Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Wanawake sayansi tunaiweza kinachotakiwa ni kujiamini: Dkt. Mugara Mahungururo
    Leo ni siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi mwaka huu mauadhui yakihimiza “Sayansi kwa Mustakabali Jumuishi kwa Wanawake na Wasichana” Kwamujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , Sayansi na Utamaduni UNESCO leo hii , wanawake wanachangia chini ya theluthi moja ya watafiti duniani, kulingana hivyo kuziba pengo hili la kijinsia si suala la haki pekee ni muhimu kwa ubora, uhalisia na mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu. Flora Nducha na taarifa zaidi 
    3 min
  • 11 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya IPU kuhusu uhasama wa wabunge, siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi, na yalitojiri katika Jukwaa la akili unde au AI lililofanyika kwa siku mbili huko Nairobi, nchini Kenya.Wabunge kote ulimwenguni wanakabiliwa na viwango vinavyoongezeka vya vitisho, unyanyasaji na vurugu kutoka kwa umma imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na Muungano wa Mabunge Duniani (IPU). Rashid Malekela na taarifa zaidi.Leo ni siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika sayansi mwaka huu mauadhui yakihimiza “Sayansi kwa Mustakabali Jumuishi kwa Wanawake na Wasichana” Kwamujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , Sayansi na Utamaduni UNESCO leo hii , wanawake wanachangia chini ya theluthi moja ya watafiti duniani, kulingana hivyo kuziba pengo hili la kijinsia si suala la haki pekee ni muhimu kwa ubora, uhalisia na mchango wa sayansi, teknolojia na ubunifu.Jukwaa la akili unde au AI lililofanyika kwa siku mbili huko Nairobi, nchini Kenya limekunja jamvi ambapo mmoja wa washiriki amesema wanaodai kuwa bara la Afrika liko nyuma kwenye teknolojia hiyo, ni dhahiri shairi hawalifahamu vema bara hilo lenye mataifa 54.
    10 min
  • 10 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na Wakili Amon Mpanju, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kutoka Tanzania aliyehudhuria Mkutano wa Kamisheni ya Maendeleo ya Kijamii (CSocD64).Mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa leo yametoa onyo kali kuhusu hali mbaya ya kibinadamu inayowakumba watoto nchini Sudan. Mashirika hayo lile la kuhudumia watoto UNICEF, la afya WHO na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu wamenasema ghasia zisizoisha, njaa na magonjwa vinawasababisha watoto kupoteza Maisha na kudhoofika, huku mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na vikwazo vya upatikanaji wa misaada vikizorotesha juhudi za kuwaokoa. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Geneva, msemaji wa UNICEF, Ricardo Pires, amesema “Katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Darfur Kaskazini, zaidi ya nusu ya watoto wote wanakabiliwa na utapiamlo mkali, si makadirio, si mfano, imethibitishwa.”.Kikosi cha 12 cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania TANZBAT 12 kinachohusumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo DRC chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kimeendelea kudumisha uhusiano wa kijamii na wakazi wa mji wa Beni Mashariki mwa DRC, kwa kutoa msaada wa vifaa vya elimu kwa wanafunzi katika shule ya msingi Ngite iliyopo eneo la Mavivi. Mkuu wa shule hiyo Neema Nyamwaka amewashukuru walinada amani hao kutoka Tanzania kwa kujali sekta ya elimu.Leo ni siku ya mikunde duniani Shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO likisistiza umuhimu kwa chakula hicho kwa lishe na mazingira. Huko Kigoma Tanzania FAO kupitia mpango wa Pamoja wa KJP imekuwa ikitoa mafunzo kwa wakulima kuhusu umuhimu wa mazao ya jamii ya mikunde huyu ni mmoja wa wanufaika wa mafunzo hayo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Atokeapo mtoto wa fuko mshike japo wawinda fuko.”Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    14 min
  • Nilirubunika nikadhani ukeketaji ni usafi kumbe ni jinamizi: Manusura Saadia Hussein
    Ukeketaji au FGM ni jinamizi linalowaandama waathirika maisha yao yote likisababisha changamoto sio tu za kimwili lakini pia za kiafya na kuwaacha na makovu yasiyofutika. Katika Kaunti ya Tana River Kusini Mashariki mwa Kenya tunakutana na manusura na shujaa mwanaharakati wa kupambana na mila hiyo potofu ya ukeketaji Saadia Hussein, raia wa Somalia anayeishi Kenya hivi sasa .Ni Mkurugenzi mtendaji na mwanzilishi wa taasisi  isiyo ya kiserikali ya Brighter Society Initiative. Anatusimulia safari yake ya machungu ya ukeketaji
    4 min
  • 09 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia walinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu mwenye ulemavu wa kutoona nchini Vietnam, na harakati za kutokomeza ukeketaji nchini Kenya.Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, (MONUSCO) umetoa taarifa kwamba umefahamishwa na Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa kuwa Afrika Kusini itaondoa vikosi na wanajeshi wake waliobaki ndani ya MONUSCO. Ninamualika Rashid Malekela aliyeifuatilia kwa kina taarifa hiyo ili atueleza zaidi.Nchini Vietnam taifa lililoko kusini-mashariki mwa Asia, mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu mwenye ulemavu wa kutoona anajitahidi kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa mawasiliano licha ya vikwazo anavyokumbana navyo kila uchao, na hii ni kwa sababu si kwamba njia ni rahisi bali kwa sababu dhamira yake ni kubwa zaidi.Ukeketaji au FGM ni jinamizi linalowaandama waathirika maisha yao yote likisababisha changamoto sio tu za kimwili lakini pia za kiafya na kuwaacha na makovu yasiyofutika. Katika Kaunti ya Tana River Kusini Mashariki mwa Kenya tunakutana na manusura na shujaa mwanaharakati wa kupambana na mila hiyo potofu ya ukeketaji Saadia Hussein, raia wa Somalia anayeishi Kenya hivi sasa. Mkurugenzi mtendaji na mwanzilishi wa taasisi  isiyo ya kiserikali ya Brighter Society Initiative anatusimulia safari yake ya machungu ya ukeketaji.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • “Tuwekeeni mazingira sahihi ili nasi tuoneshe uwezo wetu,” asema Msichana mwenye ulemavu wa kuona.
    Nchini Vietnam taifa lililoko kusini-mashariki mwa Asia, mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu mwenye ulemavu wa kutoona anajitahidi kuhakikisha anatimiza ndoto yake ya kuwa mtaalamu wa mawasiliano licha ya vikwazo anavyokumbana navyo kila uchao, na hii ni kwa sababu si kwamba njia ni rahisi bali kwa sababu dhamira yake ni kubwa zaidi. Assumpta Massoi anasimulia zaidi kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani, ILO.
    3 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners