Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UN yaadhimisha miaka 25 ya Jukwaa linalojikita katika haki za Watu wa Asili mkazo ukiweka zaidi katika changamoto za afya na mabadiliko ya tabianchi
    Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Watu wa Asili (UNPFII) limefungua kikao chake cha ishirini na tano leo Aprili 20 katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani likiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kama jukwaa la kipekee la kimataifa linalowakutanisha wadau kuhusu Watu wa Asili. Kikao hiki kinafanyika katika muktadha wa changamoto zinazoendelea duniani, zikiwemo afya, migogoro na ukosefu wa usawa. Pia kinakuja wakati ambapo mfumo wa ushirikiano wa kimataifa, ndani ya mfumo wa mipango kama Mpango wa Mageuzi ya Umoja wa Mataifa, UN80 unakabiliwa na mahitaji yanayoongezeka ya ujumuishwaji, uhalali na ufanisi. Anold Kayanda amelifuatilia tukio hilo. 
    4 min
  • Lishe yarejesha matumaini ya elimu Kigoma, Magdalena arejea shuleni na kuwa chanzo cha mabadiliko
    Elimu imeanza kung’aa tena kwa watoto katika kijiji cha Twabagondozi, ambapo njaa iliyokuwa kikwazo kikubwa cha masomo sasa inapungua kupitia mpango wa lishe na malezi bora unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Kupitia juhudi hizi, watoto kama Magdalena A. Prosper wamepata nafasi ya kurejea darasani, kujifunza na hata kuwa viongozi shuleni. Feissal kirwa anasimulia.
    4 min
  • 20 APRILI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia yaliyojiri katika Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili hapa Makao Makuu, mafunzo Kenya ya "Social Media 4 Peace" yaani ya kuondoa habari potofu na deepfakes mtandaoni, na mlo shuleni shuleni nchini Tanzania.Jukwaa la Kudumu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watu wa Asili (UNPFII) limefungua pazia leo Aprili 20 ikiwa ni kikao cha ishirini na tano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani likiadhimisha miaka 25 tangu kuanzishwa kwake kama jukwaa la kipekee la kimataifa linalowakutanisha wadau kuhusu Watu wa Asili.  Maudhim aka huu yakimulika kuhakikisha afya ya watu wa jamii za asili ikiwemo kwenye mizozo.Ni dhahiri hivi sasa watu wengi zaidi wanatumia mitandao ya kijamii katika shughuli mbalimbali na pia kupata taarifa, na kwakuzingatia ukweli huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, likishirikiana na Umoja wa wamiliki vya vyombo vya habari vya mtandaoni (Wanablogu) nchini Kenya, BAKE (inatamkwa ‘BEKI’), limeandaa mafunzo maalum jijini Nairobi yaliyopewa jina la "Social Media 4 Peace" yaani mitandao ya kijamii kwa amani. Karibu Rashid Malekela utujuze zaidi.Elimu imeanza kung’aa tena kwa watoto katika kijiji cha Twabagondozi, ambapo njaa iliyokuwa kikwazo kikubwa cha masomo sasa inapungua kupitia mpango wa lishe na malezi bora unaoungwa mkono na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Kupitia juhudi hizi, watoto kama Magdalena A. Prosper wamepata nafasi ya kurejea darasani, kujifunza na hata kuwa viongozi shuleni.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    11 min
  • Watengeneza maudhui nchini Kenya waaswa kuwa walinzi wa amani na ukweli mtandaoni - UNESCO
    Ni dhahiri hivi sasa watu wengi zaidi wanatumia mitandao ya kijamii katika shughuli mbalimbali na pia kupata taarifa, na kwakuzingatia ukweli huo, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, likishirikiana na Umoja wa wamiliki vya vyombo vya habari vya mtandaoni (Wanablogu) nchini Kenya, BAKE (inatamkwa ‘BEKI’), limeandaa mafunzo maalum jijini Nairobi yaliyopewa jina la "Social Media 4 Peace" yaani mitandao ya kijamii kwa amani. Rashid Malekela anaeleza zaidi.
    4 min
  • Zaidi ya wanawake elfu thelatini na nane wameauawa katika ukanda wa Gaza - Ripoti mpya ya UN Women
    Uchambuzi mpya wa utafiti uliotolewa leo Aprili 17 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, UN Women umeweka wazi kuwa zaidi ya wanawake na wasichana 38,000 wameauawa kati ya mwezi Oktoba mwaka 2023 na Desemba 2025 huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ikiwa ni wastani wa takribani wanawake na wasichana 47 wanaouawa kila siku. Anold Kayanda ameufuatilia utafiti huo na kutuandalia taarifa ifuatayo. 
    4 min
  • Tatizo la ukatili wa kingono kutumika kama silaha ya vita Sudan ni moja ya masuala yenye uharibifu mkubwa na maumivu makali tunayokabiliana nayo - Tonderai Chikuhwa
    Ukatili wa kijinsia na wa kingono unatumiwa kama silaha ya vita nchini Sudan, jambo ambalo limesahaulika huku migogoro ikiendelea katika maeneo mengi mengi kote duniani amesema Tonderai Chikuhwa, Mshauri Mwandamizi wa Sera katika Ofisi ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Ukatili wa kijinsia katika Migogoro, katika mahojiano na Khaled Mohamed wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa. Feissal Kirwa amefuatilia mahojiano hayo na anaeleza zaidi katika taarifa hii.
    3 min
  • 17 APRILI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya mauaji wa wanawake na wasichana Gaza, ukatili wa kijinsia na wa kingono unaotumiwa kama silaha ya vita Sudan, na msaada wa dawa na matibabu ya bure nchini DRC yanyoendeshwa na walinda amani wa MONUSCO kutoka Tanzania.Uchambuzi mpya wa utafiti uliotolewa leo Aprili 17 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, UN Women umeweka wazi kuwa zaidi ya wanawake na wasichana 38,000 wameauawa kati ya mwezi Oktoba mwaka 2023 na Desemba 2025 huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ikiwa ni wastani wa takribani wanawake na wasichana 47 wanaouawa kila siku. Anold Kayanda ameufuatilia utafiti huo na kutuandalia taarifa ifuatayo.Ukatili wa kijinsia na wa kingono unatumiwa kama silaha ya vita nchini Sudan, jambo ambalo limesahaulika huku migogoro ikiendelea katika maeneo mengi mengi kote duniani amesema Tonderai Chikuhwa, Mshauri Mwandamizi wa Sera katika Ofisi ya Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Ukatili wa kijinsia katika Migogoro, katika mahojiano na Khaled Mohamed wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa.Raia wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, waishio mji wa Oicha uliopo Mavivi katika Jimbo la Kivu Kaskazini, wamewashukuru walinda amani kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Kikundi cha Tano Cha Utayari (TANZQRF-05), kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kwa kutoa msaada wa dawa na huduma za kitabibu kwenye Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mji wa Oicha wiki hii.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min
  • Raia wa Beni DRC: Asante TANZQRF-05 kwa kutushika mkono
    Raia wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, waishio mji wa Oicha uliopo Mavivi katika Jimbo la Kivu Kaskazini, wamewashukuru walinda amani kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Kikundi cha Tano Cha Utayari (TANZQRF-05), kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo  (MONUSCO) kwa kutoa msaada wa dawa na huduma za kitabibu kwenye Hospitali Kuu ya Rufaa  ya Mji wa Oicha wiki hii. Private Habibu Shaban alikuwa shuhuda wa tukio hilo ungana naye kwa taarifa hii
    3 min
  • Simulizi za mateso na matumaini ya wakimbizi wa muda mrefu katika makazi ya wakimbizi ya Kiryandongo Uganda
    Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani. Kwa Afrika ni ya kwanza ikihifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Burundi, rwanda, Sudan, Sudan Kusini na hata Kenya. Katika mada kwa kina hii tunaangazia wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi. Abdelmonem Makki wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni ameyatembelea makazi hayo na kuzungumza na wakimbizi hao kutoka Sudan. Na sasa kwa lugha ya Kiswahili, Feissal Kirwa wa Idhaa hii anasimulia.
    6 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners