Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 04 MACHI 2026
    Miongoni mwa utakayo yasikia hii leo jaridani ni mzozo huko Mashariki ya Kati baada ya Israel na Marekani kuishambulia Iran na kisha Iran kujibu mashambulizi. Sasa nchi jirani nazo zimeathirika ikiwemo Lebanon ambapo sasa UNHCR inatoa msaada kwa wananchi. Zikiwa ni siku chache kabla ya Siku ya wanawake duniani tarehe 08 Machi, leo utasikilia simulizi ya mwanamke aliyekuwa akifanyiwa ukatili na mume wake na msaada aliopokea kutoka WLAC. Katika masuala hayo hayo ya wanawake tutasikia wanawake wa Masrabit wanavyoelimisha wenzao kukataa ukeketaji kupitia mradi wa UNFPA nchini Kenya
    14 min
  • 03 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka huko Mashariki ya Kati ambako Leo ni siku ya nne ya mzozo mabomu yameripotiwa kuendelea kulipuka. Makombora yanarindima katika ukanda huo huku ndege zisizo na rubani au droni zikisababisha maafa sasa katika nchi 12. Pia tunakuletea muhtasari wa habari kama zifuatazo.Mgogoro wa Iran ukiendelea kupamba moto, Umoja wa Mataifa na mashirika yake wanaendelea kufuatilia kwa ukaribu kuhusu hali hiyo tete huku wakiendelea kuhamasisha amani kupitia diplomasia kwani tayari madhara ya moja kwa moja kwa wanadamu yameshaonekana. Mathalani leo Msemaji wa ofisi ya Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, OHCHR, Ravina Shamdasani akirejelea  tukio moja baya la kusikitisha ambapo inaripotiwa wasichana kadhaa waliuawa na kujeruhiwa wakati shule yao ya msingi huko Minab, kusini mwa Iran, iliposhambuliwa wakati wa saa za masomo, amesema, “watoto, wasichana wadogo katikati ya siku ya shule, mwanzoni mwa siku ya masomo, wanauawa kwa namna hii, mabegi yao ya shule yakiwa na, unajua, madoa ya damu juu yake.Shirika la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki, IAEA leo limeeleza kwamba kulingana na picha mpya za satelaiti, sasa linaweza kuthibitisha baadhi ya uharibifu wa hivi karibuni kwenye majengo ya milango ya Kiwanda cha Kuchakata Mafuta cha FEP kilichojengewa chini ya ardhi huko Natanz, Iran. Ujumbe wa IAEA umefafanua kuwa hakuna athari zozote za mionzi zinazotegemewa na hakuna athari za ziada zilizobainika kwenye Kiwanda cha FEP chenyewe, ambacho tayari kilikuwa kimeharibiwa vibaya katika mzozo wa mwezi Juni.Leo ni Siku ya Kimataifa ya Wanyamapori mwaka huu kaulimbiu ya siku ikilenga “Mimea ya Dawa na Harufu nzuri inaangazia nafasi muhimu ya mimea hii katika kudumisha afya ya binadamu, urithi wa kitamaduni, na kipato cha jamii za wenyeji. Katika ujumbe wake mahususi kwa ajili ya siku hii, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akionesha wasiwasi wake kuhusu kutoweka kwa miea asili ya dawa ametoa wito akisema,ninazihimiza nchi zote ziwe watunza bustani wa rasilimali za pamoja za dunia.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min
  • IAEA yaonya hatari ya nyuklia kadri mzozo Mashariki ya Kati unavyozidi kupamba moto
    Mwelekeo mpya wa mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku yake ya tatu leo Jumatatu ukichochewa na mashambulizi ya mabomu dhidi ya Iran yaliyofanywa na Israel na Marekani, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Rafael Grossi amehimiza kurejea kwa diplomasia, akitaja “hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia” katika eneo hilo. Anold Kayanda na  maelezo zaidi.
    3 min
  • UNFPA nchini Burundi yasaka usadizi kunusuru afya za wazazi na watoto kambini Busuma
    Uhaba wa vifaa na maji safi na salama katika kambi ya muda ya wakimbizi ya Busuma iliyoko mashariki mwa Burundi umekuwa changamoto kubwa kwa wanawake wajawazito wanaojifungua kambini hapo, wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) nchini Burundi linasema katika kipindi cha mwezi mmoja takribani watoto 200 wamezaliwa. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.
    4 min
  • 02 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia huku vita vikiendelea kushika kasi nchini Iran, masuala ya afya ya wanawake na watoto nchini Burundi, na maisha ya baadaye ya watoto katika ukanda wa Gaza.Mwelekeo mpya wa mzozo katika eneo la Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku yake ya tatu leo Jumatatu ukichochewa na mashambulizi ya mabomu dhidi ya Iran yaliyofanywa na Israel na Marekani, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la nishati ya atomiki, IAEA, Rafael Grossi amehimiza kurejea kwa diplomasia, akitaja “hatari inayoongezeka kwa usalama wa nyuklia” katika eneo hilo.Uhaba wa vifaa na maji safi na salama katika kambi ya muda ya wakimbizi ya Busuma iliyoko mashariki mwa Burundi umekuwa changamoto kubwa kwa wanawake wajawazito wanaojifungua kambini hapo, wakati huu ambapo shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu na Afya ya Uzazi, (UNFPA) nchini Burundi linasema katika kipindi cha mwezi mmoja takribani watoto 200 wamezaliwa.Hakuna maisha ya baadaye! Siyaoni maisha ya baadaye kwani sioni wanaoshikamana nasi! Hayo ni sehemu tu ya maoni ya watoto walioko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima, mustakabali wao uko mashakani, na wanachohitaji kama inawezekana ni amani na ujenzi mpya wa makazi ili waweze kurejea katika maisha ya kawaida ndani ya nyumba zao na kuacha kuishi kama wakimbizi katika ardhi yao wenyewe.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • Matumaini ya maisha mapya kwa watoto katika ukanda wa Gaza yazidi kufifia
    "Hakuna maisha ya baadaye! Siyaoni maisha ya baadaye kwani sioni wanaoshikamana nasi!" Hayo ni sehemu tu ya maoni ya watoto walioko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli wakati huu ambapo makombora yanaendelea kurindima, mustakabali wao uko mashakani, na wanachohitaji kama inawezekana ni amani na ujenzi mpya wa makazi ili waweze kurejea katika maisha ya kawaida ndani ya nyumba zao na kuacha kuishi kama wakimbizi katika ardhi yao wenyewe. Rashid Malekela anatupeleka kwenye makazi yao huko Gaza! 
    4 min
  • 27 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia haki za wanawake, na uhuru wa kiraia, ujumbe wa Bi Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, na ripoti ya IPC kuhusu njaa nchini Somalia.Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu Volker Türk ameonya kuwa shinikizo linaongezeka duniani kote dhidi ya haki za wanawake, uhuru wa kiraia na taasisi za kimataifa akitoa wito kwa serikali kujitolea upya katika ushirikiano, uwajibikaji na utawala wa sheria.Kiongozi wa shirika kubwa zaidi la msaada wa chakula duniani ametangaza kujiuzulu. Bi. Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP amesema atajiuzulu wadhifa wake huo  baada ya miezi mitatu ili kuzingatia afya yake, akisema bado hajapona kikamilifu baada ya kupata kiharusi mwaka jana 2025.Fundi wa magari mwanamke kutoka nchini Ethiopia anayehudumu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, Meja Tigist Ferede ametunukiwa nishani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, kwa kusimamia jukumu muhimu la wanawake katika operesheni za kulinda amani nje ya kushika bunduki.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    11 min
  • Fundi wa magari mwanamke wa UNMISS atunukiwa nishani ya Umoja wa Taifa
    Fundi wa magari mwanamke kutoka nchini Ethiopia anayehudumu na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini, UNMISS, Meja Tigist Ferede ametunukiwa nishani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, kwa kusimamia jukumu muhimu la wanawake katika operesheni za kulinda amani nje ya kushika bunduki. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Rashid Malekela. 
    3 min
  • “Nitaachia ngazi” WFP baada ya miezi mitatu: Cindy McCain
    Kiongozi wa shirika kubwa zaidi la msaada wa chakula duniani ametangaza kujiuzulu. Bi. Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP amesema atajiuzulu wadhifa wake huo  baada ya miezi mitatu ili kuzingatia afya yake, akisema bado hajapona kikamilifu baada ya kupata kiharusi mwaka jana 2025. Flora Nducha na taarifa zaidi
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners