Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Jinsi usawa wa kijinsia na rika katika umiliki wa ardhi unavyochochea ukulima na uhakika wa chakula Kenya
    Mpango wa Usimamizi wa Ardhi uliopatiwa jina "Kusaidia kufikia Ajenda 2030 kupitia mageuzi chanya ya ugatuzi wa ardhi katika maeneo ya ardhi za jamii nchini Kenya" umeboresha uhakika wa kupatikana kwa chakula na lishe kupitia upatikanaji wa ardhi kwa wote nchini Kenya. Programu hii imezinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo na chakula FAO kwa kushirikiana na Muungano wa Ulaya (EU) katika kaunti 9 ikilenga kuimarisha sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi. Kupitia video iliyoandaliwa na FAO, Cecily Kariuki anaeleza matokeo yake.
    6 min
  • 21 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka nchini Kenya kushuhudia jinsi mpango wa Usimamizi wa Ardhi uliopatiwa wa "kusaidia jamii kufikia Ajenda 2030” ambao FAO imetekeleza kwa kaunti kadhaa. Pia tunakuletea muhtasari wa habari na uchambuzi wa neno.Hague kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ICC ambayo leo imetoa kibali cha kukamatwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Waziri wa zamani wa ulinzi Yoav Galant  na kiongozi wa kundi la kipalestina la Hamas Mohamed Diab Ibrahim al-Masri alimaarufu kama  kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na uhaifu wa vita ulitendeka wakati wa vita inayoendelea baina ya Israel na Hamas.Mjini  Baku nchini Azerbaijan mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachanama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabainchi COP29 unaelekea ukingoni  na leo ukijikita na masuala ya kijinsia na mabadiliko ya tabianchi. Miongoni mwa waliozungumzia changamoto ya tabianchi kwa wanawake ni  Jemimah Njuki, mkuu wa kitengo cha uwezeshaji wa kiuchumi katika shirika la Umoja wa Mataifa la masuala ya wanawake UN Women.“Raia  wanaoshtakiwa katika mahakama za kijeshi nchini Uganda hukosa dhamana sawa ya mchakato wa kisheria kama wale wanaoshtakiwa katika mahakama za kiraia,” amesema Volker Türk, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu hii leo kufuatia tukio la kutekwa kwa mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda Kiiza Besigye akiwa nchini Kenya.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno MHARABU”.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • COP29 Georgina Magesa: Watoto wana haki ya kuishi katika mazingira salama
    Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 unaoendelea huko Baku Azerbaijan umeleta pia watoto na vijana wanaharakati wa mazingiria kutoka kote ulimwenguni na kuwapatia fursa kuketi katika meza moja na viongozi ili kuhakikisha mustakabali wao umewekwa katika ajenda ya mkataba huo. Jukumu lao kama wachechemuzi wa mabadiliko chanya na hitaji la mazungumzo na ushirikiano kati ya vizazi lilitambuliwa rasmi katika matokeo ya Mkutano wa Zama Zijazo, SOTF mnamo Septemba 2024.Georgina Magesa, msichana mwenye umri wa miaka tisa na mwanaharakati wa mazingira, ambaye amewakilisha watoto wenzake kutoka Tanzania katika Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan. Anatoa ujumbe mahsusi akianza kwa kusistiza kuwa watoto pia wana mchango katika kutatua changamoto za mabadiliko ya tabianchi.“Watoto wenzangu duniani kote, nyie pia mnaweza kuleta mabadiliko chanya. Anza na hatua ndogo pia muwe na ndoto kubwa. Panda miti. Hifadhi maji. Jifunze kuhusu mazingira yetu. Kwa Pamoja vitendo vyetu vidogo vitageuka mabadiliko makubwa”Katika mwaka huu wa 2024 ambao viwango vya joto duniani vimevunja rekodi duniani, watoto na vijana wanaendelea kupaza sauti zao wakihimiza viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka zinazohitajika ili kushughulikia janga la mabadiliko ya tabianchi. Georgina anasema Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF liko mstari wa mbele, lakini sasa ni wakati wa mshikamano kwa ajili ya mazingira bora kwa watoto wa leo, na wa zama zijazo..“Kwa viongozi wa dunia walioko hapa leo, hii si kazi ya UNICEF pekee. UNICEF inafanya kazi nzuri na sisi watoto, lakini tunahitaji msaada wako ili kujenga ulimwengu wa kesho ambapo hakuna mtoto anayepaswa kuchagua kati ya afya na elimu yake; ambapo hakuna mtoto anayekunywa maji yasiyo salama; hakuna mtoto anayekosa shule kwa sababu ya masuala yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi; na ambapo kila mtoto ana nafasi ya kuwa na afya bora na elimu bora.”Georgina anatamatisha kwa kusisitiza kuwa janga la mabadiliko ya tabianchi limenyima watoto haki zao hivyo kwa kila mtu...“Kumbuka unapolinda mazingira unalinda afya, elimu na ndoto za watoto. Mtoto mwenye afya bora na elimu bora anaweza kubadilisha ulimwengu.”Ama kweli watoto wana haki ya kuishi katika mazingira salama!
    5 min
  • 20 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia ripoti siku ya watoto duniani, na kwa kutambua siku hii tunamulika mikutano yote yanayoendelea kwa ajili ya haki za watoto na vijana, ambao wametoa ujumbe wao kutoka Baku nchini Azerbaijan na Denmark wakiwakilisha nchi zao.Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao.Kama ulivyosikia katika taarifa yetu ya kwanza leo ni siku ya watoto duniani ikirejelea tarehe 20 Novemba mwaka 1954 kwa mara ya kwanza kabisa ilipoanzishwa na Umoja wa Mataifa kusongesha umoja na kujitambua miongoni mwa watoto duniani..Makala ikiwa leo ni siku ya watoto duniani, tunakupeleka Baku Azerbaijan katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29,  ambako Selina Jerobon amefuatilia mkutano wa watoto na vijana inayomulika mchango wao katika kuhakikisha mazingira bora.Mashinani katika kuadhimisha siku ya watoto duniani tunabisha hodi msitu wa Amazoni nchini Peru kwa mtoto Susan akitoa wito kwa dunia kuchukua hatua dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi kulinda msitu huo kunusuru kizazi cha watoto wa sasa na wa vizazi vijavyo katika taifa hilo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • UNICEF - Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya mtoto duniani yafanyika Denmark
    Leo ikiwa ni siku ya watoto duniani ikirejelea tarehe 20 Novemba mwaka 1954 kwa mara ya kwanza kabisa ilipoanzishwa na Umoja wa Mataifa ili kusongesha umoja na kujitambua miongoni mwa watoto duniani. Kisha siku hii ikaongezwa nguvu na Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto duniani mwaka 1959 na hatimaye mwaka 1989 Baraza hilo lililopitisha Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Mtoto, CRC. Mkataba unatambua haki kuu nne za msingi za mtoto: Kuishi, Kuendelezwa, Kulindwa na Kushirikishwa. Hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limefanya maadhimisho ya kimataifa huko Copenhagen Denmark, na Madina Jubilate, Mchechemu wa UNICEF Tanzania kwa Tabianchi anaelezea alivyoshiriki.
    2 min
  • Waraka kutoka kwa watoto: Kwenu watu wazima, kwa nini mnauruhusu mustakbali wetu kuwekwa rehani?
    Leo ni siku ya watoto duniani maudhui mwaka huu yakiwa "Kila mtoto, kila haki"na katika kuhakikisha sauti zao zinasikika kuhusu mustakbali wa utakao, shirika la Umoja wa Maataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF limewapa fursa ya kuandika barua kwenda kwa watu wazima kote duniani ili kutoa madukuduku yao na kutanabaisha wanachokitaka kwa ajili ya mustakbali wao. Hao ni baadhi tu ya makumi ya watoto walioandika barua , hawa ni kutoka Gaza, Tanzania na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC ambao walishika kalamu na karatasi kufikisha ujumbe wao kwa watu wazima wa dunia ya sasa iliyoghubikwa na changamoto lukuki zinazoweka rehani mustakbali wao.Kwa mujibu wa ripoti mpya ya UNICEF ya “Hali ya watoto duniani mwaka 2024: Mustakabali wa Utoto katika Ulimwengu Unaobadilika,” iliyotolewa leo sanjari na maadhimisho ya siku hii kuna masuala matatu makubwa ya kimataifa yatakatoathiri maisha ya watoto ifikapo 2050 na kuendelea. Mosi ni mabadiliko katika idadi ya watu, pili janga la mabadiliko ya tabianchi na migogoro na tatu teknolojiaUNICEF inasema yote haya ni changamoto na fursa ambazo watoto wanaweza kukabiliana nazo katika zama zijazo.Rafif mtoto mkimbizi wa ndani ameandika barua kutoka Palestina ambako vita imetamalaki, anasema“Ninatoka mjini Gaza na sasa nimefurushwa hadi Kusini mwa Gaza. kama watoto Ni haki yetu kuishi kwa usalama na kujenga mustakbali bora”Kutoka mashariki ya Kati hadi Afrika Mashariki kwa Steven akimulika afya“Na nianaandika kwenu kutoka Tanzania. Kwenye jamii yangu watoto wanaugua kila wakati , kwa nini? Huu ndio mustakbali wangu je unasikiliza?”Nako Congo DRC mitihani ni mingi, Andrea anasema“Nataka kushuhudia dunia ambayo kila mtoto anapendwa, dunia ambayo amani inashamiri ni raha na faraja. Napenda kuona hasira zinageuka na kuwa mazungumzo”Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiunga mkono suti hizo za watoto katika ujumbe wake amesema Katika Siku ya Watoto Duniani tunasherehekea washiriki wachanga zaidi wa familia yetu ya kibinadamu. Lakini leo pia ni wakati wa kutambua changamoto kubwa zinazowakabili watoto katika ulimwengu wetu uliogawanyika sana, wenye misukosuko na mara nyingi ulioshamiri ukatili.”Ripoti ya UNICEF imetoa wito wa kuwekeza katika elimu, miji endelevu na yenye mnepo kwa watoto, miundombinu inayohimili mabadiliko ya tabianchi, teknolojia, huduma muhimu na mifumo ya msaada wa kijamii na pia teknolojia iliyo salama kwa watoto ili kupambana na mzigo wa changamoto zinazowakabili.
    3 min
  • 19 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku nchini Azerbaijan kwenye mkutano wa COP29. Miongoni mwa mambo yanayopigiwa chepuo ni madini ya kimkakati yanayoelezwa kuwa ni jawabu la nishati chafuzi kwa mazingira na tunapata ufafanuzi kutoka kwa Adam Anthony, Mkurugenzi Mtendaji wa HakiRasilimali nchini Tanzania.Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amewasihi viongozi wa kundi la nchi 20 zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, G20 wanaokutana huko Rio De Janeiro, Brazil kuwaagiza mawaziri na washawishi wao huko COP29 wahakikishe wanakubaliana juu ya lengo jipya na kubwa la mwaka huu la ufadhili kwa tabianchi nchi. Guterres amesema sambamba na hilo ni vema kukabiliana na taarifa potofu kuhusu tabianchi.Huko Kusini mwa Lebanon, walinda amani wanaohudumu kwenye ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kikosi cha Mpito nchini humo, UNIFIL, wameshuhudia uharibifu mkubwa wa kutisha kwenye vijiji vilivyoko sambamba na eneo      la kati ya Israeli na Lebanon lisilopaswa kuwa na mapigano, huku hali ya watoto nchini humo ikizidi kuwa mbaya.Hii leo ni siku ya choo duniani ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema licha ya choo kuwa ni msingi wa kusongesha afya ya binadamu na kusaidia watoto wa kike na wanawake kuishi maisha ya utu, bado wakazi wengi wa dunia hususan kwenye mizozo na majanga wanaishi bila huduma hiyo ya msingi.Mashinani tunasalia huko huko Baku, kwenye COP29 ambapo nampisha msichana mwanaharakati wa mazingira kutoka Tanzania, akieleza ni nini anafanya na nini atakachoondoka nacho kwenye mkutano huo.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    12 min
  • Uganda inaendelea na mapambano ya kutunza wakimbizi licha ya changamoto za kifedha
    Kwa miongo kadhaa sasa mfumo wa Uganda wa kuwaweka wakimbizi kwenye makazi badala ya kambi, umesaidia kujengea mnepo wakimbizi na hivyo wanaweza kujitegemea. Wakimbizi wanapata huduma za msingi kama vile hata ardhi ya kulima na kufugia mifugo ili kujipatia kipato. Kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, Selina Jerobon amefuatilia hadithi ya mama mkimbizi kutoka Jamhuri ya  Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye baada ya kupitia machungu na kukimbilia nchini Uganda sasa ameanza kuwa na matumaini ingawa ukata unatishia huduma kama alivyojionea mwenyewe Fillipo Grandi, Kamishna Mkuu wa shirika hilo.
    6 min
  • Vijana wafurahia stadi za kuondokana na umaskini Sudan Kusini
    Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Shamrashamra zilitawala wakati vijana 61, wakiwemo wasichana 41 na wavulana 20 walipohitimu mafunzo ya ufundi stadi yenye lengo la kuwaondoa katika umaskini na pia kuwaepusha kutumikishwa katika mzozo unaoendelea nchini humo tangu Desemba 2013.Walifundishwa urembo wa nywele, kutengeneza sabuni, halikadhalika ushoni, mafunzo yaliyofadhiliwa na UNMISS na kutolewa na shirika la kiraia Star Trust Organization, linalohusika na kupunguza ghasia kwenye jamii kwa kuwajegena vijana uwezo.Miongoni mwao ni Suzan James, mama wa watoto wawili aliyejifunza urembo wa nywele na akiwa anamhudumia mteja wakati wa mafunzo anasema.“Ninashukuru mno, kwa sababu nimejifunza mambo mengi ambayo awali sikuyafahamu, lakini sasa ninaweza kufanya. Inanisaidia sana, na ninajivunia na nina furaha. Baada ya hili, nitaenda kufungua sehemu yangu mwenyewe ya urembo wa nywele ili kusaidia jamii.”Huyu ni Justin Alex yeye amejifunza ushoni na akiwa kwenye chereheni yake anasema.. “iwapo nitapekela hii cherehani nyumbani, nitaweza kufanya kazi na kusaidia familia yangu. Kama kijana tusikae nyumbani au tusifanye uhalifu mjini na kusababisha vifo kwa jamii zetu kwa sababu si jambo zuri. Kuanzia sasa tunahitajika kushiriki kwenye shughuli za kusaidia jamii, kama kupeleka hii cherehani nyumbani ili nisaidie jamii yangu.”Wahitimu wamepatiwa vifaa vya kuanzia kufanyie kile walichojifunza. Katika hafla ya utoaji wa vyeti UNMISS iliwakilishwa na afisa wake wa masuala ya ulinzi na ujumuishaji kwenye jamii Ibrahim Tahiru ambaye amesema..“Mradi huu unaweza kuleta amani, lakini pia mradi huu huu unahitaji amani ili uweze kuendelea. Bila amani hivi vitu vitakuwa bure. Kwa sababu wahitimu wanahitaji mazingira yenye amani ili waweze kutumia stadi zao kwa ajili ya kuboresha maisha yao na ya jamii zao. Mradi huu ni ishara ya nia yetu ya kuendelea kushirikiana na Sudan Kusini na kusaidia kufikia amani ya kudumu na kuondokana na umaskini.”Mamlaka za Tambura zina Imani kubwa na mradi huu kama asemavyo Kaimu Kamishna wa Tambura Moses Masisere.“Hakika, Tambura tumekuwa tukililia amani. Kwa hiyo kwa msaada huu tunaamini kuwa mafunzo kwa vijana zaidi kutawasaidia washiriki kwenye harakati za kiuchumi na kupunguza mauaji na uhalifu mwingine Tambura.”
    2 min
  • 18 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia wakimbizi wa ndani nchini Haiti, na mafunzo ya stadi za kujikimu kimaishwa kwa vijana Tambura Sudan Kusini. Makala inatupeleka nchini Uganda na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM.Vijana katika mji wa Tambura ulioko jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini wanageuza mafunzo ya ufundi stadi kuwa nguvu ya amani na ustawi, mafunzo ambayo yalifanikishwa na ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS.Katika makala Selina Jerobon kupitia video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi anakupeleka Uganda kuona harakati za wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kujikwamua kiuchumi baada ya machungu waliyopitia nyumbani kwao.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kusikia ni kwa jinsi gani jamii katika maeneo kame wanakabiliana na mabadiliko ya tabianchi.Mwenyeji wako ni Bosco Cosma, karibu! 
    11 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners