Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 20 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia athari ya baa la nja nchini Somalia, kampeni ya chanjo la polio nchini Malawi, na juhudi za UNMISS nchini Sudan Kusini za kuwapatia hifadhi na lishe watoto yatima huko Juba.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema hali ya upatikanaji wa chakula nchini Somalia imefikia hatua mbaya ambapo watu milioni 4.4 hivi sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kwamba ni mtu 1 tu kati ya 7 ndiye anayepata mgao wa chakula.Takribani watoto milioni 1.3 nchini Malawi wamepatiwa chanjo ya polio katika kampeni maalum ya siku nne, kufuatia kugunduliwa kwa mgonjwa mpya wa polio mwishoni mwa mwezi Januari 2026. Huyu ni mgonjwa wa kwanza kuripotiwa tangu mwaka 2022, wakati virusi vya polio pori vilivyokuwa na uhusiano wa kijenetiki na mlipuko ulioripotiwa nchini Pakistan vilipobainika.Sudan Kusini ambako mizozo inaendelea kuvuruga utoto wa watoto, kituo kidogo cha watoto yatima katika mji Mkuu Juba kinawapa makumi ya watoto walio hatarini si tu makazi, bali pia matumaini, uponyaji, na nafasi ya kujenga upya mustakabali wao. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    12 min
  • Ukata WFP wasababisha mtu 1 tu kati ya 7 apatiwe msaada wa chakula
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema hali ya upatikanaji wa chakula nchini Somalia imefikia hatua mbaya ambapo watu milioni 4.4 hivi sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kwamba ni mtu 1 tu kati ya 7 ndiye anayepata mgao wa chakula. Rashid Malekela na taarifa zaidi.
    3 min
  • 19 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina tukimsikia Barbara Batte Guevara, Mkufunzi anayefundisha lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Havana nchini Cuba. Kwa kushirikiana na Tanzania chuo hicho ambacho mwezi uliopita kimetimiza miaka 298 tangu kuanzishwa kwake, hivi karibuni kimetoa fursa kwa Wacuba kujifunza lugha ya Kiswahili.Anold Kayanda wa Idhaa hii amemtembelea Profesa Barbara Batte katika jiji la Havana nchini Cuba ili kufahamu zaidi kuhusu hatua hii na mafanikio yaliyofikiwa hadi kufikia sasa. Pia tunakuletea habari kwa ufupi kama zifuatazo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuanzishwa kwa Mfuko wa Kimataifa wa Akili Mnemba au AI wenye thamani ya dola bilioni 3, ili kuhakikisha teknolojia hiyo inawanufaisha watu wote duniani, badala ya kuwa mali ya mataifa machache au kampuni chache zenye nguvu. Akizungumza katika Mkutano wa Kimataifa wa kujadili Athari za AI huko New Delhi nchini India, Guterres amesema mustakabali wa AI unapaswa kujengwa kwa ushirikiano wa kimataifa”.Mashambulizi makali yanayoendelea kufanywa na Israeli dhidi ya maeneo ya Palestina ya Gaza na Ukingo wa Magharibi ambayo inakalia kimabavu yanatia hofu ya uwezekano wa utokomezaji wa kabila, imesema Ripoti mpya ya Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR), ya kuanzia Novemba 1 2024 hadi Desemba 31 2025. Ripoti inasema mashambulizi ya Israeli yameweka mazingira ambamo kwamo wapalestina kama kundi watashindwa kuendelea kuishi Gaza huku Ajith Sunghay, Mkuu wa Ofisi ya OHCHR Palestina akisema, “ripoti inachambua  mwenendo wa mapigano ya jeshi la Israeli, linaloendelea kuua idadi kubwa ya raia, kusababisha njaa, kuwahamisha takribani wakazi wote wa Gaza, tena zaidi ya mara moja — na kuharibu miundombinu iliyosalia ya kiraia ya Gaza.”wanamgambo wa vikosi vya Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan walitekeleza kampeni iliyoratibiwa ya uharibifu dhidi ya jamii zisizo za kiarabu ndani ya mji wa El-Fasher na viunga vyake, kampeni yenye viashiria vya mauaji ya kimbari, imeeleza ripoti mpya iliyotolewa leo na Tume Huru ya Umoja wa Mataifa ya Kuchunguza Ukweli kuhusu Sudan. Ripoti imetaja vitendo hivyo ni pamoja na kuua wanachama wa kundi la kikabila linalolindwa; kusababisha madhara makubwa ya kimwili na kiakili; ambavyo ni vipengele muhimu vya kosa la mauaji ya kimbari chini ya sheria za kimataifa.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunawasikiliza baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Havana wanaojifunza lughaya Kiswahili. Tuanze na Yibran Nunez Batte.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min
  • 18 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia masuala ya Akili Mnemba na wabunifu wa maudhui duniani kwa lugha, waumini wa dini ya kiislamu wakati huu wa Ramadhani katika ukanda wa Gaza, na matibabu ya kwanza ya ugonjwa wa kichocho huko Mwanza nchini Tanzania.Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, limesema wabunifu wa maudhui duniani kwa lugha ya kiingereza content creators wanakabiliwa na hatari ya kupoteza hadi asilimia 24 ya mapato yao ifikapo mwaka 2028 kutokana na kasi ya maendeleo ya Akili Mnemba, au AI.Waumini wa dini ya kiislamu duniani kote wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kipindi kinachoambatana na sio tu ibada bali pia mlo kama vile futari na daku. Hata hivyo kwa wakazi wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na kimabavu na Israeli hali si hali kwani mlo na mengine yanayoambatana na kipindi hiki vinasalia kuwa ndoto.Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kupitia Ushirikiano wa Upatikanaji na Ufikishaji wa Huduma (ADP), inaendesha mpango wa majaribio wa kihistoria katika mikoa ya Simiyu, Mwanza, na Kigoma ili kutoa matibabu ya kwanza ya ugonjwa wa kichocho yaliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano.Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, karibu!
    13 min
  • Wakazi katika ukanda wa Gaza wahaha kumudu mlo wakati wa mfungo wa Ramadhani
    Waumini wa dini ya kiislamu duniani kote wameanza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, kipindi kinachoambatana na sio tu ibada bali pia mlo kama vile futari na daku. Hata hivyo kwa wakazi wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na kimabavu na Israeli hali si hali kwani mlo na mengine yanayoambatana na kipindi hiki vinasalia kuwa ndoto. Assumpta Massoi anafafanua zaidi.
    3 min
  • Tanzania yajipanga kutokomeza ugonjwa wa kichocho kwa watoto wadogo
    Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kupitia Ushirikiano wa Upatikanaji na Ufikishaji wa Huduma (ADP), inaendesha mpango wa majaribio wa kihistoria katika mikoa ya Simiyu, Mwanza, na Kigoma ili kutoa matibabu ya kwanza ya ugonjwa wa kichocho yaliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Rashid Malekela na taarifa zaidi. 
    4 min
  • 17 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, ambako Magonjwa ya kimeta, miguu na midomo yanayokumba mifugo kama vile ng’ombe pamoja na mdondo unaoshambulia kuku yameendelea kuwa mwiba duniani na hata nchini Tanzania, ambako mbinu mbali mbali zimekuwa zikitumika kuyadhibiti ili kunusuru afya ya mifugo.Uchambuzi mpya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) na HRP, ambao ni mpango wa taasisi za Umoja wa Mataifa za utafiti kuhusu uzazi wa binadamu, unaonesha kuwa takribani theluthi mbili ya vifo vya wajawazito duniani hutokea katika nchi zilizoathiriwa vibaya na migogoro au zenye udhaifu wa mifumo, ambapo ujauzito ni hatari mara tano zaidi ikilinganishwa na nchi zilizo thabiti.Vita vya Ukraine vikielekea kuingia katika mwaka wa tano, zaidi ya theluthi moja ya watoto wa Ukraine bado wameyakimbia makazi yao wengi wao sasa wakilazimika kuishi katika majengo yaliyoko chini ya ardhi. Akizungumza na waandishi wa habari kutoka kwenye chumba cha chini ya jengo katika mji wa Kherson, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Ukraine, Munir Mammadzade, amesema mji huo “upo chini ya mashambulizi ya mara kwa mara,” huku mashambulizi ya kila siku yakiharibu nyumba na miundombinu muhimu, pamoja na huduma ambazo watoto na familia wanazitegemea.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu madhara yanayoweza kuwapata waathirika waliotajwa katika nyaraka zinazojulikana kama “Epstein Files”, wakisema mchakato wa utoaji wa taarifa hizo haukulinda ipasavyo faragha na usalama wao na pia wametaka hatua stahili za kisheria zichukuliwe kwa wale wote waliotajwa katika nyaraka hizo kwa mujibu wa sheria. Nyaraka hizo zinafichua maovu yaliyotendwa na watu mbalimbali kupitia mmarekani Jeffrey Epstein.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya"KOO" katika mkitadha wa wanyama.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    10 min
  • DRC: UNICEF na KOICA waboresha huduma za usafi na lishe kwa wakazi wa Tanganyika
    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakishirikiana na Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanawasaidia wananchi wa Nyunzu katika jimbo la Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC kwa miradi ya kusaidia huduma za afya ya watoto ambapo wamepanua upatikanaji wa huduma muhimu na endelevu. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners