Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Siku ya Kinamama: Mama ni nguzo ya jamii na msingi wa haki za watoto
    Je wajua nafasi ya mama katika jamii? Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya mama Jumapili Mei 10, tunakupeleka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambako nafasi mama ya katika kusongesha haki za kijamii hususan za watoto wao imewekwa bayana. Feissal Kirwa anafafanua kwenye taarifa hii itokanayo na video iliyoandalaliwa  na Redio washirika wetu Domus.
    3 min
  • 11 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres nchini Kenya, Akili Mnemba katika nafas iza ajira, na nafasi ya mama katika jamii ikiturejesha nchini Kenya kusikiliza simulizi za wamama.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Kenya kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika makao yake makuu jijini Nairobi. Uwekezaji huo unaelezwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ambayo Umoja wa Mataifa umewahi kufanya barani Afrika.Je Akili Mnemba, AI inaweza kuchukua ajira yako? Ingawa kila uchwao AI inaandika upya sheria za kazi, ubunifu na kubadili vile tunavyoishi lakini kuna kazi moja ambayo bado watu wanasema hiyo ni ya watu maalum sana na kwamba AI haiwezi kuichukua. Hapo jana jumapili tarehe 10 Mei dunia iliadhimisha siku ya wakina mama duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya Uzazi UNFPA lilitembelea viunga vya New York Marekani na kuzungumza na wanawake.Je wajua nafasi ya mama katika jamii? Dunia ikiwa imeadhimisha siku ya mama Jumapili Mei 10, tunakupeleka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambako nafasi mama ya katika kusongesha haki za kijamii hususan za watoto wao imewekwa bayana. Feissal Kirwa anafafanua kwenye taarifa hii itokanayo na video iliyoandalaliwa  na Redio washirika wetu Domus.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    12 min
  • UN yawekeza dola milioni 340 Nairobi kuimarisha kitovu chake barani Afrika
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres yuko ziarani nchini Kenya kushuhudia uwekezaji mkubwa wa Umoja wa Mataifa wenye thamani ya karibu dola milioni 340 katika makao yake makuu jijini Nairobi. Uwekezaji huo unaelezwa kuwa moja ya miradi mikubwa zaidi ya miundombinu ambayo Umoja wa Mataifa umewahi kufanya barani Afrika. Stella Vuzo kutoka kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIS Nairobi anafuatilia zira hiyo na  hii hapa taarifa yake.
    5 min
  • 08 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Kigoma nchini Tanzania tunamsikia Mwakilishi Mkazi wa FAO Tanzania Nyabenyi Tito Tipo ambaye alitembelea mkoa huo kuona hali ya utekelezaji na mgao wa vifaa vya kuimarisha sekta ya uvuvi. Pia tunakuletea muhtasari wa habariShirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani WHO limesema Virusi ya Hanta havifanani na vya COVID na kwamba wanaelewa bado watu wana kumbukumbu mbichi za ugonjwa huo. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva Uswisi msemaji wa WHO Christian Lindmeier amesema wanaendelea kuratibu na kufuatilia kwa karibu mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea kwenye meli ya kifahari ya kitalii na kwamba  “Hatari ni ndogo kabisa, hii si COVID mpya.”Matthew Hollingworth ambaye ni Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani (WFP) amerejea hii leo kutoka Somalia na kuwaeleza waaandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi yale aliyojionea akiwa ziarani nchini humo kwa wiki moja kuwa “ Nimeona familia ambazo zimeshuhudia madhara mengi  kwa wakati mmoja ikiwemo athari za hali mbaya ya hewa, migogoro na shinikizo la kiuchumi, athari zote hizo zimekuwa zikisukuma njaa hadi katika viwango vya hatari .”Na, Wanawake na wasichana nchini Lebanon wanaendelea kuuawa, kujeruhiwa na kukimbia makazi yao licha ya makubaliano dhaifu ya usitishaji mapigano yaliyoanza kutekelezwa Aprili 17 mwaka huu, limeonya leo Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake UN Women.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    11 min
  • 07 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo kandoni mwa kikao cha UNPII Flora Nducha alizungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Siku ya tano tangu kuripotiwa kwa virusi vya Hanta kwenye meli ya kifahari ya Hondius kutoka Argentina na kulazimika kutia nanga nchini Cabo Verde, hii leo Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni, (WHO) Dkt. Tedros Ghebreyesus amewaambia waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi kuwa uchunguzi kuhusu mlipuko huo uliosababisha hadi sasa vifo vya watu 3 wakiwemo wanandoa wawili unaendelea.Tukisalia na mlipuko huo wa virusi vya Hanta, Mwakilishi wa WHO nchini Cabo Verde amesema hivi sasa meli hiyo Hondius iko njiani kuelekea visiwa vya Canary nchini Hispania, “na kwenye meli tuna daktari wa Shirika la Afya Duniani (WHO), kuna madaktari wawili wa Kiholanzi ambao wameimarisha timu, na kuna mtaalamu mmoja wa magonjwa ya mlipuko ambaye atasafiri na meli hadi bandari inayofuata ambayo ni visiwa vya Canary. Kwa sasa hakuna mtu mgonjwa kwenye meli, lakini iwapo mtu ataugua, basi kutakuwa na madaktari na vifaa vya matibabu vya kuwahudumia wakati wa safari.”Nchini Tanzania hivi karibuni ripoti ya uainishaji wa viwango vya upatikanaji wa chakula nchini humo iliyoandaliwa kwa pamoja na serikali na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO ilieleza kuwa baadhi ya maeneo ya Halmashauri za wilaya za Same, Maswa na Monduli yako katika kiwango cha tatu yaani (IPC 3).Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKUNGUNI"Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    10 min
  • Miaka 25 ya Jukwaa la Watu wa Asili Tanzania imepiga hatua kutujumuisha - Ole Kulet Mwarabu
    Haki ya afya kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ni haki ya kila mtu bila kujali uko kwenye kundi au jamii gani. Huo ulikuwa ni msisitizo mwaka huu kwenye Jukwaa la jamii za watu wa asili lililokuja jamvi wiki iliyopita hapa New York Marekani. Na kandoni mwa kikao hicho Flora Nducha alipata fursa ya kuzungumza na mshiriki kutoka Tanzania kwenye jamii ya Wamaasai mwana harakati wa haki za jamii hiyo Adam Kulet Ole Mwarabu aliyeanza kwa kumueleza kwanini mwaka huu ni wa kipekee kwa watu wa jamii za asili 
    9 min
  • Serikali ya Tanzania inajali usawa na haki kwa watu wote kupata huduma kwa usawa - Profesa Malebo
    Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani  baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Feisal Kirwa wa idhaa hii alifanya mahojiano naye kwanza akitaka kufahamu Tanzania ina mikakati gani ya kuhakikisha watu wa asili wanajumuishwa katika huduma za afya kwa wote?
    3 min
  • Abiria mwingine amethibitishwa kuwa na ugonjwa wa virusi vya Hanta
    Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.  Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
    3 min
  • 06 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia maambukizi wa Hantavirus, juhudi za kutokomeza Adhabu za Viboko shuleni nchini Tanzania, na ujumbe wa Profesa Hamisi Masanja Malebo kuhusu haki za watu wa asili.Imethibitishwa kuwa abiria mwingine aliyekuwa kwenye meli ya kitalii iliyohusishwa na mlipuko wa ugonjwa wa virusi vya Hanta au Hantavirus ameambukizwa ugonjwa huo, ugonjwa ambao tayari umeua watu watatu waliokuwa ndani ya meli na kusababisha tahadhari ya kimataifa iliyoratibiwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) la Umoja wa Mataifa.Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo’ iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.Siku tano zilizopita Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefunga pazia hapa katika makao ya Umoja wa Mataifa  jijini New York, Marekani  baada ya majadiliano ya takribani wiki mbili ya wadau kutoka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu sera, mafanikio na kukabiliana na changamoto mbalimbali katika kuhudumia wananchi wao ikiwemo jamii za watu wa asili. Kwa upande wa Tanzania, mmoja wa walioshiriki ni Katibu Mtendaji wa Tume ya shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ya Taifa la Tanzania, Profesa Hamisi Masanja Malebo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners