Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • FAO nchini Tanzania yapatia wakazi wa Kigoma mafunzo ya vitendo kuhusu lishe bora
    Nchini Tanzania, kupitia Mpango wa Pamoja wa Kigoma Awamu ya Pili (KJPII) unaotekelezwa chini ya uongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), maafisa ugani wa kilimo, wataalamu wa lishe na afya mkoani Kigoma waliungana kuandaa tukio la Siku ya Afya na Lishe Mitaani au SALIMI sambamba na Siku ya Shamba la Mkulima ili kuwapatia wakulima na wanajamii elimu ya vitendo kuhusu uzalishaji na matumizi ya mazao yenye lishe. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
    4 min
  • UN: Kuanzia Lebanon hadi Sudan kote ni simulizi ya giza la vita na kukimbia makazi
    Tuanzie katika ofisi za Umoja wa Mataifa za jijini Geneva, Uswisi ambako maafisa mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezungumza na vyombo vya habari kuhusu hali tete inayoendelea duniani. Tukiangazia angalau maeneo mawili tu gharama ya kibinadamu ya vita inaendelea kujitokeza kwa namna ya kuhuzunisha kuanzia mitaa iliyoharibiwa ya Lebanon hadi janga kubwa la wakimbizi Sudan. 
    3 min
  • Mwanafunzi Ahmad Omar aongoza mabadiliko ya kijani shule ya Kisiwandui Zanzibar
    Elimu imepata maana mpya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisiwandui iliyopo Zanzibar nchini Tanzania, ambapo sasa masomo ya uhifadhi wa mazingira hayajaishia darasani pekee bali yamegeuka kuwa vitendo. Kupitia mradi wa ROTA unaotekelezwa na Shirika la Wakfu wa Elimu juu ya Mengine Yote kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini humo. Rashid Malekela anatupeleka visiwani Zanzibar kufahamu jinsi kijana Ahmad Omar Mohammed anavyoongoza wenzake katika mabadiliko haya.
    3 min
  • 10 APRILI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia vita vinavyoendelea nchini Sudan, juhudi za kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanariadha nchini Kenya, na kazi za wanafunzi katika utunzaji wa mazingira huko Zanzibar.Tuanzie katika ofisi za Umoja wa Mataifa za jijini Geneva, Uswisi ambako maafisa mbalimbali wa mashirika ya Umoja wa Mataifa wamezungumza na vyombo vya habari kuhusu hali tete inayoendelea duniani. Tukiangazia angalau maeneo mawili tu gharama ya kibinadamu ya vita inaendelea kujitokeza kwa namna ya kuhuzunisha kuanzia mitaa iliyoharibiwa ya Lebanon hadi janga kubwa la wakimbizi Sudan.Elimu imepata maana mpya kwa wanafunzi wa shule ya msingi Kisiwandui iliyopo Zanzibar nchini Tanzania, ambapo sasa masomo ya uhifadhi wa mazingira hayajaishia darasani pekee bali yamegeuka kuwa vitendo. Kupitia mradi wa ROTA unaotekelezwa na Shirika la Wakfu wa Elimu juu ya Mengine Yote kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF nchini humo. Rashid Malekela anatupeleka visiwani Zanzibar kufahamu jinsi kijana Ahmad Omar Mohammed anavyoongoza wenzake katika mabadiliko hayaBaada ya matukio ya ukatili wa kijinsia, GBV na mauaji ya wanariadha wanawake kutikisa mji wa Iten, nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linashirikiana na Kituo cha Kukuza Demokrasia na Utawala Bora nchini humo kufanya kazi na makocha, wanariadha, maafisa wa michezo na serikali ya kaunti ili kuimarisha ulinzi kupitia elimu ya utambuzi, uzuiaji na kukabiliana na ukatili wa kijinsia.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • Ukatili wa Kijinsia kwa wanariadha nchini Kenya waibua wadau, viongozi - UNFPA
    Baada ya matukio ya ukatili wa kijinsia, GBV na mauaji ya wanariadha wanawake kutikisa mji wa Iten, nchini Kenya, shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, UNFPA linashirikiana na Kituo cha Kukuza Demokrasia na Utawala Bora nchini humo kufanya kazi na makocha, wanariadha, maafisa wa michezo na serikali ya kaunti ili kuimarisha ulinzi kupitia elimu ya utambuzi, uzuiaji na kukabiliana na ukatili wa kijinsia. Leah Mushi na taarifa zaidi.
    3 min
  • 09 APRILI 2026
    Jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kusikia ujumbe wa Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Jamhuri ya Kenya ambaye alikuwa miongoni mwa washiriki wa CSW70 akieleza ni kwa namna gani Kenya inapiga hatua katika Lengo namba 5 la Usawa wa Kijinsia.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali mashambulizi makubwa ya anga yaliyofanywa na Israel dhidi ya Lebanon tarehe 8 Aprili, mashambulizi ambayo yamesababisha mamia ya raia kuuawa na kujeruhiwa, wakiwemo watoto, sambamba na kuharibu kwa kiasi kikubwa miundombinu ya kiraia. Taarifa iliyotolewa New York, Marekani na Msemaji wa Umoja wa Mataifa inamnukuu Guterres akionesha wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la vifo miongoni mwa raia na kutoa pole kwa watu na Serikali ya Lebanon, akiwatakia nafuu ya haraka wale waliojeruhiwa.Katika tukio jingine hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezindua Mfuko wa Urejeshaji wa Palestina uliopewa jina la Horizon Fund, akisisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua za haraka kusaidia wananchi wa Palestina kurejesha maisha yao na kujenga mustakabali bora. Akizungumza kupitia ujumbe wa video wakati wa uzinduzi uliofanyika Ramallah, huko Ukingo wa Magharibi eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel, Guterres amesema mfuko huo ni sehemu muhimu ya ushirikiano kati ya Umoja wa Mataifa na Taifa la Palestina.Wakati mgogoro wa Sudan ukikaribia kutimiza miaka mitatu, zaidi ya wakimbizi milioni moja wa Sudan walioko nchini Chad wanakabiliwa na hatari kubwa ya kupunguzwa kwa msaada muhimu wa kibinadamu. Onyo hilo limetolewa leo na mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa ambayo ni lile la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) pamoja na la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wakitanabaisha kuwa huduma za msingi kama chakula, maji, malazi, ulinzi na huduma za afya zitalazimika kupunguzwa zaidi katika miezi ijayo iwapo pengo la ufadhili la dola milioni 428 halitazibwa haraka.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    10 min
  • Huduma za afya ziko ukingoni kuporomoka kabisa huko Gaza kuliko wakati mwingine wowote
    Madaktari na wahudumu wa afya katika ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanaonya kuwa mfumo wa afya katika eneo hilo sasa uko karibu zaidi kuporomoka kuliko wakati mwingine wowote, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka, magonjwa ya ngozi na ya kupumua yakienea, na uwezo wa kuwahudumia watu wenye magonjwa sugu ukiendelea kupungua. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
    3 min
  • 08 APRILI 2026
    Jaridani tunaangazia sitisho la mapigano nchini Iran, hali ya afya katika ukanda wa Gaza, na elimu kwa watoto walioathiriwa na vita nchini Sudan.Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Marekani na Iran la kusitisha mapigano kwa wiki mbili, wakati huu ambapo vita hiyo iliyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran ikiingia siku ya 40. Kwa upande wa Lebanon hali bado ni tete kwani Israel inaendelea na mashambulizi katika mji wa Beirut.Madaktari na wahudumu wa afya katika ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel wanaonya kuwa mfumo wa afya katika eneo hilo sasa uko karibu zaidi kuporomoka kuliko wakati mwingine wowote, huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka, magonjwa ya ngozi na ya kupumua yakienea, na uwezo wa kuwahudumia watu wenye magonjwa sugu ukiendelea kupungua.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na  Benki ya Dunia linaendelea kurejesha matumaini ya elimu kwa maelfu ya watoto katika Jimbo la Mto Nile nchini Sudan kupitia Programu za Elimu Mbadala (ALP), baada ya miaka mingi ya vurugu na kusitishwa kwa masomo kuathiri mustakabali wao.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    11 min
  • UN wakaribisha tangazo la Marekani na Iran la kusitisha mapigano
    Umoja wa Mataifa umekaribisha tangazo la Marekani na Iran la kusitisha mapigano kwa wiki mbili, wakati huu ambapo vita hivyo vilivyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran ikiingia siku ya 40. Kwa upande wa Lebanon hali bado ni tete kwani Israel inaendelea na mashambulizi katika mji mkuu Beirut ikidai kukabili wapiganaji wa Hezbollah wanaopinga kushambuliwa kwa Iran. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners