Hii leo jaridani tunaangazia juhudi za kutokomeza sarati, mashambilizi dhidi ya misafara ya chakula katika kaunti ya Baliet, jimbo la Upper Nile, nchini Sudan Kusini na tunamulika miaka kumi na nne baada ya wakimbizi wa kwanza wa Syria kuvuka mpaka kuingia Jordan.Mabadiliko ya mfumo wa maisha na mazingira yanaweza kuzuia ugonjwa wa saratani kwa wagonjwa wanne katika kila wagonjwa kumi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani, (WHO) na shirika lake tangu la Utafiti kuhusu saratani, IARC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo Februari 4, 2026 limetangaza kusitisha shughuli zake zote katika kaunti ya Baliet, jimbo la Upper Nile, nchini Sudan Kusini kufuatia mfululizo wa mashambulizi dhidi ya msafara wake wa majini mwishoni mwa wiki iliyopita. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Miaka kumi na nne baada ya wakimbizi wa kwanza wa Syria kuvuka mpaka kuingia Jordan kusaka usalama, kambi ya wakimbizi ya Zaatari bado ni makazi ya maelfu ya watu wanaosubiri suluhu ya kudumu. Wiki hii, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi, Barham Salih, ametembelea kambi hiyo na kukutana na familia ambazo zimeishi ukimbizini kwa zaidi ya muongo mmoja wengi wao wakiwa bado na matumaini ya kurejea nyumbani, lakini tu pale ambapo itakuwa salama.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!