Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • IOM: Zaidi ya watu 20,000 wamefuriushwa ndani ya siku 4 Haiti kutokana na machafuko ya magenge ya uhalifu
    Zaidi ya watu 20,000 wamekimbia makazi yao katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince katika muda wa siku nne tu, ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 17,000 wanaohifadhiwa katika makazi 15 ya wakimbizi wa ndani, kutokana na kuongezeka kwa ghasia za magenge ya uhalifu ambazo ziumevuruga kabisa minyororo muhimu ya usambazaji wa misaada na kulitenga jiji la Port-au-Prince (POTOPRINSI) limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM. Kupitia taarifa iliyotolewa leo na IOM nmini Port-au-Prince asilimia kubwa ya watu hawa waliofurushwa makwao wametawanywa zaidi ya mara moja wakilazimika kukimbia na kuacha kila kitu walichokuwa nacho na shirikika hilo linasema kiwango hiki cha watu kutawanywa hakijashuhudiwa Haiti tangu Agost 2023.Shirika hilo linasema kufungwa kwa usafiri wa anga kufuatia shambulizi lililolenga ndege tatu za kibiashara mjini Port-au-Prince, kuzuia ufikiaji wa bandari kuu ya nchi hiyo, na barabara zisizo salama zinazodhibitiwa na makundi yenye silaha kumeliacha eneo la Katikati ya mji mkuu taabani na kutengwa bila msaada na hivyo kuzidisha mateso kwa watu ambao tayari wako hatarini.Mkuu wa IOM nchini Haiti Grégoire Goodstein ameonya kwamba "Kutengwa kwa Port-au-Prince kunaongeza janga la ibinadamu. Uwezo wetu wa kutoa misaada umewekwa njiapanda na bila msaada wa haraka wa kimataifa, mateso yataongezeka sana kwa raia wa Haiti huku kukiwa na asilimia 20 pekee ya mji wa Port-au-Prince inayofikika, wakati wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wanakabiliwa na changamoto kubwa katika kufikia watu walioathirika.”Kulingana na Ofisi ya Haki za Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OHCHR, vikundi vya uhalifu katika mji mkuu wa Hati vinaendelea kupanuka wigo vikichukua udhibiti wa vitongoji vya ziada na kutenganisha zaidi jamii.Hadi sasa ofisi hiyo inasema ghasia zinazohusiana na magenge zimesababisha karibu vifo 4,000 mwaka 2024, unyanyasaji wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na unyanyasaji wa kingono unaotumiwa kama silaha ya ugaidi, umefikia viwango vya kutisha.Pia imesema wanawake na watoto wameathiriwa kupita kiasi, huku asilimia 94 ya wanawake na wasichana waliokimbia makazi yao wakiwa katika hatari kubwa ya kudhulumiwa kingono.Licha ya changamoto hizi, IOM na washirika wake wameahidi kuendelea kutoa msaada wa kuokoa maisha.IOM pia inatoa wito wa kuongeza haraka ufadhili kwa shughuli za kibinadamu Haiti kwani hadi kufikia mwezi huu wa Novemba, ombi la dola milioni 674 la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Haiti limefadhiliwa kwa asilimia 42 pekee, na kuwaacha mamilioni ya watu bila msaada wanaohitaji.
    3 min
  • Esneda kutoka jamii ya Yukpa asema haogopi vitisho kutetea eneo la jamii yao ya asili nchini Colombia
    Jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia imevumilia miongo kadhaa ya migogoro na watu kutawanywa inayosababishwa sio tu na mabadiliko ya tabianchi mila kandamizi bali pia kupotea kwa viumbe hai na hivyo kutishia maisha yao. Esneda Saveedra, Kiongozi wa jamii ya asili ya Yukpa nchini Colombia akiwa anazungumza akiketi ndani ya msitu na kando ya mto Maracas., anasema hana hofu ya kutetea ardhi hii.Ardhi anayozungumzia ni eneo hilo la mto Maracas anayotetea dhidi ya vitisho kutoka kwa waharibifu wa mazingira kufuatia yale yaliyojadiliwa katika mkutano wa 16 wa nchi wanachama wa mkataba wa kimataifa wa bayonuai, COP16 uliomalizika Ijumaa iliyopita huko mjini Cali nchini Colombia."Sina hofu ya kutetea ardhi hii. Yale niliyopitia kama mtoto, changamoto zote hizo, yalinipa nguvu, yalinipa ujasiri, na yakaondoa hofu yangu."Video ya shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR inatupatia taswira ya juu ya eneo la makazi ya jamii ya Yukpa, msitu mnene na kisha kwenye mto Maracas, shughuli zinaendelea, wengine wakiogelea, wengine wakivua samaki, mama mmoja akisafisha kuku aliyemaliza kumchuna.Esneda anaeleza umuhimu wa mto huu kwa maisha ya jamii yake na anaendelea kujitahidi ili kulinda mazingira hayo."Huu ni mto Maracas, ambapo watu wetu, mababu zangu, walivua samaki kwa ajili ya chakula kila siku. Waliharibu mazingira kwa kukata miti yote, na matokeo yake, mto ulianza kukauka. Leo, mto Maracas hauna mtiririko wa maji kama ulivyokuwa zaidi ya miaka 20 iliyopita."Katika juhudi zake, Esneda ameanzisha mazungumzo na maafisa wa serikali katika manispaa ya Becerril, akijaribu kuleta mabadiliko na uelewa juu ya umuhimu wa kuhifadhi ardhi na utamaduni wa watu wa Yukpa."Kumekuwa na uratibu, kazi ya pamoja, na jambo muhimu zaidi kwangu kama mwanamke wa Yukpa imekuwa kuleta ufahamu kuhusu watu wa Yukpa na ardhi yetu. Mabadiliko ya tabianchi yametufikisha kwenye tatizo kubwa zaidi, ambalo ni upotevu wa mazao na ukosefu wa chakula. Leo hatuna chakula cha kutosha katika jamii zetu. Tunaendelea kupambana, lakini pia tuko hapa kusaidia dunia nzima kuendelea kupambana na kulinda mazingira, ardhi, na hewa. Na kusema: 'Tupo hapa kuchangia kwa ajili ya ubinadamu, kwa ulimwengu mzima.’"Harakati zake zimekumbwa na vitisho.“Walinitishia hapa kwa kuzungumza, na kwa kusema ukweli. Mama yangu alikuwa kiongozi thabiti—na bado ni kiongozi thabiti. Na nilipokuwa mdogo, nilimsindikiza kwenye michakato yake yote ya harakati, mipango na uongozi. Niliendeleza njia hiyo ya uongozi kwa sababu niliona ni muhimu. Ilikuwa ni wajibu wangu. Nilijiambia, ‘mimi ni mwanamke ambaye nimezaliwa kutetea eneo hili.”Kwa Esneda, kulinda ardhi ya Yukpa ni zaidi ya wajibu; ni dhamira ya kuhifadhi urithi wa mababu zake. Katika changamoto za kila siku, Esneda anabaki imara kwa matumaini kuwa jamii yake na mchango wao katika kuhifadhi mazingira utatambuliwa ulimwenguni.
    4 min
  • Anne Tek: COP29 isiwape kisogo wanawake wanaokabiliiwa na athari za mabadiliko ya tabianchi Afrika
    Mkutano wa 29 wa Umoja wa Mataifa wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi COP29 ukianza wiki ya piili mjini Baku Azerbaijan leo, wito umetolewa kwa wanawake amba oni waathirika wakubwa wa janga la mabadiliko ya tabianchi kutopewa kisogo. Anne Cheruto Tek ambaye amebeba bendera ya wanawake waathitika wa mabadiliko ya tabianchi kutoka Afrika ameiambia UN News anachokifanya COP29..“Sana sana kufuatilia haya madhara ya mabadiliko ya tabianchi hasa kwa wanawake na vijana barani Afrika. Sana sana utakuwa wanawake ndio wanaoshughulikia masuala ya maji, masuala ya kuni, masuala ya chakula , lakini mara nyingi kukiwa na janga la mabadiliko ya tabianchi kama ukame, mafuriko, wanawake ndio wanaangamia zaidi, kwa sababu wanawke ndio wanakuwa na jukumu la kuendesha nyumba na hivyo hawana nafasi ya kutafuta fedhha ambaz zinaweza kuwasaidia wakati wa majanga hayo.”Na kutokana na hayo anasema wanawake hukabiliwa na changamoto kubwa“Wengi hupata magonjwa , wengi huathhirika sana wakati wa majanga ikiwemo vifo, ukosefu wa fedha na pia ukatili wa kijinsia wakati wa shida za mabadiliko ya tabianchi.”Na nini ombi lake katika mkutano huo?Kuhakikisha kuwa hizi changamoto zinaangaziwa hasa kwa masuala ya fedha, kuhakikisha kuwa fedha zinawafikia wanawake vijijini , kuhakikisha kuwa wanaweza kuelewa masuala ya mabadiliko ya tabianchi  na pia waweze kuelezea hadithi zao jinsi wanavyoathirika na tunaomba hii COP kuangazia haya majanga hasa kwa wanawake, wasichana na watu wasiojiweza kama wenye ulemavu.”
    2 min
  • 15 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia suala muhimu wa mabadiliko ya tabianchi tukijikita kataika mkutano wa COP29 huko Baku Azerbaijan kuwasikia wanaharakati wa mazingira kutoka nchi mbalimbali.Mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi, COP29 u unaofanyika Baku Azerbaijan, leo umejikita na ongezeko la gesi chafuzi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inatokana na shughuli za binadamu ikiwemo ufugaji wa ng’ombe, na sasa nini kifanyike ili kuidhibiti.Tunasalia huko huko Baku, Azerbaijan. Wito umetolewa kwa wanawake ambao ni waathirika wakubwa wa janga la mabadiliko ya tabianchi wasipewe kisogo katika harakati za kuhimili na kukabili madhara ya janga hilo.Katika makala Bosco Cosmas anatupeleka Amerika ya Kusini kusikia harakati za mwanamke wa jamii ya asili za kulinda eneo lao.Mashinani leo Fathimath, kijana kutoka Maldives anatoa kauli kwa ajili ya hatua za dharura kupambana na mabadiliko ya tabianchi katika mkutano wa COP29.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • UNEP: Licha ya taarifa za ongezeko la gesi ya methane hatua zinazochukuliwa ni kidogo
    Mkutano wa 29 wa mkataba wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP29 unaofanyika Baku Aberbaijana leo umejikita na ongezeko la gesi ya methane ambayo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na shughuli za binadamu na nini kifanyike kuidhibiti. FKulingana na ripoti iliyozinduliwa leo na shirika la Umoja wa Mataifa wa mazingira UNEP katika mkutano huo, mfumo wa teknolojia ya hali ya juu ambao unatambua uvujaji mkubwa wa gesi ya methane umewasilisha tarifa 1,200 kwa serikali na makampuni katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, lakini ni asilimia moja tu ya taarifa hizo ndizo zilizofanyiwa kazi.Ripoti hiyo mpya iliyopewa jina  “Jicho kwenye methane: Haionekani lakini inashuhudiwa” inasema licha ya ahadi zilizotolewa chini ya makubaliano ya ahadi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi ya methane kwa asilimia 30 ifikapo 2030 hatua zinazochukuliwa hazitoshelezi kupunguza gesi hiyo.Ripoti imeangazia tahadhari za methane kutoka kwenye Mfumo wa Tahadhari na hatua dhidi ya Methane MARS, ambayo ni sehemu ya UNEP ya uangalizi wa kimataifa wa uzalishaji wa methane IMEO  ambayo unawakilisha fursa ambazo haijatumiwa kwa hatua za haraka dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.Akizindua ripoti hiyo Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa UNEP, amesema ili kuwa na nafasi yoyote ya kudhibiti ongezeko la joto duniani, uzalishaji wa methane lazima ushuke, na ushuke haraka."Tunapozingatia kuwa ni asilimia 1 tu ya taarifa 1200 ambazo tulitoa ndizo zilisababisha hatua kuchukuliwa, basi hauitaji kuwa mtaalamu wa hesabu ili kuhesabu ushindi mkubwa unaowezekana hapa. Tuna mifumo iliyothibitishwa ya kutambua uvujaji Mkubwa wa gesi ya methane ili uweze kukomeshwa haraka, mara nyingi kwa ukarabati rahisi na wakati mwingine tunazungumza juu ya kukaza mipira au kubadilisha vichungi.”Ameongeza, kuwa "Serikali na makampuni ya mafuta na gesi ambayo sehemu kubwa ya uchumi wa dunia bado inawategemea lazima waache kupiga domo kwa changamoto hii wakati majawabu yanawatazama usoni. Badala yake, wanapaswa kutambua fursa muhimu ambayo mfumo huu unatoa na kuanza kuchukua hatua kutokana na taarifa kwa kuziba uvujaji ambao unamwaga gesi ya methane ya joto kwenye angahewa.”Amehitimisha kwa kusema, "Serikali na sekta binafsi lazima zizuie uzalishaji wa methane, na lazima zifanye hivyo sasa."Gesi ya Methane kwenye angahewa ni kichocheo cha pili kikubwa cha ongezeko la joto duniani baada ya hewa ya ukaa au CO2 na ina nguvu zaidi ya mara 80 kuliko hewa ya ukaa katika kusambaa kwa muda mfupi.UNEP imesisitiza kuwa utoaji wa gesi ya methane duniani lazima upunguzwe kwa asilimia 40 hadi 45 ifikapo 2030 ili kufikia njia za gharama nafuu zinazopunguza ongezeko la joto duniani hadi kufikia nyuzi joto 1.5°C.Bado taarifa za sayansi za hivi karibuni zinaonyesha viwango vya angahewa vya methane vimepanda kwa kasi iliyovunja rekodi katika kipindi cha miaka 5 iliyopita.
    3 min
  • 14 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka Baku kwa mkutan wa COP29, amabyo washiriki wanasaka mbinu za kujumuisha makundi yote katika harakati za kukabili na kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi yanayochochewa na ongezeko la hewa chafuzi. Idhaa ya Kiswahili imezungumza na Naomi mmjoja wao kutoka Tanzania. Pata pia muhtasari wa habari na ujifunze Kiswahili.Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa wa kisukari, shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO leo limesema idadi ya watu wazima wanaoishi na Kkisukari duniani ni zaidi ya milioni 8000 ikiwa ni ongezeko la zaidi ya mara 4 tangu mwaka 1990.Baku Azerbaijan ambako mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 leo umejikita na na lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antinio Guterres ameainisha jukumu muhimu ambalo miji, mikoa, biashara na taasisi za kifedha lazima zitekeleze katika kuendesha juhudi za dunia nzima kufikia lengo la kutozalisha kabisa hewa ya ukaa katikati ya karne hii.Nchini Sudan shirika la Umojja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharida OCHA limesema ghasia za kutumia silaha na mashambulizi katika Jimbo la Aj Jazirah zinadhihirisha ukatili wa karibu miezi 19 ya vita nchini Sudan,huku kukiwa na ripoti za ubakaji, mauaji ya halaiki na uporaji mkubwa. Katika chini ya wiki mbili, OCHA inasema uhasama huko Aj Jazirah umefurusha zaidi ya watu 135,000 kutoka makwao, wengi wao walikimbilia majimbo jirani ya Gedaref na Kassala.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo mchambuzi wetu mlumbi wa Kiswahili Joramu Nkumbi kutoka nchini Tanzania, anafafanua maana ya maneno “MADHALI, WAMA, FALAU NA HOBE”Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu! 
    10 min
  • Wananchi tufahamishwe kwa kina majukumu ya MONUSCO ili kukabili habari potofu DRC
    Umoja wa Mataifa unatambua ni kwa kiasi gani habari potofu na habari za uongo kuwa ni mojawapo ya vikwazo vikuu vinavyokabili operesheni zake za  kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.  Hii imesababisha Umoja huo kuhaha kila wakati kuona ni kwa vipi itakabiliana na habari hizo, iwe ni kupitia mafunzo kwa wanahabari, au kusaidia ujenzi wa vyombo vya habari, na hata kuzungumza na wananchi. Hivi karibuni Umoja Wa Mataifa kupitia Idara yake ya Ulinzi wa Amani, kitengo cha uadilifu wa habari, ulituma Tume yake Mashariki mwa DRC kukutana na wakazi ili  kujua ni nini Umoja wa Mataifa unapaswa kufanya ili kupambana na habari potofu na za uongo nchini humo. Mwandishi wetu wa Mashariki mwa DRC, hususan jimboni Kivu Kaskazini, George Musubao alishuhudia ziara hiyo na ametuletea makala hii.
    5 min
  • Patricia Kombo COP29: Ufadhili wa fedha utakuwa jawabu mujarabu kudhibiti mabadiliko ya tabianchi Afrika
    Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COP29 leo ukiingia siku ya nne  mjini Baku Azerbaijan vijana kutoka Afrika wataka ufadhili uongezwe kutoka mataifa makubwa hususan yanayochangia zaidi hewa ukaa ili kudhibiti athari za mabadiliko ya tabianchi kwa mataifa yanayoendelea ambapomiongoni mwa waathirika wakubwa ni vijana.  Asante Bosco na mmoja wa washiriki hao ni Patricial Kombo Mumbua kutoka Kenya  akiwasilisha matakwa ya vijana katika mkutano huo, na akizungumza na UN News  kuhusu ujumbe wake kwa COP29 amesema“Kwangu kama kiongozi wa vijana jambo la kwanza ni kuweza kupata zile fedha au kuzikusanya ili ziweze kusaidia mataifa ambayo yanapambana na kukabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi . Pili ni kuhakikisha kuwa viongozi kutoka mataifa ambayo yanazalisha zaidi hewa ukaa yanawajibika ili kuyafanya matifa ambayo yanaendelea kuweza kujilinda , kunufaika , kujiinua dhidi ya janga hilo na pia kujenga mnepo dhidi ya mabadiliko ya tabianchi katika jamii zao.”Na nini anachokitarajia katika mkutano huo wa COP29?“Ni kuweza kuona kuwa hili kongamano litaweza kuhamasisha upatikanaji wa hizo hela kwa mataifa ambayo yanakabiliwa na hizi changamoto za mabadiliko ya tabianchi, Na pia wakati ambapo mataifa yanaendelea kurekebisha michango yao ya kitaifa ya mabadiliko ya tabianchi au NDCs, waweze kuleta michango ambayo inaaambatana na zile changamoto ambazo mataifa yao yanazidi kuathiirika nazo za mabadiliko ya tabianchi.”Mbali ya masuala ya ufadhil mada zingine zinazotamalaki kwenye mijadala ya leo COP29 ni masuala ya nishani safi , mifumo ya tahadhari za mapemba na athari za mabadiliko ya tabianchi kwa matifa ya visiwa vidogo vinavyoendelea.
    2 min
  • 13 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazi ufadhili kwa wakulima huku mkutano wa COP29 ukiendelea Baku, na madhara ya mafuriko kwa wakulima nchini Sudana Kusini tukimulika jinsi Umoja wa Mataifa wanavyohaha kuwasaidia. Makala inatupeleka nchini DRC na mashinani tunasalia huko huko Sudan Kusini, kulikoni?Kuongeza kiwango cha fedha kwenye ufadhili wa miradi ya kukabili na kuhimili tabianchi nchi ikiwa ni moja ya masuala muhimu yanayojadiliwa katika mkutano wa 29 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi, COP29 huko Baku, Azerbaijan, leo ikiwa ni siku ya pili ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema bila kupunguza kwa kiasi kikubwa hewa chafuzi, na kuimarisha miradi ya kuhimili na kukabili mabadiliko ya tabianchi, kila uchumi duniani utakumbwa na madhara makubwa.Huko Maban, jimboni Upper Nile, kaskazini mashariki mwa Sudan Kusini, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linajenga vifaa vya kuhifadhi maji pamoja na makinga maji ili kuepusha mashamba dhidi ya mafuriko ya msimu yanayokumba eneo hilo mara kwa mara, eneo ambalo ardhi yake ina rutuba kwa ajili ya kilimo cha mazao ya chakula na biashara.Katika Makala George Musubao, mwandishi wetu huko Jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC akimulika mkutano ulioandaliwa na watendaji wa Umoja wa Mataifa ya eneo hilo kuangalia jinsi ya kukabiliana na  habari potofu na za uongo.Na mashinani tutakuwa Sudan Kusini, ambako shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP linasaidia jamii zilizoathiriwa na mafuriko kupata suluhisho la kudumu.Mwenyeji wako ni Bosco Cosmas, karibu! 
    10 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners