Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 03 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani kesho ikiwa ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa saratani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kumulika hatua ambazo ni uzinduzi wa Mpango wa Utekelezaji wa Kitaifa wa kutokomeza saratani ifikapo mwaka 2030.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa  Duniani, WHO, leo limetoa ombi la dola bilioni moja ili kukabiliana na majanga ya afya mwaka 2026 katika dharura 36 zilizo mbaya zaidi duniani. Ombi hilo linalenga kusaidia huduma za afya zinazookoa maisha katika nchi zilizoathiriwa na migogoro na majanga, zikiwemo Gaza, Sudan, Haiti na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.Mashariki ya Kati, wakati muda ukiendelea kuyoyoma kwa maelfu ya wagonjwa mahututi huko Gaza, kufunguliwa tena kwa kivuko cha Rafah kunaleta mwanga wa matumaini. Kivuko hicho kilifunguliwa Jumatatu baada ya kufungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, chini ya mpango wa amani unaoungwa mkono na Marekani, na kuruhusu uhamisho wa kwanza wa wagonjwa tangu mwaka 2025.Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF leo liimesema linaongeza juhudi zake zamsaada wa msimu wa baridi nchini Ukraine huku watoto na familia wakikabiliwa na kukatika kwa umeme, kukosa vipasha joto na maji kufuatia mashambulizi yanayoendelea dhidi ya miundombinu ya nishati na baridi kali. Tangu Novemba, shirika hilo limesambaza jenereta 106 kote nchini kusaidia huduma za maji na mifumo ya kupasha joto, huku takribani jenereta 150 zaidi zikitarajiwa kuwasili katika wiki zijazo.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "KUNVI"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    13 min
  • 02 FEBRUARI 2026
    Chukua hatua za kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa saratani.Sudan Kusini iko nijia panda na wananchi wanalitambua hilo: UNMISS.UNCDF: Uwekezaji bunifu wasaidia wakulima Dodoma, Tanzania
    10 min
  • Hali ya njaa inatishia maisha ya watoto nchini Sudan
    Sudan inakabiliana na viwango vya hatari vya njaa, ambapo mamilioni ya watoto kama Noon wako katika hatari kubwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) liko shambani, likitoa msaada muhimu wa lishe, maji safi, na ulinzi. Hata hivyo, mahitaji ni makubwa, na msaada zaidi unahitajika haraka ili kuokoa maisha ya watoto hawa. Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi
    3 min
  • Waliofurushwa na mafuriko Msumbiji sasa wafikia 400,000- UNHCR
    Idadi ya watu waliofurushwa makwao nchini Msumbiji kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi uliopita wa Desemba inakaribia 400,000 hali inayoongeza hatari kubwa katika fursa ya kuwapatia ulinzi na huduma zinazohitajika. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR kama anavyosimulia Flora Nducha.
    3 min
  • 30 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia mafuriko nchini Msumbiji yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi uliopita, hali ya kibinadamu kwa watoto Sudan na migogoro na uhakika wa chakula Sudan Kusini..Idadi ya watu waliofurushwa makwao nchini Msumbiji kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizoanza kunyesha katikati ya mwezi uliopita wa Desemba inakaribia 400,000 hali inayoongeza hatari kubwa katika fursa ya kuwapatia ulinzi na huduma zinazohitajika. Limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR.Makubaliano ya amani nchini Sudan Kusini yanakabiliwa na vitisho na hivyo wadau lazima husika wautekeleze licha ya changamoto zilizoko, amesema Luteni Jenerali Mohan Subramanian ambaye ni Kamanda Mkuu wa kikosi cha ujumbe wa  Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Sudan inakabiliana na viwango vya hatari vya njaa, ambapo mamilioni ya watoto kama Noon wako katika hatari kubwa. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto (UNICEF) liko shambani, likitoa msaada muhimu wa lishe, maji safi, na ulinzi. Hata hivyo, mahitaji ni makubwa, na msaada zaidi unahitajika haraka ili kuokoa maisha ya watoto hawa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • 29 JANUARI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Jamhuri Africa ya Kati CAR kusikia mama mkimbizi anayesimulia aliyoyapitia, maisha ya uhamishoni na alivyojipatia nguvu iliyo kuu kuliko silaha yoyote ya vita. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na neno la wiki.Nchini Ethiopia, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limeeleza kwamba Ethiopia imefanikiwa kutekeleza mizunguko minne ya uchanjaji watoto kwa njia ya matone dhidi ya ugonjwa wa polio. Mwaka jana 2025 Ethiopia kwa kutumia chanjo ya nOPV2 ilitekeleza uchanjaji huo kupitia mzunguko mmoja wa nchi nzima na mitatu kupitia maeneo mbalimbali ya nchi na kufanikiwa kuwafikia watoto milioni 26 katika mikoa yote.Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO), Beth Bechdol, ameeleza umuhimu wa kilimo wakati wa migogoro kulingana na mafanikio aliyoyashuhudia wakati wa ziara yake nchini Haiti na majirani zao Jamhuri ya Dominika.Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Asia (ADB) wametangaza kuwa wanatekeleza mpango wa dola milioni 100 ili kuimarisha uhakika wa chakula na lishe pamoja na kurejesha kipato kinachotokana na kilimo kwa zaidi ya watu milioni moja walio katika mazingira magumu kote nchini Afghanistan.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya "SIKU ZA JANGUO."Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    12 min
  • Idadi ya wanaopatiwa msaada DRC yapunguzwa kutokana na ukata
    Kutokana na ufinyu wa ufadhili unaolazimisha Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada ya kibinadamu, OCHA kupunguza idadi ya wanaopatiwa misaada nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, serikali ya DRC  kwa kushirikiana na  OCHA wamezindua ombi la dola za kimarekani bilioni 1.4 ili kuokoa hali.  Flora Nducha na taarifa kwa kina.
    3 min
  • IOM, Marekani na wadau washirikiana kukabili uhalifu Ziwa Viktoria
    Ziwa Viktoria barani Afrika, licha ya kuwa mhimili muhimu wa maisha kwa zaidi ya watu milioni 40 nchini Kenya, Uganda na Tanzania, bado linakabiliwa na vitisho vihusianavyo na biashara haramu za magendo, usafirishaji haramu binadamu na uvuvi haramu. Ili kupatia suluhu changamoto hiyo Ofisi ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na utekelezaji wa sheria (INL) ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM), na walinzi wa pwani wa Kenya wamechukua hatua. Je ni hatua zipi? Sheilah Jepngetich na taarifa zaidi.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners