Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 07 APRILI 2026
    Jaridani tunakuletea mada kwa kina hii leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya Tafakari kuhusu Mauaji ya Kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda. Na katika kupata tafakari hiyo Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza na Mwakilishi wa Kudumu wa Rwanda kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Martin Ngoga. Balozi Ngoga anaanza kwa kuelezea mawanda ya mauaji hayo.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezisihi pande zinazo hasimiana katika mgogoro wa Mashariki ya Kati kuacha kushambulia miundombinu kwani ni kinyume cha sheria za Kimataifa. Mkurugenzi wa Huduma za Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa wa mjini Geneva Uswisi Alessandra Vellucci amewaambia waandishi wa habari kuwa “Umoja wa Mataifa ulishtushwa na matamshi yaliyoonekana katika chapisho la mitandao ya kijamii ambayo yalitishia mashambulizi ya Marekani dhidi ya mitambo ya kuzalisha umeme, madaraja na miundombinu mingine, iwapo Iran haitakubali makubaliano. Katibu Mkuu amezitaka pande zote kuzingatia wajibu wao kuhusu mwenendo wa mgogoro huo. Miundombinu ya kiraia, ikiwa ni pamoja na miundombinu ya nishati, haiwezi kushambuliwa, hata kama miundombinu maalum ya kiraia ingekuwa ikitumika kwa lengo la kijeshi. Umefika wakati wa pande husika kukomesha mzozo huu.”Leo ikiwa ni siku ya afya duniani, shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuimarisha ushirikiano na kuunga mkono sayansi kama msingi wa kuboresha afya ya binadamu. WHO imesema sayansi inapaswa kuwa msingi wa maamuzi yote ya afya katika ngazi za kitaifa na kimataifa na kutoa wito kwa serikali, taasisi na watu binafsi kuongeza ushirikiano ili kuhakikisha sera na hatua za afya zinazingatia ushahidi wa kisayansi. Kauli mbiu ya siku hii ni “Pamoja kwa Afya, Simama na Sayansi.”Na hii leo dunia inakumbuka mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 dhidi ya watutsi nchini Rwanda, matukio ya kumbukizi yamefanyika kwenye ofisi za  Umoja wa Mataifa huko Nairobi, Kenya, Geneva nchini Uswisi na hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwenye ukumbi wa Baraza Kuu. Matukio yamehudhuriwa na manusura, viongozi wa Umoja wa Mataifa na Rwanda na mashirika ya kiraia ujumbe mkuu ukiwa hatua zichukuliwe kuhakikisha mauaji ya kimbari hayatokei tena.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    12 min
  • 02 APRILI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania kupata ujumbe wa Zahra Salehe, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la ICCAO linaloshughulika na masuala ya vijana amabye kwa kuwa mwaka huu 2026 ameshiriki tena katika  mkutano wa CSW70 anatueleza ni kwa kiasi gani wameweza kulitekeleza malengo ya mikutano haya katika nchini humo.Vita Mashariki ya Kati vilivyoanzishwa na Marekani na Israeli dhidi ya Iran vikiingia mwezi wa pili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres leo hapa makao makuu ya UN jijini New York, Marekani amezungumza na waandishi wa habari akisisitiza sio tu vita hivyo vikome bali pia anaendeleza diplomasia za kusaka suluhu. Guterres amesema, Ninamtuma Mjumbe wangu Maalum Jean Arnault. Lengo ni kuunga mkono jitihada za kikanda. Lazima tupate njia ya amani ya kutoka katika hali hii. Ujumbe wangu uko wazi. Kwa Marekani na Israeli, ni wakati muafaka kusitisha vita vinavyosababisha mateso makubwa ya kibinadamu na tayari vinaanzisha athari mbaya za kiuchumi. Kwa Iran, isitishe kushambulia majirani zake.. Ripoti mpya ya Kamisheni  ya Umoja wa Mataifa kwa Uchumi wa Afrika, (ECA)  imependekeza umuhimu wa kuimarisha mifumo ya usimamizi wa deni la umma barani Afrika, ikionya kwamba uendelevu hautegemei tu kiwango cha kukopa bali pia ubora wa taasisi, mifumo ya kisheria, na uwazi. Ikitolewa leo huko Addis Ababa, Ethiopia, ripoti hiyo inataja udhaifu kama vile uwezo mdogo wa kufanya uchambuzi wa hatari, na ushawishi wa mashinikizo ya kisiasa katika maamuzi ya kukopa ikisema kuwa kuboresha usimamizi ni jambo muhimu ili kuhakikisha kuwa deni la umma linachangia ukuaji wa uchumi endelevu badala ya kuwa chanzo cha kuyumba kifedha.Wakati dunia hii leo ikiadhimisha Siku ya Uelewa wa Usonji, familia katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli,  zinakabiliwa na changamoto zinazoongezeka katika kuwahudumia watoto usonji katikati ya mzozo unaoendelea na hali mbaya ya kibinadamu. Katika kitongoji cha Sheikh Radwan kaskazini mwa Jiji la Gaza, Layan Abu Qousa mwenye umri wa miaka 16, ambaye ana usonji, anaishi na familia yake katika magofu ya nyumba yao. Familia yake inasema hali ngumu ya maisha imeongeza changamoto zinazohusiana na hali yake, huku ukosefu wa utulivu na mkwamo wa kupata huduma za kitaalamu ukiendelea kudhoofisha ustawi wake.Na katika jifunze Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye Kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “ATANGULIAYE KUFIKA HUCHAGUA PA KUKAA”Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
    12 min
  • Ni jukumu la wanawake na wanaume kuendeleza haki za kila mtu - Dkt. Rukia Nzibo
    Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao. Feissal Kirwa wa Idhaa hii ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa amezungumza na kijana huyo.
    3 min
  • Sadia Yahya, Mwanamke jasiri Sudan anayesongesha amani kwa kutegua mabomu ya ardhini
    Tarehe 4 mwezi Aprili mwaka huu ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya  kutegwa ardhini ambayo yamekuwa ‘mwiba’ kwa wananchi walioko maeneo siyo tu ya vita hivi sasa bali pia yale ambamo mapigano yamemalizika lakini masalia ya mabomu yanaendelea kutesa wananchi. Nchini Sudan mwanamke mmoja anatekeleza kwa vitendo maudhui ya siku hii mwaka huu ambayo ni Wekeza kwenye amani, wekeza kwenye hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini. Je anafanya nini? Ungana na Flora Nducha.
    3 min
  • Ukandamizaji wa uhuru wa kujieleza huko Mashariki ya Kati - Türk
    Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujieleza umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la  Mashariki ya Kati, ukiongeza hali ya hofu iliyokuwepo tayari kutokana na migogoro na misukosuko mingi, ameonya hii leo Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Volker Türk. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
    4 min
  • 01 APRILI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujielez tangu mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, mabomu ya kutegwa ardhini na ujumbe wa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kutoka Kenya.Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Marekani na Israeli dhidi ya Iran, ukandamizaji wa nafasi ya kiraia na uhuru wa kujieleza umeongezeka kwa kiasi kikubwa kwenye eneo la  Mashariki ya Kati, ukiongeza hali ya hofu iliyokuwepo tayari kutokana na migogoro na misukosuko mingi, ameonya hii leo Kamishna Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Volker Türk.Tarehe 4 mwezi Aprili mwaka huu ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini ambayo yamekuwa ‘mwiba’ kwa wananchi walioko maeneo siyo tu ya vita hivi sasa bali pia yale ambamo mapigano yamemalizika lakini masalia ya mabomu yanaendelea kutesa wananchi. Nchini Sudan mwanamke mmoja anatekeleza kwa vitendo maudhui ya siku hii mwaka huu ambayo ni Wekeza kwenye amani, wekeza kwenye hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini.Kutoka nchini Kenya, kijana aliyeshiriki mkutano wa 70 wa Kamisheni ya Hali ya Wanawake duniani, CSW70 amezungumzia jinsi vikao kama hivyo vimekuwa fursa kwa watetezi wa haki za wanawake na wasichana kuwasilisha changamoto kutoka maeneo yao na kusaka suluhu kwa pamoja na washiriki wenzao.Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    10 min
  • Elimu ya haki za kisheria inapaswa kutumia lugha inayoeleweka na jamii - Wakili Mengo
    Wiki iliyopita Kikao cha 70 cha Kamisheni ya Hali ya Wanawake Duniani CSW70 kilikunja jamvi baada ya wiki mbili za kujadili mada ya haki, haki za kisheria na kuchukua hatua kuhakikisha haki za wanawake na wasichana zinapatikana. Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya  ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.
    6 min
  • 31 MACHI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kia inayotorejesha katika mkutano wa CSW7O amabko Flora Nducha wa Idhaa hili kandoni mwa kikao hicho alipata fursa ya kuzungumza na Onyonge Mengo kijana mpigania haki za wanawake, mtafiti na wakili kutoka Mahakama Kuu ya Kenya  ambaye pia anafanyakazi na shirika la kimataifa la maendeleo la Hivos ili kufahamu kwa kina nini wanachokifanya kusongesha haki za kisheria za wanawake na wasichana.Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiwa umeingia siku ya 31 , zaidi ya watu 200,000 wamevuka mpaka wa Lebanon na kuingia Syria tangu mashambulizi baina ya Israeli na Hezbollah yaanze mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya Marekani na Israeli kushambulia Iran. Ripoti mpya ya iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP, inaonya kuwa idadi kubwa ya watu nchini Iran inaweza kutumbukia kwenye umaskini kadri misukosuko ya kiuchumi inavyozidi kuathiri maisha ya kila siku. Shirika hilo linasema hali hiyo inahatarisha kufuta mafanikio ya maendeleo yaliyopatikana kwa miaka kadhaa, huku Kiwango cha Maendeleo ya Binadamu (HDI) kikitarajiwa kushuka kwa kiasi kikubwa sawa na kupotea kwa zaidi ya mwaka mmoja wa maendeleo.Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM, leo limeomba dola milioni 277 kusaidia watu walio hatarini zaidi waliokumbwa na mizozo na ukosefu wa makazi nchini Sudan na nchi jirani kwa mwaka huu wa 2026, wakati mgogoro huo ukikaribia kuingia mwaka wake wa tatu. Mkurugenzi Mkuu wa IOM Amy Pope ameonya kuwa familia zinakabiliwa na “chaguo ngumu lisilowezekana kati ya kubaki bila huduma muhimu au kurejea katika jamii zilizosambaratishwa na vita”. Fedha hizo zitatumika kuimarisha mifumo ya kibinadamu, kupanua njia za misaada, na kuimarisha operesheni za kuvuka mipaka ili kusaidia waathirika kuishi na kujijenga upya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana na matumizi ya neno "GIDA."Mwenyeji wako ni Rashid Malekela, karibu!
    12 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners