Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 29 APRILI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa Kikanda wa Afya Barani Afrika wa mwaka 2026 unaokunja jamvi leeo, Mapambano ya kimataifa dhidi ya homa ya ini ya virusi aina ya B na C, na maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda.Mkutano wa Kikanda wa Afya Barani Afrika wa mwaka 2026 “World Health Summit 2026” umehitimishwa leo mjini Nairobi nchini Kenya, ukiwaleta pamoja zaidi ya wajumbe elfu moja kutoka takribani nchi 50 kujadili namna ya kuimarisha mifumo ya afya barani Afrika na duniani.Mapambano ya kimataifa dhidi ya homa ya ini ya virusi aina ya B na C yanaanza kuonesha mafanikio, imesema ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, iliyotolewa Aprili 28, 2026. Ripoti hiyo, imezinduliwa wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Homa ya Ini mjini Bangkok, Thailand, mkutano ulioingia leo siku ya pili na unakunya jamvi kesho.Siku 100 za maombelezo ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya Rwanda dhidi ya Watutsi yaliyofanyika yapata miaka 32 iliyopita zikiendelea . Leo tunakupeleka mjini Kigali nchini Rwanda kwenye Ofisi ya Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwake Eugene Uwimana afisa habari wa ofisi hiyo ili kupata simulizi ya kijana anayemuenzi baba yake aliyekuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa ambaye aliuawa katika mauaji hayo ya kimbari. Jina la baba huyo ni Emmanuel Turatsinze.”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    10 min
  • Lenga nyota ili ukizikosa uupate mwezi asema Alinda Mashiku, Mhandisi NASA
    Anold Kayanda wa Idhaa hii anazungumza na Dkt. Alinda Mashiku, Mhandisi wa masuala ya anga katika moja ya Vituo vya masuala ya anga za mbali nchini Marekani, NASA. Kwa kuzingatia kuwa Umoja wa Mataifa unapigia chepuo wasichana na wanawake kupata fursa katika sayansi na teknolojia, swali la kwanza la Anold Kayanda kwa Alinda Mashiku ni ameipokeaje hatua ya hivi karibuni ambapo kwa mara ya kwanza mwanamke Christina Cochameshiriki katika timu ya wana-anga waliosafiri na kufanikiwa kuuzunguka mwezi katika eneo mbali zaidi katika anga ya mbali ambako kulikuwa hakujawahi kufikiwa na  wanadamu?
    29 min
  • Kenya: Mradi wa majaribio walenga kudhibiti plastiki na kemikali kwenye kilimo
    FAO nchini Kenya inasema mradi huo wa miaka mitano uitwao FARM, unalenga kuimarisha uwekezaji katika mbinu mbadala na usimamizi endelevu wa kemikali hatari na plastiki kwenye sekta ya kilimo barani Afrika na Amerika ya Kusini. Tweet URLUkifadhiliwa na Fuko la Mazingira Duniani, GEF, mradi unafanya kazi na vikundi vya wataalamu wa kitaifa kutoka taasisi mbalimbali, kuangazia vipaumbele na changamoto za ndani ili kutengeneza mitaala ya mafunzo inayolinda mazingira. Ripoti ya mradi imebainisha kuwa matumizi ya viuatilifu yamekuwa na madhara makubwa kwa viumbe wanaosaidia uchavushaji wa mimea. Aidha, mabaki ya sumu hizi yanaweza kukaa kwenye udongo kwa zaidi ya miaka 30, jambo ambalo ni hatari sio tu kwa mazao ya chakula bali pia kwa afya za wakulima. Madhara ya matumizi kupita kiasiMatumizi yaliyopitiliza yamehusishwa na magonjwa ya saratani na matatizo ya mfumo wa mishipa ya fahamu, huku yakipunguza uwezo wa nchi kuuza mazao yao kwenye masoko ya kimataifa kutokana na viwango vya sumu kuzidi mipaka ya usalama wa chakula.  Afisa wa FAO, Oxana Perminova anasema, "plastiki na kemikali za kilimo ni jambo linalotia wasiwasi duniani kote. Suala hilo limekuwa katika ajenda za nchi nyingi. Kwa upande wa Kenya, tunaamini kuwa ushirikiano huu ambao umeanzishwa hapa na ambao kwa kweli unafanya kazi ya na unawaleta wadau wote pamoja utakuwa na manufaa makubwa kwa kanda hii. Hivyo nchi nyingine jirani zinaweza kuangalia mifano na bidhaa zitakazozalishwa ndani ya ushirikiano huu na kuzitumia mahususi kwa ajili ya kupunguza uchafuzi wa mazingira kutokana na kemikali na plastiki za kilimo na kuwalinda wakulima, hasa katika maeneo haya." Fahamu kuhusu madhara ya plastiki za vifungashioKuhusu plastiki za vifungashio vya pembejeo za kilimo, takwimu zinaonesha kuwa takriban tani 330,000 za plastiki hutumika kila mwaka kama vifungashio vya viuatilifu duniani kote. Inakadiriwa kuwa asilimia 35 ya plastiki hizi hazidhibitiwi ipasavyo, ambapo asilimia 10 huishia baharini na nyingine nyingi kubaki kwenye udongo. Grace Muchemi, ni Meneja Mkuu wa bodi ya kudhibiti bidhaa za viuatilifu, PCPB, nchini Kenya, anaeleza hatua zinazochukuliwa kuwa ni "tunapotazamia njia mbadala salama zaidi, tumekuwa tukipitia upya viuatilifu ili kuhakikisha viuatilifu vyenye hatari ndogo vinatumika ndani ya nchi. Pia, utoaji wa uelewa umefanyika ndani ya kaunti, na tunafanya kazi pamoja na mashirika mengine ya serikali na pia wadau wa maendeleo kutoa uelewa juu ya matumizi salama ya viuatilifu ili kuhakikisha chakula salama na pia kuwezesha biashara na nchi nyingine." Katika hatua muhimu ya kuleta usawa, mradi huu umehakikisha uwiano sawa wa washiriki wanaume na wanawake katika mafunzo yote yatakayotolewa. 
    3 min
  • Balozi Ngoga: Manusura wana mchango mkubwa katika ujenzi wa Rwanda baada ya mauaji ya kimbari
    Tweet URLSuala hilo la mchango wa manusura katika kuepusha mauaji kama hayo hayajirudii tena, nililimulika wakati wa mazungumzo yangu ya hivi karibuni na Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Martin Ngoga ambaye bila kumung’unya maneno alinieleza kuwa, “ wanamchango mkubwa sana kwa sababu kwanza wanapambana na hali ambayo katika hali ya kawaida ya ubinadamu ni ngumu. Chukulia mfano wetu sisi Rwanda walionusurika mauaji na waliotekeleza wanaishi pamoja kwa sababu Rwanda hakuna mgawanyiko wa kikabila wa kwamba kuna baadhi wanaishi mkoa fulani. Wanaishi pamoja katika vijiji hivyo, hivyo wanaenda shule hizo hizo wanaenda hospitali pamoja na wanaishi pamoja. Kwa mtu ambaye amepoteza familia yake nzima na anawajua wauaji walioua familia yake na anaendelea kuishi nao kijijini, ni hali ambayo kwa kweli katika akili ya kawaida unaweza usielewe lakini imetokea Rwanda.”Mwaka huu wa 2026 ni miaka 32 tangu kutokea kwa mauaji hayo ya kimbari. Hivyo Balozi Ngoga ambaye aliwahi kuwa Mwakilishi wa Rwanda kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu uliotokea Rwanda (ICTR) akafafanua kwamba, “Baadhi ambao walikuwa ni wadogo wakati huo ambao sasa ni watu wazima, wanaandika hata vitabu kueleza nini kilitokea. Lakini wamekubali kuingia katika mchakato wa maridhiano, kujenga upya taifa la Rwanda."Akaongeza kuwa, "na kama ambavyo aliwahi kusema kiongozi wetu Rais Paul Kagame wakati fulani kwamba wao walionusurika ndio wanacho cha kutoa. Wao ndio wanaombwa watoe zaidi katika kuchangia juhudi za kulijenga upya taifa kwa sababu muuaji unaenda kumuomba nini. Tunashukuru kwamba wamekubaliana na hiyo, hali ambayo katika mazingira ya kawaida ya kibinadamu ni ngumu sana. Lakini kwa miaka yote hii tunakwenda.”
    3 min
  • Kila saa moja zaidi ya wanawake na wasichana 100 wanafurushwa nchini Sudan Kusini
    Zaidi ya wanawake na wasichana 100 wanakimbia makazi yao kila saa nchini Sudan Kusini huku kuongezeka kwa mapigano na njaa kukichochea kuongezeka kwa janga la kibinadamu, Anna Mutavati, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake (UN Women) ameeleza leo baada ya ziara ya siku tano nchini humo.Kupitia taarifa ya UN Women iliyosambazwa leo kwa vyombo vya habari katika mji mkuu wa Sudan Kusini Juba na katika ofisi za Umoja wa Mataifa zilizoko Geneva, Uswisi, Anna Mutavati amenukuliwa akisema, “takribani asilimia 60 ya watu 223,641  ya waliokimbia makazi yao tangu mwanzo wa mwaka huu nchini Sudan Kusini ni wanawake na wasichana, wastani wa wanawake 104 kila saa,” na akaongeza kuwa baadhi ya wanawake na wasichana “wanakula mimea ya porini ili kuishi,” huku wengine wakikaa siku kadhaa bila kula. Amefafanua zaidi kuwa sehemu kubwa ya watu waliokimbia makazi yao ni kutoka Jimbo la Jonglei, ambako takribani wanawake na wasichana 174,197 wameathiriwa na mapigano. Bi. Mutavati amesema wanawake na wasichana ni miongoni mwa waliouawa katika mashambulizi ya kulengwa, ikiwemo shambulio la Machi katika Eneo la Utawala la Ruweng lililosababisha vifo vya watu wasiopungua 169 akionya kuwa ghasia zinazidi kuongeza hatari kwa wale waliokwishakimbia makazi yao. Pia ameeleza wasiwasi kuhusu kusambaratika kwa huduma muhimu, akisema uporaji na uharibifu wa vituo vya afya umeacha wanawake bila huduma muhimu za matibabu. “Wanawake wanajifungua bila huduma yoyote ya kitabibu kwa hatari kubwa ya kupoteza maisha,” amesema. UN Women inakadiria wanawake na wasichana milioni 5 nchini Sudan Kusini wanahitaji msaada wa kibinadamu mwaka huu, wakiwemo milioni 2.5 wanaohitaji huduma zinazohusiana na ukatili wa kijinsia.Akitoa wito wa hatua za haraka, Bi. Mutavati amesema uongozi wa wanawake lazima ubaki kuwa kiini cha juhudi za amani na ametoa wito wa kuheshimiwa kwa kiwango cha asilimia 35 cha uwakilishi wa wanawake serikalini chini ya makubaliano ya amani. “Hakuna njia ya amani ya kudumu iliyothibitika zaidi kuliko uongozi wa wanawake,” amesema, huku pia akitaka ufadhili kwa mashirika yanayoongozwa na wanawake na msaada kwa kaya zinazoongozwa na wanawake. Wakati Sudan Kusini ikielekea katika uchaguzi wa mwaka huu 2026, Mkurugenzi huyo wa Kanda ya Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika wa UN Women ametoa wito wa kuwepo kwa mchakato wa uchaguzi unaoaminika, jumuishi na wa uwazi unaohakikisha ushiriki wa wanawake katika kila hatua. Amenukuliwa akisema, “tunatoa wito wa utekelezaji kamili na wa haraka” wa makubaliano ya amani,  na akasisitiza kuwa kulinda wanawake na wasichana na kuhakikisha wanashiriki katika uamuzi ni msingi wa kufikia amani ya kudumu.
    4 min
  • UNMISS: Kwa raia wa Nasir nchini Sudan Kusini “kila penye giza nuru haikosekani”
    Mwaka mmoja baada ya mapigano makubwa kusababisha vifo na kuwafanya maelfu ya watu kuyahama makazi yao mjini Nasir, jimbo la Upper Nile, dalili za ahuweni zinaanza kuonekana. Wakazi wanarejea polepole, wakijenga upya maisha yao na kurejesha hali ya kawaida kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS. Flora Nducha anasimulia zaidi
    3 min
  • Vijana wasomi wa vyuo vikuu katika ukanda wa Gaza walazimika kufanya kazi ndogo ndogo ili kujikimu
    Hali ngumu ya kiuchumi inayoendelea kuzorota katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel imewafanya vijana waliokuwa wakisoma vyuo vikuu na wahitimu kuhangaika kufanya kazi ndogo ndogo ili kujikimu baada ya ndoto zao za masomo na taaluma kuvurugwa na vita iliyodumu kwa miaka mitatu. Leah Mushi anatuletea simulizi za baadhi ya vijana hao na shuhuli wanazozifanya hivi sasa.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners