Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • 08 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunaangazia ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya baharí duniani na kumulika ni hatua gani Zanziba zinachukua kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi. Pia tunakwenda nchini Kenya kufuatilia simulizi ya mchezaji wa raga.Bahari duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa zinazotishia afya ya mazingira na ustawi wa binadamu, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres na kutoa wito wa hatua za haraka na za pamoja kukabiliana na hali hiyo.Jamii katika mkoa wa Kaskazini Unguja huko visiwani Zanzibar nchini Tanzania wanaadhimisha siku ya bahari hii leo Umoja wa Mataifa ukielezea dhahiri mafanikio ya mradi wa uhifadhi wa mikoko na ufugaji wa nyuki unaochagiza sio tu upatikanaji endelevu wa kipato bali pia uhifadhi wa mazingira na bahari.Nyota wa mchezo wa raga ama rugby, Kevin Wekesa kutoka nchini Kenya ambaye alishiriki Michezo ya Olimpiki jijini Paris Ufaransa mwaka 2024, ameeleza nia yake ya kufanya vizuri uwanjani huku akitumia umaarufu wake kuhifadhi mazingira na kuhamasisha hatua endelevu kupitia michezo ili kujenga dunia yenye mnepo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    10 min
  • Lazima tujenge uhusiano mpya na bahari- Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
    Bahari duniani zinakabiliwa na changamoto kubwa zinazotishia afya ya mazingira na ustawi wa binadamu, ameonya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres na kutoa wito wa hatua za haraka na za pamoja kukabiliana na hali hiyo. Akizungumza kwa njia ya video katika ujumbe wake wa Siku ya Kimataifa ya Bahari inayoadhimishwa kila mwaka Juni 8, Bwana Guterres amesema bahari ni msingi wa maisha na maendeleo duniani, lakini zimekuwa zikikabiliwa na shinikizo linalozidi uwezo wake wa kustahimili."Bahari inaongoza tabianchi yetu, inalinda mifumo ya ikolojia na uchumi, na inalisha mabilioni ya watu duniani," anasema Guterres na kuongeza kuwa, "bahari ipo kwenye zahma kubwa na tunaishinikiza kupita uwezo wake."Guterres amerejelea Ripoti ya Tatu ya Tathmini ya Bahari Duniani iliyozinduliwa leo, ambayo imebainisha kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi, uvuvi uliokithiri, kupotea kwa bionuwai na uchafuzi wa bahari.Katibu Mkuu Guterres amesisitiza akisema, "hatuwezi kuendelea kuichukulia bahari kama kitu kisicho na ukomo," akihimiza kujengwa kwa uhusiano mpya na bahari unaozingatia sayansi, unaoongozwa na sheria za kimataifa na unaojengwa juu ya wajibu wa pamoja wa mataifa, sekta mbalimbali na vizazi vyote.Ametaja mafanikio ya Mkutano wa Tatu wa Bahari wa Umoja wa Mataifa uliofanyika mwaka jana pamoja na kuanza kutekelezwa kwa Makubaliano ya Baiyonuai ya Bahari katika maeneo yaliyo nje ya mamlaka ya kitaifa mwaka huu kama ushahidi kwamba ushirikiano wa kimataifa unaweza kuleta matokeo.Anasema, "hatua za pamoja za kimataifa zinawezekana na ni za lazima."Katika hitimisho la ujumbe wake wake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amewataka viongozi wa dunia, sekta binafsi na wananchi kuchukua hatua kwa haraka ili kulinda bahari kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.Anasema, "katika Siku hii ya Kimataifa ya Bahari, hebu tuchukue hatua kwa nia thabiti na kutatua mahitaji ya wakati huu."Hakika yanayosemwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yanaendana na aliyoyasema Mwenyekiti aliyechaguliwa wa ya Tume ya Kiserikali ya Bahari ya UNESCO (IOC) kwa Afrika na Nchi za Visiwa vinavyokaribia bara la Afrika (IOCAFRICA) Hellen Gichuhi alipozungumza na Idhaa ya Umoja wa Mataifa.
    3 min
  • 05 JUNI 2026
    Jaridani tunakuletea mada kwa kina. Hii leo dunia inaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani huku maadhimisho ya kimataifa yakifanyika jijini Baku nchini Azerbaijan. Maudhui ya mwaka huu ni "Sasa kwa ajili ya Tabianchi", yakiweka msisitizo mkubwa wa kuchukua hatua dhidi ya za uhifadhi wa mifumo ya ikolojia na hatua za kukabili tabianchi.Hivi karibuni, Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria pamoja na wadau, iliwasilisha Ripoti ya Hali ya Ziwa hilo ikionesha uwepo wa kemikali hatarishi, taka ngumu, plastiki, pamoja na majitaka vitu ambavyo ni hatari kwa viumbe wa majini na mazingira. Rashid Malekela wa Idhaa hii ametembelea mwalo wa Luchelele, uliopo mkoani Mwanza, kaskazini-magharibi mwa Tanzania, kufahamu jinsi wakazi wa eneo hilo wanavyochukua hatua dhidi ya Tabianchi. Anaanza na uongozi wa Kikundi cha Usimamizi wa Rasilimali za Uvuvi, BMU.Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za ... Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
    10 min
  • 04 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inatupeleka nchini nchini Rwanda. Kufuatia changamoto zinazoongezeka kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kupanda kwa gharama za mbolea na ushindani wa masoko ya kikanda, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO linashirikiana na nchi ya Rwanda kutekeleza mkakati mpya wa kuimarisha sekta ya chai lengo likiwa ni  kuboresha zao hilo na kuinua pato la mkulima.Mlinda amani wa Umoja wa Mataifa anayehudumu nchini Lebanon amefariki dunia na wengine wawili wamejeruhiwa mapema leo Alhamisi baada ya makombora ya mizinga kulenga eneo lao la kazi karibu na Marjayoun kusini mashariki mwa nchi hiyo, imesema taarifa ya Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon UNIFIL. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kutoa taarifa kuhusu tukio hilo muda wowote kuanzia sasa.Shirika la Umja wa Mataifa la afya Duniani, WHO, limesema chakula kisicho salama kinaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya umma duniani, kikisababisha takribani wagonjwa milioni 866 na vifo milioni 1.5 kila mwaka, huku watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wakiwa katika hatari kubwa zaidi. Kwa mujibu wa ripoti mpya watoto hao wadogo, ambao ni asilimia 9 tu ya idadi ya watu duniani, wanachangia karibu theluthi moja ya magonjwa yote yanayosababishwa na chakula.Leo ni siku ya watoto wasio na hatia waathirika wa ukatili duniani, maadhimisho haya yanakuja wakati ambapo ripoti ya Mwaka ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto na Migogoro ya Silaha inaonesha kwamba ukatili dhidi ya watoto katika migogoro ya silaha ulifikia viwango visivyo vya kawaida mwaka 2024, huku kukiwa na ongezeko la asilimia 25 la ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikilinganishwa na mwaka uliopita.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu ni Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya, kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “La kiliwacho kisicholiwa ni sumu”."Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
    10 min
  • Hifadhi ya Ngorongoro: Ambapo uhifadhi, utamaduni na utalii vinakutana kwa mustakabali endelevu
    Tukilekea Siku ya Mazingira Duniani hapo Juni 5, Leo tunakupeleka katika moyo wa Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamaduni, mazingira na utalii vinakutana kwa mustakabali endelevu? Ili kupata majawabu Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na Kamishna wa Hifadhi ya Ngorongoro, Abdul-Razaq Badru. Ungana nao
    10 min
  • 03 JUNI 2026
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Tanzania Kaskazini mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambako Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro inaendelea kuwa mfano wa jinsi binadamu, wanyamapori na urithi wa kitamaduni vinavyoweza kuishi pamoja huku vikichangia maendeleo ya utalii endelevu na ulinzi wa mazingira. Je nini kinafanyika kuhakikisha uhifadhi, utamaduni, mazingira na utalii vinakutana kwa mustakabali endelevu? Ili kupata majawabu Flora Nducha wa Idhaa hii amezungumza na Kamishna wa Hifadhi ya Ngorongoro, Abdul-Razaq Badru.Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ameendelea kusisitiza umuhimu wa ugunduzi wa mapema kwani hatua zikichukuliwa haraka wagonjwa wa Ebola wanapona. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Geneva Usiswi baada kurejea kutoka ziarani mashariki mwa DRC amesema, Kufikia sasa, watu sita wamepona nchini DRC na wawili nchini Uganda, jambo linaloonesha kuwa watu wanaweza kupona Ebola iwapo watapata huduma za afya na kwenda vituo vya afya mara tu wanapoanza kuonyesha dalili za ugonjwa huo.Kuelekea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia la FIFA wiki ijayo hapa Marekani na katika nchi jirani, Canada na Mexico, Shirika la Afya la Nchi za Amerika (PAHO) limetoa wito kwa nchi za bara la Amerika kuimarisha ufuatiliaji wa ugonjwa wa surua na Rubella kufuatia  mikusanyiko mikubwa inayotarajiwa na milipuko inayoendelea ya surua na ongezeko la safari za kimataifa vinaweza kuongeza kasi ya kuenea kwa ugonjwa huo. Shirika hilo linazitaka mamlaka za afya kubaini maeneo yaliyo katika hatari kubwa na kuimarisha hatua za kukabiliana haraka ili kuzuia maambukizi zaidi. Na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa asubuhi hii kwa saa za New York, Marekani wanachagua wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 1 Januari 2027 hadi 31 Desemba 2028. Kutoka Barani Afrika mgombea mmoja ni Zimbabwe ambaye hata hivyo anatarajiwa kupita kwani hana mpinzani katika nafasi hiyo. Nchi zitakazochaguliwa zinachukua nafasi za Somalia, Pakistan, Panama, Denmark na Ugiriki, ambazo mihula yao itaisha mwishoni mwa mwaka huu 2026.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

7 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners