Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Mpango wa MEMKWA Tanzania wampa fursa ya elimu mtoto Sanita
    UNICEF: Mradi wa Elimu Kwa Waliokosa warejesha matumaini kwa mtoto wa kikeNchini Tanzania Mpango wa Elimu Kwa Waliokosa au MEMKWA umemwezesha msichana mmoja kuweza kupata haki yake ya msingi ya elimu na kisha kuwa na matumiani ya kutimiza ndoto yake ya kuwa nesi au muuguzi. Simulizi ya Assumpta Massoi inafafanua kisa hicho kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo.(Taarifa ya Assumpta Massoi)Nats.. 00’00 – 00’14” (Kwa majina naitwa…. Wanaenda shule)Tupo wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma, kaskazini-magharibi mwa Tanzania Sanita huyo alishindwa kuendelea na masomo kwa kukosa vifaa vya shule.(Sauti ya Sanita)Amerejea shuleni kupitia mradi wa MEMKWA uliotambua kuwa zaidi ya watoto milioni 2 wenye umri wa kuwa shule ya msingi nchini Tanzania hawako shuleni hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau UNICEF na serikali ya Qatar wakafanikisha MEMKWA.Tangu mwaka 2022 zaidi ya watoto elfu 98 katika mikoa 3 ya Tanzania ikiwemo Kigoma, wamenufaika na MEMKWA.Nats…(Darasani) 0’30-0’36” (Shikamoo mwalimu…….la mstatili)Sasa tumo darasani na Sanita ni miongoni mwa wanafunzi. Rashid, mwalimu wa Sanita anaelezea.(Sauti ya Rashid- Mwalimu wa Sanita)Sanita anakwenda ubaoni kujibu swali. Mwalimu anauliza..Nats.. 1’00” – 1’03” (Ameweza, haya tumpigie makofi….fx makofi)Sanita anafunguka..(Sauti ya Sanita)Kitendo cha Sanita kupata haki ya elimu kinamwezesha hata Rhoedesia ambaye ni mama mzazi wa Sanita kuwaza mustakabali wa binti yake.(Sauti ya Rhoedesia) 1’11” -1’20” (NInavyomuona mwanangu anaenda…. ili apate kazi)Mwalimu Rashid anatamatisha na tathmini ya mradi wa MEMKWA na ombi mahsusi.(Sauti ya Mwalimu Rashid)
    3 min
  • Kunusuru wanawake wenzangu na jamii Gaza inanipa faraja: Alya Abu Shawish
    Alya Abu Shawish, mwanamke aliyeko mstari wa mbele kuondoa hatari ya mabomu Gaza  (OVERNIGHT)Hii leo pia hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani, imefanyika hafla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake ambayo duniani kote iliadhimishwa jana Jumapili. Katika muktadha huo huo ninamualika Anold Kayanda atupeleke Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kumwangazia Alya Abu Shawish, Mwanamke anayefanya kazi katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutoa huduma ya kutegua mabomu, UNMASakisaidia kuwaweka salama wenzake katika mojawapo ya mazingira hatari zaidi duniani. Karibu Anold.(Taarifa ya Anold)Asante Flora,Hakika Gaza ni moja ya mazingira hatari duniani kwa sasa. Alya Abu Shawish anaposhuka kwenye gari kabla ya kuingia ofis iza UNMAS zilizoko Deir al-Balah katikatimwa Gaza, anavaa jaketi la kujikinga na risasi.Ndani ya ofisi amesimama mbele ya ramani ya kidijitali, akifuatilia mienendo ya timu za wafanyakazi walioko mitaani zilizosambazwa kote katika ukanda huo wa Gaza ili kufanya kazi za kuondoa mabaki ya vilipuzi vya vita katika eneo hilo.Baada ya mipango yote kukamilika ofisini, sasa Alya Abu anaendesha gari akiwa na wenzake kuelekea kazini nje ya ofisi. Anaeleza akisema,(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Kazi yangu kama mwanamke katika eneo hili inaonyesha kwamba wanawake wanaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuhakikisha usalama na kuleta mabadiliko yanayoonekana, hata katika mazingira hatari na yenye changamoto kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza.”Alya Abu Shawish anaonekana na wenzake mitaani wakifanya kazi. Watoto wanafuata, kwa vyovyote wakitambua kazi muhimu inayofanywa na UNMAS kufanya mazingira yawe salama dhidi ya vilipuzi.Hata hivyo, nyuma ya dhamira hii ya kitaaluma kuna hadithi binafsi inaloakisi hali halisi ya maelfu ya wanawake huko Gaza.(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Kama mwanamke na mama, nimepitia changamoto nyingi ambazo wanawake wa Kipalestina huko Gaza hukabiliana nazo wakati wa vita hofu, kuhama makazi, uhaba wa mahitaji muhimu, na hali ya kutokuwa na uhakika kila wakati. Kama wanawake wengi hapa, nimelazimika kuilinda familia yangu huku nikikabiliana na hali hizi ngumu.”Licha ya changamoto hizi, Alya Abu Shawish anasema uzoefu wake umeimarisha azma yake ya kuwasaidia wengine na kumhamasisha kufanya kazi katika uwanja ambao mara nyingi huonekana kutawaliwa na wanaume.(Sauti ya Alya Abu Shawish) – Sharon“Uzoefu huu haukunidhoofisha; uliimarisha azma yangu ya kuwasaidia wengine. Ulinitia moyo kufanya kazi katika masuala ya kuondoa mabomu na usalama na UNMAS uwanja ambao mara nyingi huonekana kuwa wa wanaume. Katika jukumu hili, ninachangia kupunguza hatari zinazosababishwa na mabaki ya vilipuzi vya vita na kusaidia jamii kuishi kwa usalama zaidi.”Wanawake wengine katika timu za UNMAS pia hushiriki katika shughuli za kuhamasisha jamii kuhusu hatari za mabaki ya vilipuzi, ambayo sasa yamekuwa moja ya changamoto kubwa zaidi za kibinadamu huko Gaza kadri uharibifu unavyoendelea kuenea. Kwa Abu Shawish, juhudi hizi hubeba ujumbe unaokwenda mbali zaidi ya kazi kwani inaonesha uimara na mnepo.
    3 min
  • Mkutano wa 70 wa kamisheni ya hali ya wanawake CSW70 waanza
    CSW70 yang’oa nanga ikisistiza haki, haki ya kisheria na hatua kwa wanawake na wasichanaKikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 kimefungu pazia hii leo jijini New York Marekani, mwaka huu kikibeba maudhui “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote”.  Zaidi ya washiriki 9000 wakiwemo wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia, Umoja wa Mataifa na mashirika yake na wadau wengine wanatarajiwa kushiriki jukwaa hili litakalokunja jamvi 19 Machi likijumuisha mikutano ya kando 750. Leah Mushi amefuatilia ufunguzi huo na hii hapa taarifa yake.(TAARIFA YA LEAH MUSHI)Natts……Katika ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani …. huu ni ufunguzi wa Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 Mgeni rasmi ni Katibu Mkuu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye ameeleza…. Nats.. (SG cut 1 play under 00:06 I am so pleased to be in a…. )furaha yake kuwa katika ukumbi uliojaa viongozi waliokataa kukubali ukosefu wa usawa kama jambo lisiloepukikaKatika hotuba yake Guterres amesema dunia bado inaongozwa zaidi na mfumo dume unaowapa wanaume nafasi kubwa ya mamlaka. (SG Cut 1 – Fiesal )“Tunaishi katika ulimwengu unaotawaliwa na wanaume, na utamaduni unaotawaliwa na wanaume. Usawa wa kijinsia ni suala la mamlaka. Hakuna hatua hata moja mbele kwa haki za wanawake ambayo imewahi kutolewa. Bali imeshinda. Wameshinda vizazi vya wanawake na wasichana, watetezi na wanaharakati, viongozi wa jamii na watafuta haki. Umeshinda wewe na kabla ya kitu chochote napenda kusema Asante.”Amesema hali hiyo imekuwa changamoto kubwa katika jitihada za kufikia usawa wa kijinsia katika taasisi nyingi duniani. Hata hivyo, ndani ya UN kumekuwa na maendeleo muhimu katika kuongeza uwakilishi wa wanawake katika nafasi za juu za uongozi.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu huyo, wakati alipoanza uongozi wake, alijiwekea lengo la kuhakikisha kunakuwa na uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume katika ngazi za juu za uongozi wa Umoja wa Mataifa. Leo, amesema lengo hilo limefikiwa.(SG cut2 – Fiesal )“Kwa mara ya kwanza katika historia ya Umoja wa Mataifa, wanawake sasa wanaunda nusu kamili ya nguvu kazi ya Umoja wa Mataifa katika vitengo vya kitaaluma na vya juu zaidi. Na kwa mara ya kwanza, tulifikia usawa katika uongozi mkuu. Tumefanya hivyo ikiwa ni miaka miwili kabla ya ratiba - lakini pia natambua imekuwa ni miaka 80 imechelewa.”Katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa António Guterres amesisitiza kuwa kufikia usawa wa kijinsia si suala la haki kwa wanawake pekee, bali ni hatua muhimu kwa maendeleo ya dunia nzima. Amesema jamii ambazo wanawake wanapata haki na fursa sawa huwa na maendeleo ya haraka zaidi, uchumi imara na taasisi zenye uwajibikaji zaidi, akisisitiza kuwa kuimarisha usawa wa kijinsia ni msingi muhimu wa kufikia maendeleo endelevu duniani.Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuhakikisha wanawake wanapata haki na fursa sawa katika jamii duniani.Ametaja maeneo matano muhimu ya kuharakisha haki na usawa kwa wanawake ambayo ni kuhakikisha haki sawa za kiuchumi kwa wanawake, kuimarisha uwakilishi wao katika maamuzi ya kisiasa, kupanua upatikanaji wa elimu na fursa za kazi, kuondoa ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, pamoja na kulinda haki za wanawake katika dunia ya kidijitali.Kwa upande wake mwenyekiti wa Kikao hicho cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 Maritza Chan Valverde amezungumzia maudhui ya mwaka huu ambayo ni  “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote nakusema kila mtu anajukumu la kufanya (Maritza cut )“Ondo vikwazo na uhakikishe kwamba haki inakuwa ukweli halisi kwa…
    4 min
  • 09 MACHI 2026
    Hii leo jarida la Umoja wa Mataifa linakuletea taarifa ya ufunguzi wa Kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 jijini New York Marekani, mwaka huu kikibeba maudhui “Haki, haki ya kisheria na Hatua kwa wanawake na wasichana wote”.Zaidi ya washiriki 9000 wakiwemo wawakilishi wa serikali, asasi za kiraia, Umoja wa Mataifa na mashirika yake na wadau wengine wanatarajiwa kushiriki jukwaa hili litakalokunja jamvi 19 Machi likijumuisha mikutano ya kando 750.Pia tunakupeleka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kimabavu na Israel kumwangazia Alya Abu Shawish, Mwanamke anayefanya kazi katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kutoa huduma ya kutegua mabomu, UNMASakisaidia kuwaweka salama wenzake katika mojawapo ya mazingira hatari zaidi duniani. Jarida linaelekea pia Tanzania kupata simulizi ya mtoto aliyekuwa amekosa fursa ya kupata masomo. 
    12 min
  • 06 MACHI 2026
    Katika Jarida la Habari Hii leo Kutoka Umoja wa Mataifa Assumpta Massoi anakuletea-Mashirika ya UN yatahadharisha kuongezeka kwa vurugu Mashariki ya Kati.-Mafunzo ya haki ya kumiliki ardhi yanayotolewa na Kituo cha Msaada wa Kisehria kwa Wanawake WLAC yamebadilisha maisha ya familia ikiwemo ya Jovita Provius: WLAC-Mpango wa Jamii Rafiki kwa Mtoto wazinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF katika Kaunti ya Samburu
    12 min
  • Komesha FGM SASA: Mradi wa kupambana na ukeketaji waleta nuru nchini Kenya
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya watu na Afya ya Uzazi UNFPA nchini Kenya kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya wanatekeleza mradi wa kukomesha ukeketaji ambapo waathirika wanatumika kutoa elimu kwa mabinti na jamii ili kuondokana na mila hiyo potofu. Kaunti ya Marsabit , iliyoko Kaskazini mwa nchi ya Kenya, iko mpakani na nchi ya Ethiopia. Kaunti hii ambayo ni ya pili kwa ukubwa nchini Kenya baada ya ile ya Turkana wakazi wake wengi ni wafugaji, na mbali na changamoto za mabadiliko ya tabianchi wanawake wa hapa wamepitia masahibu ya ukeketaji au kwa lugha ya kiingerza Female genital mutilation (FGM). Audio fileShirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) chini ya Ufadhili kutoka Muungano wa Ulaya nchini Kenya wanatekeleza mradi uitwao Komesha FGM SASA Kila muathirika wa ukeketaji anayo hadithi ya kusimulia na ndio maana kwa namna ya kipekee mradi huu unawatumia waathirika hao, kuwaelimisha wanajamii wenzao ili kuondokana na tamaduni ya ukeketaji. Prisca Lekuraki ni mmoja wao. “Mimi nilipitia magumu sana, baada ya kukeketwa nilipata shida sana, ni Mungu ndio amenisaidia mpaka nimefika hapa. Nilipoenda kujifungua mtoto wangu wa kwanza nilipata shida sana, kila nikienda kuzaa nikawa napitia shida sana, sasa hivi nina watoto watatu na nikajifunga nisizae tena. Niliona vile nimeumia nikasema siwezi kukubali binti yangu naye aumie hivyo. Na hiyo ndio ilinifanya niamke niungane na wengine kuhamasisha kukataa ukeketaji.”Ameongeza kuwa katika tamaduni zao wanamila nyingi nzuri sana na wanaweza kuziendeleza na kuachana na hii mila moja ya ukeketaji kwani ni mbaya na inamadhara. Prisca amepongeza mradi wa Komesha FGM SASA wa UNFPA kwa kuwasaidia kuwafikia wale ambao awali ilikuwa ni vigumu kuzungumza nao.“Kuna mahali wametufikisha na tumeona mafanikio, hapo awali tulikuwa tunaweza kwenda kwa wamama, vijana na watoto ila wale watu ambao ilikuwa inatushinda kuwafikia ilikuwa ni wazee. Lakini hii kukutana na wazee, wamama na wanakijiji kwa ujumla imesaidia, kwasababu nilikutana na wakina mama wakaniambia ile kitu mlikuwa mnasema tumeona ni uhalisia na tumeona inaweza kufanyika.”Mwingine aliyeathirika na ukeketaji ni Nasarai Learo anasema ukeketaji umechukua nguvu zake.“Mimi sina nguvu kama yule mama ambaye hajakeketwa, nilienda kuwaambia wamama wasikekete watoto wao, lakini wakaniambia wananifahamu na nilipoolewa nilkuwa mdogo sana na wao ndio walionishika nikatetetwe nikiwa mdogo. Lakini mimi niliwaeleza mimi sikuwa najua hiki kitu ni kibaya lakini sasa hivi nimekuwa na elimu na nimejua ubaya wake.”Nasarai anaamini kuwa iwapo jamii itapata elimu basi itabadilika“Jamii yetu sanasana haina elimu, tukiona jamii yetu watu wachache ndio wamesoma na wengi wakisoma watapata hiyo elimu zaidi na watakuja kuikomesha FGM. Mimi naamini kwamba miaka 10 inayokuja mambo ya kukeketa wasichana hatutasikia tena.” Elimu ya kutokomeza ukeketaji inatolewa katika maeneo mbalimbali ikiwemo masokoni, katika vikao vya jumuiya na mashuleni. 
    5 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners