joto kali kwenye kabumbu ni dhahiri. Feissal Kirwa anamulika hilo kupitia video iliyoandaliwa na UNFCCC.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze Kiswahili.Takriban watoto milioni 138 duniani kote bado wako katika ajira za watoto, wakiwemo watoto milioni 54 wanaofanya kazi hatarishi. Hayo yamo katika ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Kazi la Umoja wa Mataifa ILO. Katika ujumbe wakwe kwenye ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Gilbert F. Houngbo, ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kubadili hali hii.“Habari njema ni kwamba hadi sasa tuna wagonjwa 19 ambao wamepona, hivyo utambuzi wa mapema na matibabu vinaokoa maisha,”  Huyo ni Mkurugenzi wa Operesheni za Tahadhari na Hatua za Dharura za Afya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani (WHO), Dkt. Abdirahman Mahamud, akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva leo kwa njia ya video kutoka Bunia katika Jimbo la Ituri, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, jimbo ambalo linachangia asilimia 94 ya wagonjwa wote wa Ebola.Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu CRPD, umeanza leo Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York na utaendelea hadi 11 Juni. Kaulimbiu ya mwaka huu ni “kuadhimisha miaka 20 ya mkataba huo na kuimarisha utekelezaji wake katika dunia inayobadilika.” Washiriki wanajadili namna ya kutokomeza ukandamizaji, ukatili na manyanyaso dhidi ya watu wenye ulemavu, kuimarisha mifumo ya huduma na msaada, pamoja na kuongeza ushiriki na uwakilishi wao katika maisha ya kisiasa na umma.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "MKWARUZO."Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners