Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • UN: Hali inaendelea kuwa mbaya Mashariki ya Kati ikikatili zaidi maisha ya watu
    Vita vya Mashariki ya Kati vimeingia mwezi wa pili huku ghasia zikiongezeka katika maeneo kadhaa, ikiwemo Lebanon, Iran na Ghuba. Mlinzi wa amani wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL ameuawa baada ya kombora kulipuka katika kituo cha Umoja wa Mataifa karibu na Adchit Al Qusayr, huku mwingine akiwa mahtuti hospitali. Flora Nducha na Taarifa zaidi
    4 min
  • Kuwa na orodha ya manunuzi kutasaidia kupunguza utupaji wa chakula
    Wakati hii leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kutozalisha taka, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa kila mtu kujifunza upya yamna ya kufanya manunuzi ya vitu na mapishi ambayo hayatasababisha umwagaji wa chakula ili kunusuru mifumo ya ikolojia na afya ya binadamu. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi. 
    3 min
  • 30 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia migogoro yanayoendelea Mashariki ya Kati, ujumbe wa Katibu Mkuu leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kutozalisha taka, na kampeni ya upatiaji mifugo dawa za minyoo na  udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa Isiolo nchini Kenya.Vita vya Mashariki ya Kati vimeingia mwezi wa pili huku ghasia zikiongezeka katika maeneo kadhaa, ikiwemo Lebanon, Iran na Ghuba. Mlinzi wa amani wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL ameuawa baada ya kombora kulipuka katika kituo cha Umoja wa Mataifa karibu na Adchit Al Qusayr, huku mwingine akiwa mahtuti hospital.Wakati hii leo dunia ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya kutozalisha taka, Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa kila mtu kujifunza upya yamna ya kufanya manunuzi ya vitu na mapishi ambayo hayatasababisha umwagaji wa chakula ili kunusuru mifumo ya ikolojia na afya ya binadamu.Nchini Kenya katika kaunti za Isiolo, Garissa, Samburu na Mto Tana, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeendesha kampeni ya upatiaji mifugo dawa za minyoo na  udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa, sambamba na kupatia wananchi fedha taslimu bila masharti kama mojawapo ya kujengea jamii mnepo wakati wa ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    12 min
  • FAO Kenya yajengea uwezo kaya ili zisiyumbe kiuchumi na kijamii katikati ya ukame
    Nchini Kenya katika kaunti za Isiolo, Garissa, Samburu na  Mto Tana, shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO limeendesha kampeni ya upatiaji mifugo dawa za minyoo na  udhibiti wa wadudu waenezao magonjwa, sambamba na kupatia wananchi fedha taslimu bila masharti kama mojawapo ya kujengea jamii mnepo wakati wa ukame unaosababishwa na mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi na maelezo zaidi
    4 min
  • Makpandu: Hofu yatanda kwa wakimbizi wa Sudan walio kambini Makpandu Sudan Kusini
    Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS.Kwa muda mrefu kambi ya wakimbizi ya Makpandu imeonekana kuwa kimbilio, lakini sasa imegeuka kuwa eneo la mashaka, na hofu. Bekia Mahadi Ali, mama wa watoto wanane aliyekimbia vita nchini Sudan akitarajia kupata hifadhi, sasa amejikuta akiishi kwa wasiwasi mkubwa baada ya ghasia kuibuka upya katika eneo hili. Furaha ya kupata usalama imetoweka, ulinzi umepungua, Bekia anahofia maisha yake na ya familia yake."Hakuna usalama kabisa hapa kambini na tunaogopa, nilikimbia na wanangu bila baba yao. Watoto hawa ni jukumu langu, tulikuja hapa kutafuta kimbilio lakini hawawezi kwenda shule, sina cha kufanya. Ninachoomba tuhamishwe kutoka kambi hii,”Wakimbizi katika kambi ya Makpandu wanaripoti kuwa watu wenye silaha huingia ndani ya kambi mara kwa mara, wakifyatua risasi hovyo, kuwatishia watu, na kupora au kuchoma moto mali za raia. Omar Ibrahim, ni mkimbizi mwingine kutoka Sudan, anafunguka."Wakati mwingine tunawachukua wanawake na watoto wetu kwenda kulala vichakani kwa sababu hakuna uhakika wa usalama ndani ya kambi. Hatuwezi hata kwenda shambani kulima. Tunaiomba Serikali na Umoja wa Mataifa waingilie kati, tulikimbia risasi nchini Sudan, lakini tumekutana na risasi zilezile tena hapa."Kufuatia shambulio la hivi karibuni lililosababisha kifo cha mkimbizi mmoja wa Sudan, kikosi cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa cha kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, kimefanya doria katika kambi hiyo ya Makpandu ili kutathmini hali ya usalama. Thomas Bazawi, ni Afisa wa Ulinzi, Mpito na Urejeshwaji wa UNMISS, anafafnua jukumu lao.“Jukumu letu ni kusaidia kurejesha imani kwa kushirikiana na jamii, mamlaka za mitaa, vikosi vya usalama na wengineo. Tunafanya kazi na wadau wote kuimarisha usalama ili watu waweze kujiamini na kuendeleza maisha yao tena.”Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa uwekezaji katika amani kupitia mpango wa Hatua kwa Ajili ya Kulinda Amani (A4P) ni muhimu kwa usalama wa wakimbizi wanaokimbia migogoro ya silaha.
    3 min
  • Somalia: FAO na EU warejesha matumaini kwa wakulima kupitia kilimo cha umwagiliaji
    Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Maisha Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi CLIMB unaolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha lishe, limeanza kubadilisha maisha ya wakulima nchini Somalia, hasa katika maeneo ya Kismayo, Marka na Jowhar yaliyokuwa yameathiriwa kwa muda mrefu na ukame na mvua zisizotabirika. FAO imekarabati zaidi ya kilomita 300 za mifereji ya umwagiliaji ili kurejesha upatikanaji wa maji katika mashamba na kwa jamii, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha ustahimilivu wa wakazi wa maeneo haya kame nchini Somalia. Wakulima wanasema wameanza kuona matumaini mapya kwani mradi huu wa CLIMB umeboresha maisha yao. Nuur Mukhtar Mohamed ni mmoja wao, anasema uhaba wa maji katika Mto Jordan ulikuwa umeathiri vibaya shughuli za kilimo.Akifafanua anasema, “hapo awali tulikumbana na changamoto kubwa kwa sababu Mto Juba uko chini kuliko mashamba yetu, hali iliyofanya umwagiliaji kuwa mgumu sana. Hata hivyo, mfereji mpya ulioinuliwa umeleta mabadiliko makubwa katika maisha yetu.”Kwa mujibu wa wakulima wengine, maboresho hayo yameleta unafuu mkubwa katika shughuli za kilimo na maisha ya kila siku. Akiwa shambani, Sadiyo Sheikh Ali, mkulima kutoka kijiji cha Bulo Bartire, anaeleza kwamba,“Kabla ya mfereji huu, maji yalikuwa haba sana kiasi cha kusababisha migogoro baina ya wakulima. Sasa hali imeimarika na tuna matumaini mapya. Tumeanza kupata utulivu wa akili.”Mbali na ukarabati wa mifereji, FAO pia inawapatia wakulima mbegu bora na kuwawezesha kuanzisha vikundi vya Akiba na Mikopo vya Kijiji (VSLA), vinavyosaidia kukuza kipato na kuimarisha mshikamano wa kijamii.Akizungumzia umuhimu wa vikundi hivyo, Yusuf Abdisalam Yusuf, Mkuu wa Kikundi cha Midinimo kutoka Goobweyn, amesema “tumeunda kikundi hiki ili kushirikiana na kusaidiana katika shughuli za kilimo na maisha kwa ujumla, bila kujali ukubwa wa msaada.”Mifereji iliyokarabatiwa sasa inaendelea kufufua matumaini na kuleta fursa mpya za kipato katika eneo la Jubaland. Hata hivyo, wakulima wanasisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongezewa pembejeo, msaada wa kifedha na mafunzo endelevu ili kuhakikisha jamii zinaendelea kustawi. 
    3 min
  • Baraza la Haki za Binadamu: Tofauti zozote zilizopo kati ya nchi hazitatatuliwa kwa kuwaua wanafunzi
    Katika mjadala wa dharura kuhusu “shambulizi la anga dhidi ya Shule ya Wasichana ya Shajareh Tayyebeh huko Minab, nchini Iran, Baraza la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limejadili tukio hilo kama ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na haki za binadamu.”Mjadala huu wa dharura unafanyika kufuatia tukio hilo lililotajwa kuwa la kutisha lililofanyika siku ya kwanza kabisa ya mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran. Simulizi ya mamaTuanze na simulizi ya Mohaddeseh Fallahat, huyu ni mama wa Iran aliyepoteza watoto wake wawili katika shambulizi hilo ambaye anasema “asubuhi ile ilikuwa kama kawaida.” Aliwafunga wanawe gidamu za viatu na kuwavalisha mabegi mgongoni na hakukuwa na dalili yoyote kwamba hiyo ingekuwa mara ya mwisho, kuonana nao.Anasema “Walipotoka mlangoni, waliniambia, ‘Mama, njoo utuchukue baada ya shule.’ Sentensi hiyo rahisi sasa inajirudia akilini mwangu mara elfu moja, na kila mara moyo wangu unaungua kwa maumivu. Hakuna mama anayewahi kufikiria atampeleka mtoto wake shuleni kwa tabasamu, kisha akumbane na ukimya. Hakuna mama aliyejiandaa kusikia maneno haya: ‘Mtoto wako hatarudi tena.’” © Mshiriki Jengo moja katika eneo la mashariki mwa Tehran likionesha dalili za uharibifu uliosababishwa na mabomu.WaokoajiAkizungumza na waandishi wa habari huko Geneva akiwa Tehran kupitia mawasiliano ya satelaiti, Mkuu wa shirika la Msalaba mwekundu na Hilal nyekundu IFRC, Maria Martinez amesema zaidi ya watu 1,900 wameuawa, wakiwemo wanawake na watoto, na takriban watu 20,000 wamejeruhiwa.Martinez amesimulia masahibu yanayowakuta watoa huduma ya kwanza “Moja ya nyakati za kushtusha na kuvunja moyo ni pale mhudumu wa uokoaji na utafutaji alipogundua miili ya wafamilia yake mwenyewe chini ya vifusi vya jengo lililoshambuliwa.Katika mji wa Qom, kusini mwa Tehran, mhudumu mwingine aliokoa mwili wa shangazi yake pamoja na mume wake na mtoto wao mdogo.” Huo ndio uhalisia wanaokumbana nao wahudumu wa kibinadamu, wanaokoa maisha huku wakibeba maumivu makubwa yasiyovumilika ya kupoteza wapendwa wao.UN GenevaMjadala wa Baraza la Haki za Binadamu ukifanyika Geneva UswisiKauli ya UNTofauti zozote zilizopo kati ya nchi na nchi, sote tunaweza kukubaliana kuwa hazitatatuliwa kwa kuwaua wanafunzi.Akizungumza katika mjadala huo wa dharura, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa Volker Türk ametoa wito kwa mamlaka za kijeshi za Marekani kuchapisha haraka iwezekanavyo matokeo ya uchunguzi wao kuhusu shambulizi hilo. Türk amesema “Mashambulizi ya mabomu katika Shule ya Msingi ya Shajareh Tayyebeh huko Minab yameibua hofu kubwa na maumivu makali. Picha za madarasa yaliyoharibiwa na wazazi waliogubikwa na huzuni zinaonesha wazi ni nani hulipa gharama kubwa zaidi ya vita: raia wasio na uwezo wowote katika maamuzi yaliyopelekea mzozo. Katika tukio hili, inaripotiwa kuwa wanafunzi, walimu, wafanyakazi wa shule, na wapendwa wao 168 wameathirika.Maafisa waandamizi wa Marekani wamesema shambulizi hilo linafanyiwa uchunguzi. Natoa wito mchakato huo ukamilike haraka iwezekanavyo, na matokeo yake yawekwe wazi kwa umma. Lazima kuwe na haki kwa madhara makubwa yaliyosababishwa.”
    4 min
  • 27 MACHI 2026
    Hii leo jaridani mwenyeji wako Flora Nducha anamulika Mashariki ya Kati, mzozo Sudan Kusini unavyoendelea kuleta machungu kwa raia. Ingawa hivyo kuna habari njema ya jinsi FAO inavyoleta nuru kwa wakulima nchini Somalia kwa kukarabati mifereji ya umwagiliaji. Karibu!===========================Vita huko Mashariki ya Kati vinaendelea leo ikiwa ni siku ya 28, mashambulizi yanasababisha hofu, mateso, na kuzidisha mgogoro wa kibinadamu katika eneo lote. Huko Geneva, Uswisi wanadiplomasia katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hii leo wanajadili shambulizi la shule lililotokea Minab, Iran, ambalo limeua zaidi ya watoto 100. Leah Mushi anasimulizi hii ya kusikitisha.Hofu imetanda kwa mara nyingine katika kambi ya wakimbizi ya Makpandu iliyopo Yambio, jimboni Equatoria Magharibi nchini Sudani Kusini, ambapo maelfu ya wakimbizi kutoka Sudan wanakabiliwa na vitisho vipya vya usalama kwa mujibu wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo UNMISS. Rashid Malekela anatupeleka kufahamu maisha ya wakimbizi huo yapoje?Shirika la Umoja wa Mataifa Chakula na Kilimo (FAO) kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa Maisha Himilivu kwa Mabadiliko ya Tabianchi CLIMB unaolenga kuongeza uzalishaji wa chakula na kuimarisha lishe, limeanza kubadilisha maisha ya wakulima nchini Somalia, hasa katika maeneo ya Kismayo, Marka na Jowhar yaliyokuwa yameathiriwa kwa muda mrefu na ukame na mvua zisizotabirika. Feissal Kirwa anaangazia zaidi.
    12 min
  • JIFUNZE KISWAHILI - NENO: NYAPANYAPA
    Sasa umewadia wasaa wa kujifunza Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana ya neno "NYAPANYAPA" katika muktadha wa uwindaji.Bwana Sigalla anasema "nyapanyapa ni tabia ya mwindaji ambayo anatembea kwa kunyata sana, pole pole ili asisikike wakati anawinda.Anakuwa ananyemelea. Lengo ni kuhakikisha anamsogelea mnyama ama kumshika au kuweza kuwinda mnyama vizuri."
    0 min
  • 26 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunamulika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC), hali Mashariki ya Kati, Amerika ya Kati, kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi huko Pemba, Zanzibar nchini Tanzania na katika kujifunza lugha ya Kiswahili ni uchambuzi wa neno, 'Nyapanyapa.'MUHTASARIMabaraza ya Umoja wa Mataifa lile la Usalama na lile la Haki za Binadamu kwa nyakati tofauti yajadili hali ya usalama na haki za binadamu huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Huko Mashariki ya Kati hali  ya usalama na kibinadamu yazidi kuwa tete Lebanon na Ukanda wa Gaza kutokana na mashambulizi yanayoendelea kila uchao.Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO azungumzia hali tete ya afya nchini Cuba kutokana na kutokuwepo kwa huduma ya uhakika ya umeme.MADA KWA KINA: Jinsimafunzo ya kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi yalivyoanza kuonesha matokeo chanya huko Pemba, Zanzibar nchini Tanzania. Mradi ni wa FAO kwa kushirikiana na SMZ.JIFUNZE KISWAHILI- Mchambuzi wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA Tanzania anafafanua maana ya neno 'Nyapanyapa.'Karibu na mwenyeji wako ni Assumpta Massoi.
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners