Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UNICEF Tanzania yaongoza kampeni kukomesha adhabu ya viboko shuleni
    Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko huadhimishwa Aprili 30 ya kila mwaka, na mwaka huu katika maadhimisho ya siku hiyo wiki iliyopita, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF, nchini Tanzania kwa kushirikiana na wadauwa haki za binadamu na elimu lilizindua kampeni iitwayo ‘No Collabo’ iliyolenga kukomesha adhabu ya viboko kwa mtindo ambao walimu zaidi ya mmoja humchapa mwanafunzi viboko kwa wakati mmoja. Rashid Malekela amezungumza na wazazi mkoani Mwanza Kaskazini Magharibi mwa nchini hiyo kupata maoni yao.
    4 min
  • 05 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumsikia kijana ambaye baada ya kukosa ajira, alichagua kujiajiri kwa kuuza miwa na juisi yake, hatua iliyomwezesha kujipatia kipato na kupambana na umaskini. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na jifunze KiswahiliShirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limesema abiria na wahudumu waliokumbwa na mlipuko wa hantavirus katika meli ya utalii iliyokuwa Bahari ya Atlantiki huenda waliambukizwa virusi hivyo kabla ya kupanda meli hiyo, ingawa maambukizi miongoni mwa watu ndani ya meli hayawezi kuondolewa kabisa licha ya kuwa ni nadra. Watu saba kati ya abiria na wahudumu 147 wameugua huku wengine wakifariki dunia.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafi wa Mikono hii leo 2026 chini ya kauli mbiu “Hatua Zinazookoa Maisha,” kikisisitiza haja ya kuimarisha uzuiaji wa maambukizi katika vituo vya afya. WHO inaonya kuwa maambukizi yanayotokana na huduma za afya bado ni tishio la kila siku katika hospitali na kliniki, yakichangia usugu wa dawa za viua vijasumu au antibiotiki, ongezeko la gharama, pamoja na vifo vinavyoweza kuzuilika.Leo Mei 5 ni Siku ya Kimataifa ya Wakunga, huku Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA, likisema wakunga ni wadau muhimu katika huduma za afya ya uzazi duniani kote. Shirika hilo linasema dunia inahitaji wakunga milioni moja zaidi ili kuboresha huduma za afya na kuokoa maisha ya wanawake na watoto wachanga. Kwa mujibu wa UNFPA, wakunga wanahakikisha ujauzito na kujifungua salama, huku pia wakisaidia kupunguza mimba zisizotarajiwa, maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na upasuaji usio wa lazima wakati wa kujifungua.”Katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Kwendako mema hurudi mema."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    10 min
  • Kenya tunashirikiana na mataifa jirani kutokomeza ukeketaji_ Hanna Wendot Cheptumo
    Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.
    3 min
  • WHO Afrika yawatoa hofu wananchi kuhusu Hantavirus
    Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika limesemalinafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka kufikia sasa watu watatu wamepoteza maisha. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
    3 min
  • 04 MEI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia ugonjwa unaotokana na virusi vya hantavirus, njaa na afya kwa raia nchini Somalia, na ujumbe wa mshiriki wa mkutano wa CSW70 Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya kuhusu ukeketaji.Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kanda ya Afrika linafuatilia kwa karibu na kutoa msaada unaohitajika kufuatia tukio la afya ya umma kuhusu ugonjwa wa Virusi vya Hanta uliothibitishwa kutokea katika meli ya kitalii iliyosafiri katika Bahari ya Atlantic ambapo mpaka sasa watu watatu wamepoteza maisha.Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi za wakimbizi na vituo vya afya mjini Mogadishu na Baidoa mwishoni mwa wiki.Ukeketaji bado ni changamoto katika maeneo kadhaa duniani na takwimu za Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani, WHO hadi mwaka jana kulikuwa na zaidi ya wasichana na wanawake zaidi ya milioni 230 walio hai waliokeketwa katika nchi 30 za Afika, Mashariki ya Kati na Asia. Kupitia mahojiano yaliyofanyika kandoni mwa Mkutano wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani, CSW70 jijini New York, Marekani, miezi miwili iliyopita, Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya anaeleza hatua zinazochukuliwa na nchi yake kupambana na hali hiyo ya ukeketaji.”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • Janga la njaa na mateso vinazidi kutuangamiza, raia nchini Somalia wamweleza Fletcher
    Wanawake na watoto waliokimbia ukame na migogoro nchini Somalia wameonya kuwa wanazidi kutumbukia katika janga la kibinadamu la njaa na mateso huku kupungua kwa ufadhili wa misaada ya kibinadamu kukiendelea kuathiri maisha ya watu kote nchini humo. Onyo lao limetolewa wakati mkuu wa masuala ya dharura na misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher, akihitimisha ziara yake katika kambi za wakimbizi na vituo vya afya mjini Mogadishu na Baidoa mwishoni mwa wiki.  Flora Nducha na taarifa zaidi
    4 min
  • 30 APRILI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo tunamsikia Dkt. Tulia Ackson, Rais wa Muungano wa Mabungeni duniani, (IPU) ambaye hivi karibuni akiwa makao makuu ya UN, Marekani aliongoza kikao kilichokuwa sehemu ya Mkutano wa CSW70. Mara baada ya kikao hicho Assumpta Massoi wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa alizungumza naye masuala kadhaa ikiwemo yale waliyopatia kipaumbele ili kusongesha usawa wa kijinsia duniani.Karibu Dkt. Tulia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo saa 3 asubuhi kwa saa za New York Marekani ameeleza kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu suala la kufungwa kwa mlango bahari wa Hormuz wakati mzozo huko mashariki ya kati ukiingia mwezi wa tatu licha ya kuwepo kwa usitishaji mapigano aliouita kuwa ni dhaifu. Katibu Mkuu ameonya kuwa kadri hali inavyoendelea, ndivyo gharama kwa ubinadamu zinavyoongezeka, akisisitiza kuwa nchi zinazoendelea zitaathirika zaidi kutokana na madeni makubwa na kupotea kwa ajira na kuwataka wahusika wote kurejesha mara moja uhuru wa usafiri kama ilivyoainishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitia Azimio namba  2817.Ripoti mpya ya pamoja iliyotolewa leo na mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayohusika na chakula, kilimo na uchumi yakishirikiana na Tume ya Muungano wa Afrika imeonesha kuna pengo kubwa kati ya ufadhili wa sasa wa umma na binafsi wa kilimo na kiwango cha ufadhili kinachohitajika ili kubadilisha mifumo ya kilimo barani Afrika. Ripoti hiyo pia inathibitisha ongezeko linaloendelea la njaa na ukosefu wa uhakika wa chakula kote barani Afrika, ikisisitiza uharaka wa ufadhili mkubwa na endelevu ili kubadilisha mifumo ya kilimo.Na leo ni siku ya kuadhimisha muziki wa jazz duniani, siku inayotukumbusha nafasi ya muziki wa jazz kama daraja la kuleta amani, umoja na mazungumzo kati ya watu wa tamaduni tofauti. Kupitia midundo yake ya kipekee, jazz imeendelea kuwa chombo muhimu cha elimu na ushirikiano, ikiunganisha jamii duniani kote. Serikali, taasisi za elimu, mashirika ya kiraia na watu binafsi huungana kusherehekea mchango wa jazz katika kujenga jamii jumuishi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • Rwanda ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua kukabiliana na homa ya ini
    Mapambano ya kimataifa dhidi ya homa ya ini ya virusi aina ya B na C yanaanza kuonesha mafanikio, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, iliyotolewa Aprili 28, 2026. Ripoti hiyo, imezinduliwa wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Homa ya Ini mjini Bangkok, Thailand, mkutano ulioingia leo siku ya pili na unakunya jamvi kesho. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
    3 min
  • Nimesahau yaliyopita na naganga yajayo baada ya kuuawa kwa baba yangu - Rwibutso
    Siku 100 za maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi yaliyofanyika yapata miaka 32 iliyopita zikiendelea . Leo tunakupeleka mjini Kigali nchini Rwanda kwenye Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwake Eugene Uwimana afisa habari wa ofisi hiyo ili kupata simulizi ya ya kijana anayemuenzi baba yake aliyekuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambaye aliuawa katika mauaji hayo ya kimbari. Jina la baba huyo ni Emmanuel Turatsinze
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners