Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Vijana lazima tubadili fikra ili kuleta mabadiliko chanya asema Mary Teye kutoka Ghana - CSW70
    Sauti za vijana zinaendelea kusikika kwa nguvu katika wiki ya pili ya kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani kinachofanyika hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo wanaharakati, watunga sera na wadau kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika kujadili namna ya kuendeleza haki , haki za kisheria na fursa kwa wanawake na wasichana. Flora Nducha amepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa vijana washiriki kutoka Ghana na kutuandalia taarifa hii
    3 min
  • UNICEF: Mradi wa intaneti shuleni waleta mapinduzi ya kidijitali nchini Kenya
    Maelfu ya wanafunzi katika eneo la Kajiado nchini Kenya wameanza kunufaika na mradi wa kusambaza intaneti shuleni uitwao ‘Last Mile Connectivity’. Mradi huu unalenga kuboresha ujuzi wa kidijitali na matokeo ya masomo kwa wanafunzi ili kuwaandaa na maisha ya baadaye, huku shule 1,000 zikitarajiwa kufikiwa. Rashid Malekela amefuatilia maendeleo ya mradi huo katika shule za Enkasiti na Moipei, na hii hapa ni taarifa yake.
    3 min
  • CSW70 imenifanya niamini mimi ninastahili kutatua changamoto - Kanyesige Imelda
    Mikutano hii inayokutanisha Umoja wa Mataifa watetezi wa haki za wanawake dunia inawapa ujasiri vijana wa kuona kuwa nao wana uwezo na fursa ya kusaka majawabu katika jamii zao. Ni kauli ya kijana wa kike kutoka nchini Uganda anayeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani (CSW70) unaoendelea hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani. Feissal Kibet wa Idhaa hii ya Kiswahili  amepata fursa ya kuzungumza na kijana huyo na kuandaa taarifa hii. 
    4 min
  • 13 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ujumbe wa kijana kutoka Uganda anayehudhuria mkutano wa CSW70, na mradi wa intaneti kwa wanafunzi nchini Kenya.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres, aliyeko ziarani huko Lebanon, ameelezea wasiwasi mkubwa kuhusu mateso yanayowakabili wananchi wa taifa hilo la Mashariki ya Kati lililotumbukizwa kwenye vita isiyowahusu.Mikutano hii inayokutanisha Umoja wa Mataifa watetezi wa haki za wanawake dunia inawapa ujasiri vijana wa kuona kuwa nao wana uwezo na fursa ya kusaka majawabu katika jamii zao. Ni kauli ya kijana wa kike kutoka nchini Uganda anayeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani (CSW70 ) unaoendelea hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.Maelfu ya wanafunzi katika eneo la Kajiado nchini Kenya wameanza kunufaika na mradi wa kusambaza intaneti shuleni uitwao ‘Last Mile Connectivity’. Mradi huu unalenga kuboresha ujuzi wa kidijitali na matokeo ya masomo kwa wanafunzi ili kuwaandaa na maisha ya baadaye, huku shule 1,000 zikitarajiwa kufikiwa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    10 min
  • 12 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia yaliyojiri katika mkutano wa CSW70, ambapo kandoni mwa mkutano huo Assumpta Massoi wa Idhaa hii alipata fursa ya kuzungumza na Lucy Kabyemera, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi na Makazi nchini Tanzania aliyeongoza kikao hicho na kumpatia ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo mabadiliko ya sera.Idadi ya watu waliokimbia makazi yao nchini Iran imeongezeka kwa kasi na kufikia takriban watu milioni 3.2 kutokana na mashambulizi makali yanayozidi kushika kasi nchini humo kutoka jeshi la Marekani na Israeli huku nayo Iran ikijibu mashambulizi. Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR, kupitia taarifa yake iliyotolewa leo jijini Geneva, Uswisi, limebainisha kuwa kaya kati ya 600,000 na milioni 1 zimepoteza makazi yao, huku wengi wakikimbia miji mikubwa kama Tehran kuelekea maeneo ya vijijini na mikoa ya kaskazini kutafuta usalama. “Hali hii imeleta hofu kubwa ya kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu kadiri uhasama unavyozidi kusambaa katika maeneo mbalimbali,” imesema taarifa hiyo.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameelezea kuhusu matumizi makubwa ya fedha kwenye silaha za kivita wakati huu ambapo dunia ina uhitaji mkubwa wa msaada wa chakula na maeneo kadhaa kuwa na hali mbaya ya chakula huku mgao wa chakula ukitolewa mara moja au mbili badala ya mara tatu sababu ya ufinyu wa ufadhili. Dkt Tedros amesema matumizi ya kijeshi duniani yamefikia $ trilioni 2.7 - katika mwaka mmoja. Na kulingana na makadirio ya Umoja wa Mataifa, kukomesha njaa duniani ifikapo mwaka wa 2030 kutahitaji $ bilioni 93 kila mwaka. “Hiyo ina maana kwamba tunatumia karibu mara 30 zaidi kila mwaka kuuana kuliko kuhakikisha kila mtu anakula.”Leo ni Siku ya Mlo shuleni. Mamilioni ya watoto duniani kote huenda shuleni kila siku bila kutia chochote tumboni. Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula duniani WFP, zaidi ya watoto milioni 100 katika nchi zenye kipato cha chini na cha kati hukabiliwa na njaa kila siku. Hali hii huathiri uwezo wao wa kuzingatia masomo, kujifunza na kufaulu darasani. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, WFP inaunga mkono serikali mbalimbali kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanapata milo shuleni ili wawe na afya njema na wawe tayari kujifunza.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    12 min
  • UNICEF: Tumesikitishwa na kustushwa na kifo cha mwenzetu huko DRC
    Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, leo limesema limesikitishwa na kushtushwa na kifo cha mfanyakazi wake mmoja, Karine Buisset kilichotokea katika shambulio linaloripotiwa kufanywa na ndege isiyo na rubani yaani droni katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, eneo ambalo kwa muda mrefu limekumbwa na mapigano na hali mbaya ya kibinadamu. Anold Kayanda na taarifa zaidi.
    2 min
  • Vijana wachagiza hatua za haraka kuhusu haki za wanawake katika mkutano wa CSW70
    Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York ukiwa umeingia siku ya 3. Na vijana hawakusahaulika wamepewa nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo yao kuhusu maudhui ya mwaka huu ambayo yanasisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuhusu haki za wanawake, usawa wa kisheria na ushiriki wa vijana. Flora Nducha amekutana na baadhi yao kusikia maoni yao
    4 min
  • 11 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia habari ya kusikitisha ya kifo cha mfanyakazi wa UNICEF nchini DRC, na ujumbe wa washiriki wa mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York.Shirika la UNICEF limesema limesikitishwa na kushtushwa na kifo cha mfanyakazi wake Karine Buisset kilichotokea katika shambulio linaloripotiwa kufanywa na droni katika mji wa Goma mashariki mwa Jamhriy a Kidemokrasia ya Congo DRC, eneo ambalo kwa muda mrefu limekumbwa na mapigano na hali mbaya ya kibinadamu. Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell kupitia mtandao wake wa kijamii wa X, amesema shirika hilo pamoja na wafanyakazi wake duniani wameumizwa sana na tukio hilo.Oluwaseun Ayodeji Osowobi, mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Nigeria amezungumzia umuhimu wa kushirikisha wanaume katika harakati za kupigania haki za wanawake duniani wasichana.Mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya wanawake Duniani CSW70 leo unaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York ukiwa umeingia siku ya 3. Na vijana hawakusahaulika wamepewa nafasi ya kutoa maoni yao na mapendekezo yao kuhusu maudhui ya mwaka huu ambayo yanasisitiza umuhimu wa kuchukuliwa kwa hatua madhubuti kuhusu haki za wanawake, usawa wa kisheria na ushiriki wa vijana.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners