
Sign up to save your podcasts
Or


Mada kwa kina leo inamulika ubunifu wa aina yake wa kugeuza mabaki ya nywele za binadamu kuwa mbolea asilia, hatua ambayo inatekeleza Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs. Je nani anafanya? Na inafanyika wapi? Ungana na Assumpta Massoi kwenye mada hii kwa kina inayoanza na utambulisho wa muhusika kutoka Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, barani Afrika.
Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MADHILA"
Miaka 20 tangu kupitishwa kwa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu (CRPD) Tanzania inasema inajivunia mafanikio makubwa ya ujumuishwaji , je ni mafanikio gani hayo na ni katika nyanja gani? Kupata undani ungana na Maryprisca Mahundi Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum nchini Tanzania akizungumza na Flora Nducha wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa.
Leo tunaangazia hatua kubwa katika mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi, VVU, ambapo Zimbabwe imekuwa miongoni mwa nchi za kwanza duniani kuanza kutoa Lenacapavir, sindano ya kinga inayotolewa mara mbili tu kwa mwaka na yenye ufanisi wa zaidi ya asilimia 96 katika kuzuia maambukizi mapya ya VVU. Hatua hiyo inaimarisha juhudi za nchi hiyo yenye kiwango cha maambukizi cha asilimia 11.2, ikilenga zaidi
makundi yaliyo hatarini, hususan wasichana balehe na wanawake vijana ambao wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa maambukizi. Hata hivyo, pamoja na matumaini hayo, changamoto za upatikanaji wa dawa hiyo, gharama, unyanyapaa pamoja na ufikiaji wa huduma katika maeneo ya vijijini bado zinaendelea kuathiri kasi ya mafanikio. Kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kupambana na UKIMWI, UNAIDS, Feissal Kirwa wa idhaa hii amefuatilia kwa kina.
Sasa umewadia wasaa wa kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA. Anafafanua maana za neno "MZIO"
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Feissal Kirwa akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya amani na usalama, usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama, haki za binadamu na hali ya hewa.
MUHTASARI1. Wimbi jipya la mashambulizi makubwa ya Urusi dhidi ya Ukraine yaliyosababisha vifo vya raia na majeruhi wengi, limelaaniwa vikali na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Ukraine, Matthias Schmale, akisisitiza kuwa raia lazima walindwe kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu.Mashambulizi hayo ya usiku yaliyoanza mwezi huu wa Agosti yamekuja baada ya mwezi Julai kuwa mwezi ulioshuhudia idadi kubwa zaidi ya vifo vya raia nchini Ukraine tangu Aprili mwaka 2022. 2. Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, kupitia msemaji wake Jeremy Laurence, ameeleza wasiwasi mkubwa kuhusu kuongezeka kwa utekelezaji wa hukumu za kifo nchini Iran. Kwa mujibu wa Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa, adhabu ya kifo inaendelea kutumiwa kama njia ya kuwatia hofu wananchi na kukandamiza sauti za wanaopinga serikali.Akizungumza leo jijini Geneva, Uswisi, Jeremy Laurence amesema,“tunazihimiza mamlaka za Iran kusitisha mara moja utekelezaji wa hukumu zote za kifo na kuelekea katika kufuta kabisa adhabu ya kifo.” 3. Utafiti wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) unaonesha kuwa uimarikaji wa mwenendo wa hali ya hewa ya El Niño unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uhaba wa chakula duniani hadi mwaka 2027. Shirika hilo linaongeza juhudi za kujiandaa na kukabiliana na athari hizo, huku El Niño ikiwa tayari imeanza kuwaathiri watu walio katika maeneo yenye hali ya njaa. MADA KWA KINAKituo kipya cha kutoa huduma kwa walioambukizwa ugonjwa wa Ebola, kinafunguliwa wiki hii huko Bunia, jimboni Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambako ndio kitovu cha mlipuko wa sasa wa Ebola ya virusi vya Bundibuvyo. Kituo hiki kitakuwa kituo kikubwa zaidi nchini humo cha kutibu Ebola. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi anatupitisha kwa kutumia video iliyoandaliwa na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA.
Hii leo jaridani mwenyeji wako ni Assumpta Massoi akikuletea Muhtasari wa Habari na Mada kwa Kina. Kwa ujumla anaangazia masuala ya usaidizi wa kibinadamu, amani na usalama pamoja na afya.
Muhtasari wa habari:Na sasa ni wasaa wa mada kwa kina inayotupeleka nchini Afrika Kusini, ambako dawa mpya ya kujikinga na Virusi Vya Ukimwi, VVU, iitwayo Lenacapavir, imeanza kutolewa kama sehemu ya jitihada dhidi ya maambukizi mapya, hasa miongoni mwa vijana walio katika hatari kubwa zaidi.
Kwa mara ya kwanza, mtu anaweza kujikinga na VVU, kwa kudungwa sindano moja tu kila baada ya miezi sita, bila kumeza kidonge kila siku. Lenacapavir imeonesha ufanisi wa zaidi ya asilimia 96 katika kuzuia maambukizi, na sasa imeanza kutolewa katika nchi tisa barani Afrika, ikiwemo Afrika Kusini, nchi yenye idadi kubwa zaidi duniani ya watu wanaoishi na VVU. Kupitia video iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na Ukimwi, UNAIDS, Feissal Kirwa wa Idhaa hii anakusimulia. Kwako Feissal.
Leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili tunakwenda Burundi, ukanda wa Maziwa Makuu barani Afrika na mchambuzi wetu ni Ntahombaye Hussein, Mwenyekiti wa Chama cha Wanahabari wa Kiswahili nchini Burundi, CHAWARUNDI. Anafafanua maana ya neno, “KUROWA”.
Hiki ni kitenzi kikimaanisha kuvua samaki na nomino yake ni mroaji.
Sentensi: Mroaji ameenda ziwa Tanganyika kuangalia iwapo atapata kitoweo cha samaki.
Hii inamaana mroaji pia ni mvuvi, na mchambuzi wetu anasema kwa ukanda wa Maziwa Makuu, mroaji ni mvuvi.
Ili kufahamu ni kwa namna gani Chuo Kikuu cha Mount Kenya kinawasaidia wanafunzi wasio na uwezo wa kifedha lakini wana uwezo wa kitaaluma ikiwa ni sehemu ya juhudi za chuo hicho kushiriki katika kuhimiza Malengo 17 ya maendeleo endelevu,SDG na kuunga mkono utekelezaji wake., Anold Kayanda wa Idhaa hii amezungumza na Profesa Peter Wanderi Mwangi ambaye alikiwakilisha chuo hicho katika Kongamano la Kimataifa kuhusu Elimu ya Juu lililofanyika mwezi uliopita hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani
Hii leo tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya, katika Kijiji cha Embulbul kilichoko Kaunti ya Kajiado, ambako Shirika lisilo la kiserikali la Tulivu Safe Haven, lililoanzishwa kwa kushirikiana na wadau wakiwemo mashirika ya Umoja wa Mataifa, linatekeleza hatua mbalimbali za kuwasaidia wanawake.
Hii ni pamoja na kuwaokoa na kuwahifadhi manusura wa ukatili wa kijinsia kwa kuwapatia makazi salama, ushauri nasaha, msaada wa kisheria na uwezeshaji wa kiuchumi, sambamba na kuwarejesha shuleni wasichana walionusurika. Je, nini kinafanyika? Kupitia video iliyoandaliwa na Redio washirika wetu Domus, Feissal Kirwa amefuatilia simulizi za manusura na kutuandalia makala hii.
Pia tunakuletea muhtasari wa habari.
Mwenyeji wako ni Anold Kyanda, karibu!
From the publisher's feed

14 Listeners

43 Listeners

5 Listeners

95 Listeners

25 Listeners

9 Listeners

18 Listeners

4 Listeners

8 Listeners

15 Listeners

8 Listeners

10 Listeners

4 Listeners

4 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners