Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 02 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri ya Kidokrasia ya Congo DRC katika mji wa Mavivi jimboni kivu kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo kusikia ni kwa jinsi gani walinda amani kutoka Tanzania wanaohudumu chini ya MONUSCO. wanavyochangia katika ulinzi wa amani na msaada wa kibinadamu.Umoja wa Mataifa umezitaka nchi zote duniani kuimarisha mifumo ya tahadhari za mapema baada ya kuthibitisha kuanza kwa hali ya El Niño, ukionya kuwa mabadiliko hayo ya joto la Bahari ya Pasifiki yataleta viwango vya juu vya joto kuliko kawaida karibu kila mahali duniani kati ya mwezi Juni mpaka Agosti na kuchochea matukio mabaya zaidi ya hali ya hewa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Katibu Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya hewa duniani WMO, Celeste Saulo amesema "Taarifa hizi ni muhimu kwa sababu El Niño ni kichocheo kikubwa cha hali ya hewa duniani na mifumo ya mabadiliko ya tabianchi, bahari yenye joto, huongeza joto na unyevu kwenye mfumo wa hali ya hewa ambao unaweza kutumika kuzidisha hali mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na joto kali, na mvua kubwa.”.’Zinakaribia siku 100 sasa tangu kuanza kwa mzozo wa Mashariki ya Kati ambao athari zake zimesambaa duniani kote kwani umevuruga njia za usafirishaji na umeongeza gharama za usafiri na kuchelewesha utoaji wa huduma muhimu. Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya watoto UNICEF limeeleza kuwa fedha nyingi sasa zinatumika kwenye usafirishaji badala ya kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watoto. Gharama za kusafirisha chanjo kwenda baadhi ya nchi barani Afrika zimeongezeka kwa hadi asilimia 70, huku gharama za kusafirisha chakula tiba, na vifaa vya elimu, nazo zikipanda kwa kiwango kikubwa. Shirika hilo linaonya kuwa hali hiyo inalazimisha kufanya maamuzi magumu kuhusu ni watoto gani wapate msaada kwanza". Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliogundulika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC na Uganda mwezi uliopita wa Mei ambapo mpaka sasa watu 49 wamepoteza maisha, 48 nchini DRC na mmoja nchini Uganda. Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amezihimiza jumuiya za kimataifa kutoa usaidizi unaohitajika ili kudhibiti mlipuko. Pia amelihimiza nchi kutoweka vikwazo vya usafiri kwa DRC, ili kuhakikisha msaada wa kiafya na kibinadamu unaweza kufikia kiwango kinachohitajika.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "CHOTORA"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    11 min
  • 01 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalumu ambapo hii leo tutaelekea jijini Kampala nhcini Uganda kuangazia uzunduzi wa awamu ya tatu ya safari ya hija ya “Twende Zetu Butiama”, kumuenzi Hayati Mwalimu Julius Kmabarage Nyerere, rais wa zamani wa Tanzania aliyedumisha amani, msikamano na kupigania maendeleo ambazo ni ajenda zinazopewa kiaumbele cha juu na Umoja wa Mataifa. Shuhuda wetu katika uzinduzi huo uliofayika mwishoni mwa wiki alikuwa ni John Kibego kutoka Radio washirika wetu Kazi Njema FM ya mjini Hoima.Tukianza na ugonjwa wa Ebola lakini leo ni habari njema, wauguzi wanne waliokuwa wamelazwa hospitalini huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC wameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupona ugonjwa huo, na kufanya idadi ya waliopona virusi vya Ebola hadi sasa kufikia watu watano. Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Duniani WHO katika taarifa yake limesema “Tunatarajia kuona watu zaidi wakipona, hasa wale wanaogunduliwa mapema na kupata huduma za afya kwa wakati, huku juhudi za kudhibiti mlipuko zikiongezwa kasi.”.’Kamati ya haki za watoto ya Umoja wa Mataifa imelaani sheria iliyopitishwa na uongozi wa Taliban nchini Afghanistan ya kuwa mtoto wa kike akisha balehe tu tayari anaweza kuolewa. Kamati imesema sheria hiyo mpya ni ukiukwaji mkubwa na wakimfumo wa sheria ya kimataifa ya haki za binadamu na kwamba Taliban wanachukulia ukimya wa wasichana kama ridhaa, na kwamba amri hiyo ni muendelezo wa mfululizo wa hatua za kibaguzi zinazochukuliwa na utawala wa Taliban,".Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, hii leo ameonya kuwa kuenea na kuhamishwa kwa njia haramu kwa silaha ndogo ndogo na nyepesi kunaendelea kuchochea migogoro, ugaidi, uhalifu na ukatili wa kijinsia duniani kote, huku akizitaka nchi kuimarisha ushirikiano wa kimataifa ili kukabiliana na vitisho vinavyoibuka.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • 29 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina maalumu ambapo tunamwangazia mmoja wa maafisa waandamizi wa Umoja wa Mataifa, Joyce Msuya. Mwisho wa wiki hii, Joyce, raia wa Tanzania ambaye pia amewahi kuhudumu katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo, UNEP na pia Benki ya Dunia anahitimisha utumishi wake katika Umoja wa Mataifa akiwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kibinadamu na pia Naibu wa Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA). Katika mazungumzo haya na Anold Kayanda wa Idhaa hii, Joyce Msuya anaanza kwa kuitafari miaka minne aliyohudumu katika nafasi hii.Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC inakumbwa na ugonjwa wa Ebola ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO, Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus amefika huko na anaeleza sababu. ‘Nimefika hapa kuzieleza jamii za Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu kusini kuwa hawako pekeyao, na kwamba tupo hapa kuwaunga mkono, na tunaelewa machungu yao, lakini pia tunafahamu wana nguvu na yote yanayohitajika kukomesha hili. Ninatumia fursa hii kuziomba jumuiya za kimataifa kuongeza usaidizi wao ili wahudumu wa afya waweze kupata vifaa tiba na vya kujilinda na maambukizi.’Kupigwa marufuku watoto kutumia mitandao ya kijamii, si suluhisho la mara moja kwa suala mtambuka lenye sura nyingi, ndio maana hii leo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ametaka hatua kali zichukuliwe na kila nchi, pamoja na makampuni ya teknolojia, ili kufanya mitandao ya kijamii kuwa salama zaidi kwa watoto, akisisitiza udhibiti, usimamizi na uwajibikaji unaofaa. Kamishna Türk amesema "Kuimarisha ulinzi wa watoto mtandaoni ni kipaumbele cha dharura ambacho tunahitaji kuhakikisha sio tu kwamba kinafanyika, bali pia kinafanyika ipasavyo,".Na ukatili wa kingono kwenye maeneo yenye migogoro ulifurutu ada mwaka 2025, hii inamanisha kuna ongezeko kubwa la ukatili wa kingono huku wanawake na wasichana ndio idadi kubwa ya waliokumbwa na madhila hayo yaliyohusisha pia waathirika hao kuuawa baada ya kubakwa. Haya yamebainika kwenye ripoti ya ukatili wa kijinsia unaohusiana na migogoro iliyotolewa na Umoja wa Mataifa leo ambayo pia imeonya kuwa kuongezeka kwa matumizi ya kijeshi duniani na kupungua kwa bajeti za misaada ya kibinadamu kulidhoofisha uwezo wa serikali na taasisi kuzuia na kuchunguza ukatili huo wa kingono. Ripoti hiyo imetoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti zaidi za kimataifa pamoja na kuhakikisha upatikanaji endelevu wa fedha ili kulinda raia, na kuwasaidia manusura wa ukatili wa kingono unaohusiana na migogoro.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    10 min
  • 28 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika nchi zinazochangia vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa, ikiwa ni pamoja na Taifa la Tanzania na Balozi Togolani Idriss Mavura mara baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza na Flora Nducha kuhusu suala hili muhimu.“Nataka niwe mkweli; hii ni moja ya changamoto zetu kubwa zaidi. Hatuwezi kufanya kazi hii kama wale wanaojaribu kusaidia wanazuiwa kufanya hivyo, au kuwekwa katika hatari.” Ni sehemu ya barua ya Dkt. Tedros Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, WHO, aliyowaandikia wananchi wa Jamhuri ya Kidemorkasia ya Congo, DRC wakati huu vikwazo kama vile mapigano jimboni Ituri, yanakwamisha harakati za kudhibiti mlipuko wa 17 wa Ebola nchini humo.Vikwazo vingine vya kudhibiti Ebola nchini DRC ni mila. Maki Baraka mkazi wa Beni jimboni Kivu Kaskazini ambako Ebola imeripotiwa mji jirani wa Butembo ana wito.Na Joyce Msuya, Naibu Mkuu wa Ofisi ya UN inayoratibu misaada ya dharura, OCHA anatamatisha jukumu lake baada ya kuhudumu kwa miaka minne. Anold Kayanda amemuuliza anachokumbuka zaidi.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min
  • 22 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika nchi za Afrika Mashariki ambazo zimezindua Siku ya Ziwa Victoria ambayo maadhimisho yake kwa mara ya kwanza yamefanyika tarehe 21 mwezi huu wa Mei huko Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania. Lengo pamoja na mambo mengine ni kuimarisha vivutio vya utalii. Uzinduzi huu ulitanguliwa na jukwaa la wadau wa Bonde la Ziwa hilo lililohudhuriwa na wadau mbalimbali akiwemo Amon Manyama, Mkurugenzi wa Miradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP, nchini Tanzania. Rashid Malekela wa Idhaa hii alituwakilisha na amezungumza naye.Pia tunakuletea muhtasari wa habari na ufafanuzi wa neno kama neno "PEKEPEKE."Mfuko wa dharura wa Umoja wa Mataifa UNCERF umetoa dola milioni 60 kusaidia muitikio wa kupambana na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Congo DRC. Tayari vifaa tiba vimewasilishwa nchini humo na sasa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO na wadau wengine wanaendelea na usaidizi ikiwemo kuweka vituo vya kuimarisha hatua za kuzuia maambukizi na kuhakikisha utunzaji salama wa wagonjwa..Mwakilishi wa mpya wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Togolani Mavura amewasilisha rasmi nyaraka zake kwa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres jijini New York Marekani na kueleza yale aliyokuja nayo.shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM limesema fedha zinazotumwa nyumbani na watu waishio ughaibuni au diaspora sasa zimezidi kiwango cha fedha za misaada rasmi ya maendeleo na uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje. IOM imeeleza pia namna diaspora walivyo na msaada mkubwa wakati wa majanga kwa kutuma fedha haraka, huduma na usaidizi kupitia mitandao ya kuaminika katika nchi mbalimbali ikiwemo Somalia, Haiti, Ufilipino na Ukraine.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "PEKEPEKE."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • 21 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika harakati za kudhibiti mlipuko wa Ebola zinaendelea huko DRC na Uganda. Maafisa wa WHO walipozungumza na waandishi wa habari huko Geneva, Uswisi walitoa ufafanuzi wa masuala kadhaa ikiwemo chanjo na nini cha kufanya ili jamii iwe kitovu cha udhibiti wa maambukizi.Hadi sasa  Tani 30 za vifaa vya dharura vya kukabiliana na Ebola zimewasili Bunia, mashariki mwa DRC, ndani ya siku nne kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa MONUSCO. Vifaa hivyo ni pamoja na dawa, vifaa vya maabara, PPE na mahema ya kuhudumia wagonjwa. Wakati huo huo MONUSCO inaendelea kuelimisha wananchi kuhusu njia za kujikinga, huku WHO ikisema zaidi ya watu 600 wanashukiwa kuwa na Ebola na vifo 139 vinavyohusishwa na ugonjwa huo vimeripotiwa tangu mlipuko huo kuanza.Tukisalia na Ebola, Ili vifaa vya Ebola vifike kwa wakati, wako mashujaa nyuma ya pazia wanaohakikisha kila mzigo unasafiri salama. Miongoni mwao ni Milton Oloo, mwenye miaka 30 ya uzoefu wa kupakia mizigo JKIA nchini Kenya, ambaye sasa yuko mstari wa mbele kusaidia safari za ndege za Umoja wa Mataifa, UNHAS. “Tunachokifanya hapa leo ni kuhakikisha kwamba mizigo inayoelekea Congo DRC imepangwa vizuri na kupakiwa ipasavyo ili isiharibike. Pia naona fahari na Maisha ya watu yanayookolewa  nafurahi”.Na jukwaa la 13 la miji dunini WUF13 linaelekea ukingoni Baku Azerbaijan likijadili changamoto ya makazi duniani, Rehema Kishoa kutoka Tanzania Mkurugenzi Msaidizi wa Uzingatiaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi kutoka Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya ardhi anasema wao wamechukua hatua kukabili changamoto hiyo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kware hutetemekea majanini.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    10 min
  • 20 MEI 2026
    Hii leo kwenye Jarida la Habari tuna Muhtasari na Mada kwa Kina.MUHTASARIOngezeko la idadi ya wagonjwa wa Ebola nchini DRCUmuhimu wa kushirikisha jamii kwenye udhibiti wa Ebola Mpango wa Tanzania wa kukabiliana na makazi duniMADA KWA KINAInaangazia uchambuzi wa ripoti ya uanishaji wa upatikanaji wa chakula nchini Tanzania ambapo tumezungumza na Afisa kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Hali iko vipi ? na nini kinafanyika kusaidia waliokumbwa na uhaba wa chakula.Msomaji wako leo ni Rashid Malekela 
    10 min
  • 19 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika Kaunti ya Kilifi Mombasa Kenya kumsikia Mbunge Martha Koki ambaye kandoni mwa mkutano wa CSW70 uliomalizika mwezi uliopita alizungumza na Idhaa hii kufafanua haki za wanawake za umiliki wa ardhi.Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO nchini Jamhuri ya kidemokrasia Congo DRC Daktari Anne Ancia amewaambia waaandishi wa habari kuwa “Kuna zaidi ya washukiwa 500 na vifo 130 vinavyohisiwa kutokana na ugonjwa wa Ebola, na maabara zimethibitisha watu 30 wanaugua ugonjwa huo.” Mbali ya DRC, wagonjwa wawili wamegundulika huko Kampala Uganda na mwingine raia wa Marekani ambaye amepelekwa nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi, wakati huu ambapo WHO bado inakumbwa na sintofahamu kuhusu chanzo cha mlipuko wa sasa wa Ebola DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD, limetoa ripoti ukionesha uchumi wa dunia unakabiliwa na mtihani mpya kutokana na mishtuko ya biashara, chakula na fedha inayosambaa kimataifa. Ripoti hiyo inaonya kuwa licha ya kuanza kwa mwaka kwa matumaini mazuri, hali ya kijiografia, vita na changamoto za masoko sasa zinatishia ukuaji wa uchumi duniani. UNCTAD inaeleza kuwa nchi zinazoendelea ndizo zilizo hatarini zaidi, zikikabiliwa na mtikisiko wa mitaji, mzigo wa madeni na hofu ya uhaba wa chakula. Shirika hilo linashauri mataifa kuchukua hatua za kuimarisha sera za uchumi, biashara na uwekezaji ili kujikinga na madhara ya mishtuko hiyo.Na panya wanazua balaa huko Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel. Wananchi wanasema kuwa panya wanaingia kwenye mahema kila siku, wanachafua akiba ya chakula, na kushambulia watoto wadogo nyakati za usiku. Ikumbukwe baada ya vita kusitishwa wananchi walirejea katika maeneo yao lakini kwakuwa nyumba zililipuliwa wengi wanaishi kwenye mahema huku mazingira yakiwa machafu na mifumo ya maji ikiwa haifanyi kazi na hayo ni mazingira mazuri kwa panya kuzaliana.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners