Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Tanzania: FAO na wadau 'wawanoa' maafisa misitu ili kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu
    Nchini Tanzania kunafanyika mafunzo kwa maafisa wa misitu yenye lengo la kulinda misitu, mafunzo yanayotekelezwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) na serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa CookFund.Tweet URLMratibu wa Mradi kutoka FAO Diomedes Kalisa akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Msaidizi wa FAO Tanzania, Charles Tulahi, amesema “mafunzo haya yanakuja wakati muafaka kwani maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Misitu yalibeba kaulimbiu, “Misitu na Uchumi.”Amesisitiza kuwa Tanzania ina zaidi ya hekta milioni 48 za misitu ambayo inachangia zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji ya nishati ya kaya kupitia nishati ya biomasi. Uvunaji haramu wa misitu ni kikwazo“Changamoto za uvunaji haramu, uzalishaji usio endelevu na udhaifu wa utekelezaji wa sheria zinalengwa kupitia mafunzo hayo yatakayojikita katika maeneo matano ya kipaumbele.” Amesema.Ametaja maeneo hayo kuwa ni usimamizi wa watoa taarifa, mbinu za ufuatiliaji, matumizi ya teknolojia, tafsiri ya sheria za misitu na marekebisho yake ya 2025, pamoja na ujuzi wa uchunguzi na utekelezaji wa sheria. Lengo namba 15 la SDG linavyomulika misituLengo la 15 la Maendeleo Endelevu (SDG15) kuhusu “Uhai juu ya ardhi,” linazingatia kulinda, kurejesha, na kuendeleza usimamizi endelevu wa misitu, kusitisha ukataji miti hovyo, na kurejesha uharibifu wa ardhi ifikapo mwaka 2030. Lengo hili linaelekeza moja kwa moja kusitisha upotevu wa bayonuai na kuimarisha mchango wa misitu katika kunasa hewa ya ukaa, hivyo kusaidia juhudi za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.Manufaa ya mafunzoMkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Misitu katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Seleboni Mushi, amesema mafunzo hayo yanayosimamiwa na FAO yanalenga kujenga uwezo wa wakaguzi na wapelelezi wa TFS kutoka maeneo mbalimbali ya nchi katika kudhibiti changamoto zinazoikabili misitu ikiwemo ukataji miti haramu, uvamizi wa misitu, kilimo haramu na uchomaji moto kwenye maeneo ya misitu. “Misitu ni urithi wa taifa na ni muhimu kuilinda kwa ajili ya vizazi vijavyo,” amesema Afisa huyo na hivyo “mafunzo haya yatawapa washiriki maarifa mapya katika maeneo muhimu kama vile usimamizi wa watoa taarifa, mbinu za ufuatiliaji, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ulinzi wa misitu, tafsiri ya sheria na kanuni za misitu, pamoja na ujuzi wa uchunguzi na utekelezaji wa sheria.” Amesisitiza kuwa mafunzo haya ni fursa kwa washiriki kujenga mitandao imara ya kitaalamu itakayosaidia ushirikiano na ubadilishanaji wa taarifa katika kuhakikisha misitu ya Tanzania inaendelea kutoa manufaa kwa wote,” amesema Bwana Mushi. 
    3 min
  • Meli zilizokuwa zikipita Hormuz zilikuwa 129 kwa siku, sasa ni 2 hadi 7 kwa siku: UNCTAD
    Tangu kuanza kwa vita huko Mashariki ya Kati baada ya Israel na Marekani kuishambulia Iran mnamo tarehe 28 Februari na kisha Iran kujibu mashambulizi, wasiwasi umekuwa ukiongezeka kuhusu kupanda kwa bei za mafuta na bidhaa nyingine. Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD linafuatilia kwa karibu hali inayoendelea na kutoa takwimu na uchambuzi ili kuzisaidia serikali na wadau wengine waweze kujipanga na kuratibu vyema mambo yao hususan yanayohusiana na usafiri wa baharini.Katikati ya vita hii inayoendelea Mashariki ya Kati kuna suala la mlango bahari wa Hormuz, hili ni eneo muhimu sana lililopo Iran ambako takriban robo ya mafuta yote duniani, meli zake hupita hapo. Bidhaa nyingine muhimu zinazopita hapo ni gesi asilia na mbolea. Ingawa mlango bahari wa Hormuz haujafungwa rasmi, lakini umewekewa vikwazo vikali, huku kukiwa na mashambulizi mengi ya Iran dhidi ya meli tangu vita vilipozuka siku 26 zilizopita. Akizungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa, Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo na Biashara UNCTAD Frida Youssef anaanza kwa kutueleza hali ilivyokuwa kabla ya vita.“Kabla tu ya mzozo, tunapoangalia wastani wa idadi ya meli kwa siku zilizokuwa zikipitia Hormuz, ilikuwa karibu meli 129, 130 na katika wiki mbili zilizopita, ilikuwa karibu meli mbili hadi saba kwa siku.”Kwa lugha nyingine upungufu ni takriban asilimia 95. Je ni maeneo gani yameathirika zaidi? “Usafirishaji wa mbolea unaathirika pamoja na bei ya uzalishaji, kwa mfano, mbolea za nitrojeni ambazo hutegemea sana gesi. Kwa hivyo, hii inabadilisha tena kuwa ni athari kwenye kilimo ambayo baadaye itaonekana kwenye kupanda kwa bei ya chakula.” UN News/Daniel DickinsonKufungwa kwa mlangobahari wa Hormuz kunaathiri biashara kwa kiwango cha kimataifa.Akiendea na tathmini yake Mkuu huyo wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi wa UNCTAD anasema hivi sasa bei za mafuta zimepanda.“Tumeona bei ya mafuta yanayotumika katika vyombo vya usafiri baharini ikiongezeka maradufu. Hii pia inaathiri gharama ya usafiri, si tu kwasababu bei ya mafuta imepanda bali pia bei, kwa mfano, ya bima. Malipo ya bima ya vita yameongezeka, katika baadhi ya maeneo imeongezeka mara nne.”UNCTAD inaendelea kufuatilia na kutoa taarifa kwa serikali na wadau kwani vita hii inayoendelea inaathari kwa kila mtu lakini nchi zenye uchumi mdogo ndio zitakazo athirika zaidi kwani zinauwezo mdogo zaidi wa kuvumilia mshtuko huu wa kiuchumi na ndio zitakazohisi athari zake kwa nguvu zaidi. “Inaathiri usafiri, inaathiri nishati, inaathiri chakula na pia inaongeza gharama na upatikanaji ni mgumu. Kwa hivyo, haya yote kwa pamoja yanakuwa na athari kwenye uchumi wa umma katika nchi, pamoja na gharama za maisha kwa kaya.” 
    4 min
  • Azimio lapitishwa kutambua biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki ni uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu
    Umoja wa Mataifa leo umekuwa na tukio la kumbukizi ya siku ya kimataifa ya kukumbuka waathiriwa wa biashara ya  utumwa kupitia bahari ya Atlanitiki ambapo nchi 123 wanachama wa Umoja huo wamepitisha azimio lililoandaliwa na mataifa 58 kutambua usafirishaji wa watu wa kiafrika na utumwa kwa misingi ya rangi ya waafrika kuwa uhalifu mkubwa dhidi ya binadamu. Nchi hizo 123 ni pamoja na zile wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, ilhali nchi 3 zilizopinga azimio ni Marekani, Israeli na Argentina. Nchi 52 hazikuonesha msimamo wowote. Mwakilishi wa Marekani akizungumza baada ya kupiga kura ya kupinga azimio hilo amesema, "tunalaani makosa yoyote yaliyofanyika kuhusiana na utumwa kuvuka bahari ya Atlantiki, jangwa la Sahara na kwingineko, lakini tumepinga azimio kwa sababu hatuoni msingi wa kulipatia kiwango cha juu hivyo cha hadhi tukio hilo. Na zaidi ya yote kama ni fidia, fidia hiyo atalipwa nani,?" amehoji.Rais wa Ghana aliwasilisha rasimu ya azimio mbele ya Baraza KuuUN/Manuel EliasRais John Mahama wa Ghana akihutubia Baraza Kuu wakati wa siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Rasimu ya azimio hilo iliwasilishwa na Rais wa Ghana John Mahama ambaye ni Balozi wa Muungano wa Afrika wa Kuendeleza Hali ya Haki na Fidia. Azimio hilo namba A/80/L.48 limepatiwa jina kutambua usafirishaji wa watu waliokuwa watumwa kutoka Afrika na utumwa kwa msingi wa rangi ya watu wa kiafrika kama mojawapo ya uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya binadamu.  Azimio hilo lililoandaliwa na mataifa 58 yakiwemo mataifa ya Afrika Mashariki, lina vipengele 16 vya utekelezaji ikiwemo kutambua usafirishaji huo wa watumwa kutoka Afrika kuwa uhalifu mkubwa zaidi dhidi ya binadamu, kurejeshwa kwa mali za kitamaduni kutoka Afrika na zaidi ya yote kulipwa fidia.Kauli ya Rais wa Baraza KuuTukio la kumbukizi lilianza kwa Annalena Baerbock Rais wa Baraza Kuu kuitisha kikao na kisha kuelekea kwenye mimbari kutoa hotuba yake akirejelea simulizi ya mtumwa Oladuk Ekwano kutoka Nigeria ya sasa akielezea machungu ya safari ndani ya meli iliyowabeba.UN/Manuel EliasRais wa Baraza Kuu la UN Annalena Baerbock akitoa hotuba katika tukio la siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Anasema Makumi ya mamilioni ya wengine kama Egvano walinyang’anywa kutoka kwa familia zao, nchi zao na tamaduni zao, wakafanywa watumwa na kupelekwa kufanya kazi katika nchi za kigeni—kwenye mashamba ya pamba hapa Marekani, na kwenye mashamba ya miwa na kahawa katika makoloni yaliyodhibitiwa na Ulaya. Katika maeneo ambayo leo yanajulikana kama Brazili, Barbados, Jamaica, na maeneo mengine mengi. Wote wakiwa mbali na nyumbani, mbali na familia, mbali na maisha yao.Tunatambua nchi zinazoomba radhi lakini hatua zaidi zahitajikaKwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amerejelea mateso waliyopata mamilioni ya waafrika waliotekwa nyara na kusafirishwa katika hali dhalili na kugeuzwa watumwa barani Amerika. Amesema kumbukumbu pekee haitoshi.Amebainisha kuwa mfumo huo haukuwa tu ukatili wa zamani bali pia ulikuwa msingi wa miundo ya uchumi wa dunia ambayo madhara yake yanaendelea hadi leo katika mfumo wa ubaguzi wa rangi wa kimfumo na ukosefu wa usawa.UN/Manuel EliasKatibu Mkuu António Guterres akitoa hotuba katika tukio la siku ya Kimataifa ya Kumbukizi ya Waathirika wa Utumwa na Biashara ya Watumwa kupitia bahari ya Atlantiki.Hotuba hiyo imesisitiza kuwa kumbukumbu pekee haitoshi. Badala yake, nchi lazima zikabiliane na dhuluma za muda mrefu zinazoendelea kuwaathiri watu wenye asili ya Kiafrika. “Kiini cha juhudi hizo, alisema, ni kutafuta ukweli, haki, na marekebisho, ikiwa ni pamoja na mijadala yenye maana na hatua kuhusu fidia,” amesema Katibu Mkuu. Guterres anasema, “Ndiyo maana Muongo wa Pili wa Kimataifa kwa Watu wenye Asili ya Kiafrika na Muongo wa Fidia wa Muungano wa…
    4 min
  • 25 MACHI 2025
    Yaliyomo katika Jarida hili la habari za UNKauli za fidia na haki zatawala tukio la kumbukizi ya biashara ya utumwa kupitia bahari ya Atlantiki.UNCTAD: Meli zilizokuwa zikipita Hormuz zilikuwa 129 kwa siku, sasa ni 2 hadi 7 kwa siku.FAO Tanzania na wadau wawanoa maafisa misitu kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu
    12 min
  • JIFUNZE KISWAHILI: METHALI
    Hii leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu  Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya,  kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Ateteaye mtuku ni tanguko la bure."Dkt. Gitonga anasema, "Mtuku ni mtu asiyefaa au asiyeweza kutegemeeka. Methali hii ina maana kwamba mtu asiyetegemeeka kamwe katika jamii na ambaye hana utu, kumtetea ni kujidhalilisha wewe mwenyewe. Ni kazi bure isiyo na faida. Ukimtetea apate labda cheo au kazi fulani utajilaumu mwenyewe kwani hatawajibika hata kamwe. Inatuelimisha kwamba iwapo utakuwa radhi kumtetea mtuku basi kuwa tayari kuhusishwa naye. Tetea walio wema si waovu."
    2 min
  • 24 MACHI 2026
    Hii leo jaridani ni:Muhtasari;Mada kwa Kina na Jifunze lugha ya Kiswahili. Jarida leo linawasilishwa na Rashid Maleka kutoka Mwanza nchini Tanzania.Muhtasari wa Jarida:dadi ya vifo kutokana na shambulio dhidi ya hospitali moja huko Darfur, Sudan, Ijumaa iliyopita imeongezeka zaidi,Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi,UNHCR limetoa wito wa msaada wa haraka wa kimataifa ili kuhakikisha urejeaji wa wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo, DRC wanaorejea kutoka Burundi unafanyika katika mazingira ya usalama na utu.Leo katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kifua Kikuu (TB) inayoadhimishwa tarehe 24 mwezi Machi kila mwaka, WHO inazihimiza nchi kuharakisha hatua za kumaliza TB na kupanua upatikanaji wa huduma za kuokoa maisha kwa kutumia ubunifu mpya ikiwemo vipimo vinavyotumia mate.Mada kwa kina: Leah Mushi amezungumza na Naibu Mrajisi wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Tanzania Chausiku Kafuti Kuya kando ya CSW70 iliyokunja jamvi wiki iliyopita hapa New York, Marekani. Jifunze lugha ya Kiswahili: Methali - “ATETEAYE MTUKU NI TANGUKO LA BURE”Karibu!
    11 min
  • Furaha ni pale ninapoweza kuhudumia familia yangu
    Katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Furaha ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 20 Machi, wakazi wa kata ya Luchelele, jijini Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania, wameeleza maana ya furaha katika maisha yao ya kila siku, ambapo kwa wengi, furaha haitokani na anasa, bali inajengwa na afya njema, upendo wa familia, na uwezo wa kuitunza familia hiyo kwa mahitaji ya msingi. Wakizungumza na Rashid Malekela wa Idhaa hii, wanawake wa eneo hilo wameeleza kuwa furaha kwao ni chanzo kikuu cha amani ya moyo. Rehema James amesema kuwa furaha yake kubwa ni kuamka salama, wakati Regina Emmanuel amegusia uhusiano wa mzazi na mtoto kama nguzo ya furaha yake, "Furaha yangu kuu inatokana na mama yangu kuwa hai na mwenye afya."Faida Anthony, mmoja wa wakazi wa eneo hilo, amefafanua kuwa kwake furaha ni matokeo ya jitihada za kutafuta riziki akisema,"Furaha ni kutafuta fedha, mboga, na kuijali familia yangu."Mitandao ya kijamii na changamoto za furahaLicha ya umuhimu wa afya na familia, matumizi ya teknolojia yameanza kuathiri jinsi watu wanavyopata au kupoteza furaha katika ulimwengu wa sasa. Duch Sababu, ambaye ni Afisa Usafirishaji maarufu ‘bodaboda’, amebainisha kuwa mitandao ya kijamii ina sura mbili; inaweza kuleta kicheko kupitia maudhui ya ucheshi au kuleta huzuni kulingana na kile mtu anachokiona, huku akitoa angalizo kwa watumiaji wa mitandao,"Furaha ni afya njema, lakini pia mitandao inaweza kuleta furaha kupitia vichekesho au huzuni kulingana na kile unachokiona."Wito wa Umoja wa MataifaMwaka huu, Umoja wa Mataifa unasisitiza kuwa furaha ya kweli kwa binadamu wote itafikiwa endapo kutakuwa na usawa, haki, na ulinzi wa mazingira kulingana na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs). Ili kufikia malengo hayo duniani, kuna uhitaji wa kuendelea kuimarisha huduma za kijamii zinazogusa maisha ya watu wa hali ya chini moja kwa moja.Kwa vijana, wameshauriwa kutumia muda wao kwenye mitandao ya kijamii kutafuta mambo yatakayowajenga kifikra na kuwapa furaha badala ya mambo yanayoweza kuwaharibia amani yao ya moyo.
    3 min
  • Fahamu jinsi serikali ya Kenya inasambaza visima vya maji kwa wananchi
    Katika mazungumzo yafuatayo kati ya Anold Kayanda wa Idhaa hii na Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Kenya, Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inajivunia kupiga hatua katika kuitatua changamoto hiyo.  Waziri Hanna Wendot Cheptumo anaeleza kwamba Kenya kupitiua mfuko ilioupa jina NGAAF yaani National Government Affirmative Action Fund, mfuko wa fecha mahususi kusaidia makundi maalumu katika jamii hususani wanawake kupitia wawakilishi wa wanawake. Pesa hizo wanazopewa wanawake si mkopo hivyo hawarudishi lakini wanatakiwa kuzitumia kijiendeleza “na hizo nidizo wanatumia kununua matanki ya maji” anasema Bi. Cheptumo. Visima vya jumuiya Pia kupitia miradi ambayo iko vijijini, Serikali ya Kenya inachimba visima vya maji vya jumuiya na wanaweka sola au mashine za kuvuta maji kwa njia ya nishati ya jua kwa hiyo hakuna mzigo au gharama ya umeme kwa wanawake hao. Waziri Hanna Wendot Cheptumo anakumbuka akisema, “hata mimi nikiwa mdogo nilikuwa ninaenda kilomita saba kwenda kutafuta maji lakini saa hizo ukienda kijijini unapata maji yako hapo na haulipishwi. Unaenda unachota maji yako na unaenda.” Mabwawa Aidha, kwa mujibu wa Bi. Cheptumo, Serikali ya Kenya imechimba mabwawa ya kusambaza maji katika vijiji na ni kazi ambayo inaendelea, “tunataka kusema hata kama maji hayajafikia kila mahali, lakini serikali iko na mikakati ambayo imewekwa ya kuhakikisha kila mtu anapata maji.Hupiti hata kilomita moja. Lakini sanasana weni sasa wana maji nyumbani.” Anahitimisha. 
    3 min
  • Madhara ya vita vya Israeli/Marekani dhidi ya Iran yazidi kudhihirika
    Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiingia wiki ya nne tangu uanze tarehe 28 mwezi uliopita wa Februari, Umoja wa Mataifa leo umeonya kuwa athari mbaya za kibinadamu na uchumi wa kimataifa zinaongezeka wakati mzozo huo ukivuruga kabisa njia muhimu za usambazaji wa bidhaa ndani ya Mashariki ya Kati na kwingineko duniani. Flora Nducha na taarifa zaidi.Asante Assumpta. Kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, mzozo unaoendelea Mashariki ya Kati sasa umevuka mipaka ya eneo hilo, ukiathiri pia Asia na Afrika, hasa katika biashara na usafirishaji.Taarifa ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Miradi na Huduma, UNOPS inaonya kuwa mamilioni ya watu wako hatarini kutokana na athari za kibinadamu na kiuchumi. Mkuu wa shirika hilo, Jorge Moreira da Silva, amesema kuvurugika kwa usafirishaji kupitia Mlango Bahari wa Hormuz kumesababisha mshtuko mkubwa wa kiuchumi duniani.Amesema “Nchi zinazoendelea barani Asia na Afrika zina uwezekano mkubwa wa kubeba gharama kubwa zaidi hali inayotishia usalama wa chakula,” na kuongeza kuwa njaa duniani inaweza kuongezeka kwa makumi ya mamilioni ya watu.Pia amesema mgogoro huu unazidisha hali mbaya iliyopo katika nchi kama Sudan, Sudan Kusini, Afghanistan, Yemen, na Somalia, ambapo mifumo ya chakula tayari ni dhaifuAmeonya pia kuwa mashambulizi dhidi ya meli na kuvunjika kwa minyororo ya usambazaji kunazuia upatikanaji wa dawa na misaada, hasa Gaza, huku vita vikienea vinaweza pia kuhatarisha fedha zinazotumwa nyumbani kwa familia, hasa Asia Kusini.Nchini Lebanon, kwa mujibu wa Sirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF, zaidi ya watu 1,000 wameuawa na wengine zaidi ya 2,500 kujeruhiwa tangu mapema Machi, wakiwemo wahudumu wa afya, wanahabari na wafanyakazi wa misaada.Watoto wanaendelea kubeba mzigo mkubwa. Naibu Mkurugenzi wa UNICEF, Ted Chaiban, anasema “Watoto wanaouawa au kujeruhiwa ni sawa na darasa moja kila siku.”UNICEF inaonya pia juu ya athari kubwa za kisaikolojia kwa watoto na wahudumu wa misaada.Katika Ukanda wa Gaza, hali inazidi kuwa mbaya. Shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestna UNRWA,  limesema  mamia ya watu wamepata ulemavu wa kudumu huku huduma za afya na misaada zikizidi kuwa finyu.Wakati huo huo, hofu ya usalama wa nyuklia inaongezeka kufuatia mashambulizi karibu kweny vituo nyeti nchini Iran na Israel. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomic IAEA,  Rafael Grossi, ameonya kuwa: “Hakuna hatua ya kijeshi inayopaswa kuhatarisha usalama wa vituo vya nyuklia.”Ingawa hakuna ongezeko la mionzi lililoripotiwa, Shirika la Umoja wa Mataifa a Afya Duniani WHO,  tayari linaanza maandalizi ya dharura.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa bila hatua za haraka za kupunguza mzozo, dunia inaweza kukabiliwa na mgogoro mkubwa zaidi wa kibinadamu na kiuchumi.
    4 min
  • 23 MACHI 2026
    Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Assumpta Massoi anakuletea-Mzozo wa Mashariki ya Kati waingia wiki ya nne, vifo vyaongezeka, uchumi wa dunia waathirika, hofu ya nyuklia linaendelea huku Un ikionya kuhusu athari za kouchumi-Kenya yajivunia hatua nzuri katika kuwaondolea wanawake changamoto ya maji, utamsiki Waziri wa Masuala ya wanawake wa Kenya akifafanua hilo-Tarehe 20 Machi iliadhimisjwa Siku ya Furaha Duniani utawasiki baadhi ya wakaazi wa Mwanza Kaskazini-Magharibi mwa Tanzania wakielezea nafasi ya mitandao ya kijamii katika kujenga au kubomoa furaha ya binadamu.
    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners