Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Tanzania yajipanga kutokomeza ugonjwa wa kichocho kwa watoto wadogo
    Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kupitia Ushirikiano wa Upatikanaji na Ufikishaji wa Huduma (ADP), inaendesha mpango wa majaribio wa kihistoria katika mikoa ya Simiyu, Mwanza, na Kigoma ili kutoa matibabu ya kwanza ya ugonjwa wa kichocho yaliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Rashid Malekela na taarifa zaidi. 
    4 min
  • 17 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania, ambako Magonjwa ya kimeta, miguu na midomo yanayokumba mifugo kama vile ng’ombe pamoja na mdondo unaoshambulia kuku yameendelea kuwa mwiba duniani na hata nchini Tanzania, ambako mbinu mbali mbali zimekuwa zikitumika kuyadhibiti ili kunusuru afya ya mifugo.Uchambuzi mpya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) na HRP, ambao ni mpango wa taasisi za Umoja wa Mataifa za utafiti kuhusu uzazi wa binadamu, unaonesha kuwa takribani theluthi mbili ya vifo vya wajawazito duniani hutokea katika nchi zilizoathiriwa vibaya na migogoro au zenye udhaifu wa mifumo, ambapo ujauzito ni hatari mara tano zaidi ikilinganishwa na nchi zilizo thabiti.Vita vya Ukraine vikielekea kuingia katika mwaka wa tano, zaidi ya theluthi moja ya watoto wa Ukraine bado wameyakimbia makazi yao wengi wao sasa wakilazimika kuishi katika majengo yaliyoko chini ya ardhi. Akizungumza na waandishi wa habari kutoka kwenye chumba cha chini ya jengo katika mji wa Kherson, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) nchini Ukraine, Munir Mammadzade, amesema mji huo “upo chini ya mashambulizi ya mara kwa mara,” huku mashambulizi ya kila siku yakiharibu nyumba na miundombinu muhimu, pamoja na huduma ambazo watoto na familia wanazitegemea.Wataalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa wameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu madhara yanayoweza kuwapata waathirika waliotajwa katika nyaraka zinazojulikana kama “Epstein Files”, wakisema mchakato wa utoaji wa taarifa hizo haukulinda ipasavyo faragha na usalama wao na pia wametaka hatua stahili za kisheria zichukuliwe kwa wale wote waliotajwa katika nyaraka hizo kwa mujibu wa sheria. Nyaraka hizo zinafichua maovu yaliyotendwa na watu mbalimbali kupitia mmarekani Jeffrey Epstein.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mlumbi wa lugha ya Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya"KOO" katika mkitadha wa wanyama.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    10 min
  • DRC: UNICEF na KOICA waboresha huduma za usafi na lishe kwa wakazi wa Tanganyika
    Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakishirikiana na Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanawasaidia wananchi wa Nyunzu katika jimbo la Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC kwa miradi ya kusaidia huduma za afya ya watoto ambapo wamepanua upatikanaji wa huduma muhimu na endelevu. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
    3 min
  • Mkutano wa AI waanza New Delhi Mjumbe wa UN asisitiza ujumuishi wa nchi zote
    Mkutano wa kimataifa unaofahamika kama AI Impact 2026 umeanza leo mjini New Delhi, India ukiwakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali za dunia ili kujadili namna akili mnemba (AI) inavyoweza kuendelezwa na kutumika kwa uwajibikaji kuchangia maendeleo endelevu. Amandeep Singh Gill, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia teknolojia za kidijitali na zinazoibuka, amesisitiza ushiriki mpana wa kimataifa kwani ni muhimu ili kuhakikisha AI inanufaisha nchi zote. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
    3 min
  • 16 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia mkutano wa kimataifa unaofahamika kama AI Impact 2026 mjini New Delhi, India, hali ya kibinadamu nchini Cuba, na huduma za Afya, maji safi na salama nchini DR Congo.Mkutano wa kimataifa unaofahamika kama AI Impact 2026 umeanza leo mjini New Delhi, India ukiwakutanisha viongozi kutoka sehemu mbalimbali za dunia ili kujadili namna akili mnemba (AI) inavyoweza kuendelezwa na kutumika kwa uwajibikaji kuchangia maendeleo endelevu. Amandeep Singh Gill, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia teknolojia za kidijitali na zinazoibuka, amesisitiza ushiriki mpana wa kimataifa kwani ni muhimu ili kuhakikisha AI inanufaisha nchi zote.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imetoa onyo kali kuhusu kuzorota kwa hali ya kiuchumi nchini Cuba, ikisema uhaba wa mafuta na vikwazo vya muda mrefu vinaathiri vibaya huduma za msingi kote nchini humo.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF wakishirikiana na Shirika la Maendeleo la Korea KOICA wanawasaidia wananchi wa Nyunzu katika jimbo la Tanganyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo DRC kwa miradi ya kusaidia huduma za afya ya watoto ambapo wamepanua upatikanaji wa huduma muhimu na endelevu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • Cuba: Hali ya kibinadamu imefikia pabaya yaonya OHCHR
    Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imetoa onyo kali kuhusu kuzorota kwa hali ya kiuchumi nchini Cuba, ikisema uhaba wa mafuta na vikwazo vya muda mrefu vinaathiri vibaya huduma za msingi kote nchini humo. Flora Nducha na taarifa zaidi
    3 min
  • Vipindi vya Redio ya Umoja wa Mataifa vilitoa tafsiri sahihi ya wapigania uhuru
    Leo ni siku ya redio duniani ambayo msingi wake unatokana na kuanzishwa kwa redio ya Umoja wa Mataifa tarehe 13 Februari mwaka 1946 jijini New York, Marekani. Kwa mantiki hiyo ikiwa mwaka huu redio hiyo ya Umoja wa Mataifa inatimiza miaka 80 tumeangazia mchango wa vipingi vyake vilivyokuwa vinarushwa na redio zingine ikiwemo iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD)  nchini Tanzania  wakati huo. Assumpta Massoi amemulika suala hilo.
    4 min
  • Redio Okapi iliokoa maisha yangu: Mkimbizi Bahati Yohane
    Katika maeneo ya migogoro, redio huwa nguzo ya utulivu. Mathalani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Radio Okapi ya Umoja wa Mataifa imekuwa sauti ya kuaminika na kuwasaidia wakimbizi kusaka usalama tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO. Mmoja wa wakimbizi kutoka Mashariki mwa DRC ambaye sasa anaishi kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda amemweleza John Kibego kutoka Redio washirika wetu Kazi Njema FM ya mjini Hoima jinsi matangazo ya redio Okapi yalivyonusuru maisha yake wakati wa vita
    4 min
  • 13 FEBRUARI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia Siku ya Redio Duniani likitupeleka nchini Tanzania kusikia jinsi ambavyo redio inavyochochea maendeleo ya kijamii, nchini Uganda kumsikia mkimbizi kutoka DRC, na katika ukanda wa Gaza ambako redio inaunganisha tena jamii ndani ya vifusi.Leo ni siku ya redio duniani ambayo msingi wake unatokana na kuanzishwa kwa redio ya Umoja wa Mataifa tarehe 13 Februari mwaka 1946 jijini New York, Marekani. Kwa mantiki hiyo ikiwa mwaka huu redio hiyo ya Umoja wa Mataifa inatimiza miaka 80 tumeangazia mchango wa vipingi vyake vilivyokuwa vinarushwa na redio zingine ikiwemo iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) nchini Tanzania wakati huo. Assumpta Massoi amemulika suala hilo.Katika maeneo ya migogoro, duniani redio huwa nguzo ya utulivu na wakati mwingine daraja la kuokoa maisha. Na ndivyo ilivyokuwa kwa mkimbizi Bahati Yohane kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwani kwake, redio haikuwa tu combo cha habari ilikuwa dira ya kuokoa maisha yake.Kabla ya vita vya sasa kuanza katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina lilalokaliwa kimabavu na Israel, Redio ilikuwa chombo muhimu kwa umma na kwa hakika umuhimu wake haujakoma isipokuwa huduma ya matangazo ya redio ndio iliyokuwa imekoma kutokana na vituo vya redio kusambaratishwa kwa makombora, lakini sasa juhudi zinafanyika kuirejesha huduma hiyo muhimu.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners