Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 19 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina leo baada ya takribani wiki mbili mkutano wa 70 wa CSW70 unakunja jamvi.  Maudhui yalikuwa kuendeleza Haki, Sheria na Kuchagiza Hatua kwa ajili ya wanawake na wasichana, na sasa washiriki wanaeleza Idhaa hii wanachoondoka nacho.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo akizungumza na waandishi wa habari Mjini Brussels Ubelgiji kuhusu kinachoendelea Mashariki ya Kati akiwa a na Rais wa Baraza la Muungano wa Ulaya António Costa, ametoa ujumbe mahsusi kwa wahusika wakuu wa mzozo huo. Amesema “Kwanza kwa Marekani na Israel, ni wakati muafaka kumaliza vita hivi ambavyo viko hatarini kutodhibitiwa kabisa, vikisababisha mateso makubwa kwa raia, na athari zake zinaenea katika uchumi wa dunia kwa kiwango cha kutisha, zikiwa na uwezekano wa kusababisha madhara makubwa zaidi hasa kwa nchi zenye maendeleo duni”Kisha ujumbe wake wa pili ni “Kwa Iran, acheni kushambulia majirani zenu. Hawakuwa sehemu ya mgogoro huu. Baraza la Usalama limelaani mashambulizi haya na kuamuru yasitishwe, pamoja na kuagiza kufunguliwa kwa Mlango Bahari wa Hormuz.”Na kuelekea Siku ya Kimataifa ya Furaha hapo Kesho Machi 20 raia Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, eneo lililoghubikwa na mizozo ya silaha wanaeleza furaha kwao inamaanisha nini.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    11 min
  • 18 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko na uhakika wa chakula katika mshariki ya kati, na kazi ya walinda amani wa Umoja wa mataifa nchini Sudan Kusini.Mgogoro unaoiendelea Mashariki ya Kati unaendelea kuzorotesha hali ya kibinadamu katika ukanda huo huku watu wakikimbia makazi yao, wasiwasi wa usalama wa nyuklia ukiongezeka, na vitisho vikiongezeka dhidi ya usafiri wa baharini..Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) linaonya kuwa kuongezeka kwa mgogoro katika Ghuba ya Uajemi au Mashariki ya Kati kunahatarisha mifumo ya chakula duniani, likitaja kupanda kwa gharama za nishati, mbolea na uzalishaji wa chakula kama athari kuu.Mji wa Bentiu ulioko Kaskazini mwa Sudan Kusini ni eneo linalokumbwa na mafuriko yanayoharibu makazi na migogoro inayowafanya maelfu ya watu kuishi kwenye kambi za wakimbizi. Katika mazingira haya magumu, Afisa wa Polisi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS, Wafaa Assri Sameeh Al-Goussous kutoka nchini Jordan, anafanya kazi ya kujenga uaminifu na uhusiano madhubuti kati ya jamii na vyombo vya dola kupitia doria na mafunzo. Rashid Malekela anatupeleka huko kufahamu maisha ya kila siku ya Afisa Wafaa yakoje.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min
  • 17 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kutoka hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha CSW70. Leo Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka DRC.Nelly ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaeleza kuwa idadi ya wakimbizi wa ndani inazidi kuongezeka, mathalan huko Lebanon watu 816,000 sawa na asilimia 14 ya watu wote wamekimbia makazi yao. Na huko Iran watu milioni 3.2 wanakadiriwa kukimbilia maeneo ya Kaskazini mwa taifa hilo na vijijini wakikimbia machafuko. Namba ya dharura ya msaada ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi UHCHR inapokea zaidi ya simu 1,000 kwa siku za watu wakiomba msaada.Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limeonya kuwa njaa duniani inaweza kufikia viwango vya juu mwaka huu iwapo mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea na bei ya mafuta itabaki kuwa juu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Carl Skau amesema “Ongezeko la gharama za chakula na mafuta duniani zinaweza kuacha mamilioni ya familia zikiwa nje ya uwezo wa kununua vyakula, hasa katika nchi zinazotegemea uagizaji bidhaa kama vile Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia. Kwa hakika, uchambuzi wetu unakadiria kwamba, kama mzozo wa Mashariki ya Kati utaendelea hadi mwezi Juni, watu zaidi ya milioni 45 wanaweza kuingizwa kwenye njaa kali kutokana na bei kuwa juu na hii itaweka rekodi ya juu ya njaa duniani kote. Na haya ni matarajio mabaya.".Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa hii leo moja ya matukio ya kando ya Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 ni Kushughulikia vikwazo vya haki ya kijinsia kupitia mfumo wa Mahakama ya Mtandao nchini Tanzania kwa lengo la kufanikisha haki kwa wanawake na wasichana. Barke Sehel ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani nchini Tanzania anasema mashinani mfumo unatumia simu zisizo janja na akisema mobile app ni apu ya kwenye simu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • “Sauti ya Mama Mukongomani” inamuwezesha na kumlinda mwanamke wa DR Congo: Nelly Mbangu
    Hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye Kikao cha Kamisheni ya Hali ya wanawake duniani CSW70, Flora Nducha wa Idhaa hii anazungumza na mshiriki Nelly Mbangu Lumbulumbu, mwanasheria na mwanaharakati wa Haki za binadamu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasa ya Congo DRC, ambaye ni mwanzilishi na mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la “Sauti ya Mama Mukongomani” lililoanzishwa mwaka 2008, anaanza kwa kumueleza kwa nini alinzisha shirika hilo.
    6 min
  • Raia nchini Iran wanabeba gharama ya vita inayoendelea - Mtaalamu
    Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa ifuatayo.
    3 min
  • WFP na wadau wake waboresha maisha ya kijana mkulima nchini Uganda
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake chini ya mpango Kilimo na Msaada wa Masoko (AMS), vijana nchini Uganda wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki. Mafunzo hayo yamewasaidia kukimu mahitaji yao kupitia uzalishaji wa asali. Feissal Kirwa anaangazia simulizi ya kijana mmoja mnufaika wa mradi huo.
    3 min
  • 16 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia vita nchini Iran, sauti za vijana katika wiki ya pili ya mkutano wa CSW70, na mafunzo ya vitendo kwa vijana nchini Uganda kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki.Katika siku ya 16 ya vita nchini Iran iliyoanza baada ya Marekani na Israeli kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati na kisha lenyewe kujibu mashambulizi yanayosambaa hadi ukanda mzima wa eneo hilo, hii leo suala hilo limepatiwa kipaumbele kwenye Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu huko Geneva, Uswisi ambapo mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi na Mwakilishi wa Iran wametoa maoni yao kuhusu kinachoendelea na nini kifanyike.Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na wadau wake chini ya mpango Kilimo na Msaada wa Masoko (AMS), vijana nchini Uganda wamepata mafunzo ya vitendo kuhusu mbinu za kisasa za ufugaji nyuki. Mafunzo hayo yamewasaidia kukimu mahitaji yao kupitia uzalishaji wa asali.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners