
Sign up to save your podcasts
Or


Nchini Tanzania hususan visiwani Zanzibar, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) tangu mwaka 2019, kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wanaimarisha sekta ya mwani, kwa kuwekeza katika mafunzo yanayolenga kuongeza uzalishaji, tija na kipato. Miongoni mwa walionufaika zaidi ni vikundi vya wanawake, ambavyo vimejengewa uwezo kuhusu mbinu bora za uzalishaji, uanikaji na uhifadhi wa mwani, pamoja na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Assumpta Massoi anatuletea taarifa inayomhusu mnufaika mmoja wa mafunzo hayo.
(Taarifa ya Assumpta Massoi)
Jumla ya vikundi 33 vya wanawake vimewezeshwa kwa chanja bora za kuanikia mwani na maturubai maalum ya kuufunika wakati wa mvua.
Aidha, wanawake wamejengewa uwezo kuhusu teknolojia ya kilimo mchanganyiko inayowawezesha kulima mwani sambamba na kufuga majongoo bahari.
Teknolojia hii inalenga kuongeza tija, kuboresha matumizi ya rasilimali za bahari na kuwawezesha wanawake kupata vyanzo mbalimbali vya kipato.
FAO pia imewawezesha vijana kupitia Zanzibar Technology and Business Incubator (ZTBI), kwa kuwapatia mafunzo kuhusu usindikaji, ubunifu na uongezaji thamani wa bidhaa za mwani.
Mafunzo hayo yamejikita pia katika uboreshaji wa ubora, upatikanaji wa ithibati na masoko, huku vijana wakipatiwa vifaa vya kuendeleza uzalishaji na ujasiriamali katika sekta ya mwani.
Zoezi la siku tano la utoaji chanjo dhidi ya polio limekamilika katika mkoa wa Banadir nchini Somalia, likiwafikia watoto zaidi ya 122,000 walio chini ya umri wa miaka mitano. Kampeni hiyo imeendeshwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Somalia, mashirika ya Umoja wa Mataifa na wadau wengine. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Flora Nducha.
(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)
Kampeni hiyo imetekelezwa katika wilaya za Daynile, Garasbaley na Kahda, ambako kuna familia nyingi zilizolazimika kuyakimbia makazi yao na ambazo imekuwa vigumu kuwafikia watoto wao katika kampeni zilizopita.
Kwa muda wa miezi mitatu, Wizara ya Afya ya Somalia, utawala wa mkoa wa Banadir, Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani WHO, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF na wadau wengine walifanya maandalizi ya kina ili kuwafikia watoto walio hatarini zaidi.
Katika utekelezaji wake, timu 178 zilitumwa kutoa chanjo ya matone dhidi ya polio nyumba kwa nyumba, katika vituo maalumu, maeneo ya vituo vya mpito na kupitia timu zinazohamahama.
Timu hizo zilitumia takwimu za idadi ya watu, ramani za kijiografia na taarifa kutoka maeneo husika kutambua makazi na watoto ambao hawajapata chanjo.
CHANGAMOTO MIJINI
Katika taarifa yake kutoka Mogadishu nchini Somalia, WHO imeeleza kuwa kufikia kila mtoto katika maeneo ya mijini bado ni changamoto.
Mkoa wa Banadir unapokea watu wengi wanaokimbia maeneo mengine kutokana na ukosefu wa usalama nchini Somalia. Baadhi yao huishi katika makazi yasiyo rasmi na kuhama mara kwa mara, hali inayofanya iwe vigumu kuwatambua na kuwafuatilia watoto ambao hawajapatiwa chanjo.
Licha ya changamoto hizo, watoto 122,067 walipatiwa chanjo, sawa na asilimia 94 ya lengo la awali. Juhudi zinaendelea, watoto waliokosa chanjo watatafutwa na kupatiwa huduma hiyo haraka.
Mwakilishi wa WHO nchini Somalia, Dkt. Mohamed Ali Kamil, amesema “Kumfikia kila mtoto kunahitaji uongozi imara wa serikali, ushiriki wa jamii na ushirikiano madhubuti wa wadau wote. Kampeni hii ni fursa muhimu ya kujaribu mbinu inayolenga zaidi mahitaji na kuimarisha uwajibikaji katika utoaji chanjo mijini.”
KWA NINI CHANJO YA POLIO?
Chanjo hiyo ni muhimu kwa sababu polio inaweza kusababisha ulemavu wa kudumu, lakini pia inaweza kuzuilika kwa chanjo.
Somalia imekuwa ikikabiliana na mlipuko wa polio tangu mwaka 2017, hivyo kumfikia kila mtoto ni hatua muhimu katika kuziba pengo la kinga, kukomesha maambukizi na kulinda kizazi kijacho.
Karibu usikilize jarida la habari za UN ambalo leo habari zake zote zimetoka barani Afrika.
Utasikia kuhusu juhudi za kutoa chanjo wa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 huko nchini Somalia.
Utasikia namna FAO inavyowasaidia wananchi huko Zanzibar kuongeza ubora wa zao la Mwani.
Na mwisho utasikia ufinyu wa bajeti unavyoathiri utoaji wa misaada ya kibinadamu nchini Sudan Kusini.
Karibu kusikiliza jarida ambapo leo utasikia mahojiano na kijana kutoka nchini Kenya Feisal Kirwa aliyekuwa akishiriki mafunzo kwa Vitendo katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani kwa muda wa miezi sita na sasa amehitimu mafunzo hayo.
Pia utapata fursa ya kusikiliza muhtasari wa habari.
Katika jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea
-Harakati za kutokomeza Ebola ya virusi vya Bundibugyo huko Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, zinakumbwa na mkwamo kwani wananchi wamesema wanahitaji sio tu matibabu dhidi ya ugonjwa huo, bali pia maji, chakula, matibabu ya malaria, chanjo na huduma za afya uzazi, mama na mtoto.
-hirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mpya kuhusu ubora wa maji ya kunywa, likizitaka nchi kuimarisha kanuni, ufuatiliaji na usimamizi wa hatari zozote zinazoweza kujitokeza . Licha ya maendeleo yaliyopatikana, watu bilioni 2.1 bado hawana huduma ya maji ya kunywa inayosimamiwa kwa usalama
-kingo wa Magharibi eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Kibinadamu, OHCHR, imezisihi mamlaka za Israel kusaidia familia za Wapalestina ambazo zimezingirwa na walowezi ndani ya nyumba zao kwa siku kadhaa, huku kampeni ya kuwapokonya ardhi yao ikizidi kushika kasi.
-Na katika mada kwa kina leo tunajikita na Akili Mnemba (AI) na kilimo na kilimo biashara Afrika utamsikia Afisa wa FAO Meshack Malo
Katika Jarida la habari hii leo Flora Nducha anakuletea
-Leo ni Siku ya vijana Duniani Umoja wa Mataifa wasisitiza umuhimu wa kuwasikiliza, kuwapa fursa na kuwasaidia vijana kuchangia na kushamiri katika jamii
-Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi duniani, ILO kuhusu ajira kwa kundi la vijana inasema ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana duniani umeongezeka, huku ukuaji dhaifu wa uchumi na upungufu wa nafasi mpya za kazi ukiwaweka vijana katika mazingira magumu ya kuingia katika soko la ajira.
-Katika mada kwa kina utamsikia kijana kutoka Tanzania Zephania Opiyo aliyepata fursa ya mafunzo kwa vitendo Umoja wa Mataifa sasa amehitimisha na anatanabaisha safari yake na wito kwa vijana wenzie
Katika Jarida la Habari za Umoja wa Mataifa hii leo Feissal Kirwa anakuletea
-Idadi ya vifo na majeruhi kufuatia tetemeko la ardhi nchini Colombia inaongezeka huku Umoja wa Mataifa ukianza kuwasilisha msaada muhimu kwa waathirika na kuwa tayari kusaidia kwa kila hali
-Nchini Tanzania serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbbali likiwemo Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto UNICEF inahakikisha kila mtoto anasajiliwa pindi anapozaliwa
-Na kuelekea Siku ya Kimataifa ya Vijana itakayoadhimishwa kesho Agosti 12 leo utasikia sauti za vijana mbalimbali wakigusia ajira, elimu na maisha kwa ujumla.
From the publisher's feed

14 Listeners

43 Listeners

5 Listeners

95 Listeners

25 Listeners

9 Listeners

18 Listeners

4 Listeners

8 Listeners

15 Listeners

8 Listeners

10 Listeners

4 Listeners

4 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners

0 Listeners