Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

By United NationsNewsDaily News
Download on the App Store

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu episodes

  • Uganda imechukua hatua kuhakikisha Kiswahili kinazungumzwa shuleni hadi bungeni: Dkt. Tendo
    Kwa kutambua thamani na mchango Mkubwa wa lugha ya Kiswahili katika Kanda ya Afrika Mashariki na kimataifa,  sasa serikali ya Uganda imeivalia njuga lugha hiyo kwa kuweka mikakati maalum ya kuhakikisha inafundishwa na kuzungumzwa kuanzia shuleni hadi Bungeni. Flora Nduha wa  Idhaa hii aliyeko mjini Havana Cuba kutujuza yanayojiri katika kongamano la kimataifa la Kiswahili amebainni hayo alipozunggumza na mmoja wa washiriki kutoka nchini Uganda.
    7 min
  • Guterres ampongeza Donald J. Trump kwa kuchaguliwa Rais wa Marekani
    Kufuatia Donald J Trump kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne Novemba 5,  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa salamu za pongezi. Taarifa iliyotolewa Jumatano asubuhi jijini New York, Marekani na msemaji wa Umoja wa Mataifa, imemnukuu Guterres akisema napongeza wananchi wa Marekani kwa ushiriki wao katika mchakato wa demokorasia.Kisha akasema nampongeza Rais Mteule Donald J. Trump na ninarejelea imani yangu kwamba ushirikiano kati ya Marekani na Umoja wa Mataifa ni nguzo muhimu ya uhusiano wa kimataifa.Guterres amesema Umoja wa Mataiifa uko tayari kufanya kazi kwa kina na serikali ijayo ya Marekani il ikutatua changamoto kubwa zinazokabili dunia hivi sasa.Trump ambaye anawakilisha chama cha Repablikani, anakuwa Rais wa 47 wa Marekani.Amemshinda Makamu wa Rais Kamala Harris ambaye alikuwa anagombea kiti cha urais kupitia chama cha Demokrati.Hii ni mara ya pili Trump ataongoza Marekani kwani alikuwa Rais wa  45 wa Marekani kuanzia Januari 20, 2017 hadi Januari 20, 2021 baada ya kushinda uchaguzi wa mwaka 2016.
    2 min
  • 06 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini Marekani, na watoto wanaotumikishwa jeshini na waasi nchini DRC. Makala tunakupeleka Havana nchini Cuba, na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Kufuatia Donald J. Trump kutangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa Marekani uliofanyika Jumanne Novemba 5, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa salamu za pongezi.Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC za kunasua watoto na vijana wanaotumikishwa vitani zinaendelea na tukio la hivi karibuni zaidi ni la kijana..Makala leo inatupeleka Havana Cuba ikiwa imesalia siku moja tu kabla ya kuanza kwa kongamano la kimataifa la Kiswahili lililobeba maudhui “Kiswahii  na teknolojia, na Kiswahili kama nyenzo ya kudumisha  amani na maendeleo”.Mashinani tutaelekea nchini Kenya kwa mwanamke mwandishi wa habari akitueleza jinsi wanavyochochea haki za binadamu.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    11 min
  • Simulizi ya Ombeni baada ya kutoroka waasi na kurejea uraiani huko DRC
    Harakati za ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC za kunasua watoto na vijana wanaotumikishwa vitani zinaendelea na tukio la hivi karibuni zaidi ni la kijana.Katika video ya MONUSCO iliyochapishwa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Ombeni anasimulia jinsi waasi wa FDLR mashariki mwa DRC walivyowakamata msituni."Tulikuwa vijana watanoFDLR walitukamata na kutupeleka msituni. Maisha ilikuwa ngumu sana na hatukuweza kutoroka"Kazi wanatumikishwa bila mshahara na zaidi ya yote."Kila saa ni mateso, kazi mingi bila malipo."Alitumikishwa msituni kwa miaka minane, akionesha makovu ya vipigo alivyopatiwa."Tuliteseka sana, tulitumikishwa kwa muda wa miaka minane, tukachapwa viboko, tuliumizwa sana na kubaki na majeraha"Lakini siku moj aliweza kutoroka. Akiwa Kibirizi akamweleza mkubwa wake ya kwamba.." Siku moja nikamwambia mkubwa wangu naenda kusalamia rafiki yangu, wakati huo tukapata nafasi ya kutoroka."Katika harakati hizo akakutana na MONUSCO. Anasema kwamba, "Njiani nikakutana na wanajeshi wa MONUSCO, nikainua bunduki juu na kujisalimisha, nikisindikizwa na mkubwa wao nikaeleza kile tulichopitia"Sasa Ombeni anashiriki programu za kumjumuisha tena kwenye jamii, DDR-S inayondeshwa na MONUSCO huko Beni, jimboni Kivu Kaskazini.
    3 min
  • 05 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia uvuvi katika mji wa Kalokol karibu na fuo za Ziwa Turkana Kaskazini mwa Kenya. Pia tunakuletea muhtasari wa habari zikiwemo za mkutano wa WUF12 Cairo Misri, chanjo ya malaria Sudan, siku ya Tsunami, na mashinani.Mkutano wa 12 wa Jukwaa la Miji Duniani, WUF12 umeingia siku ya pili hii leo huko Cairo, Misri, ambako Ming Zing ambaye ni Mkurugenzi wa Miji, Mnepo na Ardhi kutoka Benki ya Dunia amezungumzia umuhimu wa kujumuisha wanawake na vijana katika mipango miji.Sudan imekuwa nchi ya 16 barani Afrika na ya kwanza katika Ukanda wa WHO wa Mashariki na Mediterania kuanzisha chanjo dhidi ya Malaria kwa watoto wasiozidi umri wa miezi 12. Chanjo imeanza kutolewa jana katika majimbo ya Gedaref na Blue Nile ambapo WHO na wadau wamesema mwaka 2025 na 2026 chanjo itapelekwa katika maeneo 129 nchini kote Sudan.Na leo ni siku ya kimataifa ya kuhamasisha umma kuhusu tsunami, ambayo ni mawimbi makubwa ya maji yatokanayo na tetemeko chini ya bahari. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika ujumbe wake anasema pamoja na kukumbuka waliopoteza maisha kwa tsunami miaka 20 iliyopita,  tunaahidi tena kulinda zaidi ya watu milioni 700 duniani kote walio hatarini kukumbwa na Tsunami.Mashinani tutaelekea Sudan kusini kuangazia  harakati za Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani nchini humo, UNMISS za kuimarisha ulinzi wa wanawake katika migogoro na majanga.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    12 min
  • Walinda amani wa UN kutoka Tanzania wasaidia watoto yatima huko Beni, DRC
    Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, mapigano kati ya jeshi la serikali, FARDC na vikundi vilivyojihami, yamesababisha vifo na hata watu kufurushwa makwao. Watoto wamesalia yatima na hawana walezi. Vituo vya kulea watoto yatima vimebeba jukumu la kuwatunza, lakini navyo viko taabani. Walinda amani wa Umoja wa Mataifa, kutoka Tanzania, TANZBATT-11 wanaohudumu katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani DRC, MONUSCO waliguswa na kuamua kujiongeza na kuwasilisha msaada kwa watoto hao. Afisa Habari wa TANZBATT-11 Kapteni Fadhillah Nayopa anasimulia kile walichofanya.
    4 min
  • UN: Baada ya janga la njaa, sasa kipindupindu na homa ya kidingapopo yaikumba Sudan
    Nchini Sudan ambako vita na njanga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia  sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa  la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani. Asante Assumpta kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswisi na mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA na lile la afya duniani WHO, hali inazidi kuwa mbaya Sudan ambako katikati ya vita majanga mingine ya kiafya yanazuka.OCHA imeripoti zaidi ya wagonjwa 28,000 wa kipindupindu na vifo vimefikia 836 katika majimbo 11 kati ya 22 Julai na 28 Oktoba mwaka huu huku likihofia kwamba idadi kamili ya wagonjwa huenda ni kubwa zaidi.Pia shirika hilo limeonya juu ya kuendelea kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa homa ya kidingapopo na mvua zinazonyesha na kusababisha mafuriko makubwa zimeongeza hatari ya kusambaa kwa magonjwa hayo.Nalo shirika la WHO linasema milipuko hii imezuka wakati mfumo wa huduma ya afya nchini Sudan umzidiwa uwezo, huku hospitali nyingi hazifanyi kazi au zimefungwa kabisa kutokana na usambazaji mdogo wa vifaa na uhaba wa mafuta. Shirika hilo linasema hadi asilimia 80 ya vituo vya afya katika maeneo yenye migogoro ikiwa ni pamoja na Al Jazirah, Kordofan, Darfur na Khartoum  aidha havifanyi kazi au vimefungwa.Na linaonya kwamba "Kuporomoka huku kwa mfumo  wa afya  kunazuia mipango ya chanjo ya watoto,  kuongeza kasi ya kuenea kwa magonjwa yanayozuilika, na kuzua wasiwasi kuhusu uwezekano wa milipuko mikubwa zaidi ya magonjwa."Kwa sasa mashirika hayo yamesema majimbo yaliyoathirika zaidi na kipindupindu ni Kassala Gedaref, Al Jazirah, na Northern wakati homa ya kidingapopo imeghubika zaidi majimbo ya Kassala na Khartoum.Pia changamoto nyingine kubwa ya kutoa huduma za afya katikati ya milipuko hii mashirika hayo yanasema ni mashambulizi dhidi ya vituo vya afya ambayo tangu kuanza kwa vita 15 Aprili mwaka jana  yamefikia 116 na kusababisha vifo 188 na majeruhi 140.
    2 min
  • 04 NOVEMBA 2024
    Hii leo jaridani tunaangazia machafuko nchini Sudan unaosababisha janga la njaa, na mradi wa maji Galmudug Somalia kwa ajili ya maji safi na salama pamoja na mifugo. Makala tunakupeleka nchini DR Congo na mashinani nchini Kenya, kulikoni?Nchini Sudan ambako vita na janga la njaa vinaendelea kuwa mwiba kwa raia      sasa wahudumu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa wanaonya juu ya tishio lingine kubwa  la milipuko ya magonja ya kipindupindu na homa ya kidingapopo huku mfumo mzima wa afya ukiwa taabani.Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika.Makala inakupeleka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC ambako Kapteni Fadhillah Nayopa, Afisa habari wa kikosi cha 11 cha walinda amani wa Tanzania, TANZBATT-11 katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini DRC, MONUSCO anazungumzia usaidizi waliopatia watoto yatima.Mashinani kupitia video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa chakula, tunakutana na Geoffrey Nawet, Mwanafunzi katika shule ya Kakuma nchini Kenya akitueleza jinsi ambavyo programu ya Mlo shuleni ya lishe bora umewawezesha wanafunzi kumakinika shuleni na kupata motisha ya kuendelea na masomo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu! 
    10 min
  • UNICEF na wadau Somalia wafanikisha mradi wa maji kwa wakazi wa Galmudug
    Nchini Somalia, ni asilimia 52 tu wananchi ndio wanapata huduma ya maji safi na salama. Wengine hulazimika kutembea umbali mrefu kuteka maji ambayo si ya uhakika. Hata hivyo kwa msaada wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini humo pamoja na wadau, hali sasa inaanza kuimarika. Tuko Adale, mji wa ndani zaidi wa jimbo la kati mwa Somalia, Galmudug. Hapa zaidi ya kaya 2,000 sasa zina huduma ya maji safi na salama, kufuatia ukarabati wa kisima cha maji.Salada Mohammed Omar, yeye ni mfugaji na ni shuhuda wa mradi huu uliotekelezwa na serikali ya jimbo la Galmudug kwa ufadhili wa shirika la Marekani la Misaada ya kimaendeleo USAID na UNICEF.“Tulisafiri muda mrefu kuteka maji, lakini sasa kisima kiko karibu na makazi yetu, tunapata kwa urahisi maji ya kupikia, kufulia na kufanyia usafi.”Video ya UNICEF inaonesha raia na ngamia wakiwa kisimani. Mohammed Yusuf Dirshe ambaye ni kiongozi wa kijamii hapa Adale anasema “awali hakukuwa na tanki la maji wala pampu. Kwa hiyo ilikuwa vigumu kupata maji kwa ajili ya mifugo. Lakini sasa unaona hawa ngamia wanatoka umbali wa hadi wa kilometa 35.”Issack Mohammed, kutoka Kituo cha Amani na Demokrasia mdau wa mradi huu anaeleza kilichofanyika.“Ukarabati ulihusisha kujengea juu matanki, kuweka pampu inayotumia nishati ya jua, na kioski cha maji ili wavulana, wasichana na wanawake waweze kuteka maji kwa urahisi.UNICEF inasema mradi huu unarejesha uhai hapa Adale, kwa kuhakikisha watoto wanakua wakiwa na afya njema, jamii zinastawi na mbinu za kujipatia kipato zinakuwa endelevu.
    3 min
  • Asante WFP kwa msaada wa pesa taslim uliotuwezesha kiuchumi - Esther Josephine
    Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Mpango wa Chakula Duniani WFP,  ungali unaendelea kuwasaidia wakimbizi wa ndani nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kurejesha tabasamu la waliopoteza makazi yao kutokana na hali ya ukosefu wa usalama nchini humo. Chakula na pesa taslimu zilitolewa kwa wale wanaohitaji jimboni Kivu Kaskazini Mashariki mwa DRC. Mwandishi wetu George Musubao amekutana na Esther Josephine, mama wa watoto 3 aliyekimbia kutoka Kitsanga kwa sababu ya mapigano kati ya jeshi la serekali ya DRC (FARDC) na waasi wa M23, na anatueleza jinsi mama huyu amewezakujikwamua kiuchumi katika makala hii.
    4 min

About Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

From the publisher's feed

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

More shows like Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain by United Nations

ONU Info - L'actualité mondiale Un regard humain

14 Listeners

ONU en minutos by United Nations

ONU en minutos

43 Listeners

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas by United Nations

ONU News - Perspectiva Global Reportagens Humanas

5 Listeners

UN News Today by United Nations

UN News Today

95 Listeners

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事 by United Nations

联合国新闻 - 全球视野, 常人故事

25 Listeners

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы by United Nations

Новости ООН - Глобальный взгляд Человеческие судьбы

9 Listeners

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية by United Nations

أخبار الأمم المتحدة - منظور عالمي قصص إنسانية

18 Listeners

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां by United Nations

यूएन समाचार - वैश्विक परिप्रेक्ष्य मानव कहानियां

4 Listeners

UN Interviews by United Nations

UN Interviews

6 Listeners

UNcomplicated by United Nations

UNcomplicated

15 Listeners

The Lid is On by United Nations

The Lid is On

8 Listeners

UN Weekly by United Nations

UN Weekly

9 Listeners

UNiting Against Hate by United Nations

UNiting Against Hate

4 Listeners

amplifyHER by United Nations

amplifyHER

4 Listeners

世界进行时 by United Nations

世界进行时

0 Listeners

前方视野 by United Nations

前方视野

0 Listeners

Podcast ONU News by United Nations

Podcast ONU News

0 Listeners

Actualités by United Nations

Actualités

0 Listeners